Ikhlasi katika kauli na vitendo ni wajibu na hamna budi nayo kwani Allah
Subhanahu Wataala hapokei (haikubali) kauli wala kitendo bila ya ikhlasi ya
kumkusudia Allah Subhanahu Wataala Aliyesema:-
ﭽ ﮆ ﮇ
ﮈ ﮉ ﭼ الزمر:
٣
“Wa kuitakidiwa Mola ni Allah tu”.
ﭽ ﮘ ﮙ
ﮚ ﮛ ﮜ
ﮝ ﮞ ﮟ ﭼ البينة: ٥
“Wala
hawakuamrishwa ila kumuabudu Allah kwa kumtakasia Dini”.
ﭽ ﯞ ﯟ ﯠ
ﯡ ﯢ ﯣ ﯤ ﯥ
ﯦ ﭼ
النساء: ١٤٦
“Isipokuwa wale waliotubu (baada ya unafiki wao) na
wakajitengeneza na wakamshika Allah na wakaukhalisisha utii wao kwa Allah.”
Amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam katika hadithi Al-Qudsiy:- “Ikhlasi
ni siri katika siri yangu nimeihifadhi katika moyo wa niliompenda katika waja
wangu”. Ameitoa Al-Hassan. Aliy bin Taalib
amesema: Msitie wasi wasi kwa upungufu wa amali (vitendo) walakini mtie
wasiwasi kwa kukubaliwa kwake hivyo vitendo kwani Mtume Salallahu Alayhi
Wasalam amesema kumwambia Muadh bin Jabal:- “Ikhalisishe amali yako yakutosha
kidogo katika hiyo”. Na amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :- Watu wa
mwanzo wanaoulizwa Siku ya Kiyama watu watatu, mtu amepewa na Allah elimu basi
ataulizwa na Allah Subhanahu Wataala : “Umeifanyia nini elimu uliyopewa?
Atajibu Ewe Mola wangu nilikuwa nikiitumia (kwa kukuabudu) usiku na mchana”
atamjibu Allah Subhanahu Wataala umesema uwongo na watasema Malaika umesema
uwongo bali ulikuwa wataka uambiwe (na watu) kuwa fulani ni Mwanachuoni
(mtaalamu) na umeambiwa hivyo. Na mtu Allah Subhanahu Wataala amempa mali
akamwambia Allah umeifanyia nini akajibu nilikuwa naitolea sadaka usiku na
mchana Akasema Allah Subhanahu Wataala umesema uwongo na wakasema Malaika
umezua, bali ulikuwa wataka uambiwe kuwa fulani karimu na umeambiwa hivyo. Na
mtu ameuliwa katika jihadi (katika njia ya Allah) na Amwambia Allah umefanya
nini. Na hujibu ewe Mola wangu nimeamrishwa kupigana jihadi na nikapigana mpaka
nikauliwa basi Allah Subhanahu Wataala humjibu umesema uwongo na wasema Malaika
umesema uwongo bali ulikuwa wataka uambiwe fulani shujaa na umeambiwa hivyo,
akasema Abu Huraira kisha akanipiga Mtume Salallahu Alayhi Wasalam pajani na
akasema:-
( يا أبا هريرة أولئك أول خلق
تسعر نار جهنم بهم يوم القيامة)
“Ewe Aba Huraira hao ni watu wa mwanzo Moto wa Jahannam utakokwa
nao Siku ya Kiyama.”
Kifuatacho ni kisa cha mja na mti:-
Inasemekana kuwa kulikuwa na mja ambaye imemfikia habari kuwa kuna watu
wanaabudu mti fulani. Akatoka kwa kila ikhlasi nae ameazimia kwenda kuukata
akamjia Iblisi wakati yuko njiani enda huko (kuukata mti) akamuuliza Je waenda
wapi? Akamjibu naenda kuukata ule mti (unaoabudiwa) pasi na Allah Subhanahu
Wataala. Basi yule Iblisi akampa nasaha asifanye hivyo akamwambia sio wewe
unaouabudu huo mti. Lakini hakuikubali nasaha yake na mwishowe ikafikia hiyo
hali kuwa wapigane mieleka ikasalia yule mja kumshinda Iblisi. Akasema Iblisi
Je nikuoneshe kitu kitakachokufaa zaidi kuliko kukata huo mti mimi nakupa ahadi
kuwa kila siku utapata dinari mbili chini ya mto wako kila asubuhi, wewe
masikini zitumie dirham mbili hizo kwa watoto wako, kuwapa sadaka ndugu zako
(Waislamu wenzako) na kuwaliwaza mafakiri, nawe unajua fadhila gani iliyokuweko
katika kutoa sadaka. Ama kuukata huo mti haitakupatia thawabu yoyote na pengine
hao wanaouabudu wapande badala yake mti mwengine au pengine wakugomee (kuukata)
na wakudhuru kwa hiyo utajitia kwa mkono wako katika hilaki. Yule mja
yakamwingia na akayakubali yale maneno. Akarudi asubuhi akazikuta zile dirham
mbili kama alivyomuahidi yule Iblisi, akaongeza matumizi yake na miongoni mwake
akazitolea sadaka na siku ya pili ikiwa kama
siku ya kwanza. Ama siku ya tatu hakukuta kitu basi akaghadhibika na akachukua
shoka lake kwenda mtini akakutana na yule Iblisi kama mara ya kwanza na akataka
kumzuia hakukubali na mwishowe wakapigana mieleka na Iblisi akamshinda yule mja
na akampiga mhuri katika kifua chake na akasema (yule mja kumwambia Iblisi)
vipi hivi umenishinda mara hii? Iblisi
akasema nimekushinda mara hii kwa sababu umekuja mara hii umeghadhibika kwa
ajili ya zile dinari mbili na ama mara ya kwanza ilikuwa ghadhabu yako kwa
ajili ya Allah, basi akawa pamoja na wewe kwani yule aliyekuwa Allah yu pamoja
naye hashindwi na kitu. Na kisa hichi kinaayidiwa na kauli ya Allah Subhanahu
Wataala :
ﭽ ﮏ ﮐ
ﮑ ﮒ ﭼ الحجر:
٤٠
“Isipokuwa wale waja wako katika wao waliosafika kweli kweli”
Kwani hawezi kushindwa yule aliyeisafisha amali (kitendo) yake kwa ajili
ya Allah.
Baadhi yao
wamesema kufanya ikhlasi muda wa saa moja tu ni kuokoka kwa milele. Na
yasemekana elimu ni mbegu na vitendo ni vipando (vinavyopandwa) na maji yake ni
ikhlasi. Na wamesema wataalamu kwa yule anaefanya amali ajikurubisha kwayo kwa
Allah lakini ndani yake kuna uchafu (wa kutaka radhi ya mwingine pasi na Allah)
kuwa kitendo hicho hakina ikhlasi kwa Allah na wamepigia mfano kitendo hicho
kama mtu aliefunga kutaka kujikurubisha kwa Allah lakini pamoja na hivyo kataka
kupunguza chakula kwa kupata siha nzuri (anafanya “diet”). Na vile vile mfano
mwingine kama mtu asali kwa kujikurubisha kwa Allah Subhanahu Wataala (Sala ya
usiku) kwa sababu amekosa usingizi au alinda bidhaa au alinda masahibu wake na
haya ni mambo madogo kabisa ambayo huyafikirii kuwa yanaweza kuharibu ikhlasi
je vipi yule anaetoa sadaka ili amridhishe yule anaempa hiyo sadaka na
mengineyo kama hayo? Kwa hivyo kwa ujumla anaefanya kwa ajili ya Allah Subhanahu
Wataala na kwa jili ya maslaha ya nafsi yake hapo inatoweka ikhlasi yake na
kuchafuka usafi wa kitendo chake. Na bila ya shaka ametokana na ujumla huu yule
aliyelala, kwa mfano, ili apate nguvu ya kusimama kusali Sala za usiku kwani
huyu ijapokuwa yeye anapata katika huku kulala faida ya haraka (ihusikayo na
Dunia) isipokuwa yeye makusudio yake ni kupata hadhi ya Akhera (faida ya Akhera
yaani Al-Jannah na radhi ya Allah). Kwa hiyo imesemwa kuwa kulala kwa aliye
funga ni ibada na vile vile kula kwa niya ya kupata nguvu ya kumuabudu Allah Subhanahu
Wataala ni ibada na kama hivyo kwenda mtu na mkewe kwa niya ya kujizuiya
kutazama (mume kutazama wanawake wa nje na mke kutazama wanaume wa nje) na
kuvunja matamanio na kwa kutaka kupata mtoto kitendo hichi ndani yake kuna
faida ya haraka ya Duniani lakini niya imekibadilisha kupata mafanikio ya Dunia
na Akhera. Inawezekana mtu kufanya mambo akaamini kuwa amali hiyo ni safi kwa
(ina ikhlasi) ajili ya kupata radhi ya Allah Subhanahu Wataala kumbe ndani yake
yameingia mambo madogo (yanayo haribu hiyo ikhlasi) na hatanabahi nayo hayo na
kujiepusha nayo isipokuwa aliepata tawfiiq katika Dini yake na mwenye kuifanyia
hesabu nafsi yake na hakika tawfiiq iko katika mikono ya Allah Subhanahu
Wataala:
ﭽ ﮧ ﮨ
ﮩ ﮪ ﭼ التغابن:
١٦
“Mcheni Allah muwezavyo (mwisho wa jitihada yenu).”
Na hii Aya iliyoko katika kitabu cha Allah inampa mtu moyo kuwa afanye
kadiri ya uwezo wake (mwisho wajitihada yake) na baada ya hapo Allah hamkalifu
kiumbe wake zaidi ya uwezo wake. Naye ni Mwingi wa Rehema na Maghufira.
Anasema Imam Al-Ghazaliy:- Viumbe waliokuwa na khatari kubwa zaidi
kusibiwa na fitina hii (ya kuchafuka ikhlasi yao) ni wataalamu kwa sababu lengo
la wengi wao la kueneza elimu ni kutaka aonekane hakuna kama yeye katika elimu
na kufurahika kwa kufuatwa na watu (wafuasi) na kutaka ashukuriwe na asifiwe na
Iblisi awapambia hayo na kuwaambia kuwa lengo lenu ni kutaka kueneza Dini ya
Allah na kuitetea sharia ya Dini aliokuja nayo Mtume Salallahu Alayhi Wasalam.
Utamuona mtoaji mauidha (nasaha na kumbusho) anamsumbulia Allah Subhanahu
Wataala kwa kukumbusha kwake watu na kunasihi kwake wafalme na afurahika kwa
watu kukubali kauli yake na kumkusanyikia kwa wingi katika muhadhara wake
lakini ajidai kuwa furaha yake hiyo ni kwa urahisisho alioupata wa kunusuru
Dini ya Allah Subhanahu Wataala lakini husikitika na hapendezewi akimuona
katika jamaa yake aliye hodari zaidi kuliko yeye kwa mauidha na kuwa watu
waondoka kwake kumuendea yeye na lau kwamba nia yake ni nzuri ya kueneza Dini
ya Allah angelishukuru kuwa Allah Subhanahu Wataala amempunguzia uzito huu kwa
kumpa mwengine aufanye badala yake. Basi huyo shetani hamwachi na huzidi
kumshawishi kuwa wewe kusikitika kwako ni kwa kukukatikia thawabu sio kwa
kukuondokea watu kwani lau kwamba wangenufaika na ukumbusho wako ungepata wewe
thawabu kwa hiyo kusikitika kwako huku kwa jili ya kukosa thawabu kuzuri basi
sijui kama angesikitika Omar RA kwa kuwa Abu Bakkar RA amemtangulia kwa Uimamu
na ukhalifa ingekuwa kusikitika kwake kuzuri au kubaya bila shaka mwenye Dini
yake hawachi kun’gamua kuwa kusikitika kwake kungekuwa kubaya. Na huenda mtu
akakhadaika na udanganyifu wa shaitani na kujisemesha nafsi yake kuwa angetokea
alie bora kuliko yeye kwa jambo hili angelifurahi lakini akitokea mtu huyo
hubadilika na kurejea kutokana na fikira yake hiyo. Hayatambui haya isipokuwa
mjuzi wa vitimbi vya shetani na nafsi na amejishughulisha navyo muda mrefu.(Mwisho
wa kunukuu)
Ukweli:
Ukweli ni wajibu nao ni kinyume ya uwongo. Uwongo mwenye kuwa nao
achukiwa na alaaniwa. Basi ukiwa uwongo katika hali kama
hiyo bila shaka ukweli (uliokuwa kinyume ya uwongo) ni tabia yenye kusifika na
kupendwa. Na Mtume Salallahu Alayhi Wasalam amewasifu sana wakweli (wanaume kwa wanawake) na
anaejizowesha ukweli hubadilika akapata cheo cha Siddiq. Na Allah Subhanahu
Wataala Amewachagulia cheo hichi wengi katika Mitume wake na Abu Bakkar Siddiq
RA ameitwa Siddiq kwa sababu ya wingi wa ukweli wake na kumwaamini kwake Mtume
Salallahu Alayhi Wasalam bila ya hata ya kumsikia mwenyewe Mtume Salallahu
Alayhi Wasalam anazungumzia habari hiyo ya Israa na Miraji wakati aliporejea
Mtume Salallahu Alayhi Wasalam kutoka Beit Al-Maqdis na akawaambia Maqureish
nao hawakumsadiki wakasema haiwezekani mtu kutoka Makka kwenda Shaam katika
usiku mmoja na juu ya kuwa kawaletea dalili zinazothibitisha ukweli wake lakini
bado hawakumsadiki. Hapo ndipo walipotoka baadhi yao kwenda kwa Abu Bakkar kama
kumkebehi wakamwambia umesikia maneno anayoyasema sahibu yako, niya yao
wampoteze, amesema hivi, hivi, akawajibu Abu Bakar إن كان قال فقد صدق
yaani “Ikiwa kasema maneno hayo basi amesema kweli” na hapo ndipo
alipoitwa Siddiq na Allah Subhanahu Wataala kwa njia ya Jibriil AS, alipoulizwa
vipi umemsadiki akajibu mimi namsadiki katika habari ya mbingu (inayotoka
mbinguni) na mbingu iko wapi kutokana na sisi basi vipi nisimsadiki katika
habari ya ardhi tuliyo sisi tumo ndani yake au maneno aliyoyasema (Siddiq RA)
yako katika maana hii.
Amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :- “Hakika ukweli unaongoza
kwenye mambo mema (ya kumtii Allah Subhanahu Wataala) na mambo mema yanaongoza
kwenye Al-Jannah. Na hakika mtu anasema ukweli mpaka anaandikwa kwa Allah Subhanahu
Wataala “Siddiq” na hakika uwongo unapeleka kwenye mambo maovu (maasi) na mambo
maovu yapeleka Motoni na hakika mtu anasema uwongo mpaka huandikwa kwa Allah
kuwa muongo. Ameitoa hadithi hii Ibn Masoud. Inatosha kujua kuwa ukweli una
fadhila kubwa kuwa neno la “Siddiq” limetolewa kutokana na “Sidq” ukweli.
Amesema Ibn Abbas:- Mwenye kuwa na mambo manne amefaidika:- Ukweli, haya, tabia
njema na shukrani na wamesema baadhi ya wanavyuoni:- Wamekubaliana wataalamu
kuwa mambo matatu akiwa nayo mtu basi humuokoa sharti yote yajumuike: Uislamu
safi usiokuwa na bidaa wala matamanio (ya nafsi) na ikhlasi katika vitendo kwa
Allah Subhanahu Wataala na riziki halali kwa ajili ya Allah (chakula halali).
Haijuzu kudanganya kwa hali yoyote ile isipokuwa katika hali tatu ambazo
wanavyuoni wameruhusu kudanganya ndani yake nazo:
Katika kupatanisha watu wawili unaweza ukasema kitu kisichokuwa kweli
kwa ajili ya kulainisha nyoyo za hao unaowapatanisha.
Akiwa mtu ana wake wawili anaweza akamwambia mmoja wao maneno yasiyokuwa
na asili ya ukweli ili kumridhisha sharti yasilete madhara katika mali
au nafsi.
Kuwahadaa maadui wa Dini wakati wa vita na kuna kauli ambayo inatia
nguvu maneno haya:
(
إن في المعاريض لمندوحة عن الكذب )
“Katika kusema neno ambalo halifunui uwazi wa jambo kunatoa
ukumbi wa kuepukana na uwongo”
Na hali kama hii inatokea mara nyingi na inamuepusha mtu kusema uwongo kama vile akilazimika kufanya “taqiya” (kumwambia Mfalme dhalimu neno ambalo dhahiri
yake litamsalimisha na ujabari wake lakini undani wake lina maana nyengine) au
kukataa kufanya jambo jema ambalo hana uwezo wa kulifanya au mfano huo.
Inasemekana kuwa kuna mtu aliitwa na mfalme Jabbar wakati yuko nyumbani
kwake (huyo mtu) akamwambia mkewe achore mstari katika ardhi kisha aweke vidole
vyake juu yake halafu amwambie hayupo hapa yule Jabbari akafikiri kuwa hayuko
nyumbani kumbe yeye kamaanisha kuwa hayupo katika ule msitari. Akasalimika nae.
Alikuwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam akitaka kwenda vitani avistiri
(hivo vita) kwa kusema neno lenye maana nyingine hata akisikia mtu hilo neno han’gamui kuwa
Mtume Salallahu Alayhi Wasalam anakwenda vitani. Imetolewa kutokana na Mtume
Salallahu Alayhi Wasalam kuwa wakati fulani bibi mmoja mzee alimtaka amuombee
kwa Allah Subhanahu Wataala amtie Peponi akamjibu:
(
العجائز لا يدخلن الجنة )
“Wanawake wazee hawaingii Peponi”
Basi hapo akalia (kumuona hivyo akamuonea huruma) na akamwambia kuwa
maana yake mwanamke mzee atarudishwa kuwa kijana akiingia Peponi.
Qur’ani imewasifu wale watu wenye ukweli na Allah na wenye ukweli na
watu:
ﭽ
ﭑ ﭒ
ﭓ ﭔ ﭕ
ﭖ ﭗ ﭘﭙ
ﭚ ﭛ ﭜ
ﭝ ﭞ ﭟ
ﭠﭡ ﭢ ﭣ
ﭤ ﭼ الأحزاب: ٢٣
“Wapo watu miongoni mwa walioamini waliotimiza waliyoahidiana na
Allah. Baadhi yao wamekwisha maliza umri wao
(wamekwisha kufa) na baadhi yao wanangoja (siku yao kufika), wala hawakubadilisha (ahadi yao) hata kidogo”.
Basi hii ndio shahada sahihi ambayo anatakiwa Muumini aitegemee, sio
shahada za Kidunia ambazo wanazipata watu baada ya masomo (k.m. BA, PHD n.k).
Basi anaeipata shahada hii na akairidhia huyo ndie aliyefuzu hakika. Na sio
kuwa shahada hii ni hasa kwa wale masahaba ambao Aya hiyo hapo juu imeteremshwa
kwa ajili yao bali imewakusanya wao na wengineo walio wakweli na Allah na
wakapigana jihadi na adui yake na kumuabudu kwa ikhlasi na wako wapi mfano wa hawa
leo wakati hima za watu zimekuwa dhaifu na nafsi zimetosheka na kuhadaika na
raha ya Dunia na zimesahau raha ya milele (Peponi) walioekewa na Allah wale
wanaopigana jihadi katika njia yake na wanaotoa nasiha kwa Dini yake na
wakaipendelea Akhera zaidi ya Dunia na wakaogopa kikao cha Allah (siku
wataokutana na Allah) katika siri yao na dhahiri na wakiwa peke yao au pamoja
na watu. Ikiwa siri ya muumini na dhahiri yake imekuwa sawa sawa huwa na nguvu
katika makao mawili ya Dunia na Akhera na awajibika kusifiwa, lakini uwazi wake
ukienda kinyume na undani wake basi hapati malipo yoyote (mazuri) kwa
anayoyatenda isipokuwa tabu. Amesema mtu katika watu wema:- Ikiwa undani wa
muumini unawafikiana na uwazi wake Allah Subhanahu Wataala Amsifu kwa Malaika
wake.
Kufanya kazi kwa ajili ya kupata maisha ni wajibu na haifai mtu kuwa
mzigo kwa mwenzake yaani amtegemee mwenzake kwa maisha yake na Allah Subhanahu
Wataala Muumbaji wa viumbe na Mgawaji wa riziki ameijaalia Dunia nyumba ya kufanya
kazi na Akhera nyumba ya malipo mazuri na mabaya. Kwa hiyo kila anaetafuta
maisha yake kwa njia ya halali anapewa mafanikio katika Dunia na apewa thawabu
(pepo) Akhera na anaetafuta maisha yake kwa njia haramu apata hasara katika
Dunia na Akhera. Mtume Salallahu Alayhi Wasalam amesema :-
“Anaekusanya mali
katika njia ya unyan’ganyi na kuiba, Allah Subhanahu Wataala, ampeleka kwenye
hilaki na kuingia Jahannam”. Allah atuepushe nayo. Kutafuta maisha ni njia
inayopeleka kwenye malipo mazuri na uvivu na kutegemea wengine sio katika sifa
za Muumin.
Amesema Noor Ddiin Assalmy (rehema za Allah ziwe juu yake) Nampenda mtu
mwenye azimio la nguvu (katika moyo wake na kutaka kufanya kazi) anaefanyia
Dunia na Akhera kwa bidii kubwa, amma mwenye kupenda usingizi (kulala) huyo
hakaribishwi.
Na uzuri ulioje wa mali
halali unaompeleka sahibu yake Peponi. Na kitu gani kizuri zaidi kama Dini na Dunia vikikutana! na ubaya ulioje ukafiri na
kufilisika ukikutana katika binaadamu!
Allah Subhanahu Wataala ameamrisha kutafuta kipato katika kitabu chake
kitukufu:-
ﭽ ﭫ ﭬ
ﭭ ﭮ ﭯ
ﭰ ﭱ ﭼ الجمعة:
١٠
“Tawanyikeni katika ardhi mtafute fadhila za Allah.”
Na amesema:-
ﭽ ﭺ ﭻ
ﭼ ﭽ ﭾ
ﭿ ﮀ ﮁ ﭼ المزمل:
٢٠
“Na wengine wanasafiri katika ardhi wakitafuta fadhila za
Allah”.
ﭽ ﭳ ﭴ
ﭵ ﭶ ﭷ
ﭸ ﭹ ﭺ ﭼ البقرة:
١٩٨
“Si vibaya kwenu kuitafuta fadhila za Mola wenu (kwa kufanya
biashara njiani mnapokwenda kuhiji).”
Na amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-
( من الذنوب ذنوب لا يكفرها
إلا الهم
في طلب المعيشة )
“Yako madhambi ambayo hakuna kinachoyafuta
isipokuwa wasiwasi wa kutafuta maisha.”
Na amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-
( التاجر الصدوق يحشر يوم
القيامة مع
الصديقين والشهداء )
“Mfanya biashara mkweli atafufuliwa siku ya
Kiyama pamoja na Masidiqiin na Mashahidi (waliokufa katika njia ya Allah).”
Na amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-
( من طلب الدنيا حلالا وتعففاً عن المسألة وسعيا
على عياله وتعطفاً على جاره لقي الله ووجهه كالقمر ليلة
البدر )
“Mwenye kutaka Dunia kwa kutafuta riziki ya halali na
kuepukana na kuomba (watu msaada wa maisha) na kuwatoshelezea mahitaji ya
watoto wake na kumhurumia jirani yake akutana na Allah na uso wake kama mwezi
usiku wa mbaa mwezi”.
Siku moja alikuwa Mtume Salallahu Alayhi
Wasalam amekaa na masahaba zake wakamuona kijana anasulubu na nguvu na ametoka
mapema atafuta riziki wakasema, ole wake huyu, kama
ungekuwa ujana wake na usulubu wake katika njia ya Allah. Akasema Mtume
Salallahu Alayhi Wasalam :-
( لا تقولوا هذا فإنه إن كان يسعى على نفسه ليكفيها
عن المسألة
ويغنيها عن الناس فهو في سبيل الله وإن كان يسعى على أبوين
ضعيفين أو ذرية ضعاف ليغنيهم ويكفيهم فهو في سبيل الله وإن كان يسعى تفاخراً
متكاثراً فهو في سبيل الشيطان )
“Msiseme hivyo kwani ikiwa
katoka atafuta riziki ili aitosheleze (haja ya) nafsi yake kwa kujiepusha
kuomba na kuwategemea watu basi ni katika njia ya Allah. Na ikiwa katoka kwa
ajili ya wazee wake wawili dhaifu au watoto wake dhaifu ili awatosheleze haja
zao ni katika njia ya Allah. Na ikiwa atafuta riziki ili ajifakharishe na
azidishe mali
yake basi ni katika njia ya shaitani”. Ameitoa hadithi hii Attabariy.
Kadhalika amesema Mtume Salallahu Alayhi
Wasalam :-
( عليكم بالتجارة فإن فيها
تسعة أعشار الرزق )
“Ishikeni biashara kwani ndani yake kuna
sehemu tisa katika sehemu kumi za riziki”.
Na akasema Salallahu Alayhi Wasalam:-
( لأن يأخذ أحدكم حبله فيحتطب على ظهره خير
له من أن يأتي رجلا أعطاه الله من فضله فيسأله أعطاه أو منعه )
“Kuchukuwa mmoja wenu kamba
yake na kukusanya kuni na kujitwika juu ya mgongo wake ni bora kuliko kumuendea
mtu ambaye Allah kampa katika fadhila zake, ili amuombe basi amkubalie kumpa au
asimpe”.
Na akasema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-
( من فتح على نفسه باباً من
السؤال فتح الله عليه سبعين باباً من الفقر )
“Aliejifungulia nafsi yake mlango mmoja wa
kuomba Allah amfungulia milango sabini ya ufakiri”.
Na alisema Luqman mwenye hekima RA:-
( يا بني استعن بالكسب الحلال عن الفقر فإنه ما افتقر أحد قط إلا أصابه
ثلاث خصال رقة في دينه وضعف في عقله وذهاب مروءته وأعظم من هذه الثلاث استخفاف
الناس به )
“Ewe mwanangu jisaidie kwa
kipato cha halali uepukane na ufakiri kwani hafukariki mtu katu isipokuwa
hupatwa na mambo matatu:- ulaini katika Dini yake, udhaifu katika akili yake na
unaondoka utu wake (mambo yake mazuri ya kuonesha ubinaadamu wake) na juu ya
yote haya matatu kudharauliwa na watu”
Alisema Omar RA: Asikae mmoja wenu akawa
hatafuti riziki akasema “Ewe Mungu wangu
niruzuku, kwani mnajua kuwa mbingu hainyeshi dhahabu wala fedha”.
Wamesema baadhi ya wataalamu:-
“Kwa sisi
kufanya ibada sio kuinyoosha miguu yako (miwili katika Sala) na
kumuachia mwenzako kazi ya kukutafutia chakula lakini uanze kuutafuta mkate
wako ukishaupata fanya ibada”
Hadithi hizi zihishimikazo hazimaanishi kuwa
ujizamishe katika (kutafuta maisha ya) Dunia na ujichokeshe kufanya hivyo.
Sivyo hivyo lakini zamaanisha kuwa utafute maisha yako kiasi ya kujiepusha na
kuomba watu na bila ya kusahau wajibu wako unaokulazimikia kwa Mola wako,
lazima utanabahi sana
na kitu hichi. Ama kuuza na kununua kuna masharti yake, anaetaka kufanya kazi
hiyo juu yake arejee kwenye vitabu vya fiqhi kwani ndani yake atayapata
yatakayo muongoza na kumfundisha na kumuokoa na biashara za haramu hasa katika
wakati wetu huu wamejishughulisha watu kukusanya mali
kwa wingi bila ya kujali nini chanzo cha mali hayo. Haya mabenki
yaliyoondosha baraka na kuwaletea watu mambo mazito (adhabu) na yakawadanganya
watu kwa madai yake yaliyopambwa na wakawa watu wanayadhania ni mepesi (na
sivyo hivyo) na hayo mabenki yanyan’ganya zaidi kuliko yanavyotoa (hapa
Duniani) na huko Akhera adhabu yake ni zaidi. Allah Subhanahu Wataala ni Mjuzi
zaidi kitu gani yatakuletea mambo hayo, hesabu iliyo ndefu na adhabu iumizayo
huko Akhera. Akifikiria huyu aliechukua huo mkopo wa riba (interest ya Benki)
kuwa ataweza kulilipa hilo
deni, vipi ataweza kufanya hivyo? Na nani atakaemlipa kwani hiyo mali
imechanganyika yaani imewahusu watu chungumzima na inamsabibishia (huyo mtu aliechukua
huo mkopo) moyo wake kuwa na “rain” yaani kufunikwa na maasi na mtu kama huyu
hafaliwi tena mauidha Allah Subhanahu Wataala atuepushe na hali kama hiyo.
Enyi ndugu zangu biashara si kitu chepesi kama wanavyofikiria watu wengi. Hebu chukueni zingatio na
mfano kutokana na kisa kilichotolewa juu ya Imam Abdul Wahab Arrustumiy na
mtoto wake Aflah radhi za Allah ziwe juu yao.
Inasemekana kuwa Aflah amemuomba baba yake ruhusa kwenda kufanya biashara
akamwambia kwanza jifundishe fiqh ya biashara kisha niambie, basi alipoazimia
safari yake akaleta vipando vyake na akamwambia baba yake. Hapo baba yake
akamuuliza maswali mia tatu yanayohusu biashara na akamwambia ukinijibu
nitakupa ruhusa. Yasemekana kuwa Aflah alijibu maswali 297 katika 300 na
akasita katika maswali 3 kisha akayajibu. Hapo baba yake akamwambia bora
uakhirishe kwenda mwanangu usije ukatulisha haramu basi hebu pima hali yao hao na wafanya
biashara wa wakati wetu wa leo.
Tumekwisha taja katika jezuu ya tano ya kitabu hichi kitu kidogo
kinachohusu tabia njema. Ama katika jezuu hii tatuzungumzia kwa mapana zaidi
ili kuwahimiza vijana kukamata tabia njema na sira za watu wema zinazotakiwa
kufatwa ili kupata ridhaa ya Allah Subhanahu Wataala na tawfiiqi inatoka kwake
Mola Subhanahu Wataala. Amesema Mwenye zi Mungu Subhanahu Wataala kumwambia
Mtume wake Salallahu Alayhi Wasalam:-
ﭽ ﮛ ﮜ
ﮝ ﮞ ﭼ القلم: ٤
“Na bila shaka una tabia njema kabisa”
Amesema Assidiiqa(msema kweli) Aisha bint Assidiiq (msema kweli) Allah Subhanahu
Wataala awaridhie wakati alipoulizwa juu ya tabia ya Mtume Salallahu Alayhi
Wasalam akasema “Tabia yake ni Qur’ani” na alimuuliza mtu Mtume Salallahu
Alayhi Wasalam juu ya tabia njema akasema Salallahu Alayhi Wasalam kauli ya
Mola Subhanahu Wataala:-
ﭽ ﭵ ﭶ ﭷ
ﭸ ﭹ ﭺ ﭻ ﭼ الأعراف:
١٩٩
“Shikamana na kusamehe na amrisha mema na wapuuze masafihi”.
Kisha akasema:-
( هو أن
تصل من قطعك وتعطي من حرمك وتعفو عن من ظلمك )
“Nayo (hiyo tabia njema) ni
kumtembelea aliekukata(asiyekuzuru) na kumpa aliyekunyima na kumsamehe
aliyekudhulumu”.
Akasema:-
( بعثت متمماً لمكارم الأخلاق )
“Nimetumwa ili kukamilisha tabia njema”.
Akasema Salallahu Alayhi Wasalam:
( أثقل ما يوضع في الميزان يوم القيامة تقوى الله وحسن الخلق )
“Kilicho kizito zaidi
kinachoekwa juu ya mizani Siku ya Kiyama ni kumcha Allah na tabia njema”.
Alikuja mtu kwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam
mbele yake akamuuliza:- nini Dini? Akamjibu “tabia njema” akamjia kushotoni
kwake akamuuliza nini Dini? Akamjibu “tabia njema” kisha akamjia nyuma yake akamuuliza:
Ewe Mtume wa Mungu: nini Dini akamgeukia (na kumwambia) huelewi? Ni kuwa
usighadhibike. Akaulizwa ewe Mtume wa Allah ni nini الشؤم yaani “mkosi” (kinyume cha baraka) akajibu
Salallahu Alayhi Wasalam الخلق سوء yaani
“tabia mbaya”. Mtu mmoja kamwambia Mtume
Salallahu Alayhi Wasalam niusie akamjibu اتق الله حيثما كنت“Mche
Allah popote pale ulipo”. Akamwambia nizidishie akamwambia Salallahu Alayhi
Wasalam أتبع السيئة الحسنة تمحها “Fatilia ubaya kwa uzuri utafuta (ubaya)”.
Wasema wanavyuoni uzuri unaofuatia ubaya ni toba (utubie lile baya
ulilolifanya). Akamwambia yule mtu Mtume Salallahu Alayhi Wasalam niongeze
akamwambia:-
خالق الناس بخلق حسن “Kuwa na watu mwenye tabia njema”.
Aliambiwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam kuwa:-
Fulani (mwanamke) afunga mchana na asimama usiku (kusali) isipokuwa tabia yake
mbaya awaudhi majirani zake kwa ulimi wake akajibu لا خير فيها هي من أهل النار “Hana kheri naye ni katika watu wa Motoni”.
Akasema Salallahu Alayhi Wasalam:-
( سوء الخلق يفسد العمل كما يفسد الخل العسل )
“Tabia mbaya yaharibu
vitendo kama siki inavyoharibu asali”.
Kasema Wahab ibn Munabbih:- Mfano wa tabia
mbaya ni kama chombo cha udongo kilichovunjika
hakiwezi kuungika wala kukifinyanza tena mara nyingine. Amesema Ibn Abbaas RA:-
“Kila jengo lina msingi na msingi wa Uislamu tabia njema”. Kauli za wanavyuoni
katika tabia njema zimekithiri na mimi nasema kauli naomba iwe sawa:- “Tabia
njema imeelezwa katika kauli ya Mtume Salallahu Alayhi Wasalam:-
(المسلم
من سلم المسلمون من لسانه ويده)
“Muislamu ni yule aliewasalimisha Waislamu
na ulimi wake na mkono wake”.
Huenda mtu akawa mwenye tabia nzuri lakini
anaudhi kwa ulimi wake na huenda mtu mwenye tabia ya kutoa (kusaidia watu kwa
njia tofauti) lakini awasengenya watu. Na ndivyo hivyo ukamilifu kwa binadamu
tabu sana na
ukamilifu ni wa Allah Subhanahu Wataala Peke yake. Na wanasema wanavyuoni kuwa
msingi wa tabia njema ni mambo manne:-
Hekima
Ushujaa
Kujiepusha
na haramu
Uadilifu, na yaliyobakia ni matawi.
Na hakuna aliyekamilika katika mambo haya manne
isipokuwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam na watu wengine baada yake Salallahu
Alayhi Wasalam wametofautiana katika kukaribiana nae na kuwa mbali nae na
hapana shaka kuwa anaekaribiana nae Mtume Salallahu Alayhi Wasalam basi yeye ni karibu na ridha
ya Allah Subhanahu Wataala. Na Qur’ani tukufu imetoa ishara kuonesha tabia hizi
wanazosifika waumini.
Amesema Subhanahu Wataala:-
ﭽ
ﮬ ﮭ
ﮮ ﮯ ﮰ
ﮱ ﯓ ﯔ
ﯕ ﯖ ﯗ
ﯘ ﯙ ﯚ
ﯛﯜ ﯝ ﯞ
ﯟ ﭼ الحجرات:
١٥
“Wenye kuamini kweli kweli ni wale waliomuamini Allah na Mtume
wake; kisha wakawa si wenye shaka, na wakapigania Dini ya Allah kwa mali
zao na nafsi zao. Hao ndio wenye kuamini kweli kweli.”
Na hapana budi mtu kupigana jihadi na nafsi yake katika kujaribu kuitengeneza
tabia yake kwani haipatikani (tabia njema) isipokuwa kwa kujizoeza. Ama
walioumbwa nayo ni kidogo sana kama Manabii kwa
mfano na wengineo kidogo ambao Allah Subhanahu Wataala amewajaalia na tabia
njema katika maumbile yao.
Na kila Muislamu akijitahidi kufanya mambo ya taa (utiifu) aongezewa thawabu na
apewa na Allah tawfiiqi.
ﭽ
ﮠ ﮡ
ﮢ ﮣ ﮤﮥ
ﮦ ﮧ ﮨ
ﮩ ﭼ
العنكبوت: ٦٩
“Na wale wanaojitahidi kwa ajili yetu, kwa yakini Tunawaongoza
kwenye njia zetu. Na bila shaka Allah Yu pamoja na wafanyao mema”.
Tabia mbaya yasababishwa zaidi na ghadhabu na shahawa (matamanio ya
jimaa na kula chakula). Kwa hiyo Muislamu atakiwa ajichunge na mambo haya
mawili yasimtawale na ijapokuwa hayo ni katika maumbile ya mwanaadamu na
hayawezi yakaondoka kabisa na yakiondoka basi kutakuwa na uharibifu mkubwa, kwa
mfano ikiondoka shahawa ya chakula moja kwa moja itamsababisha mtu kuhilikika
kwa njaa, na kadhalika ikiondoka shahawa ya jimaa (kuingiliana mke na mume)
kitakatika kizazi, na ikitoweka ghadhabu hatoweza Muislamu kujitetea na
yanayomhiliki, kwa hiyo ataingia katika haramu kwani kujitetea mtu nafsi yake
na mali yake ni wajibu, lakini muradi unaotakiwa kuwa kila kitu kiwe cha kiasi
na wastani kama ilivyowasifu Qur’ani Masahaba waliopata radhi ya Allah kwa
kauli yake:-
ﭽ ﭗ ﭘ
ﭙ ﭚ ﭛ ﭼ الفتح:
٢٩
“Ni wenye nyoyo thabiti mbele ya makafiri na wenye kuhurumiana
wao kwa wao.”
Yaani wao wanaweka ukali katika mahala pake na wanaweka huruma katika
mahala pake. Na kila jambo likiwa wastani ndilo lapendeza na kusifiwa. Kwa mfano
ukarimu ni sifa iliyo katikati baina ya israfu na ubakhili, ushujaa ni sifa
iliyo baina ya uoga na kujitia mtu katika hatari bila ya dharura na kujali. Na
vile vile kujitenga na haramu ni sifa iliyo katikati baina ya kufanya kila kitu
(halali na haramu) na kujizuia kufanya lolote. Kuchanganyika na watu kuna
taathira kubwa kwa mtu kwani ikiwa kuchanganyika huko ni pamoja na watu wema
basi atapata kutoka kwao tabia nzuri. Ama ikiwa kuchanganyika huko ni pamoja na
watu waovu hapati kwao isipokuwa tabia mbaya. Wametoa mfano wa haya kama
anaekaa na muuzaji mafuta mazuri na anaekaa na mfua vyuma, wa kwanza akutia
harufu nzuri na wa pili akusibu na
macheche ya moto. Basi ajichagulie mwenye akili nani kati ya hawa ataka kukaa
nae. Na kawaida ya mambo kuwa tabia inaiba tabia nyingine (yaani watu wakikaa
pamoja tabia zao hulingana kwa njia ya mmoja kumwiga mwenzake) na kuna methali
ya Ki-Omani inayosema:- “Mfunge farasi pamoja na punda atachukua mlio na
mngurumo wake”. Mtume Salallahu Alayhi
Wasalam amemsifu Muumini kwa sifa nyingi na zote zimeashiria kuwa ni tabia
njema. Amesema:-
( المؤمن يحب لأخيه ما يحب لنفسه )
“Muumini ampendelea ndugu
yake kile anachojipendelea nafsi yake.”
Na amesema Salallahu Alayhi Wasalam:
( من كان يؤمن بالله واليوم الآخر فليكرم
ضيفه )
“Anaeamini Allah na siku ya
mwisho basi amkirimu mgeni wake”.
Na amesema Salallahu Alayhi Wasalam:-
( من كان يؤمن بالله واليوم الآخر فليقل
خيرا أو ليصمت )
“Anaeamini Allah na siku ya
mwisho basi aseme lililo na kheri au anyamaze”
Na amesema Salallahu Alayhi Wasalam:-
( أكمل المؤمنين إيمانا أحسنهم أخلاقا )
“Waumini waliokamilika mno Imani
zao ni wale walio na tabia njema zaidi”.
Na amesema Salallahu Alayhi Wasalam:-
( إذا رأيتم المؤمن صموتا وقورا فادنوا منه فإنه يلقن الحكمة )
“Mkimuona muumini mkimya,
mpole (upole wa kufikiri na kusubiri) muendeeni (ili mpate faida kwake) kwani
huyo anafahamishwa hekima”.
Na amesema Salallahu Alayhi Wasalam:-
( من سرته حسنته وساءته سيئته فهو مؤمن )
“Mwenye kufurahishwa na
vitendo vyake vizuri na kuhuzunishwa (kuona vibaya) na vitendo viovu basi huyo
ni muumini.”
Na amesema Salallahu Alayhi Wasalam:-
( لا يحل لمؤمن أن يشير إلى أخيه بنظرة تؤذيه
)
“Si halali kwa muumini
kumuashiria ndugu yake (muumini) mtazamo utakaomuudhi (asimtazame kwa macho
makali, kwa uadui)”.
Na amesema Salallahu Alayhi Wasalam:-
(لا يحل لمسلم أن يروع مسلماً )
“Si halali kwa Muislamu
amtishe Muislamu (mwenzake)”.
Na amesema Salallahu Alayhi Wasalam:-
( إنما يتجالس المتجالسان بأمانة الله عز وجل فلا يحل لأحدهما أن يغشى
على أخيه ما يكرهه )
“Hakika wakaa (kuzungumza)
wazungumzaji wawili kwa amana ya Allah Aliye na nguvu na kutukuka basi
haimuhalalikii mmoja wao kumtolea kitu mwenzake anachokichukia kutolewa”.
Na hadithi ziko nyingi sana katika hayo tumezitaja hapa baadhi yake
ili kuhimizana kusoma na kutafuta elimu zaidi. Ahnaf bin Qays aliambiwa
umejifundisha subira kutoka kwa nani? (ikiwa mtu amemkosea humsamehe hata ikiwa
ana uwezo wa kumlipiza). Akajibu kutoka
kwa Qays bin Aasim alikuwa siku moja azungumza na marafiki zake akaletewa mtoto
wake ameuliwa na mtoto wa ndugu yake amefungwa, akaambiwa huyu mtoto wa ndugu
yako kamuua mtoto wako, akasema: Wallahi hakuacha alichokuwa akikifanya wala
hakukata maneno yake. Kisha akamgeukia mtoto wa ndugu yake akamwambia kitu gani
kilichokufanya ewe mwanangu uukate mkono wako wa kulia kwa mkono wako wa
kushoto. Halafu akawambia watoto wake mfungueni pingu mtoto wa ami yenu na
mtayarisheni ndugu yenu (kwenda kumzika) na mpelekeeni mama yenu diya yake
kwani yeye sio katika kabila yetu. Mara moja aliugua akaona vibaya kwa sababu
watu hawakuja kumtembelea akauliza sababu yake akajibiwa kuwa watu wamuonea
haya kwa sababu ya madeni anaowadai basi hapo akaamrisha mtu apige mbio sokoni
kuwa yeyote anayedaiwa na Qays bin Aasim kasamehewa deni lake. Akasema alietowa
hadithi hii kuwa siku ya pili ilivunjika ngazi ya nyumba yake kwa wingi wa watu
waliokwenda kumtizama.
Malezi mema ya watoto yanawahusu zaidi wazee wawili kwani wao wana
sehemu kubwa ya kufanya katika kuwalea watoto wao. Na nadra kuona mtoto
amelelewa vizuri bila ya maangalizi ya wazee wake wawili na kumfuatilia katika
harakati zake na tulitangulia kusema kuwa ni wajibu wa baba kuchagua mwanamke
mwenye Dini na asili ili mtoto awe kama wazee wake wawili kama
ilivyosema hadithi tukufu ya Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-
( اختاروا لنطفكم فان العرق دساس )
“Chagueni kwa ajili ya
vizazi vyenu kwani mzizi wafukika”(asili ya mama na tabia yake inaendelea na
hujitokeza katika mtoto).
Moyo wa mtoto ni johari yenye thamani kubwa
hautakiwi uachwe bila ya kutiwa nakshi nao unakubali kila kinachonakishiwa juu
yake ukinakishiwa kitu kizuri juu yake nao unakuwa mzuri na ukinakishiwa kitu
kibaya nao unakuwa mbaya. Na wazee wawili washiriki katika ubaya au uzuri wa
mtoto na ni kitu cha ajabu sana
kuwa wazee wawili wamkinga mtoto wao na kila kinachomdhuru kwanini basi
hawamkingi na madhara makubwa kabisa nayo ni kuporomoka (kuhiliki) Duniani na
adhabu kubwa huko Akhera, ghafla gani hii waliyokuwa nayo wazee na asema:
وليس يضر القوم موت خيارهم ولكن يضر
القوم أن خدج النسل
Hawadhuriki watu kwa kufiwa na wabora wao
lakini hudhurika na kizazi kikiwa kasoro.
Msiba gani kwa mtu kumlea mtoto wake na
kumtaabikia akiwa mdogo na akiwa mkubwa ampoteza na kuwa pamoja na wapumbavu na
wahuni ambao huchukiwa na watu na kutizamwa mtizamo mbaya. Hasara gani hii kwa
wenye akili amma walio kuwa hawafikirii, nafsi zao zimekufa, hawajali usalama
wa nafsi zao vipi watajali usalama wa watoto wao. Basi inataka kwa mababa
wawashughulikie watoto wao kutoka wakati wa kunyonyeshwa mpaka wakati wa
kubaleghe. Akibaleghe na hali amefaliwa na ulezi basi hiyo ni fadhila kubwa
kutoka kwa Allah Subhanahu Wataala kwa wao wote. Na ikiwa haukumfaa ulezi na
baada ya kubaleghe anahiliki mtoto na hali hii ni nadra kutokea kwani uasi
(ubaya) huwa umemzidia huyo mtoto. Na hapa wazee wanakuwa hawana la kufanya
wala hawalaumiwi wala wasijin’gate kiganja kwa majuto ya kuharibu malezi ya
mtoto wao lakini hapana shaka anaewajibika kulaumiwa ni yule ambaye alipuuza
kumlea mtoto wake akaja akagutuka (kutaka kumlea mtoto) umekwisha pita wakati
wa kumlea na kumrudisha mtoto wake kutoka katika upotevu wake.
Wanawajibika wazee wawili kumtizama na
kumpeleleza katika kulala, kula, kuvaa na kusoma kwake na akirudi kutoka shule
wamuulize amesoma nini na wapi amekwenda, nani amesuhubiana nae njiani, amekula
nini, na nani amempa na kwanini amempa hata ajue kuwa nyuma yake kuna maswali
atakayoulizwa. Wasimwache ende kama mnyama azurure ovyo na wasiseme kuwa shule
inatosha kumuilimisha na kumfundisha adabu na kumtengeneza awe mtu mwema sio
hivyo bali shule sehemu yake ya kumlea mtoto ni ile wakati mtoto anapokuwa
asoma ndani yake akimaliza ni kazi ya wazee wawili na mara nyingi mtoto anaharibika
katika ule wakati anapokuwa baina shule na nyumbani ikiwa wazee hawampelelezi
harakati zake.
Kitu cha kwanza kinachodhirika katika ulezi wa
mtoto udogoni kwake ni haya, ukimuona mtoto aona haya wakati unapoonekana utupu
wake au kikifanyika kitu kibaya basi hiyo ni dalili ya kupambazuka kwa nuru ya
akili yake nayo ni bishara inayoonyesha kuwa mustakbali wake ni mzuri basi kama
huyu haifai kupuuzwa bali furusa hii ya wingi wa akili yake itumiwe na
afahamishwe vitendo vizuri avijue na vibaya kadhalika. Na aambiwe sira za watu
wema ili achukue mfano wao na watu wabaya ili ajiepushe nao, na kama hivi
isiachiwe fursa ipite bila ya kufaidika nayo, ahimizwe kuhifadhi Qur’ani na
hadithi za Mtume Salallahu Alayhi Wasalam na aqiida iliyo sahihi na mambo
waliyosema maimamu kuhusu hayo, hivyo wanakuwa wazee wake wawili ni washirika
wa thawabu wa vitendo vizuri atakavyovifanya na hata baada ya kufa kwao
zinaendelea thawabu hizo kuwafikilia kwa mujibu wa hadithi iliyosema:-
الدال على الخير كفاعله
“Anayeionyesha heri ni kama
anayeifanya”
Na vile vile
hadithi:-
كل عمل ابن آدم
ينقطع بعد موته إلا من ثلاث ولد يدعو له أو نهر أجراه أو مصحف وقفه
“Kila kitendo cha binadamu chakatika baada
ya kufakwake isipokuwa mambo matatu mtoto anaemuombea Dua, au mfereji (wa maji)
ameupitisha na msahafu ameuweka waqfu”.
Wasiwazoeshe watoto wao maisha ya raha na
yanayosahaulisha Akhera kwani hayo si katika alama za watu wema. Na wamhifadhi
asichanganyike na watu wa raha na michezo na vile vile ajitenge na mashairi
yanayotajwa ndani yake mapenzi na mambo ya utupu (matusi) na wote
wanayoshughulika na hayo kwa hoja kuwa huo ndio ujanja na tabia nzuri (kama
kumsema mtu fulani hafifu) na ukweli wa mambo hayo yapanda katika nyoyo za
watoto mbegu ya ufisadi. Basi ndio hivyo kila ikidhihirika kwa tabia njema
inapasa asifiwe na kukirimiwa hata ajue kuwa amefanya kheri na aendelee nayo na
upande mwingine asichukuliwe akifanya makosa na hasa kugombezwa mbele ya watu
au hata akiwa peke yake, ikiwa akirudia basi hapo anapasa kupewa nasiha akiwa
peke yake na ikiwa haikumfaa nasiha hapo atiwe adabu ili asijasiri kufanya
maovu.
Baba yangu aliniona siku moja nimekojoa bila ya
kujipangusa na jiwe “Istijmaar” (siku hizi makaratasi ya “tissues” yatumiwa
badala ya mawe halafu ndio “Istinjaa” yaani kujiosha kwa maji) na mimi umri
wangu miaka kumi akanipiga, vile vile kaniona siku nyingine nimepatwa na hamu
ya kula chakula kigeni kimeletwa akanipiga na akaninyima hicho chakula kwa
ajili ya hamu (uroho) iliyonishika kula hicho chakula na mimi umri wangu wakati
huo sijapindukia miaka sita basi zikabakia kumbukumbu hizi katika moyo wangu
kila kikija chakula au nikikidhi haja (kwenda chooni) yanijia hofu mpaka sasa
nami mtu mzima umri wangu umepindukia miaka sitini. Alikuwa baba yangu Allah
amjazi kheri hacheki na sisi wala hafanyi mzaha na sisi kwa kutahadhari tusije
tukajasiri kufanya kitu kibaya akitukataza kukifanya kwani tutakuwa hatumuogopi
tena kwa vile alivyokuwa katuzoesha kutufanyia mzaha. Mithali yasema:-
لا تري الصبي سنك فيريك إسته
“Usimuoneshe mtoto wako jino lako asije
naye akakuonesha utupu wake (ukimchezesha na kumlegezea mtoto wako hatokuogopa,
kila kitu kwa wastani).”
Maradhi manne yanayomuandama Muislamu ambayo
habandukani nayo ila kwa jitihada kubwa. Maradhi hayo nayo ni tumbo, utupu,
ulimi na jicho na kiongozi wa maradhi haya ni nafsi kwani yote hayo manne
yamsibu mtu kwa kuamrishwa na nafsi. Na kila makosa yanayofanywa na Muislamu
ukipeleleza utaona kuwa asli yake ni haya manne. Tumbo kwa mfano lamletea mtu
matamanio na unajua hatari ambayo inaletwa na matamanio kama
baba yetu Adam AS na mkewe Hawaa walivyokuwa katika Al-Janna Allah Subhanahu
Wataala aliwaruhusu kula kila kilichokuwa humo katika vinavyoliwa isipokuwa mti
mmoja kawakataza kula ndani yake. Yakawapelekea matamanio ya matumbo yao kutaka kula katika huo
mti waliokatazwa kuula kisha zikiwadhihirikia aibu zao wakatolewa nje ya
starehe za Pepo kwenda katika taabu ya Dunia. Ikiwa haya yamewatokea Adam AS na
Hawaa na daraja yao
waliokuwa nayo mbele ya Allah Subhanahu Wataala vipi basi wengineo. Tizameni
hatari ya matamanio licha ya kuwa wameruhusiwa miti yote katika Pepo isipokuwa
mti mmoja tu juu ya hivyo hawakuweza kujiepusha nao kwa matamanio mtu akiyaweka
mbele.
Na akishashiba mtu mambo mengi yasababishwa na
shibe kwani ni chanzo cha matamanio na mara nyingi amehimiza Mtume Salallahu
Alayhi Wasalam kupunguza kula kama katika
kauli yake:-
( الفكر نصف العبادة وقلة الطعام هي العبادة )
“Fikra ni nusu ya Ibada na kula kidogo
ndiyo Ibada”.
Imekuja habari kuwa Mtume Salallahu Alayhi
Wasalam alikuwa akaa na njaa kwa kutaka mwenyewe sio kwa kuwa hana chakula.
Amesema Salallahu Alayhi Wasalam:-
( لا تميتوا القلوب بكثرة الطعام والشراب فإن القلب كالزرع يموت إذا
كثر عليه الماء )
“Msiziuwe nyoyo zenu kwa
kula na kunywa sana kwani moyo kama
kipando kinakufa kikizidiwa na maji”.
Amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-
( ما ملأ ابن ادم وعاء شرا من بطنه حسب ابن
ادم لقيمات يقمن صلبه وإن كان لابد فاعلا
فثلث لطعامه وثلث لشرابه وثلث لنفسه)
“Hakujaza binaadamu chombo
cha shari zaidi kuliko tumbo lake, vyamtosha binaadamu vitonge (kiasi ya)
kumsimamisha mgongo wake na ikiwa hana budi kufanya (kula chakula) basi
theluthi iwe ya chakula chake na theluthi iwe ya kinywaji chake na theluthi iwe
ya pumzi yake”.
Imetolewa hadithi kuwa Aba Hujeifah alipiga
mbwewe katika majlisi ya Mtume Salallahu Alayhi Wasalam akamwambia punguza
kupiga mbwewe kwako kwani watu watakao kuwa na njaa zaidi Siku ya Kiyama wale
wanaoshiba zaidi Duniani. Isichukuliwe maana ya hadithi hizi moja kwa moja
ambazo daima zinakataza shibe iliyopindukia kiasi inayomzuia mtu kufanya wajibu
wake lakini pengine shari ya kukaa na njaa ikawa zaidi kuliko kuwa na shibe, na
pengine njaa ikawa shari kuliko kuvimbiwa”. Inakuwa njaa iko karibu zaidi na
ukafiri kuliko shibe lakini shari yake (shibe) ni kuwa inasababisha matamanio
ambayo yamtoa Muislamu nje ya radhi ya Allah Subhanahu Wataala na kufanya
yaliyokatazwa kama tulivyotangulia kusema juu
ya kisa cha Nabii Adam AS. Inasemekana kuwa Nabii wa Allah Issa AS alikutana na
Ibliis mara moja akamwambia Je uliwahi hata mara moja kunipoteza? Akamjibu:
Ndio mara moja ulishiba na ikakusahaulisha shibe kumtaja (kumkumbuka) Allah Subhanahu
Wataala akasema Issa AS basi tokea leo sitashiba tena na akasema
Ibliis nami tokea leo simpi nasaha mtu yoyote.
Maradhi yanayohusika na
utupu:
Nao ni mfalme mwenye nguvu isipokuwa kwa yule
aliyewafikiwa akaimiliki nafsi yake. Na inasemekana kuwa ikisimama dhakari ya
mwanamme basi theluthi mbili ya akili yake haifanyi kazi na imetolewa kutokana
na Mtume Salallahu Alayhi Wasalam kuwa amesema:-
( النساء حبائل الشيطان ولولا هذه الشهوة لما
كان للنساء سلطة على الرجال )
“Wanawake ni kamba za
sheitani (zinazofungiwa watu kuwavuta kwa sheitani yaani kuwapoteza) na lau kama sio kwa haya matamanio basi mwanamke asingekuwa na
uwezo juu ya mwanamme”.
Wamesema baadhi ya watu kuwa sheitani humwambia
mwanamke wewe ni nusu wa askari wangu na wewe ndiwe mshare wangu ambao
nikiurusha sikosei (kuwapata watu ili kuwapotosha) na wewe ndiwe mahala pa siri
yangu na wewe ni mjumbe katika haja yangu kwani nusu ya askari wake ni matamanio
na nusu ya pili ni ghadhabu.
Amesema Al-Ghazaliy: Na makubwa ya matamanio ni
matamanio ya wanawake na matamanio haya yana kupindukia mpaka, yaliyopungua sana yakawa yametoweka na
yaliyokuwa katikati yaani yako wastani. Yaliyopindukia mpaka hayo yatawala
akili mpaka yakasababisha hima ya mwanamme iwe katika kustarehe na wanawake na
huyu anakuwa mbali na njia ya Akhera au (hayo matamanio) yatawala Dini mpaka
yakapelekea kufanya madhambi makubwa na
yaliyopunguwa humfanya mwanamme asitake wanawake au kuwa dhaifu katika
kustarehe. Nao aina zote mbili hizi za matamanio zina makosa na hazitakiwi amma
iliyokuwa yatakiwa ni kuwa matamanio yako wastani na kuwa yanafuata amri ya
akili na sheria katika kuzuia kwake na kutoa kwake na yakizidi kutaka
kupindukia mpaka basi huvunjwa kwa njaa na kwa kuoa.
Amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-
( معاشر الشباب عليكم بالباءة فمن لم يستطع فعليه بالصوم فالصوم له
وجاء )
“Enyi vijana jitahidini kuoa
na aliyekuwa hawezi basi afunge kwani
funga ni kinga ya matamanio kwake.”
Amesema Saeed bin Al-Musayyab:
Hakuvunjika moyo Ibliis na mtu (kwa kushindwa
kumpoteza) isipokuwa atamjia kwa upande wa wanawake na asema (haya) na yeye
umri wake wakati huo miaka themanini na nne na jicho lake moja limepoteza nuru
na la pili lakaribia kupoteza kuwa hakuna kitu kinachoniogopesha zaidi kuliko
wanawake na anaeweza kujimiliki nafsi yake katika hali ambayo anaweza kutimiza
matamanio yake basi huyo ni mtu kamili. Na mtu wa kwanza wa aina hii ni Yusuf
Assadiiq AS na kisa chake kimo ndani ya Qur’ani tukufu basi na kila anaefanya kama yeye huyo amejifundisha kutoka kwake. Amesema Mtume
Salallahu Alayhi Wasalam :-
( من عشق فعف فكتم فمات مات شهيدا )
“Aliyependa kisha akajizuia
(kuzini) halafu akaficha (asimwambie mtu siri hiyo) akafa basi amekufa
shahidi”.
Amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-
“Watu saba Allah Subhanahu Wataala Awafunika
katika kivuli chake akawahisabu na miongoni mwao mtu ameitwa na mwanamke mwenye
sura nzuri ili azini nae akasema mimi namuogopa Allah Subhanahu Wataala Mola wa
walimwengu”. Na hii daraja kubwa haiwafikii isipokuwa wanaume waliokamilika
inawezekana akatokea mwanamme kujizuia kuzini na mwanamke kwa sababu hana nguvu
ya uume au kwa kumuonea haya mtu fulani au mengineo yanayomzuia sio mtu kama huyu
aliokusudiwa na hadithi zilizotajwa hapo juu lakini aliekusudiwa ni yule
mwanamme aliyesabiliwa kila uwezekano wa kuzini akajikataza nafsi yake kwa hofu
ya Allah Subhanahu Wataala huyu ndiye mwanamme aliyekamili.
Kudhulumu ni katika mambo yanayopendwa na nafsi
na ukimpata anaeweza kujizuia na zinaa basi huyo hadhulumu. Sababu ziko nyingi
amma sababu ya kumcha Mungu ndio sababu inayoshukuriwa.
Matamanio ya Ulimi
Ulimi ni neema kubwa katika neema nyingi za
Allah Subhanahu Wataala na licha ya udogo wake kimwili haubainiki ukafiri
kutokana na Imani ila kwa ulimi na uongofu wa waja haupatikani na kulingania
Dini ya Allah Subhanahu Wataala isipokuwa kwa ulimi na uwanja wake ni mkubwa
sana hauna mipaka sio kama viungo vingine kwani manufaa yake yana mipaka.
Inataka kutumiwa neema hii ili kufikia radhi za
Mola Subhanahu Wataala kwani kama Angelitaka angekujaalia bubu kama mnyama basi Je inapendeza kwa aliye huru kurudisha
ubaya kwa uzuri (wema) kwa hiyo amche Allah Subhanahu Wataala juu ya kile
alichomruzuku asikitumie katika kutekeleza matamanio yake. Ulimi una matamanio
mengi yanayomtia sahibu wake Motoni kama alivyosema Mtume Salallahu Alayhi
Wasalam :-
( و هل يكب
الناس على وجوههم أو قال على خياشيمهم إلا حصائد ألسنتهم )
“Je yawamwaga watu Motoni
kuangukia nyuso zao au amesema kuangukia pua zao isipokuwa mavuno ya ndimi zao.”
Yafuatayo ni maradhi ya ulimi yanayosababishwa
na matamanio yake:-
Kusema zaidi ya haja.
Kujifanya bingwa wa kuzungumza hasa wale
watoaji hotuba na wale wenye fasaha na wepesi wa kutoa maneno.
Kuzungumzia yalio batili (kinyume ya haki).
Kujadiliana katika kununua.
Kufanyiana khusuma.
Kusema kwa kuyatolea maneno kooni.
Maneno machafu, matusi, ulimi mrefu
(unaochukiza).
Kulani mnyama au kilichokuwa hakina roho au
binadamu.
Kuimba na kutoa mashairi yaliyo haramu.
Mzaha.
Kejeli na stihizai.
Kutoa siri za watu.
Kuvunja ahadi.
Kusema uongo.
Kuapa kwa kitu batili.
Nyuso mbili – kuwa na huyu kwa uso na mwingine
kwa uso tofauti.
Kusifiana.
Kuwauliza watu wa kawaida (wasiokuwa na elimu)
juu ya sifa za Allah Subhanahu Wataala.
Kusengenya.
Kufitinisha.
Haya maradhi ishirini ni baadhi tu ya mengi
yaliyokuwa hayakutajwa na yote katika madhambi makubwa na kusengenya na
kufitinisha ni yaliyo mabaya zaidi katika hayo na wanavyuoni wamepima kwa haya
madhambi mawili makubwa kuwa madhambi yote mengine yanayovunja udhu na Saumu
vile vile katika makubwa kwa hadithi iliyokuja ya Mtume Salallahu Alayhi
Wasalam:-
( الغيبة والنميمة ينقضان الوضوء ويفطران الصائم
)
“Kusengenya na kuchonganisha
(kufitinisha au usabasi) kwavunja udhu na kwamfungulisha aliefunga”.
Kwa hiyo baadhi ya wanavyuoni wamesema kuwa
madhambi makubwa yote yatengua udhu na yafungulisha aliefunga kwa kuchukulia
kipimo cha madhambi haya mawili na wengine wamesema kuwa yanayovunja Saumu na
udhu ni haya haya mawili tu kama ilivyosema
hadithi. Kwa hiyo sheria imehimiza na kutilia mkazo kunyamaza kwa kutahadhari
na maafa yanayoletwa na ulimi. Mtume Salallahu Alayhi Wasalam amesema:- من صمت نجا
“Mwenye kunyamaza aokoka” na amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam
:- الصمت حكم وقليل فاعله “Kunyamaza ni hekima na watu kidogo wafanyao
hivyo” na mmoja katika masahaba alimwambia Mtume Salallahu Alayhi Wasalam
:- Nijulishe kitu katika Uislamu ambacho
sitahitajia kumuuliza juu yake mtu yeyote mwingine baada yako akamwambia
Salallahu Alayhi Wasalam:-
( قل آمنت
بالله ثم استقم )
“Sema nimemwamini Allah kisha nenda mwendo
mzuri”.
Nikasema (yaani anaendelea huyo sahaba
kumuuliza Salallahu Alayhi Wasalam) nijiepushe na kitu gani? Akafanya Mtume
Salallahu Alayhi Wasalam ishara kwa mkono wake kuonyesha ulimi wake. Na akasema
Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-
( و من يتكفل لي بما بين
لحييه ورجليه أتكفل له بالجنة )
“Mwenye kunipa dhamana ya
kilicho baina ya taya zake mbili (ulimi) na baina ya miguu yake miwili (utupu
wake) nampa
dhamana ya kupata Pepo.”
Na amesema Salallahu Alayhi Wasalam:-
(من وقي شر
قبقبه وذبذبه ولقلقه فقد وقي الشر كله )
“Anayeepushwa na shari ya
tumbo lake na utupu wake na ulimi wake basi
ameepushwa na shari yote.”
Na shari hizi tatu ndizo zinazowahilikisha watu
wengi, twamuomba Allah Subhanahu Wataala atuepushe nazo Amin.
Amesema Anas bin Malik RA amesema Mtume
Salallahu Alayhi Wasalam:-
لا يستقيم إيمان
العبد حتى يستقيم قلبه ولا يستقيم قلبه حتى يستقيم لسانه ولا يدخل رجل الجنة لا
يأمن جاره بوائقه )
“Haiwi nzuri imani ya mja
mpaka moyo wake uwe mzuri na hauwi mzuri moyo wake mpaka unyooke ulimi wake na
haingii Al-Janna mtu ambaye hamuepushii jirani yake kero lake(maudhi yake).”
Hadithi iliyotolewa na Saeed bin Jubeir
kutokana na Mtume Salallahu Alayhi Wasalam kasema:-
( إذا أصبح
ابن آدم أصبحت الأعضاء كلها تذكر اللسان تقول : اتق الله فينا فإنك إن استقمت
استقمنا وإن اعوججت اعوججنا )
“Akiamka
binaadamu viungo vyote vyaukumbusha ulimi vikauambia:- Mche Allah juu yetu
kwani ukenda mwendo mzuri nasi tutakuwa na mwendo mzuri (tutanyooka) na ukenda
mwendo mbaya nasi tutakwenda mwendo mbaya (tutapotea).”
Amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam:
(ألا أخبركم بأيسر العبادة وأهونها
على البدن الصمت وحسن الخلق )
“Je
niwaambieni ibada iliyokuwa nyepesi zaidi juu ya mwili: kukaa kimya na tabia
njema.”
Nabii Suleiman bin Dawood AS amesema:-
Ikiwa kuzungumza ni fedha basi kunyamaza ni
dhahabu.
Nabii Eessa AS amesema:-
Ibada ni sehemu kumi, tisa miongoni mwa hizo ni
katika kunyamaza na sehemu moja katika kuwakimbia watu (kuepukana nao).
Ameandika Omar bin Abdul Aziz:- “Amma baada:
mwenye kukithirisha kukumbuka mauti anaridhika na kidogo Duniani na mwenye
kuyahisabu mazungumzo yake kuwa ni miongoni mwa vitendo vyake basi huyafupisha
mazungumzo yake isipokuwa (huzungumza) katika kile kinachomhusu”. Imetolewa na
Bilal bin Al-Haarith kuwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam amesema:-
( إن الرجل
ليتكلم بالكلمة من رضوان الله ما يظن أن تبلغ به ما بلغت فيكتب الله له بها رضوانه
إلى يوم القيامة وإن الرجل ليتكلم بالكلمة من سخط الله ما يظن أن تبلغ به ما بلغت
فيكتب الله عليه بها سخطه إلى يوم القيامة )
“Hakika mtu huenda akasema
neno katika yanayomridhisha Allah Subhanahu Wataala bila ya kufikiria kuwa
(neno hilo) limefika hapo lilipofika (daraja
kubwa).Basi Allah akamwandikia kwa hilo
neno Radhi yake mpaka Siku ya Kiyama. Na hakika mtu huenda akasema neno katika
(maneno) yanayomghadhibisha Allah Subhanahu Wataala bila ya kudhania kuwa (neno
hilo) limefika
hapo lilipofika (daraja ya chini). Basi Allah humwandikia kwa hilo neno ghadhabu yake mpaka Siku ya Kiyama.”
Yasemekana kuwa mtu fulani alimsifu mtu
mwingine mbele ya Mtume Salallahu Alayhi Wasalam basi akasema Salallahu Alayhi
Wasalam:-
( ويحك قطعت
عنق صاحبك لو سمعها ما أفلح ) ثم قال : ( إن كان أحدكم لا بد مادحا أخاه فليقل
أحسب فلانا ولا يزكي على الله أحداً حسيبه الله إن كان يرى أنه كذلك )
“Ole wako umeikata shingo ya
mwenzio kama angesikia (huko kumsifu kwako) basi asingefuzu” kisha akasema “Ikiwa mmoja
hana budi ila kumsifu ndugu yake aseme namfikiria hivyo fulani na siwezi mimi
kujua zaidi ya Allah Subhanahu Wataala kuwa mtu fulani mzuri, Allah ndiye
anayemjua ikiwa kweli kama nilivyomfikiria
mimi.”