Tuesday, 19 January 2016

Juzuu 5 Nguzo za Dini ya KiislamuKujenga-- Uongofu katika nyoyo za Vijana--



 

           ﭖﭗ  ﭘﭙ                                                                 ﭷﭸ            البقرة: ١ - ٥



"Alif Lam Mym (1) Hiki ni Kitabu, kisichokuwa na shaka ndani yake, ni uongozi kwa wamchao (Allah)  (2) Ambao huyaamini yasiyoonekana (maadam yamesemwa na Allah na Mtume wake) na kusimamisha Sala na hutoa katika yale tuliyowapa (3) Na ambao wanaamini yaliyoteremshwa kwako, na yaliyoteremshwa kabla yako na waamini (kuwa iko) Akhera  (4) Hao wako juu ya uongozi utokao kwa Mola wao na hao ndio wenye kuongoka (5)."



Uislamu ni kufuata kwa ukamilifu na kunyenyekea amri za Allah (Subhanahu Wataala) na sharia zake, kuamini Allah na Malaika wake na Vitabu vyake na Mitume wake na Siku ya Mwisho na Kadari, shari yake na heri yake, kuwa inatokana na Allah (Subhanahu Wataala).


Nao umejengwa kwa nguzo tano:

Shahada, Sala, Saumu, Zaka na Hija. Vile vile umekusanya utendaji, baina ya mja na Mola wake na haya yako chini ya kifungu cha Ibada mbali mbali kama mfano wa Sala, Zaka, Saumu n.k na utendaji baina ya mja na mwenzake (binaadamu mwenzake) na haya yako chini ya kifungu cha dharura za maisha.


Basi Allah (Subhanahu Wataala) ataka Waislamu maisha yao yote yawe kama ilivyokuja katika Dini ya Allah katika yanayohusu mambo ya ibada na mipango (nidhamu) inayomhusu mtu binafsi na inayowahusu jamii (watu baina yao wenyewe kwa wenyewe). Anasema Allah (Subhanahu Wataala):


                       ﯘﯙ             البقرة: ٢٠٨

“Enyi Mlioamini! Ingieni katika hukumu za Uislamu zote, wala msifuate nyayo za Shetani; yeye kwenu ni adui dhahiri”.


Na Aya za kitabu cha Allah (Subhanahu Wataala) na Sunna ya Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) zimeweka wazi kabisa njia inayowapasa Waislamu kufuata katika maisha haya ya Dunia.

Na nguzo za Dini zimesimama juu ya mambo matano wala hakuna cho chote (katika Dini) kinachoepukana na hayo (matano). Nayo:

1.Wajibu : Nao ni kila aliloamrisha Allah (Subhanahu Wataala) lifanywe katika yafuatayo:

Kumjua Allah na kumpwekesha

Kuamini Mitume yake yote na kwa namna mahsusi baina yao Mtume wetu Muhammad (Salallahu Alayhi Wasalam).

Kuamini Vitabu vyake vyote na kwa namna mahsusi baina yake kitabu chetu kitukufu ambacho ni Qur’an.

Kuamini Malaika wake wote na kwa namna mahsusi baina yao Malaika wanne nao: Jibril, Mikaaiil, Israfiil na Malaika wa mauti.

Kuamini Siku ya mwisho nayo ni siku ambayo watafufuliwa waliokufa kutoka makaburini na watapelekwa kukusanywa pale alipowataka Mola Subhanahu Wataala.

Basi mtiifu miongoni mwao ni yule aliyekuja hali ametekeleza ahadi ya Allah; huyo ataingizwa Peponi kama alivyoahidi Allah (Subhanahu Wataala).


Na aliekufa katika hali ya kumshirikisha Mola Subhanahu Wataala au hali ya kufanya madhambi makubwa na hajatubu kwa Mola Subhanahu Wataala (huyu ni Muislamu lakini ameendelea kufanya ‘Kabira’ kwa mfano: zina, kuiba, kunywa pombe na kula riba mpaka kufa kwake bila ya kutubu) huyu Allah (Subhanahu Wataala) Atamuingiza Motoni - Mola Subhanahu Wataala atukinge na hali kama hiyo - kama Alivyoahidi Subhanahu Wataala, kwani Yeye Hahalifu ahadi yake ya malipo mazuri (Al-Jannah) wala Hahalifu ahadi yake ya malipo mabaya (Jahannam). Haiwezekani kabisa kauli yake kubadilishwa. Na wala Hadhulumu Subhanahu Wataala waja wake.


Pia ni wajibu kusali, kutoa Zaka, kufunga Ramadhani, kuhiji na kuamrishana mazuri (mema) na kukatazana maovu na kufanya mengineyo yalokuwa wajibu.

Na vitu hivi anapata thawabu mtu akivifanya na anapata madhambi kwa kuviwacha.


2.“Al-Mahdhoor” yaani kilichokatazwa (Haraam).

Kila alichokikataza Allah (Subhanahu Wataala) kufanywa ikiwa ni kuacha kufanya wajibu (kama Sala, Zaka, Saumu nk) au kufanya yaliyoharamishwa kama kwa mfano kuzini, kula mali ya watu bila ya haki, kunywa aina zote za vileweshaji (pombe), kumsengenya Muislamu na kuchonganyisha (watu ili wagombane) na mengineyo yaliyokatazwa na sharia.

Mambo haya Muislamu hupewa thawabu kwa kuyawacha na huadhibiwa kwa kuyafanya. Amesema Allah (Subhanahu Wataala):


                    طه: ٨٢

“Na hakika mimi ni msamehevu sana kwa anayetubia na kuamini na kutenda wema, tena akashika Uongozi bara bara.”


3.Yaliyohimizwa kufanywa (Sunna)

Nayo ni kila jambo sheria imehimiza kulifanya katika vitendo vya kheri, tabia njema, kusaidia Waislamu, kuwaondolea kila kinachowaudhi njiani (kinachowadhuru kwa mfano miba, vigae, mawe nk) na kutoa sadaka, mbali na Zaka ambayo ni faridha, na mengineyo. Na mwenye kuyafanya haya hupewa thawabu na haadhibiwi mwenye kuyaacha na hakuna mtu aliyekuwa hahitajii thawabu za Allah (Subhanahu Wataala). Kwa hiyo Muislamu ajitahidi awezavyo asiyawache haya. Na kufanya haya yaliyohimizwa ni kukamilisha yaliyopungua katika mambo ya wajibu (faridha) na wameutolea mfano kama ujani katika mimea, amesema Mtume wa Allah (Salallahu Alayhi Wasalam):


Hakika Allah (Subhanahu Wataala) Amesema:

( من عادى لي ولياً فقد آذنته بالحرب ، وما تقرب إلي عبدي بشيء أحب إلي مما افترضته عليه ، ولا يزال عبدي يتقرب إلي بالنوافل حتى أحبه ، فإذا  أحببته كنت سمعه الذي يسمع به وبصره الذي يبصر به ويده التي يبطش بها ورجله التي يمشي عليها ، ولئن سألني لأعطينه ، ولئن استعاذني لأعيذنه )

 “Anayemfanyia uadui mpenzi wangu basi huyo nimekwisha mtangazia vita. Na hakujikaribisha mja wangu kwangu kwa kitu ninachokipenda zaidi kuliko yale niliyomuamirisha kuyafanya (fardhi kwa mfano Sala, Zaka, Saumu na Hija n.k). Na bado mja wangu azidi kujikaribisha kwangu kwa “Nawafil” (Nawafil ni yale yaliyohimizwa kufanywa) mpaka nampenda, na nikishampenda huwa Mimi ndio masikio yake anayosikilia na macho yake anayoonea na mkono wake anaokamatia na mguu wake anaoendea (anaotembelea), na kwa yakini akiniomba nitampa na akijikinga kwangu nitamkinga.”


4.Makruhu – Ni kila kinachochukiza katika sheria:

Kama kutawadha (kutia udhu) wima kwa mfano au kutawadha uchi au kuzungumza wakati wa kutawadha na mengi mengineyo yaliyotajwa katika vitabu vya fiqh.


Na mambo haya mwenye kuyawacha hupewa thawabu na haadhibiwi anapoyafanya ikiwa hakusudii kwenda kinyume na “Sunna”; akikusudia kwenda kinyume na “Sunna” basi ameangamia (amehiliki). Allah atuepushie hayo. Amin.


5.“Al-Mubaah” – Ni kufanya mambo yaliyoruhusiwa, kama kula chakula kizuri, kupanda kipando kizuri, kuvaa vazi la fahari au kwenda kujipumzisha (mahala pa zuri na watoto) vitu hivi vyote vimeruhusiwa kwa anayevifanya kwa nia nzuri lakini hali hiyo yabadilika ikiwa makusudio yake ni mabaya. Anayekusudia kufanya ufahari akipanda gari nzuri basi kwa nia yake hii mbaya amekifanya kitendo hicho kuwa haramu na akusudiae anapokula chakula kizuri kumshukuru Allah (Subhanahu Wataala) kwa neema yake au kupata nguvu ili amtii Mola Subhanahu Wataala anairudisha mubaah kwa nia yake nzuri hii kuwa kama aliyefanya wajibu, yaani aliyoamrishwa kuyafanya kwa mfano Sala, Zaka nk.


Aina zote hizi zimekuja wazi katika hadithi ya “Arrabii” kutoka kwa Abu Ubaidah kutokana na Jabir bin Zayd kutoka kwa Abi Huraira amesema: “Amesema Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam): Farasi huwa thawabu kwa mtu, na huwa sitara kwa mtu, na huwa madhambi juu ya mtu”.

Thawabu, sitara na madhambi yote haya yamepatikana kwenye kitu kimoja, farasi, na kila mmoja apata tofauti na mwenzake kwa kutofautiana nia. Na nia ni msingi wa kila kitendo na bila ya nia kitendo hicho kinapotea bure wala hakihisabiki.


Tazama ukarimu wa Allah (Subhanahu Wataala) kwa mja wake pamoja na kuwa hamhitajii kitu, na tizama upande mwingine kutokujali kwa mja mbele ya Mola wake pamoja na kuwa humhitajia kwa kila kitu na kila wakati. Akitia nia mja kufanya jambo jema Allah amuandikia jema moja hata ikiwa hakulifanya na akilifanya huandikiwa mara kumi, na akitia nia ya kufanya ubaya haandikiwi kitu juu yake ikiwa hakulifanya na akilifanya haundikiwa baya moja. Imetolewa hadithi kutoka kwa Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) kuwa amesema:

( يؤتى بالعبد يوم القيامة ومعه الحسنات أمثال الجبال فينادي مناد من كان له على فلان مظلمة فليجئ فليأخذ ، فيجيء أناس فيأخذون حسناته حتى لا يبقى له من الحسنات شيء فيبقى الرجل حيراناً، فيقول له ربه إن لك عندي كنزاً لم أطلع عليه أحدا من ملائكتي ولا أحدا من خلقي ، فيقول يا رب ما هو ؟ فيقول نيتك التي كنت نويتها من الخير كتبتها لك سبعين ضعفا)

 “Analetwa mja Siku ya Kiyama ana mema (aliyoyafanya) mfano wa milima (kwa wingi) basi ataita hapo muitaji nani ambaye kadhulumiwa na fulani na aje ili achukue. Basi waja watu wachukua mema yake mpaka hakimbakilii kitu katika mema yake (aliyoyafanya) kisha hubakia mtu huyo hajui nini la kufanya, hapo ndipo Mola wake atamwambia hakika wewe una hazina kwangu sikumuonyesha (hazina hiyo) yeyote katika Malaika wangu wala yeyote kati ya viumbe vyangu, atamwambia: Ewe Mola, kitu gani hicho? Atamwambia: Nia yako ambayo ulinuia kufanya mambo ya kheri nimekuandikia mara sabini nyongeza” (ya aliyotia nia kuyafanya).


Na hadithi nyengine:

( يؤتى بالعبد يوم القيامة فيعطى كتابه بيمينه فيقرأ فيه الحج والجهاد  والزكاة والصدقة وغير ذلك نواه ولم يعمله فيقول العبد في نفسه ما عملت من هذا شيئا وليس هذا كتابي فيقول الله تبارك وتعالى : اقرأ فإنه كتابك عشت دهرا وأنت تقول :  لو كان لي مال لحججت ولو كان لي مال لجاهدت وغزوت وفعلت وعرفت ذلك من نيتك أنك صادق فأعطيتك ثواب ذلك كله )

 “Analetwa mja Siku ya Kiyama na hupewa Kitabu chake kwa mkono wake wa kulia kisha husoma ndani yake: Hija, Jihadi, Zaka, Sadaka na mengineyo ambayo ameyatilia nia lakini hakuyafanya basi atasema huyo mja katika nafsi yake: Sikufanya kitu katika haya  na wala hichi sio kitabu changu. Hapo Allah (Subhanahu Wataala) atasema: Soma kwani hiki ni kitabu chako umeishi muda mrefu na wewe unasema: Kama ningekuwa na mali ningehiji na kama ningekuwa na mali ningefanya jihadi na ningekwenda kupigana (katika njia ya Allah) na ningefanya. Na nimejua hayo kutokana na nia yako kuwa ulikuwa mkweli basi kwa hiyo nikakupa thawabu ya hayo yote.”

           

Inavyotakiwa mtu akitaka kufanya cho chote cha kumtii Allah aseme:

 أتـقـرب إلى الله بعمل كذا

Yaani: Najikaribisha kwa Allah kwa kitendo changu kadha. Basi huandikiwa thawabu ya hicho kitendo na thawabu ya nia ya kujikaribisha.


Na hapa tutazungumzia kwa kirefu yaliyokuja kuhusu kumpwekesha Allah (Subhanahu Wataala) na kuamini kile kilichowajibika kukiamini kama ilivyokuja katika Aya tukufu Kasema Mola Subhanahu Wataala:


                                            ﭸﭹ             ﭿﮀ       ﮃﮄ        البقرة: ١٧٧

“Na wanawapa mali juu yakuwa wanayapenda, jamaa na mayatima na maskini na wasafiri  (walioharibikiwa) na waombao na katika (kuwakomboa) watumwa, na wakawa wanasimamisha Sala na kutoa Zaka na watekelezao ahadi zao wanapoahidi na wavumiliao katika shida na dhara na katika wakati wa vita, hao ndio waliosadikisha (Uislamu wao), na hao ndio wamchao Mungu”.


Na kwa mujibu ilivyokuja katika hadithi sharifu ya Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) katika maneno ya Jibril marefu ambayo yamekuja kama ifuatavyo:

( أخبرني عن الإيمان قال : أن تؤمن بالله وملائكته وكتبه ورسله واليوم الآخر وتؤمن بالقدر خيره وشره أنه من الله تعالى)

 “Niambie juu ya Imani akasema: Umuamini Allah na Malaika wake na Vitabu vyake na Mitume yake na Siku ya Mwisho na Uamini Kadari kheri yake na shari yake kuwa imetoka kwa Allah (Subhanahu Wataala).”


Kwa hivyo Imani ya Allah ndio msingi wa “Itikadi ya Dini” ambayo imekusanya mambo saba:-


1. Kumjua Allah na Majina Yake Mazuri na Sifa zake Tukufu na dalili za kuweko kwake na yanayodhihirisha Ukubwa wake katika Ulimwengu (Universe) na katika Tabia (Nature).


2. Kutumia dalili za viumbe vyake vikubwa kama mbingu na ardhi na upepo na bahari na mito na hewa na mawingu na miti na miji na vinginevyo katika viumbe vyake ambavyo havina budi kuwa na Muumbaji alieviumba naye Yuhai Mwenye uwezo ndie Mwangalizi wa vitu vyote Hahitajii msaidizi wala muokozi. Ni Mmoja katika Dhati yake, ni Mmoja katika Sifa zake na ni Mmoja katika vitendo vyake.


                                                                                             البقرة: ١٦٤

“Hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi, na (katika) kuandamizana usiku na mchana, na (katika mwendo wa) vyombo ambavyo hupita katika bahari kwa (kuchukua vitu) viwafaavyo watu, na (katika kumiminika) maji aliyoyateremsha Allah kutoka mawinguni, na kwa (maji) hayo akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake, na akaeneza humo (ulimwenguni kwa ajili ya maji hayo) kila aina ya wanyama; na katika mabadiliko ya pepo, na mawingu yanayoamrishwa kupita baina ya mbingu na ardhi, bila shaka (katika haya) zimo ishara kwa watu wenye akili (kuwa yuko Allah na ni Mmoja tu)”.


Na inampasa mwenye kumpwekesha Allah awe na itikadi (imani) kuwa kumpwekesha kwake (Allah) ni neema ya Allah juu yake na kama Angetaka Subhanahu Wataala angemfanya mnyama au katika wanaomshirikisha Allah au wanaoamini hakuna maisha ila ya duniani na hawafishwi ila na wakati.


      ﯶﯷ          ﯼﯽ     ﯿ                                  الحجرات: ١٧

“Wamekusumbulia kwa kuingia kwao Uislamuni. Sema ‘Msifanye kuwa ni ihsani kwangu kusilimu kwenu, bali Allah ndiye aliyekufanyieni ihsani kwa kukuongozeni kwenye Uislamu, ikiwa nyinyi ni wakweli’.”


Ni wazi kuwa Imani sio tu kusema kauli:   لا إله إلا الله  kwani haitomfaa (kauli hiyo) mtu kitu ikiwa hatofuatilia kwa kufanya vitendo vilivyo wajibu juu yake.


                                                   ﭲﭳ               الأنعام: ١٥٨

“Siku zitakapofika baadhi ya Ishara za Mola wako, basi mtu (kafiri) haitamfaa imani yake ambaye alikuwa hakuamini zamani, au (Muislamu) hakuchuma kheri katika Uislamu wake. Sema: Ngojeni, sisi pia tunangojea”.

           

Na hakika kitu kinachotakiwa (mtu afanye) ni kunena kwa Ulimi, na kutenda kwa mujibu wa nguzo (za Kiislamu) na kuamini kwa moyo Imani iliyojaa moyoni mpaka ikatoka humo athari yake na athari yake ni vitendo (vyema) kama miangaza inavyotokana na Jua.


3. Kuamini Malaika wa Allah: Na huko ni kuamini kuwa Allah anao waja wenye kukirimiwa

Kasema Allah katika Sura Attahrim aya ya 6:


                التحريم: ٦

“Hawamuasi Allah kwa amri zake na wanatenda wanayoamrishwa (yote)”.


Wametakaswa na upungufu na maasi, wameumbwa na tabia ya aliekuwa hafanyi maasi, chakula chao ni kufanya “tasbiih” na “tahmiid” (kumsabih na kumshukuru Mola Subhanahu Wataala). Kila mmoja katika wao amekalifishwa kufanya kazi fulani hachoki kuifanya wala haghafiliki nayo wala haipuuzi (kuifanya hiyo kazi). Wala hawasifiki kwa sifa za kula wala kunywa wala kukojoa wala kutema mate na mengineyo katika uchafu unaotoka mwilini.


Na faida kubwa ya Imani hii (ya Malaika) ni kuisafisha ‘Itikadi’ ya kumpwekesha Allah (Subhanahu Wataala) na masalio ya ushirikina, kitu ambacho kilikithiri kwa Waarabu katika ujahiliya wao kwani walikuwa wakiwafanya Malaika ni Miungu bila ya Allah au wakiwafanya vizazi vyake Subhanahu Wataala.


Malaika amewaumba Allah (Subhanahu Wataala) kwa nuru kama alivyomuumba Adam kwa udongo, na kama alivyowaumba majini kwa Moto usiokuwa na moshi.


Amesimulia Assidiqa (Aisha) binti Assidiq (Abu Bakar) RA kutokana na Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) amesema:

 ( خلقت الملائكة من نور وخلق الجان من مارج من نار وخلق آدم مما وصف لكم )  ( رواه مسلم )

 “Wameumbwa Malaika kwa nuru, na wameumbwa Majini kwa Moto usiokuwa na moshi (safi) na ameumbwa Adam kwa kile mulichosimuliwa (mlichoambiwa).” Ameitoa Muslim.


Na Allah (Subhanahu Wataala) Amemchagua miongoni mwao Malaika wa kuhishimika (mbora) naye ni Jibril AS, naye ndiye Mjumbe wake kwa Mitume. Ama hakika yao na vipi wameumbwa haya mambo hatukuambiwa cho chote juu yake, lakini tulichoamrishwa ni kuamini kuwepo kwao na tuilinde haki ya kusuhubiana nao na vile vile tuimarishe uhusiano wetu nao kama alivyotuelekeza Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) katika kauli yake:

 (إن معكم من لا يفارقكم إلا عند الخلاء وعند الجماع فاستحيوا منهم وأكرموهم )

 “Hakika wako pamoja na nyinyi wasiowabandukeni isipokuwa wakati wa haja na wakati wa “jimaa” (anapomuingilia mtu mkewe) basi waoneeni haya na wahishimuni” (hao ni Malaika).


4. Kuamini Vitabu vya Allah ambavyo kaviteremsha kwa Manabii wake na Mitume wake, kwani ameteremsha vitabu kwa Ibrahim, Shiith na kwa Nooh lakini havikujulikana majina yake na havikujulikana isipokuwa Vitabu vinne:

Azzabuur kimeletwa kwa Dawood AS

Attawraah kimeletwa kwa Moosa AS

Al-Injil kimeletwa kwa Issa AS

Al-Qur'an kimeletwa kwa Muhammad Salallahu Alayhi Wasalam


Na hii “Qur'an” imefuta vitabu vyote vilivyotangulia isipokuwa “Tawhiid” kwa sababu mwito uliokuja kwa “Tawhiid” umelingana katika vitabu vyote vya Allah basi kwa hivyo haijuzu kuvifuata vitabu hivyo vilivyotangulia.

Kasema Mola Subhanahu Wataala katika Sura Al-Umran aya ya 85:


                           

آل عمران: ٨٥

“Na anayetaka Dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye khasara (kubwa kabisa)”.


Bali ni wajibu kuviamini tu (bila ya kuvifuata)


                                                                      آل عمران: ٢ - ٤

“Allah, hakuna aabudiwaye kwa haki isipokuwa yeye mwenye uhai wa milele, na muendeshaji wa mambo yote (2) Amekuteremshia Kitabu kwa haki, kinachosadiki yaliokuwa kabla yake. Na aliteremsha Taurat na Injil (3) Zamani ziwe uwongozi kwa watu. Na akateremsha vitabu vyengine vya kupambanua”.


Na Qur'an imekusanya yote yaliyomo katika vitabu vilivyotangulia katika mambo ambayo Allah kayafanya wajibu kwa waja wake.

Kasema Allah katika Sura Al-Shura aya ya 13:

 

          ﭿ                       ﮊﮋ             الشورى: ١٣

“Amekupeni Sharia ya Dini ile ile aliyomwusia Nuhu na tuliyokufunulia wewe na tuliyowausia Ibrahim na Musa na Isa kwamba simamisheni Dini wala msifarikiane kwayo”.


Na Allah (Subhanahu Wataala) Ameihifadhi Qur'an na hawakuweza (wala hawawezi) mmoja katika maadui zake kubadilisha ndani yake kitu walau herufi moja kama vilivyobadilishwa vitabu vilivyotangulia.


                           ﮛﮜ             فصلت: ٤١ – ٤٢

  “Bila shaka hicho ni kitabu kihishimiwacho (41) Haitakifikia batili mbele yake wala nyuma yake; kimeteremshwa na mwenye hikima ahimidiwaye (42).”


Na Mola ameitakia Qur'an ibakie milele mpaka kitakapokuja Kiyama. Na ameifanya iwe nyepesi kukumbukwa, kuhifadhiwa na kufahamika haiwataabishi watu kufahamu wala kuifuata (kutekeleza maamrisho yake na kuacha makatazo yake)


                   القمر: ١٧

“Na kwa yakini tumeifanya Qur'an iwe nyepesi kufahamika ili iwe kikumbusho. Lakini (jee) yuko anayekumbuka?”


Na hakika katika Qur'an kuna habari za kila kilichopo kama alivyotuambia Mtume wa Allah (Subhanahu Wataala) katika kauli yake:

(ستكون من بعدي فتن كقطع الليل المظلم قيل له : وما المخلص منها يا رسول الله قال : كتاب الله فيه نبأ من قبلكم وخبر ما بعدكم وحكم ما بينكم وهو الفصل ليس بالهزل ، من تركه من جبار قصمه الله،  ومن ابتغى الهدى في غيره أضله الله وهو حبل الله المتين ونوره المبين والذكر الحكيم والصراط المستقيم وهو الذي لا تزيغ به الأهواء ولا تتشعب معه الآراء ولا يمله الأتقياء ولا يخلق على كثرة الرد، وهو الذي لم تنته الجن إذ سمعته أن قالوا : إنا سمعنا قرآنا عجبا ، من قال قوله صدق ومن حكم به عدل ،  ومن عمل به أجر ،  ومن اعتصم به فقد هدي إلى صراط مستقيم)

“Kutakuwa baada yangu mitihani kama vipande vya usiku wa giza, akaambiwa (akaulizwa): Nini kitakachotutoa na hiyo (mitihani) (au kitachotuokoa) akasema: Kitabu cha Allah, humo ndani yake mna habari ya waliokuwa kabla yenu na habari itakayokuwa baada yenu na hukumu baina yenu, nacho ni mpambanuo (baina ya haki na batili) siyo mzaha, anaekiwacha (hicho kitabu) miongoni mwa waonevu wa watu (wanaoua watu katika ghadhabu “Jabbar”) basi Allah humvunja, na anaetaka uongofu kwengine pasi na Qur'an Allah humpoteza, nayo ni Kamba ya Allah iliyo na nguvu, na Nuru yake iliyo wazi, na kumbusho lililo na hekima, na njia iliyonyooka, kwa hiyo (Qur'an) mapendekezo hayapotei, wala rai hazikhitilafiani pamoja nayo, wala wachamungu hawachoki nayo, wala haichakai (katika nafsi za watu) juu ya kurudia kuisoma mara kwa mara, na ndio hiyo ambayo hawakumaliza majini baada ya kuisikia (inasomwa) isipokuwa wakasema: Hakika tumesikia kisomo cha ajabu. Anaesema kauli yake (Qur'an) amesema ukweli, na anayehukumu kwayo amefanya uadilifu, na anaetenda kwa mujibu wake anaongozwa kwenye njia iliyonyooka.”


5. Kuamini Mitume wa Allah Rehema zake ziwe juu yao, kwa kauli yake Mola Subhanahu Wataala :


                ﮞﮟ                             ﮫﮬ       البقرة: ٢٨٥

“Mtume ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake, na Waislamu (pia wameamini hayo): Wote wamemwamini Allah, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume yake; (nao hao Waislamu na Mitume wao husema): ‘Hatutafautishi baina ya yoyote katika Mitume wake (wote tunawaamini)’.”


Na ikiwa Muislamu ameamini baadhi tu ya Mitume na hakuamini baadhi nyingine basi huyo ni kafiri kwa mujibu wa kauli yake Mola Subhanahu Wataala :


                              ﭿ                           ﮋﮌ            النساء: ١٥٠ – ١٥١

  “Hakika wale wanaomkataa Allah na Mitume yake, na wanataka kutenga baina ya Allah na Mitume yake, kwa kusema: ‘Wengine tunawaamini na wengine tunawakataa’, na wanataka kushika njia iliyo kati kati ya haya (si ya Kiislamu khasa wala ya kikafiri). Hao ndio makafiri kweli, na tumewaandalia makafiri adhabu ifedheheshayo”.


Na lengo la kuletwa Mitume ni kuwaita watu kwenye Ibada ya Allah na kusimamisha Dini yake. Amesema Mola Subhanahu Wataala :


                                        الأنبياء: ٢٥

“Na hatukutuma kabla yako mtume ila tulimfunulia ya kwamba hapana anayestahiki kuabudiwa ila Mimi basi niabuduni.”

Na Amesema Subhanahu Wataala:


                     النحل: ٣٦

“Na bila shaka tulimpeleka Mtume katika kila umati ya kwamba Muabuduni Allah na mwepukeni (Iblis) mwovu”.


Na katika hao Mitume ambao Qur'an imewasimulia na kuwataja majina yao basi hao ni wajibu kuwaamini kwa kirefu kila mmoja wao peke yake kama Nuuh na Ibrahim na wengineo. Na wale waliokuwa hawakutajwa kwa jina ni wajibu kuwaamini kwa ujumla.

Anasema Allah (Subhanahu Wataala) :


                   النساء: ١٦٤

“Na wako Mitume (tuliwapelekea wahyi) tuliokuhadithia (habari zao) zamani na Mitume ambao hatuku kuhadithia (habari zao).”


Na Mitume wote hao wamekuja kuwaongoza na kuwaokoa watu kutokana na upofu (upotofu) na yametoweka mafundisho yao hao Mitume na zimefutwa Sharia zao isipokuwa Tawhiid (kumpwekesha Allah (Subhanahu Wataala)), kwani wameafikiana Mitume wote juu yake (Tawhiid), na imebakia sharia ya Mtume wetu Muhammad (Salallahu Alayhi Wasalam) ambayo imekuja kufuta sharia zote zilizopita na wala haijuzu kabisa kufuata sharia yoyote nyingine (ya Vitabu vilivyotangulia) mpaka Siku ya Kiyama. Kwa hivyo inawabidi watu wote kumuamini Mtume Muhammad (Salallahu Alayhi Wasalam) na kuamini aliokuja nayo. Na wala mtu asiwasikilize wale wanaosema kuwa zote hizo ni sharia zilizokuja kutoka Mbinguni kwa hiyo anayefuata yoyote katika hizo ni sawa. Ni wajibu kumuamini Muhammad kuwa ni Mtume Mkweli kutoka kwa Allah (Subhanahu Wataala) na kuwa uongozi wake ni kamili hauna upungufu wala kosa na kuwa yeye ni Mtume wa mwisho aliekuja kwa Umma huu Salallahu Alayhi Wasalam. Na amepewa na Allah (Subhanahu Wataala) “Al-Wasila” na Al-Fadhila”.


Na katika wajumbe (Mitume) wale wanaoitwa “Ulu Al-Azmi “yaani wenye azimio la nguvu na subira kubwa, na Allah (Subhanahu Wataala) amewataja katika kauli yake:


                          ﭝﭞ          الأحزاب: ٧

  “Na wakumbushe tulipochukuwa ahadi kwa Manabii (wote) na kwako wewe na Nuhu na Ibrahim na Musa na Issa mwana wa Mariamu na tulichukuwa kwao ahadi ngumu”.


Na dalili inayoonesha kuwa Mtume Muhammad (Salallahu Alayhi Wasalam) ni Mtume wa Mwisho na hakuna Mtume mwengine baada yake kwa mujibu ya kauli ya Allah (Subhanahu Wataala):


                              الأحزاب: ٤٠

“Muhammad si baba wa yoyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Mungu na mwisho wa Mitume”.


Na mitume wote wengine kila mmoja kati yao amepelekwa kwa watu maalumu isipokuwa Mtume Muhammad yeye ameletwa rahma kwa viumbe wote na watu wote. Na wakati atakapokuja Issa AS basi  atashuka kwa sharia ya Mtume Muhammad (Salallahu Alayhi Wasalam) na sio kuwa atakuja na sharia mpya.


6. Kuamini Siku ya Mwisho: Nayo ni Siku ya Kiyama. Na kuamini siku hii ni sehemu katika fungamano (ahadi baina ya Allah na mja wake) ambalo haitimii Imani isipokuwa kwa hilo (fungamano). Na atambue Binaadamu kuwa hakuumbwa bure bila ya kusudio lolote bali ameumbwa kwa ajili ya kumuabudu Allah.


Kasema Allah katika Sura Adhaariyat aya ya 56 na 57


                           ﭿ          الذاريات: ٥٦ – ٥٧

  “Sikuwaumba Majini na Watu ila kwa ajili ya kuniabudu. Sitaki kwao riziki wala sitaki wanilishe”.


Na kwa akili inafahamika kuwa anaetaka kwako jambo fulani hapana budi akutake ulitekeleze hilo jambo. Amesema Allah (Subhanahu Wataala):


                 المؤمنون: ١١٥

“Je! Mlidhani ya kwamba tumekuumbeni bure (kwa upuuzi) na ya kwamba ninyi kwetu hamtarudishwa?


Na Amesema Mola Subhanahu Wataala :


                                                                                                       القيامة: ٣٦ - ٤٠

“Je! Anafikiri  (anadhani) binaadamu kuwa ataachwa bure (ovyo tu), asipewe amri za Allah wala makatazo yake? Hakuwa tone la manii lililotonwa? Kisha akawa kidonge cha damu, kisha akamuumba na akamsawazisha (mwanadamu kamili)? Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke. Je! Hakuwa huyo ni muweza wa kuhuisha wafu?”


Na Amesema Subhanahu Wataala:


          ﮘﮙ                           ﮦﮧ                 يس: ٧٨ - ٧٩

“Na katupigia mfano, na kasahau kuumbwa kwake (kwa manii) akasema: “Nani atakayehuisha mifupa na hali imesagika?” Sema: “Ataihuisha yule aliyeiumba mara ya kwanza, naye ni mjuzi wa kila (namna ya) kuumba”.



Na Allah amewajibu washirikina (wanaoabudu wakati) juu ya kauli yao:


                                الجاثية: ٢٤

“Haukuwa uhai ila ni uhai wetu huu wa Dunia, (hakuna mwengine); tunakufa na tunaishi, wala hakuna kinachotuangamiza isipokuwa huu huu ulimwengu (kwani ndio ada yake kufisha na kuhuisha).”


Vile vile Mola Subhanahu Wataala amewajibu manasara (wakristo) ambao wanaamini Siku ya Mwisho isipokuwa wao wanaamini kuwa Nabii Isa AS atajitolea mhanga (fidia) ili awaokoe na adhabu ya Siku ya Kiyama. Na atawaepusha na malipo mabaya wanayostahiki kwa maovu waliyoyatenda.

Na pia amewajibu Subhanahu Wataala mayahudi ambao wanaamini kuwa katika Siku ya Kiyama lipo  lengo kuu kwa ajili yao na wao wamesema:


      المائدة: ١٨

“Sisi ni wana wa Allah na wapenzi wake.”


Na wote hao wamesema uongo, na Qur'an imewajibu wao jawabu kali kabisa. Na Siku ya Mwisho inaanza kwa kubadilika huu Ulimwengu wakati inapopasuka mbingu na nyota zinapopukutika na majabali (milima) yanapokwenda (yanamung'unyika na kuruka angani) na wakati inapobadilishwa hii Ardhi yetu (Dunia) ikaletwa ardhi nyengine na mbingu vile vile zikabadilishwa na kuletwa nyengine na kila kitu kilichokuweko sasa hivi kitavunjwa vunjwa:


                       ﯼﯽ     ﯿ              ﰆﰇ                              الأنعام: ٩٤

  “Bila shaka nyinyi mmetujia mmoja mmoja tu, (kila mtu peke yake na hana mtoto wa kumsaidia wala watumwa wala.....) kama tulivyokuumbeni mara ya kwanza, na mmeyaacha nyuma yenu tuliyokupeni, na hatuwaoni waombezi wenu pamoja nanyi ambao mlidai kuwa ni washirika (wa Allah) kwenu, yamekatika (mahusiano) yalivokuwa kwenu na yamekupoteeni mliyokuwa mkidai.”


7. Kuamini kadari kheri yake na shari yake kuwa inatoka kwa Allah (Subhanahu Wataala) kwa kauli yake Allah Taala:


       ﭿ                                 الحجر: ٢١

“Na hakuna cho chote ila asili yake inatokana na sisi, wala hatukiteremshi ila kwa kipimo maalum (si ovyo ovyo tu).”


Na kwa kauli yake:


                            القمر: ٤٩

“Kwa hakika Sisi Tumekiumba kila kitu kwa kiasi (chake makhsusi).”


Na kwa kauli yake:


                                  ﯟﯠ                الحديد: ٢٢

“Hautokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu ila umekwisha andikwa katika kitabu cha (Allah) kabla hatujauumba. Kwa yakini hayo ni rahisi kwa Allah.”


Na kauli yake Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) katika hadithi aliyoitowa Arrabii Ibn Habiib :

( يا عبدي إنك لن تؤمن ولن تبلغ حقيقة الإيمان حتى تؤمن بالقدر خيره وشره أنه من الله، قال كيف لي أن أؤمن بالقدر خيره وشره ؟  قال : تعلم أن ما أصابك لم يكن ليخطئك وما أخطأك لم يكن ليصيبك فان مت على غير هذا دخلت النار )

 “Ewe mja wangu kwa yakini wewe hutoamini na wala hutoufikia ukweli wa Imani mpaka uamini kuwa Kadari kheri yake na shari yake ni kutoka kwa Allah, Akasema: Vipi hata niweze kuiamini Kadari kheri yake na shari yake? Akamjibu: Ujue kuwa yaliyokusibu (au yaliyokupata) haiwezekani kuwa yangeweza kukukosa kukusibu na (vile vile) yaliyokosa kukusibu haiwezekani kuwa yangekusibu, na ukifa nawe unaamini vinginevyo  basi utaingia Motoni”.


Alipokwenda Omar bin Al-Khattab RA huko Amwaas kwa ajili ya kupigana vita akasikia kuwa kuna “Taawuun” (maradhi yaambukizayo kwa haraka, na yanayoua watu) katika mji huo basi hakuuingia. Na alikuwa Abu Ubaidah bin Al-Jarrah RA amemuwahi kwa kuingia huo mji akamuambia: Je (hukuingia) kwa kukimbia kadhaa ya Allah ewe Amiri wa Waumini (kukimbia yaliyokwisha amuliwa na Allah kuwa yatatokea). Akasema: Lau kama angeyasema maneno haya mwengine (sio wewe) ewe Aba Ubaidah. Ndio twaikimbia kadhaa ya Allah kuindea Qadari yake (Allah (Subhanahu Wataala). Na Omar RA alikuwa kisha washauri Masahaba katika jambo hilo akasema Abdul Rahman bin Auf: Nimehifadhi katika jambo hili hadithi ya Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) asema:

 ( إذا سمعتم به بأرض فلا تقدموا عليه ،  و إذا وقع بأرض وأنتم بها فلا تخرجوا فراراً منه )

“Mkiusikia umo katika ardhi (huo ugonjwa wa “Taawuun”) basi msiende huko, na kama ukitokea katika ardhi nyie mmo ndani yake basi msitoke kuukimbia”


Basi Omar akamshukuru Allah (Subhanahu Wataala) na kumsifu kisha akaondoka.

           

Ametoa Abu Ubaidah kutokana na Jabir bin Zayd kuwa amesema: imenifikia habari kutoka kwa Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) kuwa amesema:

 (كل شيء بقـضاء وقـدر حتى العجز والكيس )

“Kila kitu (kinatokea) kwa kadhaa na kadari hata udhaifu wa kufanya mambo na uhodari.”


Na aliporudi Ali bin Abi Talib kutoka Safiin, mzee mmoja alimuuliza: Ewe Amiri wa Waumini tuambie kuhusu kwenda kwetu “Shaam” je kulikuwa kwa “Kadhaa” na  “Kadari”. Akasema: Naapa kwa yule aliyeipasua punje (ya mbegu ikatoa mmea) na akaumba binaadamu hatukukanyaga mahala wala hatukushuka bonde wala hatukupanda mlima isipokuwa kwa Kadhaa na Kadari. Akasema yule mtu mzima: Naifikiria ile taabu yangu (niliyoipata katika huo msafara wa vita) sidhani Wallahi kama nitapata malipo yoyote mazuri. Akasema Ali: Bali ewe mzee Allah amewapa malipo makubwa nanyi mnakwenda katika mwendo wenu na katika kurejea kwenu na hamkuwa mmelazimishwa katika yote mliyoyafanya wala haikuwa dharura ikiwafanya mtende hayo. Akasema yule mzee: Vipi hatukulazimika kutenda tuliyoyatenda na Kadhaa na Kadari ndio iliyotupeleka huko na ndio iliyoturejesha kutoka huko. Basi hapo akasema Ali: Ole wako ewe mzee, unadhania kuwa kadhaa hiyo ni ya kulazimishwa na kadari hiyo haina budi iwe; basi kama ingekuwa hivyo kusingekuwa na thawabu wala adhabu (malipo mabaya) na kusingekuwa na kuahidiwa malipo mazuri (kwa afanyae vitendo vizuri) na kuahidiwa malipo mabaya nayo ni Moto (kwa afanyae vitendo viovu), na vile vile kusingekuwa na kuamrishana kufanya mema na kukatazana mabaya, vile vile kusingekuwa na lawama kwa afanyae madhambi wala kusifiwa kwa afanyae mazuri, pia asingekuwa mtu mwema ndio wa kusifiwa badala ya mtu muovu, wala mtu muovu ndio wa kulaumiwa badala ya mtu mwema, kauli kama hizo ni za wale wanaoabudu masanamu na askari wa shetani na wenye ugomvi na “Arrahman” na wanaotoa ushahidi wa batili (dhulma) na waliopotoka katika njia ya sawa na hao ndio “Kadariya” wa Umma huu na ndio Majusi wake (wanaoabudu Moto). Kwa hakika Allah ameamrisha kwa hiyari yake mtu na amekataza kwa kumhadharisha mtu na mabaya (adhabu) na amekalifisha kwa wepesi na wala hakuasiwa kwa kushindwa na wala hakutiiwa kwa kuwalazimisha watu (wamtii) na wala hakupeleka Mitume bure na hakuumba mbingu na Ardhi bila ya kusudio.


      ﭜﭝ                   ص: ٢٧

“Hii ni dhana ya wale waliokufuru basi adhabu kali ya Moto itawathibitikia wale waliokufuru”.


Hapo yule mzee akasimama naye amefurahi na sio maana ya Kadari kutegemea na aseme mtu:- Nikiandikiwa kitu hicho kitanipata na huu ni udhaifu kwani mja ameumbwa ili afanye (vitendo vizuri na ajikataze na maovu) na Allah (Subhanahu Wataala) afanya ayatakayo na bora ya afanyayo mtu ili ajikaribishe kwa Mola wake ni kufanya zile faridha (Sala tano, Zaka, kufunga Ramadhani na Hija) ambazo amemlazimisha kuzifanya.

Na vile vile tabia njema zinakuwa pamoja na hizo faridha. Na Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) amehimiza haya katika kauli yake:

 ( بعثت متمما لمكارم الأخلاق )

“Nimetumwa ili nitimize tabia njema”


Na akasema:

( لو كان حسن الخلق رجلا لدخل الجنة )

Kama ingelikuwa tabia njema ni mtu angeingia Peponi.”


Imetolewa kuwa Ali bin Abi Talib amesema: Ewe Allah ulietakasika, kitu gani kilichowafanya watu wengi wakatae kufanya kheri, amenistaajabisha mtu anaejiwa na ndugu yake kumtaka haja kisha asijione katika nafsi yake mwenye kumiliki kufanya kheri, kwani kama tungekuwa hatungojei thawabu (malipo mazuri) au hatuogopi malipo mabaya basi juu ya hivyo tungelazimika kuwa na tabia njema kwa sababu zinatuonesha njia ya kuokoka. Akasimama mtu akasema: Nakutolea mhanga baba yangu na mama yangu ewe Amiri wa Waumini, je umesikia hayo kwa Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam)? Akasema: Ndio na kilichokuwa bora kuliko hayo: Tulipojiwa na mateka wa “Teyyii” akasema mtoto wa kike (katika hao mateka):  Ewe Muhammad, ameangamia baba yangu na amepotea msaidizi wangu, na ni bora uniwachie wala usiwafanye waarabu wanifurahikie (kwa kuchukuliwa mateka na kushindwa) kwani mimi ni binti wa kiongozi wa watu wangu, alikuwa baba yangu akimsaidia mwenye matatizo, na akimshibisha mwenye njaa na amuhami aliedhulumiwa na humfariji alie na uzito na alisha chakula na atoa Salamu (kuwaamkia watu) wala hamrudishi mtu haja yake hata kidogo: mimi ni mtoto wa Haatim Taaiy. Basi hapo akasema Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam):

(يا جارية هذه صفة المؤمن لو كان أبوك إسلاميا لترحمنا له خلوا عنها فإن أباها كان يحب مكارم الأخلاق والله يحب مكارم الأخلاق)

 “Ewe mwana mwari (mtoto wa kike bado hajaolewa) hizi ni sifa za muumini, kama angekuwa baba yako Muislamu basi tungelimuombea rehema (arehemewe na Allah), muachieni kwani baba yake alikuwa apenda tabia njema, na Allah azipenda tabia njema.”


Na katika mambo aliyokuwa akiyahimiza Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) na aliyoyausia ni mwendo mzuri katika kuingiliana na watu na katika biashara na kujikataza kufanya khiyana na kughishi  na mwendo mbaya  wo wote ule na kwa vyovyote vile.


Kwa hakika mwendo mzuri (maingiliano mzuri na watu) ni katika ibada ambazo zinamkaribirisha mtu na Allah (Subhanahu Wataala) na hupenda Mola Subhanahu Wataala waja wake wawe na mwendo mzuri kwa kuwahurumia na kuwapenda. Imetolewa hadithi kuwa Ali bin Abi Talib alisema: “Kwa yakini Allah (Subhanahu Wataala) ameweka thawabu kwa wanaomtii na adhabu kwa wanaomuasi kwa ajili ya kuwakimbiza waja wake kutokana na adhabu yake na kuwapeleka katika Pepo yake”. Vile vile amesema: Tahadhari asikuone Allah (Subhanahu Wataala) katika kumuasi na asikukose kwenye kumtii ili usiwe katika waliohasirika. Na ukiwa na nguvu tumia nguvu hizo katika kumtii Allah, na ukidhoofika basi uwe dhaifu wa kushindwa kuyafanya maasi ya Allah. Pia amesema: Chochote unachokiona wewe ni kheri lakini chasababisha kuingia Motoni hicho si kheri, na unachokiona ni shari lakini chasababisha kuingia Peponi hicho sio shari, na kila raha (ya Duniani) isiyokuwa raha ya Pepo (“Al-Jannah”) ni upuuzi tu, na kila balaa isiyokuwa adhabu ya “Jahannam” ni kheri.


Na wamesema wafasiri wa Qur'an katika kauli yake Subhanahu Wataala:

        البقرة: ٨٣

“Na semeni na watu kwa wema”


Yaani kauli nzuri isiyokuwa na ukali ndani yake, na kauli nzuri (au njema iliyohimizwa katika Aya hii) imechukua kila aina ya wema anaoufanya binaadamu kwa binaadamu mwenzake au hata wanyama kwani imesemwa: kama ungefanya wema kwa kila kitu lakini ukamfanyia ubaya kuku basi ungekuwa mbaya (si mwema).


Vile vile imepokewa katika hadithi:

 ( المسلم من سلم المسلمون من لسانه ويده )

“Muislamu ni yule ambaye Waislamu wanasalimika na (shari) ya ulimi wake na mkono wake.”


Na Allah (Subhanahu Wataala) asema katika kitabu chake kitukufu:


                                   النساء: ١١٤

“Hakuna kheri katika mengi wanayoshauriana kwa siri, isipokuwa (mashauri yao) wale wanaoamrisha kutoa Sadaka au kufanya mema au kupatanisha bina ya watu.”


Basi katika kutekeleza maamrisho ya Aya hii na zilizo mfano wake ni matengeneo ya jamii na hubakia imeshikamana katika mambo yanayohusu haki za watu baadhi yao kwa baadhi kwani huwafanya kuoneana huruma, kupenda kutizamana, kupendelea wenziwao juu ya nafsi zao. Na kujitolea mhanga kwa maslaha ya jamii. Na jamii (mujtamaa) kuchukua dhamana ya kusuluhisha baina ya wanaogombana ni katika mambo ambayo sharia ya Kiislamu imeshughulika nayo sana na imeyahimiza.

Kasema Allah katika Sura Annisa aya ya 114:


                     النساء: ١١٤

“Na atakaefanya hivi kwa kutaka radhi ya Allah, basi tutampa ujira mkubwa.”


Na kupatanisha watu ni miongoni mwa mambo bora yanayomkaribisha mja kwa Mola wake.

Na nani aliekuwa nafsi yake haitaki kupata kila kilicho bora katika Dunia na Akhera, hakuna isipokuwa aliye dhaifu.


Inasemekana kuwa Omar bin Abdul-Aziz rehema za Allah ziwe juu yake- amesema: Sikupata daraja katika Dunia isipokuwa nafsi yangu ikatamani kupata daraja ya juu zaidi (kuliko ile ya kwanza) mpaka nikafikia kupata Khilafa Tukufu (Utawala wa uadilifu wa hukumu ya Allah), hapo nikaikataa Dunia na nafsi yangu ikatamani Pepo (“Al-Janna”).


Na Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) ameisifu daraja hii mpaka akasema:

(ألا أخبركم بأفضل من درجة الصيام والصلاة والصدقة؟ قالوا : بلى يا رسول الله، قال صلاح ذات البين، فإن فساد ذات البين هي الحالقة)

 “Je niwaambie iliyo bora kuliko daraja ya Saumu na Sala na Sadaka? Wakasema: Ndio ewe Mtume wa Allah, akasema: Kusuluhisha waliogombana kwani kuwaachia wanaogombana bila ya kuwapatanisha huzidi uhusiano kuharibika hatimaye huutia udhofu Uislamu.”


Qur'an imeusia kupatanisha wanaogombana katika kauli yake Subhanahu Wataala:

               ﯡﯢ           الحجرات: ١٠

“Kwa hakika Waislamu ni ndugu; basi patanisheni baina ya ndugu zenu, na mcheni Allah, (msipuuze jambo la kupatanisha) ili mrehemewe”.


Basi ni lazima familiya zishikane, na mshikano wenye nguvu zaidi baina yao ni mshikano wa Tawhiid (Kumpwekesha Allah (Subhanahu Wataala) yaani mshikano wa Uislamu), kisha mshikano wa mapenzi na kuwasiliana baina ya “Arhaam” (jamaa wanaohusiana kwa damu) na kutambua haki zao, na kuwatembelea mafakiri kwa kuwapa Zaka kutoka kwa matajiri na mengineyo yasiokuwa Zaka kama sadaka zilizozidi katika mali.


Imetolewa hadithi isemayo:

 ( جبلت النفوس على حب من أحسن إليها وبغض من أساء إليها )

“Nafsi zimeumbwa na tabia ya kumpenda yule anayezifanyia wema na kumchukia yule anayezifanyia uovu”.


Kwa haya na mfano wake kunatokea kupendana na kushikana baina ya watu na yatekelezwa kauli ya Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam):

( المؤمنون بعضهم أولياء بعض يسعى بذمتهم أدناهم ، و يرد عليهم أقصاهم ،  وهم يد على من سواهم )

“Waumini ni marafiki wao wenyewe kwa wenyewe, ahadi yao inachungwa na wote hata anapoitoa mnyonge wao, na anawakatalia ahadi hata aliye mbali kati yao, na wao ni mkono mmoja (hushirikiana) dhidi ya maadui zao.”


Na kauli yake Salallahu Alayhi Wasalam:

( مثل المؤمنون  في توادهم وتراحمهم وتعاطفهم مثل الجسد الواحد إذا اشتكى منه عضو تداعى له سائر الجسد بالسهر والحمى )

“Mfano wa Waumini katika kupendana kwao na kuhurumiana kwao na kufikiriana kwao ni kama mwili mmoja kikishtakia kiungo kimoja ndani yake basi mwili mzima huyahisi yale maumivu ukakesha na kupata homa.”


Inabainika kuwa mambo haya ndio msingi wa uhusiano baina ya watu katika mujtamaa (jamii) ya Kiislamu bali ni juu ya Waislamu mkubwa wao na mdogo wao, tajiri wao na maskini wao, kiongozi wao na raia wao wawe katika msingi huu wa uhusiano baina yao. Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) amekanusha Imani ya mtu aliyekuwa hampendelei mwenzake kama anavyojipendelea nafsi yake, akasema (Salallahu Alayhi Wasalam):

 ( لا يؤمن أحدكم حتى يحب لأخيه ما يحب لنفسه )

“Haamini mmoja wenu mpaka ampendelee ndugu yake (katika Uislamu) kile anachojipendelea nafsi yake.”


Na Amesema Salallahu Alayhi Wasalam:

 (والله في عون العبد ما دام العبد في عون أخيه )

“Na Allah yuko katika kumsaidia mja wake madamu huyo mja yuko katika kumsaidia ndugu yake(katika Uislamu).”


8. Na akaitoa mali (kuwasaidia watu) juu ya kuwa anaipenda (hiyo mali). Akawapa jamaa zake, mayatima, maskini, na wapita njia (waliokatikiwa na watani wao), wanaoomba, na katika kuwakomboa (kuwapa uhuru) watumwa.


Inadhihirika hapa kuwa mahimizo haya Allah ameyaleta katika sadaka sio Zaka ya mali, kwa sababu Amesema katika mwisho wa Aya hii (Sura Al-Baqarah Aya ya 177) baada ya mahimizo haya:

وآتى الزكاة   “na kutowa Zaka”.

Na kusudio la kuamrishwa mtu atoe mali yake kwa mujibu wanavyosema wataalamu ni kujikomboa na pingu za kun`gan`gania mali, na kujipendelea kheri nafsi yake tu. Vile vile kusudio lake ni kuikomboa nafsi na pingu za kupenda mali kwa hiyo anakuwa mtu huyu huru kutokana na utumwa wa mali na kuin’gan’gania Dunia. Kuin’gan’gania Dunia (kushughulika nayo sana) inawafanya watu kuwa dhalili. Na wale wenye nafsi zilizo huru na matamanio ndio walio huru katika jamii (mujtamaa).


Na kupeana kunaifanya jamii ikamatane baina ya wadogo na wakubwa, kuwasiliana kwa mali ndiko kunakotia nguvu uhusiano baina ya Waislamu hasa wanaohusiana kwa damu. Kama ilivyokuja katika hadithi ya Arrabii katika kitabu chake cha kutegemeka, na vile vile ameitoa Al-Bukhari kutoka kwa Anas bin Malik RA: Alikuwa Abu Talhah katika Maansari waliokuwa na mitende mingi zaidi huko Madinah, na ilikuwa katika mali yake anayoyapenda zaidi (shamba liitwalo) “Baiyrahaa” na ilikuwa mbele ya Msikiti (wa Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam)), na alikuwa Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) anaingia ndani yake na kunywa maji yake mazuri. Basi ilipoteremka Aya:

             آل عمران: ٩٢

“Hamtaweza kuufikia wema khasa mpaka mtowe katika vile mnavyovipenda”.


Akasimama Abu Talhah akasema: Ewe Mtume wa Allah, asema Mola Subhanahu Wataala : “Hamtaweza kuufikia wema khasa mpaka mtowe katika vile mnavyovipenda” na kwa hakika katika mali yangu niyapendayo zaidi ni Baiyrahaa nayo ni sadaka nimeitoa kwa Allah. Nataraji kupata malipo yake mazuri kwake Mola Subhanahu Wataala, basi yaweke ewe Mtume wa Allah pale anapokuonesha Allah. Akasema Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam): “Bakhin” “Bakhin” (neno hili lasemwa katika kuridhika na kusifu kitu) mali hiyo imepata faida, mali hiyo imepata faida. Na katika hadithi nyingine “mali hiyo inakwenda, mali hiyo inakwenda Peponi”. Na nimesikia uliyoyasema na mimi naona uwape mali hayo jamaa zako, akasema Abu Talhah: Nafanya hivyo Ewe Mtume wa Allah akayagawa Abu Talhah baina ya jamaa zake na watoto wa Ami yake. Na huu mfano ni wa juu kabisa katika kutoa mali.


Na kama alivyofanya katika wafuasi wa hao (Masahaba) Imamu wetu Muhammad bin Abdullah Al-Khaliliy -Allah (Subhanahu Wataala) Amrehemu- naye alikuwa miongoni mwa matajiri katika zama zake na akafa naye haoni kuwa Dunia hii ina thamani yoyote. Mali yake yote ameitoa kwa kuitia nguvu Dola ya Kiislamu (yeye ndiye Imamu au Khalifa wa Dola hiyo hapa Oman) akafa naye apendwa na raia zake na apendwa na Mola wake na wala hakudhurika kwa kutokuacha kitu.


Inasemekana kuwa anaependa kuiendea Akhera basi na atangulize mali yake huko kwa kuitoa katika njia ya kheri.


Na hapana budi katika kutoa mali kuwe na mambo mawili, kwanza niya nzuri (kuwa unafanya hivyo kufuata amri ya Allah na kujikaribisha kwake sio kutaka kusifiwa na watu) na pili kuamini kuwa utalipwa malipo mazuri na Allah (Subhanahu Wataala) na bila ya hayo mawili anakhasiri mtu mali yake na Akhera yake.

Na kuamrishana mema na kukatazana mabaya ni katika mshikamano ulio na nguvu zaidi baina ya Waislamu. Na anayeamrishwa au kukatazwa kitu ijapokuwa atachukiwa wakati huo anapokatazwa na kuona uzito, lakini hatimaye atashukuru wakati atakapoona faida yake katika nafsi yake na jamii yake. Na methali inasema: Kwenye kupambazuka kwa Asubuhi ndio watu waushukuru mwendo wa usiku. Na subira haina budi kwa anayeamrisha na anayeamrishwa na anayekataza na anayekatazwa. Ndiyo maana Allah (Subhanahu Wataala) amemalizia wasiya wa Luqman kwa mtoto wake:


                                          لقمان: ١٧

“Ewe mwanangu! Simamisha Sala, na uamrishe mema, na ukataze mabaya, na usubiri juu ya yale yatakayokusibu.” (Sura Luqman Aya 17).


Na Allah (Subhanahu Wataala) asema:


                                      العصر: ١ - ٣  

“Naapa kwa zama (zako ewe Nabii Muhammad au zama zote tokea mwanzo mpaka mwisho) kuwa Binaadamu yuko khasarani isipokuwa wale walioamini na wakafanya vitendo vizuri, na wakausiana (kufuata) haki na wakausiana (kushikamana) na Subira, (kustahamiliana)”.


Kwa hiyo unaona kuwa hapana budi kuwa na subira katika hali yoyote ile.


Zitatengenea jamii na koo iwapo kutakuwepo na kuamrishana mema na kukatazana mabaya, na huendelea kuwa katika hali hiyo ya kheri madamu wanakutanika juu ya msingi huu (wa kuamrishana mema na kukatazana mabaya). Ama akiachwa anaetaka kufanya mabaya bila kukamatwa mkono wake na kuzuiwa kufanya hivyo hapo ndipo inapo enea balaa kwa wote kwa wale wanaofanya hayo mabaya na vile vile wale wanaonyamaza. Na mfano wao hawa ni mfano wa wale waliopanda jahazi na kisa chao maarufu kilicho tajwa katika Al-Bukhari: “Mfano wa aliesimama kwenye mipaka ya Allah na alietoka nje yake ni kama watu walioingia jahazini kwa kura wengine wakapata kuingia juu na wengine wakaingia chini. Na wakawa wale walio chini wakitoka kuchota maji lazima wawapitie walio juu yao basi wakasema lau kama tungelitoboa hili jahazi tukapata mahitajio yetu bila ya kuwaudhi walio juu yetu. Basi kama wangewaacha, wale walio juu, wafanye watakavyo wangeangamia wote, na kama wangewazuia wasifanye hivyo wangeokoka wao na wakaokoka wote (walio jahazini).”


Na hii ndio shani ya watu ambao hawakatazani mabaya, hakika wataangamizwa wote pamoja kwa haraka au wapewe muda mpaka baadaye.


      ﭿ    ﮁﮂ           المائدة: ٧٩

“Hawakuwa wenye kuzuiana (kukatazana) mambo mabaya waliyokuwa wakiyafanya, uovu ulioje wa jambo hili walilokuwa wakilifanya”.


Na miongoni mwa mambo yanayoleta uadui baina ya jamaa na jirani ni kushindaniana juu ya Dunia na kupenda mali kiasi cha kuingia katika maasi na kutojali njia ya kuipata hiyo mali ijapokuwa njia hiyo inawaudhi jamaa zake au jirani zake na huu ndio umasikini hasa. Amesema Abu Attayyib:

“Anaetumia masaa chungu nzima katika kukusanya mali kwa kuuogopa umasikini basi hivyo alivyofanya ndio umaskini wenyewe”.

Pia amesema:

“Kutajikana kwa mtu ni umri wake wa pili, na anachohitaji ni kiasi anachokula, kutafuta zaidi ni mashughulisho.”

Anasema Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam):

 (من جمع مالا من تهاوش أذهبه الله في نهابر )

“Anaekusanya mali kwa kuchanganya halali na haramu, Allah ataiondoa kwa njia za maangamizo”.


Namuomba Allah Mwenye uwezo wa kila kitu aihami nchi hii (Oman) na kila uharibifu na mharibifu na kila anayeiingia kwa kuitakia ubaya kwa husda na chuki.

Ewe Mola anaeitakia nchi hii au watu wake huo ubaya basi mrudishie ubaya huo mwenyewe na vijaalie vile vitimbi vyake ndio kuangamia kwake. Na hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kwa Allah.


Vile vile kama inavyompasa Muislamu kuamini kufufuliwa inampasa kuamini mauti pia.

Na mauti ni kutoka  roho kwenye mwili (kufarikiana roho na mwili), na kitu hicho chajulikana na Muislamu na kafiri na kila mtu atambua kitu hichi kwa sababu kinampitia kila mtu anapoona watu wanakufa kila siku. Na juu ya haya inabidi kuamini mauti kwa kauli yake Subhanahu Wataala:


      آل عمران: ١٨٥

“Kila nafsi itaonja Mauti”


Kila kitu hakina budi kuwa na mwisho hata visivyo na roho kwa kauli yake Subhanahu Wataala:

          القصص: ٨٨

“Kila kitu kitaangamia isipokuwa yeye Allah”

           

Na sifa yake mauti ni kuonekana Malaika wa Mauti na roho (ya binaadamu) basi mara tu roho inapomuona huyo Malaika wa mauti inavutika kwenda kwake kama namna ya smaku (magnet) inavyovuta chuma. Hivi ndivyo isemwavyo. Na Allah ndiye Mjuzi zaidi (wa kila kitu).


Na katika kaburi, nalo ndio mlango wa mwanzo kuingia Akhera, anajua maiti nini mwisho wake kwani kaburi ima ni bustani katika mabustani ya Pepo kwa Muumini au shimo katika mashimo ya Moto kwa kafiri. Basi anabakia humo kaburini ima katika raha ikiwa ni Muumini au anaadhibiwa ikiwa ni kafiri. Bali kabla ya hivyo kila mmoja katika Muumini na kafiri anajua nini mwisho wake kabla ya kutoka roho yake wakati anapowaona Malaika wamehudhuria kukamata roho yake, kwani wanaikamata roho ya Muumini Malaika wapole wenye huruma, ile kuwaona hao Malaika inamsahilishia Muumini tabu ya Mauti kwa sababu atajua kuwa hataadhibiwa baada ya wakati huu.

Kasema Allah (Subhanahu Wataala):


                ﭧﭨ        ﭬﭭ           يونس: ٦٤

“Wao wana bishara njema katika maisha ya dunia na katika Akhera. Hapana mabadiliko katika maneno ya Mwenyezi Mungu. Huko ndiko kufuzu kukubwa.”


Na wanakamata roho ya kafiri Malaika wakali wenye nguvu wasiokuwa na huruma, na wanain’goa roho yake kwa nguvu na fujo kitu kinachomzidishia maumivu na kukereka na dhiki kwa sababu hapo anajua kuwa yatakayo kuja baada ya mauti yatakuwa ya taabu zaidi kuliko mauti yenyewe.


                                                 الفرقان: ٢٢ - ٢٣

“Siku watakayowaona Malaika haitokuwa furaha siku hiyo kwa waasi, (itakuwa ndio siku ya kutolewa roho zao); na watasema siku hiyo): Mungu atuepushie mbali!. (Lakini haitafaa kitu Dua hiyo). Na tutayaendea yale waliyoyatenda katika amali zao tuzifanye kama mavumbi yaliyotapanywa (yaliyotawanyika)"


Unaona kuwa Allah (Subhanahu Wataala) Amesema juu ya Waumini kuwa watakuwa na furaha (Bushra) na amesema juu ya waasi watakuwa hawana furaha siku hiyo na vitendo vyao vizuri walivyovifanya havitawafaa kitu (vitakuwa bure kwa sababu hawakuwa Waumini). Kasema Allah:


                                                   الأنعام: ١٥٨

 “Siku zitakapo fika baadhi ya Ishara za Mola wako, kuamini hapo hakutomfaa mtu kitu, ikiwa hakuwa ameamini kabla yake, au amefanya kheri katika Imani yake”.


Na wasema wafasiri wa Qur'an katika Aya iliyotangulia maana ya حجرا محجورا  ni kuomba kinga ya kuepushwa na Malaika wa mauti.


Wakati yalipomjia mauti Amru bin Al-Aas mtoto wake Abdullah bin Amru akamwambia: Ewe baba angu ulikuwa wasema: Laiti nimpate mtu mwenye akili anielezee mauti yakoje na sasa wewe ndie yule mwenye akili tuelezee yakoje, akasema: “Naona kama mbingu imebatana na ardhi na najiona kama navuta pumzi kutokana na tundu ya sindano na kama roho yangu inavutwa kutoka mwilini mwangu kama mfano wa sufi inayovutwa kwa nguvu katika miba” au hivyo ni maana ya hadithi hiyo ijapokuwa haikuja kwa lafdhi hiyo. Basi hebu angalia ikiwa roho ya anayempwekesha Allah (Subhanahu Wataala) (Muwahhid) inatolewa hivyo vipi itakuwa roho ya kafiri!!


Twamuomba Allah (Subhanahu Wataala) salama!


Wakati Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) alipokuwa akitokwa na roho yalikuwa maumivu yake yanamzidi akasema: “Hakika mauti yana maumivu makubwa (yana shida)” na akaomba Umma wake upunguziwe maumivu. Allah amjazi kheri kwa kuwaonea huruma Umma wake.


Na hakuna mtu anaejua wapi roho inakwenda baada ya mauti kwani mfano wake ni kama mwangaza wa taa ikizimika haujulikani wapi umekwenda, isipokuwa kwa habari iliyokuja kuhusu roho za Mashahidi (waliokufa vitani) kuwa zitakuwa katika vifua vya ndege wa kijani zilizotundikwa chini ya Arshi na kitu hichi chawahusu Mashahidi tu. Na ni mdhaifu na ni mkosefu wa hima yule anayeiwacha shahada (kufa kwa ajili ya kunyanyua jina la Allah (Subhanahu Wataala)) wakati inapomjia na akayataka maisha ya Dunia.


Na baada ya mauti hakuna budi kufufuliwa na siku hiyo ndio Siku ya Kiyama ambayo imekwisha zungumziwa habari yake. Ama wanyama, wao vile vile watafufuliwa na Allah (Subhanahu Wataala) akishapitisha anachokitaka kwao atawaamrisha wawe udongo:


                                       النبأ: ٤٠

“Hakika tunakuhadharisheni adhabu iliyo karibu kufika, siku ambayo mtu atakapoona yaliyotangulizwa na mikono yake miwili, na kafiri atasema: Laiti ningelikuwa udongo (nisipate adhabu hii inayoningoja sasa). (sura An-Nabaa Aya 40.)


Yaani wakati huo atatamani kafiri awe mnyama kisha ageuke udongo kwa ile shida anayoiona ya siku hiyo na adhabu yake. Lakini atayapata wapi hayo anayoyataka wakati atakuwa amekamatwa vizuri kabisa wala hawezi kuponyoka, haiwezekani kabisa hivyo hakuna kitachomuokoa au kumsaidia siku hiyo. Basi hapo husema:


                                 المؤمنون: ١٠٧ - ١٠٨

“Mola wetu! Tutowe humu (Motoni, uturejeshe tena ulimwenguni, tukafanye amali nzuri) na tufanyapo tena (mabaya) bila shaka tutakuwa madhalimu (wa nafsi zetu kweli kweli). Atasema Allah: Hizikeni humo wala msinisemeshe”.


Twamuomba Allah atuepushe na kila balaa.

Wala hawezi kufa mtu kabla ya kufika muda wake na hawezi kuchelewa hata kidogo ukishamalizika muda wake.


           ﯖﯗ      النحل: ٦١

“Na unapofika muda wao hawawezi kukawilia saa moja wala hawawezi kuutangulia.”


Hapana budi mtu kuimaliza riziki yake aliyoandikiwa na Allah, kwani riziki inamfuata kiumbe kama yanavyomfuata mauti. Kama ingekuwa Allah (Subhanahu Wataala) angeijalia riziki ya kiumbe chake katika jiwe gumu lililothibiti katikati ya bahari basi lingepasuka hilo jiwe ili achukue huyo kiumbe alichojaaliwa katika riziki yake.


Nataja hapa kisa kinachohusu riziki ya mtu kuwa haiwezi kumkosa. Tulikuwa tuko njiani tunakwenda Makka na gari yetu inakwenda kama upepo, kutahamaki ghafla ikatusimamikia tukateremka na baadhi yetu wakenda kukidhi haja zao. Kulikuwa na wadi sehemu hiyo nikalikuta battikhi (tikiti) limeiva nikalichuma na nikarudi nalo garini tukalikata kisha tukalila na hapo gari ikawashwa na ikafanya kazi. Hakuna kilichoifanya isimame wenyewe isipokuwa ile riziki tuliyoandikiwa mahala hapo.


Masikini wakati alipokhadaika Al-Hajjaj bin Yusuf Athaqafiy na utawala wake akasema: ‘Hakika Allah ametutosheleza riziki  yetu na akatukalifisha vitendo (tufanye amali), laiti angetutosheleza amali na akatukalifisha riziki.’ Sababu ya kusema hivi alipoona mali nyingi ilioko chini ya milki yake katika Beit Al-Maal akadhania kuwa mali hiyo ameipata kwa nguvu yake na ujanja wake. Na hakuna ajabu, amemtangulia kwa msimamo huo kabla yake Qaaruun aliposema:


               القصص: ٧٨

“Hakika nimepewa haya kwa sababu ya elimu niliyonayo”.


Na Allah Akamjibu:


                                           القصص: ٧٨

“Je hakujua ya kwamba Allah amewaangamiza kabla yake watu waliokuwa wenye nguvu zaidi kuliko yeye na wenye mkusanyo mwingi zaidi (kuliko wake yeye)?.”


Wanasema Muutazila kuwa alieuliwa amekufa kabla ya kumalizika muda wake, nayo ni rai potofu iliyo wazi upotofu wake.


Na ni wajibu kuiamini Hisabu nayo ni kufananua vitendo (amali) vya waja kuvijua viovu na vilivyo vyema. Na hisabu sio kama hisabu wanayoijuwa watu bali kama anavyoitaka Allah (Subhanahu Wataala):

              النحل: ١١١

“Wakumbushe siku ambayo kila nafsi itakuja kujitetea”.

           

Inafahamika kutokana na Aya hii kuwa wataachiwa kuzungumza lakini bila ya faida yoyote (bila ya mazungumzo hayo kusaidia kitu). Na Attirmidhiy ametoa:

( لا تزول قدما عبد يوم القيامة حتى يسأل عن أربع: عن عمره فيم أفناه؟ وعن علمه ما عمل به؟  وعن ماله من أين اكتسبه؟ وفيم أنفقه ؟ وعن جسمه فيم أبلاه؟ )

 “Haunyanyuki mguu wa mja Siku ya Kiyama mpaka aulizwe juu ya mambo manne: juu ya umri wake ameutumia katika nini? Na juu ya elimu yake ameifanyia nini? Na juu ya mali yake ameipata wapi na vipi ameitumia? Na juu ya mwili wake ameuchakaza wapi?”


Inasemekana kuwa binaadamu Siku ya Kiyama atatolewa vitabu vitatu:

Kitabu ndani yake vimeandikwa vitendo vizuri.

Kitabu zimeandikwa ndani yake dhambi zake.

Kitabu zimeandikwa ndani yake neema za Allah juu yake.


Hapo Allah (Subhanahu Wataala) huiambia ile neema ndogo kabisa katika kitabu cha neema: chukua thamani yako katika vitendo vyake vizuri. Na inachukua na kuvimaliza vitendo vyote vizuri. Kisha inasema (hiyo neema): Naapa kwa Nguvu zako bado sijatosheka (yaani nimevimaliza vitendo vyote vizuri na bado thamani yangu imebakia) basi hapo zitabakia dhambi na neema. Vitendo vizuri vyote vimekwisha chukuliwa na ile neema moja tu. Basi Allah akitaka kumrehemu mja wake husema: Ewe mja wangu nimekuzidishia mema yako na nimekusamehe maovu na nimekugaiya au nimekutunukia neema zangu.


Na hisabu watahusika nayo wale waliokasoro kufanya mema na hatimaye wakatubia na pia wale mafasiki waliofanya madhambi makubwa. Na hekima katika kuvihisabu vifungu viwili hivi ni kumfanya yule Muumini aliekasoro katika amali (vitendo vizuri) aijue neema ya Allah juu yake katika kumghufuria madhambi yake na kumstiri aibu zake. Na hekima ya kumfanyia hisabu fasiki ni kumfanya azidi majuto kwa kuacha kufanya vitendo vizuri kwani wakati anapoona vitendo vyake alivyovifanya ambavyo vingeweza kuwa sababu ya kumghufuria madhambi vimefutwa na vitendo vingine viovu alivyovifanya basi huzidi huzuni na majuto.


Vile vile hekima katika kuwafanyia hisabu viumbe vyake ni kuonesha uadilifu wake kwa viumbe vyake, kwa kuwa yeye hawadhulumu watu kitu lakini watu wenyewe ndio wanaojidhulumu nafsi zao (kwa kufanya maasi). Na wasiokuwa katika vikundi viwili hivi wao ama wataingizwa Peponi bila ya hisabu na hao ndio waumini waliotekeleza wajibu wao, au wataingizwa Motoni bila ya hisabu na hao ni washirikina. (Haya yamo katika kitabu cha “Bahjat Al-Anwaar”)


Na ni wajibu kuamini kuweko kwa Pepo na Moto na kuwa ndio makazi ya viumbe vyake Subhanahu Wataala katika majini na binaadamu. Nayo ni malipo yao kwa waliyofanya Duniani watakaa humo milele bila ya kuwa na mwisho (atakayefanya mema ataingizwa Peponi na atakaemuasi Allah ataingizwa Motoni). Amezieleza Mola Subhanahu Wataala sehemu mbili hizi maelezo ambayo hayawezi kuzidishwa tena juu ya hayo katika kauli yake mnamo sura ya Assafat alipo wataja waja wake wema:


           ﯡﯢ                                                                              ﯿ                       

الصافات: ٤١ – ٤٩

“Hao ndio watakaopata riziki maalumu, Matunda ya kila namna, na watahishimiwa, katika bustani za neema wako juu ya vitanda, (viti vya enzi) vya fahari, wamekabiliana (wanazungumza) wanazungushiwa gilasi zenye (vinywaji) safi, vyeupe vyenye ladha kwa hao wavinywao, kwa vinywaji hautakuwa udhia wala kuondokwa na akili, na pamoja nao watakuwa wanawake wenye heshima hawatizami isipokuwa waume zao tu na wenye macho mazuri makubwa (safi) wanawake hao kama mayai  yaliyohifadhika.”

           

Mpaka Akasema:


                                                                                                                 الصافات: ٦٢ - ٦٨

“Je, karibisho la namna hii silo bora au kupata mti wa Zakkum (mti mchungu kabisa watakaolishwa watu wa Motoni). Kwa yakini sisi tumeufanya ni adhabu ya hao madhalimu wa nafsi zao. Hakika huo ni mti unaotoka (unaota) katikati ya Jahannam. Panda za matunda yake (zinatisha) kama kwamba ni vichwa vya mashetani. Bila shaka wao watakula katika mti huo, na kwa huo wajaze matumbo yao, kisha bila shaka utawathibitikia (juu ya uchungu wa mti huo) mchanganyiko wa maji ya Moto. Halafu, kwa yakini, marudio yatakuwa huko huko kwenye Jahannam, (hawana mahala pengine).”


Na vile vile Allah amesema katika sura ya Al-Waqia:


                                                                                                                                                                                         ﭿ                                                                                                                                                                                                                                                 ﯿ                                                                                                                         الواقعة: ١٠ - ٥٦

“Na walioko mbele kabisa (katika kheri), nao ndio walioko mbele; hao ndio watakaokaribishwa (kwa Allah) katika bustani zenye neema. Sehemu kubwa (katika hawa) ni miongoni mwa (watu) wa mwanzo (huko). Na sehemu ndogo ni miongoni mwa (watu) wa mwisho. Watakuwa juu ya viti vya fahari vilivyotonewa (vilivyotiwa mapambo). Wataviegemea waelekeane (wanazungumza). Wawe wanawazungukia wavulana, (watumishi watoto wanaume) walio daima na sura za ujana za kupendeza kwa vikombe na mabirika, na gilasi za vinywaji vinavyotoka katika mito inayoonekana kwa mapitio yake. Hawaumwi na vichwa kwa (kuvinywa vinywaji) hivyo wala hawatatokwa na akili. Na matunda (namna kwa namna) kama watakayopenda. Na nyama za ndege kama watakavyotamani (wenyewe). Na wanawake wenye macho mazuri na makubwa (ya vikombe), (wanapendeza na safi) kama kwamba ni lulu zilizofichwa (kwenye chaza yake, ndio kwanza zinapasuliwa). Ni jaza ya hayo waliyokuwa wakiyatenda, hawatasikia humo maneno ya upuuzi wala maneno ya dhambi, isipokuwa maneno ya usalama na amani. Na wale watu wa kheri nao; watakuwa namna gani watu hao wa kheri! (watakuwa) katika vivuli vya mikunazi isiyo na miba, na migomba iliyopangiliwa uzuri. Na (katika) vivuli vyengine vilivyonyooka kila upande, na maji yanayomiminika kwa vizuri. Na matunda mengi (ya kila aina). Hayatindiki, (hayakatiki) wala hayakatazwi (kwa kuwa si yake tu huyu au yanamdhuru). Na wanawake watukufu; (hawa waliokuwa nao Duniani). Tutawaumba kwa umbo (bora zaidi). Na tutawafanya bikra (vijana kama kwamba ndio kwanza wanaolewa). Wanapendana na waume zao (walio) hirimu moja nao, (yote haya yatafanywa) kwa ajili ya watu wa kheri. Sehemu kubwa katika hawa watu wa kheri ni miongoni mwa (watu) wa Umma za mwanzo na sehemu kubwa pia ni miongoni mwa (watu) wa mwisho (wa huu Umma wa Nabii Muhammad). Na watu wa shari (waovu); watakuwa namna gani hao watu wa shari! (Watakuwa) katika upepo wa Moto na maji yachemkayo, na kivuli cha moshi mweusi sana, si cha kuleta baridi wala si cha starehe. Bila shaka wao walikuwa kabla ya haya wakiishi maisha ya anasa, na walikuwa wakishikilia, (wakiendelea) kufanya madhambi makubwa, na walikuwa wakisema; ‘Tutakapokufa na tukawa udongo na mifupa, ndio tutafufuliwa? (uongo huo). ‘Au wazee wetu wa zamani (ndio watafufuliwa pia?).’ Sema: ‘Bila shaka wa kwanza na wa mwisho, watakusanywa kwa wakati uliowekwa katika siku maalum. Kisha nyinyi, mliopotea (na) kukadhibisha kwa yakini mtakula mti wa Zakkum. Na kwa huo mtajaza matumbo yenu, na juu yake mtakunywa maji Moto yanayochemka. Tena mtakunywa kama wanywavyo ngamia wenye kiu sana, (na kila wakinywa kiu haiweshi).’ Hiyo ni karamu yao siku ya malipo.” (sura Al-Waaqia Aya 10-56)

           

Na ni wajibu kuamini kuweko kwa Hodhi nalo ni Hodhi la Mtume Muhammad (Salallahu Alayhi Wasalam) lilioko katika msimamo wa Siku ya Kiyama ambalo wataliendea Waumini na katika hadithi :

( حوضى مسيرة شهر وزواياه سواء وماؤه أبيض من اللبن وأحلى من العسل وريحه أطيب من المسك وكيزانه كنجوم السماء ومن شرب منه لا يظمأ أبداً ولا يسود وجهه أبداً )

 “Hodhi langu (lina umbali wa) mwendo wa mwezi na pande zake (vile vile mwendo wa mwezi) sawa na hivyo. Na maji yake ni meupe kuliko maziwa na matamu kuliko asali na harufu yake nzuri kuliko miski na makopo yake kama nyota mbinguni  na anaekunywa ndani yake hapati kiu milele na wala uso wake hauwi mweusi milele”.


Na watafukuzwa baadhi ya watu watakaokuja kunywa ndani yake basi atawaona Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) na hatapendezewa kufukuzwa kwao na atasema: Masahaba zangu, Masahaba zangu na ataambiwa: Hakika wao wamebadilisha (mambo ya Dini) baada yako (kuondoka kwako) basi hapo akasema: Potoleeni mbali poteleeni mbali. Na kwa hayo inatudhihirikia kuwa haiwezekani kunywa katika hodhi hilo isipokuwa yule alietekeleza Dini ya Allah na akafa yungali katika hali hiyo.

Vile vile inapasa kuamini kuweko kwa mizani nayo ni kwa maana ya Uadilifu (haki) na usawa na sivyo kama wanavyosema wengine kuwa maana yake ni hii mizani ya kawaida tunayoijua, yaani nguzo na mikono yake miwili, na kuwa Allah anaisimamisha Siku ya Kiyama na juu yake vitapimwa vitendo vya waja, na yule ambaye vitendo vyake vyema vitakuwa vizito zaidi kuliko vitendo vyake viovu basi ataingia Peponi ama yule ambaye mkono wa vitendo vyake viovu utakuwa mzito zaidi kuliko mkono wa vitendo vyake vyema ataingia Motoni; haya hayakuthibiti katika dalili yoyote, na uzito au wepesi wa mizani ulioelezwa hapa maana yake ni kuokoka na adhabu ya Motoni (na kuingia Peponi) au kuangamia yaani kuingia Motoni. Na utumiaji wa neno “mizani” kimethali ni maarufu kwa Warabu; mmoja wao asema:


“Lau wangewaweka baba zangu katika mizani yao wangeinamisha mizani kwa uzito na baba yako akanyanyuka nayo kwa wepesi”


Na Allah (Subhanahu Wataala) Asema:


                  الأنبياء: ٤٧

“Nasi tutaweka mizani za uadilifu Siku ya Kiyama”

           

Unaona hapa kuwa Uadilifu umewekwa badala ya (mahala pa) Mizani siyo kutowa wasifu wake (Mizani). Na vitendo vya waja ni “Aaraadh” yaani unavifikiria akilini lakini huwezi ukavishika au ukaviona kwa hiyo ni muhali kuvipima katika mizani (Kitabu “Bahjat Al-Anwaar”).


Na vile vile inatuwajibikia kuamini kuweko kwa الصراط  kwa mujibu wa kauli ya Mola Subhanahu Wataala:


                                 الملك: ٢٢

“Je! Anayekwenda akisinukia kwa uso wake ni muongofu au anayekwenda katika njia iliyonyooka?”.


Na ni Yeye Mola aliyemuamrisha mja wake aseme:


       الفاتحة: ٦

“Niongoze njia iliyonyooka”.


Nayo (hiyo الصراط ) ina maana ya haki na huwakilisha hali mbili za mtiifu na anayeasi na pia huwakilisha hali za wale wanaokwenda na kufuata njia zilizo baina ya aliyepewa tawfiiq na aliyekosa hiyo tawfiiq, na wala sivyo wanavyodai baadhi ya watu kuwa الصراط  ni daraja limewekwa juu ya mapana ya Jahannam. Na masuala mawili haya (“Sirat” “Mizan”) sio katika masuala yenye dalili zisizo shaka (za wazi na uhakika) ambayo hayafai kuhitilafiana juu yake; bali kila mtu aweza kufasiri namna yake. Sio kama masuala ya kumuona Allah (Subhanahu Wataala) na kutoka Motoni kwa waliokufa katika maasi (bila ya kutubu) na kupata Uombezi kwa aliyekufa naye yungali afanya madhambi makubwa (Al-Kabair), kwani masuala haya matatu haiwezekani kuhitilafiana juu yake kwa sababu haki iko kwa mmoja tu, naye ni yule anayesema: Allah (Subhanahu Wataala) haonekani, na anayeingia Motoni hatoki humo (hukaa humo milele) na kuwa Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) hamuombei isipokuwa anayemcha Allah. Na dalili za masuala haya matatu zimekwisha zungumzwa kwa kirefu katika kitabu hiki kutoka kwa Sheikh Ahmed bin Hamed Al-Khalily – Allah ampe afya. Amin.


Na nimeona katika kitabu: “Bahjat Al-Anwaar” cha Sheikh wetu Noor Din, Allah amrehemu, ametowa hadithi ndefu asema: Na katika athari kuwa Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) alikaa juu ya membari yake Salallahu Alayhi Wasalam kisha akasema:

(الصلاة جامعة –رحمكم الله – ثم قال يا عباس عم رسول الله ويا فاطمة بنت محمد ويا آل محمد جميعا إني والذي نفسي بيده عند ربي لمطاع مكين فلا تغرن امرءا نفسه يقول أنا عم رسول الله صلى الله عليه وسلم أو تقول بنت محمد أو من آل محمد اشتروا أنفسكم من الله فإنكم إن لم تفعلوا هلكتم مع من عرفتم هلاكه ، إني على الحوض يوم القيامة فارط (اي متقدم ) فيرد علي أناس من أصحابي ليحتلقن نقرة رأسه ثم لآخذن بحجزته فأقول: أرسلوه إنه من أصحابي فيؤخذ بيدي فكاكا، أرسل، أرسل، فإنه والله ما مشى من بعدك قدما ولكنه مشى القهقهري، ليدخل جهنم، فلا أستطيع شيئا، فالحذر الحذر يا آل محمد إني والله لا أغني عنكم من الله شيئا)

 “Njooni kusanyikeni katika Sala, Allah awarehemu. Kisha akasema: Ewe Abbas Ammi wa Mtume wa Allah, na ewe Fatima binti Muhammad na enyi watu (jamaa) wa Muhammad nyote, kwa yakini mimi, naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko katika mikono yake, mbele ya Mola wangu ni mwenye kutiiwa na mwenye kuwezeshwa, basi isije ikamdanganya mtu nafsi yake, akasema: Mimi Ami wa Mtume wa Allah Salallahu Alayhi Wasalam au aseme mimi binti Muhammad au katika watu (jamaa) wa Muhammad. Zinunuweni nafsi zenu kutoka kwa Allah (kwa kufanya mema na kumtii) kwani hakika nyie ikiwa hamtafanya hivyo mtaangamia pamoja na wale mnaowajua kuangamia kwao (katika mushrikiin na wanafiki). Mimi nitakuwa katika hodhi Siku ya Kiyama nimetangulia (huko hodhini) watanijia watu katika masahaba zangu kisha atanijia mtu namjua naye ni miongoni mwa masahaba zangu na kisha atachukuliwa mikononi mwangu kwa nguvu (kwa kubabaduliwa) huku ikisemwa: mwache, mwache kwani yeye wallahi hakwenda baada yako kimbele mbele lakini amekwenda (baada ya kufa kwa Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam)) kinyume nyume (ameacha kufuata Dini ya Allah) basi na aingie Jahannam, basi siwezi (kuwasaidia) kitu kwa hiyo tahadharini, tahadharini enyi jamaa wa Muhammad kwa sababu hakika mimi Wallahi siwezi kuwafaa kitu mbele ya Allah (Subhanahu Wataala).”


Na uombezi aliopewa peke yake Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) sio wa kuwaombea watu waingizwe Peponi bali ni wa kuwaokoa watu na shida (hali ngumu sana) ya msimamo wa Siku ya Kiyama na Uombezi huo ndio unaojulikana kwa jina la الشفاعة العظمى  yaani Uombezi Mkuu, na kwa jina la المقام المحمود  yaani Kisimamo Kisifiwacho, wakati wanaposhindwa Mitume kuufanya huo Uombezi hapo atasimama Bwana wao Muhammad Salallahu Alayhi Wasalam akisema: Huo ni wangu mimi, huo ni wangu mimi (yaani mimi nitaufanya Uombezi huo).


Na haya yaliyotajwa katika mlango huu ndio yanayompasa Muislamu kuyaamini kwani huo ndio ukweli wa Imani na nguzo zake.


Twamuomba Allah (Subhanahu Wataala) atuwafikishe kufanya kila anachokipenda na anachokiridhia. Amin

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.