Tuesday, 19 January 2016

Jezuu 7 Zaka------Kujenga uongofu katika nyoyo za vijana-----




            

           ﭖﭗ  ﭘﭙ                                                                 ﭷﭸ            البقرة: ١ - ٥

“Alif Laam Miym. Hiki ni kitabu, kisichokuwa na shaka ndani yake, ni uongozi kwa wamchao (Allah). Ambao huyaamini yasioonekana (maadamu yamesemwa na Allah na Mtume wake) na husimamisha Sala na hutoa katika tuliyowapa. Na ambao wanaamini yaliyoteremshwa kwako na yaliyoteremshwa kabla yako na wanaamini (kuwa iko) Akhera. Hao wako juu ya uwongozi utokao kwa Mola wao, na hao ndio wenye kuongoka”.



Zaka ni nguzo katika nguzo tano za Kiislamu nazo: Shahada, Sala, Zaka, Saumu na Hija kwa mwenye uwezo.

Inasemekana kuwa Zaka imefaridhishwa katika mwaka wa pili wa Hijra baada ya kufaridhishwa Zaka ya Fitri. Pia imesemwa imefaridhishwa kwa ujumla huko Makka (yaani kabla ya mwaka wa pili wa Hijra) na kwa ufafanuzi zaidi katika Madina.

Maana yake kilugha ni kukuwa na kuzidi. Ama maana yake kisheria ni kile kinachotolewa katika mali au wanyama kwa mpango maalumu na kupewa watu mahsusi (mafakiri, maskini na wale wanaokusanya Zaka n.k.)




Amesema Sheikh Noor Addin Allah amrehemu:

Anasema Allah Mtukufu:


                ﮢﮣ             ﮧﮨ        التوبة: ١٠٣

“Chukua Sadaka katika mali zao, uwasafishe kwa ajili ya hizo (sadaka zao) na kuwataja kwa vizuri (mbele yangu) na uwaombee Dua. Hakika kuwaombea kwako kutawapa utulivu (watengenekewe); na Allah ndiye asikiaye na ajuwaye”.


Basi kama isingekuja katika fadhila ya kutoa Zaka isipokuwa Aya hii tu ingetosha kwa sababu imekusanya (Aya hii) baina ya faida mbili kubwa kwa mtoaji Zaka:


Ya kwanza: Kuwa inamsafisha na madhambi.

Ya pili: Kustahiki kuombewa Dua na Mtume Salallahu Alayhi Wasalam kwa kuitoa hiyo Zaka na hiyo ipo katika kauli yake Subhanahu Wataala وصل عليهم  na uwaombee Dua, na hii ndiyo tafsiri ya Ibn Abbas.


Amesema Asshaafiiy: Na katika sunna kuwa Imam akipokea sadaka kutoka kwa mwenye kuitoa hiyo sadaka amuombee:

  آجرك الله فيما أعطيت وبارك لك فيما أبقيت  “Allah akulipe kwa ulichokitoa na akubarikie kwa ulichokibakisha.


Na imepokewa kutoka kwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam kuwa amesema:

 ( حصنوا أموالكم بالزكاة وداووا مرضاكم بالصدقة واستدفعوا أنواع البلايا بالدعاء )

Hifadhini mali zenu kwa Zaka na wagangeni wagonjwa wenu kwa sadaka na jiepusheni na kila aina ya balaa kwa Dua.”


Na amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :

 (ما نقص مال من صدقة ، وما تواضع عبد إلا رفعه الله بها عزا)

“Haipungui mali kwa (kutoa) sadaka, wala hawi mja mnyenyekevu (kwa Waislamu wenzake) isipokuwa Allah humpandisha kwa huo (unyenyekevu wake) akawa na heshima (na nguvu mbele ya watu)”


Na amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :

 ( من أدى الزكاة وأقرى الضيف وأدى الأمانة فقد وقي شح نفسه )

“Mwenye kutuo Zaka na kumkirimu mgeni na kuhifadhi Amana basi ameepushwa na ubakhili wa nafsi yake”.


Na amesema Salallahu Alayhi Wasalam:

( عليكم بالصدقة فإن فيها ست خصال ثلاث في الدنيا وثلاث في الآخرة فأما التي في الدنيا فتزيد في الرزق وتكثر المال وتعمر الديار وأما التي في الآخرة فتستر العورة وتصير ظلا فوق الرؤوس وتكون ستراً من النار )

“Shikilieni kutoa sadaka kwani ina faida sita, tatu (hupatikana) Duniani na tatu Akhera. Ama zilizo Duniani, huzidisha riziki na hukuza mali na huimarisha majumba, na ama zilizo Akhera, husitiri utupu na hugeuka kivuli juu ya vichwa na huwa sitara ya Moto”.


Baadhi ya Wenye Hikima wamesema: Hakika katika sadaka kuna faida chungu nzima katika hizo Duniani na nyinginezo Akhera.


Ama zilizo katika Dunia:

1. Hifadhi ya mali kwa mujibu wa kauli yake Salallahu Alayhi Wasalam:

Hifadhini mali zenu kwa Zaka حصنوا أموالكم بالزكاة

2. Kutahirisha kwa mwili kwa mujibu wa kauli ya Allah Subhanahu Wataala:


                ﮢﮣ             ﮧﮨ        التوبة: ١٠٣

“Chukua Sadaka katika Mali zao, uwasafishe kwa ajili ya hizo (sadaka) na kuwataja kwa vizuri (mbele yangu) na uwaombee Dua. Hakika kuwaombea kwako kutawapa utulivu (watengenekewe) na Allah ndiye asikiaye na ajuaye”.


3. Inaingiza furaha kwa masikini miongoni mwa walioamini.

4. Baraka katika Mali na huzidisha riziki kwa kauli yake Subhanahu Wataala:


        ﯿ    ﰁﰂ                سبأ: ٣٩

“Na cho chote mtakachotoa basi yeye (Mola) atakilipa, naye ni mbora wa wanaoruzuku.”


5. Inaepusha balaa na maradhi kwa mujibu wa kauli yake Salallahu Alayhi Wasalam:  داووا مرضاكم بالصدقة    wagangeni wagonjwa wenu kwa sadaka.


Na ama zilizo katika Akhera:

Inakuwa kwa mwenye kuitoa, kivuli kinamfunika na shida ya joto na humfanyia hisabu ikawa nyepesi na humzidishia uzito wa mizani na humpandishia daraja katika Pepo. Na kama ilivyokuwa fadhila zake ni kubwa vile vile kuna maonyo makubwa kwa mwenye kuwacha kuitoa. Allah Subhanahu Wataala ameiweka pamoja na Sala katika sehemu mbali mbali katika Qurani. Na akatoa maonyo makali kwa mwenye kuiwacha kwa hiyo haifai kuiwacha wala kuifanyia upuzi kwani kuipuuza kuitoa mwishoe hufikishia katika kuiwacha kabisa. Kwa kuwa anaekaribia mahala palipohadharishwa huenda akaingia ndani yake.


Anasema Allah Subhanahu Wataala :


                                                   ﮙﮚ                                  التوبة: ٣٤ - ٣٥

“Na wale wakusanyao dhahabu na fedha wala hawazitoi katika njia ya Allah, wape habari za adhabu inayoumiza (inayowangoja). Siku (mali zao) yatakapotiwa Moto katika Moto wa Jahannam, na kwa hayo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao, (na huku wanaambiwa): Haya ndiyo (yale mali) mliojilimbikiza (mliojikusanyia) nafsi zenu, basi onjeni (adhabu ya) yale mliyokuwa mkikusanya”.


Na anasema Subhanahu Wataala:


                فصلت: ٦ - ٧

“Na adhabu itawapata wanaomshirikisha (Allah) ambao hawatoi Zaka”.


Basi adhabu imejaaliwa kwao kwa sababu ya kuacha kutoa Zaka kama ilivyojaaliwa kwao kwa kumshirikisha Allah.


Amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :

 ( يكون كنز أحدكم يوم القيامة شجاعاً أقرع يفر منه صاحبه وهو يطلبه حتى يلقمه أصابعه )

“Itakuwa hazina ya mmoja wenu Siku ya Kiyama jichatu (shujaa) lililokuwa halina nywele kichwani kwa wingi wa sumu yake na umri wake mrefu basi huyo sahibu wake atalikimbia na yeye atamkimbiza mpaka amtie vidole vyake kinywani”.


Na amesema  Mtume Salallahu Alayhi Wasalam:

 ( ما من رجل لا يؤدي زكاة ماله إلا جعل الله له يوم القيامة في عنقه شجاعا ثم قرأ علينا مصداقه من كتاب الله :                              ﯽﯾ  ﯿ                     ﰂﰃ            ﰉﰊ         ﰎﰏ           آل عمران: ١٨٠

“Mtu yeyote asiyetowa Zaka Allah atamwekea shingoni mwake jichatu (shujaa) Siku ya Kiyama. Kisha akatusomea katika Kitabu cha Allah Aya inayosadikisha hayo:-


“Wala wasione wale ambao wanafanya ubakhili katika yale aliyowapa Allah katika fadhila zake kuwa ni bora kwao (kufanya ubakhili huo). La, ni vibaya kwao, watafungwa kongwa (madude ya kunasa shingoni) za yale waliyoyafanya ubakhili, siku ya kiama. Na urithi wa Mbingu na Ardhi ni wa Allah. Na Allah ana khabari za yote mnayoyafanya”.


Na amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :

 ( ما من صاحب ذهب ولا فضة لا يؤدي منها حقها إلا إذا كان يوم القيامة صفحت له صفائح من نار فأحمي عليها من نار جهنم فيكوى بها جنبه وجبينه وظهره كلما بردت أعيدت له في يوم كان مقداره خمسين ألف سنة حتى يقضي بين العباد فيرى سبيله)

 “Mtu ye yote mwenye dhahabu au fedha na hatoi haki yake (yaani hailipii Zaka)  Siku ya Kiyama atachomwa na sahani za Moto. Zinapashwa Moto (hizo sahani) na Moto wa Jahannam kisha aunguzwe nazo mbavuni mwake na kipajini mwake na mgongoni mwake. Na kila zikipata baridi zinachochewa tena katika siku iliyo na kadiri ya miaka elfu khamsini (atakuwa katika hali hiyo) mpaka Allah Subhanahu Wataala amalize kuwahukumu waja wake kisha atizame nini la kumfanya. Akaambiwa ewe Mtume wa Allah: Je Ngamia? Akasema:

 ( ولا صاحب إبل لا يؤدي منها حقها إلا إذا كان يوم القيامة بطح لها بقاع قرقر أوفر ما كانت لا يفقد منها فصيلا واحداً تطأه بأخفافها وتعضه بأفواهها كلما مر عليه أخراها رد عليه أولاها في يوم كان مقداره خمسين ألف سنة حتى يقضي بين العباد فيرى سبيله )

“Wala mwenye ngamia asietoa haki yao Siku ya Kiyama ataangushwa katika ardhi tambarare laini na watamjia hao ngamia wote bila ya kukosekana mmoja (katika hao aliokuwa hakuwatolea Zaka) na watamkanyaga kwa miguu yao na watamn`gata kwa midomo yao kila akimpitia wa mwisho wao humrudia wa mwanzo wao katika siku yenye kukadiriwa miaka elfu khamsini mpaka Allah Subhanahu Wataala amalize kuhukumu waja wake kisha atizame nini la kumfanya.”


Akaulizwa: Ewe Mtume wa Allah Je n`gombe na mbuzi akasema:

 ( ولا صاحب بقر ولا غنم لا يؤدي منها حقها إلا إذا كان يوم القيامة بطح لها بقاع قرقر لا يفقد منها شيئاً ليس فيها عقصاء ولا جلحاء ولا عضباء تنطحه بقرونها وتطأه بأظلافها كلما مر عليه أخراها رد عليه أولها في يوم كان مقداره خمسين ألف سنة حتى يقضي بين العباد فيري سبيله )

“Wala mwenye n’gombe wala mbuzi hatoi haki yao (hawalipii Zaka)  Siku ya Kiyama ataangushwa katika ardhi tambarare laini na hatampotea mmoja katika hao (n’gombe na mbuzi isipokuwa watahudhuria katika uwanja huo) hamna kati yao wenye pembe za kusokotana wala wasiokuwa na pembe wala wenye pembe zilizokatika watampiga kwa mapembe yao na kumkanyaga kwa kwato zao kila akishamaliza kumpitia wa mwisho wao hurudi wa mwanzo wao katika siku yenye kukadiriwa miaka elfu khamsini mpaka Allah Subhanahu Wataala amalize kuhukumu waja wake kisha atizame nini la kumfanya.”


Akaulizwa Ewe Mtume wa Allah Je farasi? Akasema: “Farasi watatu, yuko farasi alie kwa sahibu yake (bwana wake) ni mzigo wa madhambi, na farasi ni sitara kwa bwana wake na farasi anampatia bwana wake malipo mazuri. Ama yule alie mzigo wa madhambi ni yule ambaye bwana wake amemfunga kwa kujionesha au kwa kujifaharisha na ni uadui juu ya Waislamu. Na yule mwenye kumsitiri bwana wake ni yule ambaye bwana wake amemfunga kwa njia ya Allah kisha hakusahau haki ya Allah Subhanahu Wataala (Zaka) kwa anachombebesha juu ya mgongo wake au shingo yake (mali anayoipata huitolea Zaka). Ama yule (farasi) anayempatia bwana wake thawabu ni yule anayemtoa kwa Waislamu ili kupigana kwa njia ya Allah (Jihadi) na kumfunga malishoni au katika bustani basi huwa hali hapo malishoni au bustanini au kitu cho chote isipokuwa huandikiwa (huyo mwenye kumtoa huyo farasi kwa ajili ya Allah) idadi ya anachokila thawabu na aandikiwa idadi ya vinyesi vyake na mikojo yake thawabu. Na wala hakati kamba yake akalishia katika mnyanyuko au minyanyuko miwili isipokuwa huandikiwa idadi ya athari ya alichokula na alichokunywa thawabu, wala bwana wake hakumpitisha mtoni akanywa ndani yake wala hakutaka kumnywesha isipokuwa Allah humuandikia (huyo mwenye farasi) idadi ya alichokunywa thawabu.”


Akaulizwa: Ewe Mtume wa Allah Je Punda? Akasema: Hakuteremsha Allah kitu kuhusu Punda isipokuwa Aya hii yenye kukusanya maana kubwa:


                               الزلزلة: ٧ - ٨

“Basi anayefanya wema hata kiasi cha uzito wa mdudu chungu ataona jaza yake. Na anayefanya uovu hata wa kiasi cha uzito wa mdudu chungu ataona jaza yake”.


Nasema: Siku hizi gari zimechukua mahala pa farasi basi na ifuatwe hiyo migawanyiko mitatu waliopewa farasi. Na Allah hakifichiki kitu kwake.


Na iliyotolewa ni sehemu ndogo ya malipo makali atakayopata mwenye kuacha kulipa Zaka na iwapo atatubu kwa Allah na akarudi kwake basi inamlazimu alipe Zaka zote alizoacha kulipa kwa mujibu wa kauli sahihi iliyo kwa Sheikhe wetu Noor Addin Allah amrehemu akisema: Zimejengwa ruhusa juu ya msingi wa kurahisisha mambo na kutoa habari njema (kuwapa moyo wa kupata malipo mazuri),  na Rehema za Allah Subhanahu Wataala zimeenea na msamaha wake mkubwa.


Mali zinazowajibika kutolewa Zaka ni dhahabu, fedha, biashara na mifugo kama ngamia, ng’ombe, mbuzi na kondoo na masharti yake ni kufika “nisaab” (kiwango maalumu) na kutimiza mwaka mzima baada ya kutimia “nisaab”.




Inamuwajibikia Muislamu Zaka katika aina mbali mbali ya mali yake kama dhahabu na fedha ni sawa sawa iwapo ni pesa au mapambo au mapande ya maadini hayo yahifadhiwayo au deni amemkopesha mtu (mali ya Muislamu yaliyoko kwa mtu mwingine yahisabiwa katika kutoa Zaka).


Inawajibika Zaka katika biashara aina yoyote ya biashara hata ikiwa ya mchanga.

Hakuna budi kuweka mwezi maalumu wa kuilipa Zaka na bora kuwa mwezi wa Ramadhani kwa sababu malipo katika mwezi huu huongezwa na unaweza ukachagua mwezi wo wote mwingine.



Iwapo kwa mfano mwezi aliouchagua mtu wa kulipa Zaka ni mwezi wa Ramadhani, basi ahisabu mwisho wa Shaabani pesa zote alizoziweka (savings) na zile alizozitia katika biashara ikiwa zimetimia mwaka au hazikutimia ni juu yake kutizama mali yote aliyonayo katika mwezi aliouchagua kutoa Zaka azitolee Zaka ikiwa zimefika “Nisaab” (kiwango maalumu ambacho ni wajibu mali kuitolea Zaka ikiifikilia).


Na “Nisaab” ni mithqaal ishirini ya dhahabu au mithqaal mia mbili ya fedha ikifika hapo basi ni wajibu kuitolea Zaka na hutolewa robo ya moja kwa kumi (1/40) yaani 2.5% (asilimia) ya mali hiyo iliyotimia kiwango hicho maalumu kilichotajwa hapo juu kisha hutolewa kwa wowote katika watu wa namna nane zilizotajwa na Allah Subhanahu Wataala katika Aya ya Zaka katika sura ya Attawbah:


                                ﮰﮱ       ﯕﯖ          التوبة: ٦٠

“Sadaka hupewa (watu hawa): Mafakiri na Masikini na wanaozitumikia na wanaotiwa nguvu nyoyo zao juu ya Uislamu na katika kuwapa Uungwana watumwa na katika kuwasaidia wenye deni na katika kutengeneza mambo aliyoamrisha Allah na katika kupewa wasafiri (walioharibikiwa). Ni faradhi inayotoka kwa Allah, na Allah ni mjuzi na mwenye hikima.”


Na Zaka ya Riyali (currency) zitumikazo baina ya watu katika nchi hutolewa (Zaka yake) ifikapo thamani yake sawa na mithqaali 20 ishirini ya dhahabu au sawa na mithqaali 200 mia mbili ya fedha (hiyo “Nisaab” ifikapo kwa kila 100 mia hutolewa  2.5 mbili na nusu).

Namna ya 3 na ya 4 za Zaka hazikabidhiwi kwa watu binafsi bali kwa Maimamu (wanaotawala kwa Sharia ya Kiislamu).

           

Na akipata mali, ijapokuwa nyingi, baada ya kupita mwezi aliouchagua kutoa Zaka kwa mfano imemuingilia mali hii katika Shawwaal na mwezi wake wa kutoa Zaka ni Ramadhani basi hatazitolea Zaka pesa hizi ikiwa zitamtoka kabla ya mwezi wa Ramadhani ufuatao.


Na pia haitolewi Zaka milki yoyote aliyonayo mtu kama nyumba, gari n.k (possessions) isipokuwa kama inatumiwa kibiashara yaani ikiwa anunua nyumba au gari kisha auza.


Vile vile ikiwa dhahabu peke yake haitimii “nisabu” (kiwango cha Zaka) isipokuwa ikichanganywa na fedha hutimia basi na zichanganywe. Kama mfano ikiwa Muislamu ana mithqaali 10 kumi za dhahabu (nusu ya nisabu) na ana mithqaal 100 mia za fedha (nusu ya nisabu) basi azichanganye zitimie nisabu kisha atoe katika hiyo “Nisaab” robo (¼) ya moja katika kumi (1/10) yaani 2.5% asilimia.


Na katika biashara inahisabiwa mali yote (aina yote ya mali) iliyotiwa ndani yake inachanganywa yote pamoja na itakapojulikana hisabu yake na itolewe 2½% asilimia Zaka. Na vile vile katika mapambo yanapimwa kila mwaka na kutolewa Zaka yake robo ya moja kwa kumi yaani asilimia 2.5%.

           

Vile vile inabidi kuchaguliwa mwezi maalumu wa kutoa Zaka ya wanyama kama ngamia, ng’ombe, mbuzi na kondoo, wachanganywe waume kwa wake na wadogo kwa wakubwa, mbuzi kwa kondoo kwani wao ni aina moja (jinsi moja) na n’gombe kwa nyati vile vile wao ni katika jinsi moja.


Anatolewa Zaka kwa kila mbuzi arubaini mbuzi mmoja na katika kila ngamia watano mbuzi mmoja wasiyetumiwa kwa kazi (waitwao “sawaim”) hivyo ni kwa mujibu wa hadithi ya Anas: Alikuwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam achukua sadaka (Zaka) katika ngamia, ng’ombe na mbuzi wakiwa hawatumiwi kwa kazi wanalishia katika nyasi zilizoruhusiwa kwa watu wote (mali ya jamii) kwa muda wa mwaka mzima.


Na Zaka ya ngamia na n’gombe kila watano hutolewa mbuzi mmoja, na wakiwa kumi hutolewa mbuzi wawili, na kumi na tano hutolewa mbuzi watatu, na ishirini hutolewa mbuzi wane, na watakapofika ishirini na tano hutolewa ngamia mke bint Makhaadh (na huyo ni mtoto wa kike wa ngamia umri wake mwaka mmoja). Na anaetaka maelezo kwa kirefu na atizame katika vitabu vya fiqh. Na majina ya ngamia yatafuatiana na majina ya ngo’mbe.


Na hakuna Zaka kwa wenye makwato kama farasi, punda na nyumbu na wala watumwa kwa mujibu wa hadithi:

 (عفى عن أمتي زكاة الخيل والبغال والحمير )

“Umesamehewa Umma wangu Zaka ya farasi, nyumbu na punda.”


Na hadithi nyingine:

( ليس على المسلم صدقة في عبده ولا فرسه )

“Muislamu si juu yake kutoa Sadaka (Zaka) ya Mtumwa wake na farasi wake.”


Na ama mazao na nafaka (kama ngano, mtama, maharage) Zaka ya vitu hivi haifungamani na muda wa mwaka bali yatolewa katika (wakati wa) mavuno kwa mujibu wa kauli yake Subhanahu Wataala:


         الأنعام: ١٤١

“Na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake.”


Na ni wajibu kutoa Zaka ya tende ikifika uzito wa mazao ya mitende Manni 160 mia na sitini (kila manni 1 ni sawa na kilogram 4 nne). Ikifika uzito huu basi itolewe Zaka sehemu moja kwa kumi yake. Ikiwa ni tende mbivu (inayotiwa katika madebe) au tende kavu au nyingineyo isipokuwa ikiliwa mbichi (ratab) hiyo haina Zaka. Lakini ikiwa hiyo tende mbichi (ratab) itaanikwa juani na kushindiliwa na kuuzwa kwa pesa basi itatolewa Zaka hiyo thamani yake sehemu moja kwa kumi (1/10), ikiwa hiyo mitende yatiliwa maji kwa mifeleji au haitiliziwi maji kabisa. Lakini ikiwa hiyo mitende yatiliziwa maji kwa wanyama (ngamia, n’gombe n.k) basi hutolewa Zaka nusu ya sehemu moja kwa kumi (½ ya 1/10) kwa sababu njia yake hiyo ina mashaka (yaani namna ya kutilia maji). Vile vile zabibu hufuatia njia hiyo ya tende katika kutoa Zaka.


Zaka ya Nafaka ni Kama Ifuatavyo:

Ngano, shairi, adesi, mahindi, ufuta, mtama, kunde, maharage, mbaazi, mchele na kila kiliwacho katika nafaka zinazoliwa.

Amesema Sheikh wetu Noor Addin Assaalmiy:

Wala hakuna Zaka kwetu (kwa mujibu ya maarifa yetu) isipokuwa kwa hivyo vilivyotajwa kwa makubaliano ya Umma.

Na hivyo vilivyotajwa (nafaka) vyote vyawajibika kutolewa sehemu moja kwa kumi (Zaka) vikitimia kiwango cha “Nisaab”, nayo ni pishi mia tatu, na nadhani pishi moja ni sawasawa na kilogram mbili kwa mujibu wa elimu yangu, na waulizwe wanavyuoni kuhakikisha zaidi juu ya hilo.


Kitu cha kuzingatia na cha msingi kinachobainisha vinavyolazimika kutolewa Zaka ni kuwa kila kiliwacho na kuweza kuhifadhiwa kama tende, zabibu, ngano n.k. (hivi hutolewa Zaka) ama tikiti (batikhi) na viazi, hivi kwa sababu haviwezi kuhifadhiwa havina Zaka na vinginevyo vilivyofanana na hivi na vile vile viko vyakula ambavyo havitegemewi katika maisha ya watu yaani watosheka bila ya kuvipata kama matunda yote kwa sababu yanaliwa kwa kujifurahisha wakati yapatikanapo na kama zaituni na nazi ambazo zinatumiwa kama viungo katika chakula (vyaongezwa katika chakula kuongeza ladha).


Tizama Ukarimu wa Allah Subhanahu Wataala juu yako, amekupa vingi na ameridhika kutoka kwako kwa kidogo ili kukujaribu juu ya utiifu wako kwake na juu ya yote hayo manufaa yarudi kwako wewe mwenyewe yeye hahitajii utiifu wako:


            ﮪﮫ                   فاطر: ١٥

“Enyi watu! Nyinyi ndio wenye haja kwa Allah, na Allah Mkwasi (na nyinyi hakuhitajieni), asifiwaye (kwa neema zake juu ya viumbe vyake vyote)”


                     ﯭﯮ            البقرة: ٢٤٥

“Na nani atakayemkatia Allah sehemu bora ya mali yake (kwa kuwapa masikini na kwa kutoa katika mambo mengine ye kheri) ili Allah amzidishie mzidisho mwingi, na Allah ndiye anayezuia na ndiye anayetoa, na kwake (nyote) mtarejea.”


    ﭿ                                    ﮍﮎ           ﮒﮓ        البقرة: ٢٦١

“Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika njia ya Allah Subhanahu Wataala ni kama mfano wa punje moja iliyotoa mashuke saba; ikiwa katika kila shuke pana punje mia. Na Allah Subhanahu Wataala humzidishia amtakaye, zaidi kuliko hivi; na Allah Subhanahu Wataala ni mwenye wasaa mkubwa na mwenye kujua.”


                                                       ﭧﭨ           البقرة: ٢٦٥

“Na mfano wa wale wanaotoa mali zao kwa kutafuta radhi ya Allah na kujithibitisha nafsi zao katika Dini yake, ni kama mfano wa bustani iliyo mahali pa juu, ikaifikia mvua kubwa na ikaleta mazao yake mara mbili na zaidi (kuliko ada yake); na kama haifikiwi na mvua kubwa basi mvua ndogo (huitosheleza) na Allah anayaona mnayoyatenda.”


         ﭦﭧ                 ﭮﭯ         ﭳﭴ          البقرة: ٢٧١

“Kama mkitoa sadaka kwa dhahiri ni vizuri; na kama mkitoa kwa siri na kuwapa mafakiri, basi huo ni ubora zaidi kwenu; na atakuondoleeni (sehemu ya) maovu yenu (mkifanya hivyo); na Allah anazo habari za (yote) mnayoyatenda.”


            ﮈﮉ              ﮏﮐ                         البقرة: ٢٧٢

“Na mali yoyote mtakayoyatoa ni faida kwa nafsi zenu. Wala msitoe ila kwa kutafuta radhi ya Allah. Na mali yoyote mtakayoyatoa mtarudishiwa kamili (thawabu zake) wala hamtadhulumiwa.”


                                       البقرة: ٢٧٤

“Wale watowao mali zao usiku na mchana, kwa siri na dhahiri, wana ujira wao kwa Mola wao; wala haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika”.


Na kuhusu Zaka ya Fitri tumekwisha izungumzia katika jezuu ya sita ya kitabu hichi.

           


Sadaka

Amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam:

 ( تصدقوا ولو بشق تمرة تكنون به وجوهكم عن النار )

“Toweni sadaka ijapokuwa nusu (ubale) ya tende muzihifadhi nyuso zenu na Moto (wa Jahannam)”


Na imesimuliwa:

( تصدقوا ولو بظلف محرق )

“Toweni sadaka ijapokuwa ukwato wa mbuzi uliounguzwa”


Na imesimuliwa:

( تصدقوا ولو بتمرة ، فإنها تسد من الجائع وتطفئ الخطيئة كما يطفئ الماء )

“Toweni sadaka ijapokuwa kwa chembe moja ya tende kwa sababu inasaidia kuondoa njaa na inazima kosa kama maji yanavyozima (Moto)”


Na imesimuliwa:

)ما من عبد يتصدق بصدقة من كسب طيب ولا يقبل الله عز وجل إلا طيبا إلا كان على الله عز وجل يأخذها فيربيها كما يربي أحدكم فصيله وفي رواية مهره ، حتى تبلغ الثمرة مثل أحد)

 Hakuna mja yeyote anayetoa sadaka kwa mali yake halali na Allah Subhanahu Wataala hapokei isipokuwa kilichokuwa kizuri (halali) isipokuwa Allah mwenye nguvu mtukufu huipokea kisha akailea kama anavyomlea mmoja wenu ngamia wake mchanga au katika hadithi nyengine “farasi wake mchanga” hata tunda moja likafika ukubwa wake kama Mlima wa Uhud.”


Amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam kumwambia Abi Addardaa:

 ( إذا طبخت مرقة فأكثر ماءها ثم انظر أهل بيت من جيرانك فأصبهم منه بمغروف )

“Ukipika mchuzi, uongezee maji mengi kisha uangalie waliomo katika nyumba ya jirani uwapelekee utacho chota katika huo mchuzi.”


Na akasema Salallahu Alayhi Wasalam:

 ( ما أحسن عبد الصدقة إلا أحسن الله عز وجل له الخلافة على  تركته )

“Hakuna mja atoa Sadaka vizuri isipokuwa Allah Subhanahu Wataala anamtizamia vizuri atakavyoviacha baada yake (watoto na mali yake).”


Na akasema Salallahu Alayhi Wasalam:

 ( الرجل في ظل صدقته يوم القيامة حتى يقضى بين الناس )

“Mtu atakuwa katika kivuli cha sadaka yake Siku ya Kiyama mpaka watakapo hukumiwa watu.”


Na akasema Salallahu Alayhi Wasalam:

 ( الصدقة تسد تسعين باباً من الشر )

“Sadaka inafunga milango tisini ya shari.”


Amesema Salallahu Alayhi Wasalam:

 ( ما المعطي من سعة بأفضل أجراً من الذي يقبل من حاجة )

“Hapati, mwenye kutoa (sadaka) katika wasaa (neema), malipo bora zaidi kuliko anayepokea (sadaka) katika haja (shida).”


Amesema Salallahu Alayhi Wasalam:

 ( أفضل الصدقة أن تتصدق وأنت صحيح شحيح تأمل البقاء وتخشى الفاقة ولا تمهل حتى إذا بلغت الحلقوم قلت لفلان كذا ولفلان كذا ولفلان كذا وقد كان لفلان )

“Sadaka iliyo bora zaidi ni ile unayoitoa ungali katika hali ya afya na ubakhili unategemea kuishi na unaogopa umasikini wala usingojee mpaka roho ifike kooni (wakati wa kukata roho) useme: cha fulani kiasi hichi, cha fulani kiasi hichi, cha fulani kiasi hichi, na hali kishakuwa cha fulani.”


قال صلى الله عليه وسلم : تصدقوا

Amesema Salallahu Alayhi Wasalam: “Toweni Sadaka.”

 ( فقيل : عندي دينار قال : لنفسك )

Akaambiwa! Nina Dinari, akasema: hiyo ni yako mwenyewe.

 ( قيل : وآخر قال : أنفقه على زوجتك )

Akaambiwa: Je nyingine (dinari) akasema: Itowe kwa matumizi ya mke wako.

 ( قيل: وآخر قال : أنت أبصر به )

Akaambiwa: Je nyingine akasema: Wewe unajua zaidi wapi pa kuitumia.


Amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :

 ( ردوا مذلة السائل ولو بمثل رأس الطائر من الطعام )

“Ondoa madhila ya muombaji (kwa kumpa) chakula ijapokuwa kama mfano wa kichwa cha ndege (uwingi wake).”


Amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :

( لا تقطعوا المسألة حتى تفرغ ثم ردوا بوقار ولين، أو ببذل يسير أو برد جميل فإنه قد يأتيكم ملك ينظر كيف  صنعكم فيما خولكم الله )

 “Msikatize muombaji maneno yake mpaka amalize kisha mjibuni kwa upole na hishima au kwa msaada kidogo au kwa jibu zuri kwani huenda akawajieni Malaika kutizama mnafanya nini kwa alichowapa Allah Subhanahu Wataala.”


Akasema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam:

( ولو صدق السائل ، ما أفلح من رده )

"Ikiwa muombaji ni mkweli hatofuzu yule aliyemrudisha (asimpe kitu)."


Amesema Issa AS:

 ( من رد سائلاً خايباً لم تغش الملائكة بيته الذي هو فيه سبعة أيام وقيل يوماً )

“Mwenye kumrudisha muombaji mikono mitupu basi hawataingia Malaika nyumba yake anayoishi muda wa siku saba, na imesemwa ni siku moja”.


Na alikuwa Mtume wetu Salallahu Alayhi Wasalam anaweka maji yake ya kutawadhia usiku kwa mkono wake na kuyafunika na huwapa masikini.

Na Malaika huja usiku kuomba kama (mfano wa) binaadamu na wakipanda huulizwa na Malaika wenzao: Je mmeona vipi? Basi hujibu: fulani karimu na wao husema: Ewe Mola mghufirie, Ewe Mola mruzuku, Ewe Mola mbarikie na umkinaishe. Na hujibu (vile vile) fulani bakhili, hatoi (kusaidia muhitaji) ni mkali wa maneno. Basi humuombea: Ewe Mola mfanyie kitu fulani. (jambo lisilo zuri).


Amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :

( ليس المسكين من ترده التمرة أو التمرتان واللقمة واللقمتان إنما المسكين المعفف اقرأوا إن شئتم : لا يسئلون الناس إلحافاً )

 “Sio masikini yule inayomrudisha tembe moja ya tende au tembe mbili na tonge moja (ya chakula) au tonge mbili lakini masikini ni yule anayejizuia kuomba.”


Someni mkitaka (kauli ya Allah) :


      البقرة: ٢٧٣

“Hawaombi watu wakafanya ung’ang’anizi.”


Na amesema Salallahu Alayhi Wasalam:

 (ما من مسلم يكسو مسلماً إلا كان في حفظ الله تعالى ما دامت منه رقعة )

“Hakuna Muislamu amvikae (nguo) Muislamu (mwenziwe) isipokuwa huwa katika hifadhi ya Allah madamu kimebakia japo kiraka cha hiyo nguo katika mwili wake.”


Na amesema Salallahu Alayhi Wasalam :

 ( الصدقه تقي مصارع السوء وترفع ميتة السوء )

“Sadaka inaepusha maafa yanayohilikisha na inazuiya kifo kibaya.”


Amesema Salallahu Alayhi Wasalam :

 ( نفقة الرجل على أهله صدقة )

“Matumizi ya mtu kwa ajili ya ahli yake (mkewe na watoto wake nyumbani) ni sadaka.”


Amesema Salallahu Alayhi Wasalam:

 ( من أطعم مسلماً تمرة أطعمه الله من ثمار الجنة ومن سقاه جرعة سقاه الله من الرحيق المختوم)

“Mwenye kumlisha Muislamu tembe moja ya tende Allah atamlisha katika matunda ya Peponi na mwenye kumnywisha chubuo (la maji) Allah atamnywisha katika (hodhi la) Rahiiq Al-Makhtuum.”


Na amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :

 ( إنما المسكين الذي لا يجد غني يغنيه ولا يفطن له فيتصدق عليه ولا يقوم فيسأل الناس )

“Kwa kweli maskini ni yule ambaye hapati cha kumtosha haja yake wala hatambulikani hata akapewa sadaka wala hapiti kuomba watu.”


Na amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :

 ( من أنفق زوجين نودي في الجنة : يا عبد الله : هذا خير ، و يدعى المتصدق من باب الصدقة  والمصلي من باب الصلاة ، والصايم من باب الريان ويدعى الواحد منها جميعا، ورجا رسول الله صلى الله عليه وسلم أن يدعى أبو بكر رضي الله عنه منها جميعاً )

 “Anaetoa (sadaka) vitu viwili (kama viatu au chakula akatoa kwa mfano unga na samli au mchele na nyama) huitwa katika Pepo: Ewe mja wa Allah : Hii kheri, na aitwa anaetoa sadaka katika mlango wa sadaka na mwenye kusali kwenye mlango wa Sala na mwenye kufunga kwenye mlango wa Rayyan, na anaitwa mwingine kwenye milango yote hiyo na akatarajia Mtume Salallahu Alayhi Wasalam kuwa Abu Bakr RA ataitwa kwenye milango yote hiyo.”


Na mwenye kutoa sadaka kisirisiri atakuwa katika kivuli cha Al-Arshi siku ambayo hapatakuwa na kivuli isipokuwa kivuli chake.


Na ilipoteremka kauli ya Allah Subhanahu Wataala :


                             ﭛﭜ         البقرة: ٢٢٥

“Allah hatakushikeni kwa sababu ya kuapa kwenu kwa upuzi – upuzi. Bali atakushikeni kwa sababu (ya vile viapo) vilivyofanyiwa nguvu na nyoyo zenu. Na Allah ni mwingi wa kusamehe (na) Mpole sana.  (Sura ya Al-Baqara Aya 225)


Na kauli yake Subhanahu Wataala:


                                        الحديد: ١١

“Ni nani atakaye mkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema, ili amrudishie mardufu, na apate malipo matukufu.”


Akasema Abu Addahdaah:

Nawatoa mhanga kwa ajili yako baba yangu na mama yangu ewe Mtume wa Allah, atukopa sisi Allah naye hana haja na sisi?

Akasema Salallahu Alayhi Wasalam:  Ndio, (kwa sababu) ataka kuwaingiza Peponi.

Akasema : Je! Nikimkopesha Mola wangu atanipa dhamana ya (kuingia) Pepo?

Akajibu Salallahu Alayhi Wasalam : Ndio anayetoa sadaka basi hupewa huko Peponi mfano wa hiyo sadaka aliyoitowa.

Akasema : Na mke wangu Um Addahdaah yu pamoja na mimi (katika Pepo)

Akajibu Salallahu Alayhi Wasalam : Ndio

Akasema : Na binti yangu Addahdaah yu pamoja na mimi (katika Pepo)

Akajibu Salallahu Alayhi Wasalam : Ndio

Akasema : Mimi ninazo bustani mbili (mashamba mawili) moja katika hizo iko chini katika mitende ya Madina na nyingine iko juu, na Wallahi sina nyinginezo nizitoe mkopo kwa Allah Mtukufu.

Akasema Salallahu Alayhi Wasalam: Ijaalie moja katika hizo ya Allah Subhanahu Wataala na nyingine kwa maisha yako na ya watoto wako.

Akasema : Basi shuhudia ewe Mtume wa Allah kuwa nimeijaalia ya Allah iliyo bora katika hizo mbili ni ukuta kuna ndani yake mitende mia sita.

Akasema Salallahu Alayhi Wasalam : Basi Allah atakulipa Pepo kwa hiyo bustani kisha akasema: Makole mangapi mazito ya tende makole mangapi makubwa (ya tende) na nyumba (ngapi) zenye manukato mazuri za Abi Addahdaah huko Peponi!.


Amesema Adhahaak : Anaetoa sadaka dirham moja kwa kutaka radhi ya Allah basi atalipwa dirham mia saba Duniani na dirham milioni moja Siku ya Kiyama.


Amesema Abu Huraira: Tulikuwa twahisabu wakati Mtume Salallahu Alayhi Wasalam yuko baina yetu : matumizi ya mtu kwa nafsi yake na kwa wenzake na kwa kipando chake (farasi n.k) katika Jihadi hupata mara milioni mbili zaidi ya alivyotoa.


Amesema Urwah bin Azzubair :

Hakika Aisha RA alitoa sadaka dirham khamsini elfu na hali nguo yake ina kiraka.


Na kutokana na Mujaahid kuwa kauli ya Allah:


                 الإنسان: ٨

“Na huwalisha chakula masikini na mayatima na wafungwa (mateka), na hali ya kuwa wenyewe wanakipenda (chakula hicho).”


Yaani amesema Mujaahid nao wanakitamani hicho chakula.

Na kutokana na Omar RA alikuwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam asema : Ewe Mola ijaalie fadhila (mali na utajiri) kwa walio bora wetu ili wairejeshe kwa wenye haja katika sisi.


Na amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :

 ( بعض الصدقة تبلغك نصف الطريق والصوم يبلغك باب الملك)

"Baadhi ya sadaka inakufikisha nusu ya njia na Saumu inakufikisha kwenye mlango wa Mfalme (Allah Subhanahu Wataala )."


Na amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :

( بعض الصدقه تفك لحيي سبعين شيطاناً وفضل سرها علانيتها بسبعين ضعفاً )

"Baadhi ya sadaka inafungua matama ya mashetani sabini (ikiwa midomo yao wazi kwa jinsi wanavyoudhika mtu akitoa sadaka) na fadhila (ubora) ya sadaka ya kificho juu ya sadaka ya uwazi ni mara sabini."


Na kutokana na Ibn Masoud : Kuwa mtu mmoja ameabudu Allah Subhanahu Wataala miaka sabini kisha akazini basi amali ikaporomoka (ikaharibika) halafu akampitia masikini akampa sadaka ya kipande cha mkate basi Allah Subhanahu Wataala akamghufuria dhambi zake na akamrudishia amali zake za miaka sabini.


Na amesema Luqman kumwambia mtoto wake: -

Ukifanya kosa basi toa sadaka.


Na mwingine akasema:

Sijui chembe iliyo na uzito wa milima ya Dunia isipokuwa chembe ya sadaka.


Na wamesema :

Kuficha sadaka ni katika hazina za Pepo na matumizi yako kwa watoto wako ni sadaka.


Na alikuwa Ibn Omar anatoa sadaka ya shukrani (kumshukur Allah Subhanahu Wataala kwa neema zake juu yake).

Kwa mujibu wa kauli yake Subhanahu Wataala:


             آل عمران: ٩٢

“Hamtaweza kuufikilia wema khasa mpaka mtowe katika vile mnavyovipenda.”


Na baadhi wametoa sadaka ya kisima kwa ajili ya kupata malipo mazuri, yaliyokuja katika Aya hii.

Na watafufuliwa watu hali wana njaa bila ya kiasi basi alielisha (watu na masikini hasa) kwa ajili ya Allah Subhanahu Wataala basi Allah atamshibisha (siku hiyo) na anaenywisha kwa ajili ya Allah kadhalika Subhanahu Wataala atamnywisha (siku hiyo). Angetaka Subhanahu Wataala angewafanya watu wote matajiri lakini amewafanya matajiri na masikini kwa kuwafanyia mtihani.


Na kutokana na Ashshaabiy: Yule asiyejiona nafsi yake kuwa ana haja zaidi ya thawabu ya sadaka yake anayoitoa kuliko haja ya fakiri kwa hiyo sadaka yake basi huyo ameiharibu sadaka yake na hupigwa nayo usoni mwake.


Amesema Al-Hussein kumwambia mtu aliempitia pamoja na kijakazi wake : Je  unaridhika kwa thamani yake dirhamu moja au mbili. Akasema : Hapana. Akamwambia : nenda kwani Allah Mtukufu ameridhika kwa thamani ya “Huur Aliin” (wanawake wa Peponi) kwa pesa moja au tonge moja.

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.