ﭽ
ﯦ ﯧ
ﯨ ﯩ ﯪﯫ
ﯬ ﯭ ﯮ
ﯯ ﯰ ﯱﯲ
ﯳ ﯴ ﯵ
ﯶ ﯷ ﯸ
ﯹ ﯺﯻ ﯼ
ﯽ ﯾ ﯿ
ﰀ ﰁ ﰂ
ﰃﰄ ﰅ ﰆ
ﰇﰈ ﰉ ﰊ
ﰋ ﰌ ﰍ ﭑ ﭒ
ﭓﭔ ﭕ ﭖ
ﭗ ﭘﭙ ﭚ
ﭛ ﭜ ﭝﭞ
ﭟ ﭠ ﭡ
ﭢ ﭣ ﭤ
ﭥ ﭦ ﭧ
ﭨ ﭩ ﭪﭫ
ﭬ ﭭ ﭮ
ﭯ ﭼ الأنعام:
١٠٠ - ١٠٣
“Na (juu ya hivi) wamemfanyia Allah (Subhanahu Wataala) Majini
kuwa washirika wake, hali yeye ndiye aliyeumba (si majini). Na wamemsingizia (Allah (Subhanahu Wataala) ) kuwa ana
watoto wa kiume na wakike. (wanasema haya) pasipo kujua. Ameepukana (Allah) na upungufu,
na yu juu kuliko yale wanayomsifu nayo”.
“Yeye ndiye
Muumba wa Mbingu na Ardhi. Inamkinikaje awe na mwana, hali hana mke. Naye ndiye
aliyeumba kila kitu. Naye ni mjuzi wa vitu vyote. Huyo ndiye Allah, Mola wenu.
Hakuna anayeabudiwa kwa haki ila yeye, Muumba wa kila kitu. Kwa hivyo,
muabuduni yeye tu, Naye ni Mlinzi wa kila kitu”.
“Macho
hayamfikii (kumuona yaani haonekani) bali yeye anayafikia macho (kuwaona wenye
macho na wasiokuwa na macho). Naye ni mwenye kujua yaliyofichikana na yaliyo
dhahiri”.
Suala:
Sheikhe
wetu mkubwa Mufti Ahmed bin Hamed Al-Khaliliy: Zipi hizo dalili za kiakili na
zilizonukuliwa zinazoonesha kutoonekana kwa Allah (Subhanahu Wataala) katika
Dunia na Akhera.
Jawabu:
Kwa jina la
Allah Mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na Mwenye kuneemesha neema ndogo
ndogo. Shukrani zote anastahiki Allah, Mola wa walimwengu wote na Rehema zake
na Amani zake zimwendee Mbora wa Mitume Bwana wetu Muhammad na ziwaendee jamaa
zake na Sahaba zake wote. Ama baada ya haya. Ni katika mambo yanayojulikana
kabisa kuwa Allah (Subhanahu Wataala) yeye ni kinyume na viumbe vyake vyote
katika sifa zake zote kwani havifanani nae kwa chochote wala yeye (Allah (Subhanahu
Wataala)) Hafanani navyo kwa chochote, basi kwa hivyo Hasifiwi Subhanahu
Wataala kuwa Yeye ni dhati yaani kuwa ni kitu kinachochukua nafasi (جوهر ) (k.m. dhahabu, udongo,
mbao) wala kuwa ni sifa (عرض)
(k.m. rangi, umoto, ubaridi) wala kuwa ni mwili (k.m. kitu hai, gilasi,
karatasi). Wala hasifiki Mola Subhanahu Wataala kuwa amekuweko pahala fulani au
ametokeya wakati Fulani, kwani pahala na nyakati hazina athari kwa Allah (Subhanahu
Wataala) kwasababu Yeye Subhanahu Wataala Yupo kabla ya kuumba wakati na
pahala. Yeye yupo kama alivyotangulia kuwepo haonekani
kwa jicho wala hatafutwi kwa kuulizwa pale alipo.
Basi sifa
zote za viumbe ni muhali kwake Subhanahu Wataala kwa hivyo yabainika kuwa Dhati
yake Subhanahu Wataala (ukweli wake) haiwezi kuonekana kwani haiyumkiniki
kujulikana Subhanahu Wataala kwa jicho wala kwa hisia yoyote (sense) katika
hisia za mwanadamu, kama alivyokuwa muhali kujulikana kwa kumfikiri. Na hakika
kikomo cha mwanadamu kuijua Dhati ya Allah (Subhanahu Wataala) ni kukubali
kwake kushindwa kuitambua (yaani kukubali kwa binaadamu kuwa ameshindwa kumjua
Mola Subhanahu Wataala basi ndio kumjua kwake) kama
ilivyotolewa kutokana na Assidiq RA kuwa amesema:
‘Kushindwa
kumjua (Allah (Subhanahu Wataala)) ndio kumjua’.
Umma wa
Kiislamu umekhitilafiana katika kumuona Mola Subhanahu Wataala, na kauli ya
haki iliyokuwa haina shaka ndani yake ni kuwa Allah (Subhanahu Wataala) haifai
kusemwa kuwa aonekana (au ataonekana) hapa Duniani wala huko Akhera na hayo
ndiyo Aliyoyasema Yeye Mwenyewe Subhanahu Wataala juu ya Nafsi yake, basi
haifai kupinga cho chote Alichokieleza Subhanahu Wataala juu ya Nafsi yake au
juu ya kingine. Bali Anasema Allah (Subhanahu Wataala) katika kujieleza Nafsi
yake:
ﭽ
ﭥ ﭦ
ﭧ ﭨ ﭩ
ﭪﭫ ﭬ ﭭ
ﭮ ﭼ الأنعام: ١٠٣
“Macho
hayamfikilii (kumuona) bali yeye anayafikilia macho (kuyaona na kuwaona hao
wenye macho). Naye ni mwenye kujua yaliyofichikana na yaliyo dhahiri."
Na wale
wanaotaka kuthibitisha kuonekana kwa Allah (Subhanahu Wataala) katika Akhera au
katika Dunia na Akhera wamefasiri neno الإدراك (kufikilia) katika Aya hii kwa maana ya الإحاطة
maana yake “kuzunguka” na hiyo haisihi kabisa kwasababu الإدراك halifasiriwi kwa الإحاطة
kwani huwezi kukuta katika makamusi ya lugha ya kiarabu kuwa “Al-Idrak”
limefasiriwa kwa maana ya “Al-Ihaatah” kama ilivyokuja katika “Al-Qamoos” na
“Sherehi” yake na katika “Lisaan Al-Arab”. Imekuja vile vile katika “Lisaan
Al-Arab” kuwa “Adraktuhu Biayniy” kwa maana nimemuona na hivyo hivyo imekuja
katika sherehi yake katika kitabu hiki cha lugha kikubwa kinachotegemewa na
waarabu wote vipi basi itasemwa kuwa Al-Idraak katika Aya hii imekuja kwa maana
ya Al-Ihaata الإحاطة .
Inasemwa
vile vile “Adraktu hayaat fulaan” na kauli hii inaweza ikatokana na mtu ambaye
hakumwahi mwenzake kutoka mwanzo mpaka mwisho basi vipi liletwe neno la
“Idraak” hali ya kuwa hakuuwahi uhai wake tokea mwanzo mpaka mwisho. Vile vile
husemwa “Adrakahu Assahmu” ikiwa (mtu amelengwa na mkuki) ukamfikia na
kumchoma, kwa hiyo halina maana neno hilo
kuwa mkuki umemzunguka pande zote. Kisha Waarabu waiita mvua isiyokatika:
“Al-Matar Al-Mutadaarik” na maana yake matone yake yameshikana wala haina maana
kuwa kila tone limezunguka matone mengine kitu ambacho hakiwezekani kabisa. Na
Allah (Subhanahu Wataala) amesema juu ya watu wa Motoni:
ﭽ ﭥ ﭦ
ﭧ ﭨ ﭼ الأعراف:
٣٨
“Mpaka watakapokusanyika
wote humo.”
Wala
haikusudiwi kwa “Hattaa Idha iddaarakuu” isipokuwa maana ya kufikiana (au
kukusanyika).
Na upande
mwengine twamuona Mama wa Waumini Aisha RA anakanusha huu mchanganyiko uliopo
katika kuifasiri Aya hii tukufu: Ameitoa Imam Al-Rabii na Mashekhe wawili
(Bukhari na Muslim) na wengineo kwa njia ya Bibi Aisha RA kuwa amesema:-
“Asemaye moja katika mambo matatu amezusha uwongo mkubwa juu ya Allah” Hadithi
hii amesema Masrook kutokana na Bibi Aisha: “Anaesema kuwa Muhammad amemuona
Mola wake basi amemzulia Allah uwongo mkubwa” Akasema Masrook: Na nilikuwa
nimeegemea nikakaa nikasema ewe Mama yangu, nipe wasaa wala usiniharakishe: Je
Hakusema Allah (Subhanahu Wataala):
ﭽ ﮍ ﮎ
ﮏ ﮐ ﭼ النجم:
١٣
“Na hakika
(Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam)) akamuona (Jibril) mara nyingine (kwa sura
ile yake ya ki-Malaika katika usiku wa Miraji)”
Na je
Hakusema Mola Subhanahu Wataala:
ﭽ ﮭ ﮮ
ﮯ ﮰ ﭼ التكوير:
٢٣
“Na hakika
yeye alimuona (Jibril) kwenye upeo wa macho uliosafi wa mbinguni”
Akasema
(bibi Aisha RA):- Mimi ni mtu wa mwanzo katika Umma huu (wa Kiislamu) kumuuliza
Mtume Salallahu Alayhi Wasalam jambo hilo
akasema: Huyo ni Jibril AS sikumuona katika sura yake aliyemuumba nayo Allah (Subhanahu
Wataala) isipokuwa mara mbili. Kisha
akasema (Bibi Aisha RA): Hukusikia kuwa Allah Anasema:-
ﭽ ﭥ ﭦ
ﭧ ﭨ ﭩ
ﭪﭫ ﭼ الأنعام: ١٠٣
“Macho
hayamfikii (kumuona) bali yeye anayafikia macho (kuyaona na kuwaona hao wenye
macho)”.
Jee basi
itafichika kwa Mama wa Waumini Aisha RA maana ya neno “Al-Idraak” kama ingekuwa maana yake ni “Al-Ihaata”? Naye in mwenye
ulimi wa kiarabu na amekulia katika ulezi wa Utume na akanyonya maziwa ya Wahyi
na akafahamu maana ya Qur'ani na maana ya maneno ya waarabu.
Je
inawezekana kuwa itafichika maana ya neno “Al-Idraak” (kufikia) kutokana na
kumbukumbu ya huyu mjuzi mwenye maarifa (Bibi Aisha RA) na waje kujua waliokuja
baada yake kuwa maana yake ni Al-Ihaata (kuizunguka).
Basi Aya
hii tukufu inakanusha kufikia (“Al-Idraak”). Na kufikia katika kila kitu ni kwa
mujibu kilivyo. Kwani kufikia (Idraak) kwa mkono ni kukamata kwake, kufikia
(Idraak) kwa jicho ni kuona kwake, kufikia (Idraak) kwa sikio ni kusikia kwake
na kufikia (Idraak) kwa silaha ni kupata shabaha, na vivyo hivyo inasemwa
kuhusu “Idraak” ya ujumla kuwa maana yake ni kufikia kama vilivyoonesha hivyo
vitabu vya lugha ya kiarabu.
Wako
waliodai kuwa Aya hii tukufu imekusudiwa kukanusha kumuona Allah (Subhanahu
Wataala) katika maisha ya Dunia bila ya maisha ya Akhera. Jawabu la dai hilo ni
kama ifuatavyo: Sifa za Allah (Subhanahu Wataala) hazibadiliki kwani Allah (Subhanahu
Wataala) amejisifu kwa sifa nyingi na amejikanushia Dhati yake iliyotukuka
mambo mengi ambayo hayawafikiani na utukufu wake na ukubwa wake. Mfano wa hayo
kauli yake Subhanahu Wataala katika kujikanushia sifa ya kusinzia na kulala:-
ﭽ ﮫ ﮬ
ﮭ ﮮ ﮯ ﭼ البقرة:
٢٥٥
“Kusinzia hakumshiki wala
kulala”
Na kauli
yake Subhanahu Wataala katika kujikanushia dhulma:
ﭽ ﮗ ﮘ
ﮙ ﮚ ﭼ الكهف:
٤٩
“Na Mola
wako hamdhulumu yeyote”.
Na kauli
yake katika kujikatalia mke na mwana:
ﭽ ﭪ ﭫ
ﭬ ﭭ ﭮ
ﭯ ﭰ ﭱ ﭲ ﭼ الجن: ٣
“Na kwa hakika utukufu wa
Mola wetu umetukuka kabisa, hakujifanyia mke wala mwana.”
Na kauli
yake Subhanahu Wataala katika kujikatalia kuzaa na kuzaliwa:
ﭽ ﭙ ﭚ
ﭛ ﭜ ﭝ
ﭞ ﭟ ﭠ
ﭡ ﭢ ﭣ ﭼ
الإخلاص: ٣ - ٤
“Hakuzaa
wala Hakuzaliwa, Wala hana anayefanana naye hata mmoja”.
Basi je!
Inawezekana kusemwa kuwa mambo
aliyojikatalia Allah (Subhanahu Wataala) nafsi yake mwisho wake ni huu uhai wa
Dunia bila ya kuendelea katika uhai wa Akhera? Na isemwe kuwa Allah (Subhanahu
Wataala) yawezekana kusifika huko Akhera kuwa Anazaa? Anazaliwa? Ana mke?
Adhulumu? Ametukuka Subhanahu Wataala na hayo, na kuwa huko Akhera yuko
aliyefanana naye? Na mengineyo aliyojikanushia Subhanahu Wataala nafsi yake.
Basi hayo yote yatuonesha dalili wazi kuwa Allah (Subhanahu Wataala) Ametaka
kwa kauli yake {لا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ} (kutufahamisha) kujikatalia Nafsi yake kuonekana
katika Dunia na huko Akhera.
Wamedai
baadhi ya wale wanaothibitisha kuonekana kwa Allah kuwa Yeye Subhanahu Wataala
hajisifu kwa kilichokanushwa (لا تدركه
الأبصار) bali
wathibitisha badala yake (hicho kitu alichojikanushia Subhanahu Wataala) kitu
kilichopo. Na ikikanushwa kuonekana kwake Subhanahu Wataala kinakuwa kitu
kisichokuwepo na haiwezekani Allah (Subhanahu Wataala) kujisifu kwa kitu kama hicho. Na wamesema ukweli uliopo ni kuwa Allah
amejisifu Nafsi Yake kwa ukanusho kwa sababu katika kujisifu huku au katika
kujikanushia huku ipo maana nyingine ya kuthibitisha (sifa) wakasema kuwa
makusudio ya kauli yake Subhanahu Wataala:
(لا تأخذه سنة
ولا نوم)
nikuthibitisha sifa ya Usimamizi wa kila jambo, na kusudio la kujikatalia Allah
kuwa na mke na mtoto ni kujithibitishia sifa ya upweke, na kusudio la
kujikatalia kudhulumu ni kujithibitishia uadilifu, na kama hivyo katika
kukanusha kila kinachokanushwa na Dhati Yake Subhanahu Wataala kunakusudiwa
kuthibitisha maana fulani (kama katika maelezo yaliyopita).
Ama
kuonekana kwa Allah (Subhanahu Wataala) (imekuja katika Qur'ani kwa njia ya
kukanushwa) haina (kama mengineyo) maana ya
kuthibitishwa ambayo hujisifu nayo Allah (Subhanahu Wataala) kwa
kujithibitishia Nafsi yake. Hivi ndivyo alivyosema Ibn Al-Qayyim kumfuata
Shekhe wake Ibn Taiymiya.
Na jawabu lake ni
kuwa Allah (Subhanahu Wataala) amejikanushia Dhati Yake yale aliyojikanushia
kwa sababu hayawafikiani na ukubwa wa shani yake, Kibriyaai Yake na Utukufu
wake. Na kama tungelisema kuwa inafaa kuthibitisha yale Aliyojikanushia Subhanahu
Wataala Nafsi yake basi tungelifanya jambo lenye hatari sana na tungeliyakataa maneno ya Allah (Subhanahu
Wataala). Na tafsiri kama hii aliyoitaja Ibn
Al-Qayyim inapelekea kukimbia kutoka mnamo uwazi kwenda kwenye matatizo na
kutoka mnamo uhakika kwenda kwenye njozi.
Na kama tungetaka kumjibu (Ibn Al-Qayyim) kwa njia ile ile
aliyoitumia tungesema:-
Katika
kukanusha kumuona Allah (Subhanahu Wataala) iko mukabili wake maana ya
uthibitisho vile vile nayo ni kusifika Subhanahu Wataala kwa Ukubwa au Utukufu
(Kibriyaau) na (Al-Jalaalu) kwani mkanusho (wa kumuona Subhanahu Wataala)
uliokuja katika Aya hii umekuja katika maonesho ya kuisifu Dhati ya Allah (Subhanahu
Wataala) kwa Ukubwa na Utukufu, vipi tena isemwe kuwa kukanusha kumuona Subhanahu
Wataala ni kitu kisicho na maana hakuna ndani yake kitu cha uthibitisho kinyume
na zile sifa nyingine alizojikanusha nazo. Na mbali ya yote hayo twaziona
hadithi sahihi za Mtume Salallahu Alayhi Wasalam ambazo zinakanusha kuonekana Subhanahu
Wataala, na katika hadithi hizo ni ile aliyoitoa Muslim katika Sahihi yake kwa
njia ya Abi Dhar RA kuwa amemuuliza Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) Je
umemuona Mola wako usiku uliopelekwa “Israa”? Mtume ziwe juu yake bora ya
Rehema na Amani akamjibu “Nuru vipi nimuone?”.
Basi huku
ni kukanusha kwa Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) kumuona Allah (Subhanahu
Wataala) na kama tulivyosema kuwa sifa zake Subhanahu Wataala za Dhati
hazibadiliki kama ilivyokuwa Dhati Yake (Yeye
Mwenyewe Subhanahu Wataala) haibadiliki, basi kwa hivyo hayumkiniki kuonekana
Mola Subhanahu Wataala Duniani wala Akhera.
Vile vile
ziko hadithi nyingine nyingi zinazokanusha kuonekana kwa Dhati Yake tukufu Subhanahu
Wataala. Na licha ya dalili hizo zipo dalili nyingine za kiakili na miongoni
mwa hizo kuwa kitendo cha kuona kunalazimika kuwepo baadhi ya mambo ambayo hayo
hayawezekani kwa Allah (Subhanahu Wataala) kama kuwa kile kitu kinachoonekana
katika mahali fulani na mahali hapo pawe upande uliokabiliana na muonaji, na
kiwe (hicho kinachoonekana) hakikugandana na jicho linalotizama wala kisiwe
mbali nalo umbali mkubwa, na kisiwe mwili uliofichika sana ukawa haunekani kwa
uwezo wa kuona wa kawaida (macho yetu ya kibinaadamu) kama hewa, na kisiwe
kidogo sana, na hiyo inahitilafiana na uwezo wa kuona na mambo mengineyo
yanayopingana na Utukufu wa Allah (Subhanahu Wataala) na Nguvu Yake na Ukubwa
wake.
Ama zile
dalili za kiakili na zilizomo katika Kitabu na Sunna wanazozitumia wanaodai
kuonekana kwa Allah (Subhanahu Wataala) hazikubaliki. Katika dalili za kiakili
walizozitumia kuwa wamesema: Kuwa Allah (Subhanahu Wataala) Yupo na kila
kilichopo kinaweza kuonekana. Maneno haya sio kweli; kwa mfano akili ipo na je
akili ya mtu yaonekana? Na Roho ipo katika mwili je inaonekana? Maneno yapo je
yaonekana? Basi hivyo hivyo vitu vyote vingine visivyoonekana, bali upepo
hauonekani na hali upo. Na wametumia pia dalili za Qur'an na Sunna na katika
hizi kauli ya Allah (Subhanahu Wataala) :
ﭽ ﭙ ﭚ
ﭛ ﭜ ﭝ
ﭞ ﭟ ﭠ
ﭼ القيامة: ٢٢ - ٢٣
“Nyuso nyingine siku hiyo
zitangara kweli kweli. Zitamsubiri Mola wao (Awape rehema zake)”.
Na sisi
tunawaambia kuwa kauli yake Subhanahu Wataala:
Kwanza: وجوه
يومئذ ناضرة chanzo chake ni النضارة kwa
herufi ya ض na
maana yake ni uzuri wa sura (na kun’gara),
إلى ربها ناظرة yaani zinangojea rehema
yake Allah (Subhanahu Wataala) na kuingizwa katika Pepo yake kwa dalili kuwa Subhanahu
Wataala Amesema baada ya hivyo:
ووجوه يومئذ باسرة maana ya باسرة
zitakunjana ambayo inakabiliana na kauli yake Subhanahu Wataala ناضرة kwa
ض .
Kisha akasema تظن أن يفعل بها فاقرة
yaani zinangojea jambo ambalo litakata tindi za migongo yake, na (kauli)
hii ndio inayokabiliana na kauli yake Subhanahu Wataala إلى
ربها ناظرة na kama
ingesemwa kuwa kauli yake Subhanahu Wataala
إلى ربها ناظرة inakusudiwa kuwa hizo
nyuso zitamtazama Allah (Subhanahu Wataala) ingesemwa juu ya hizo nyuso
nyingine (zinazokabiliana na hizi):
ووجوه يومئذ باسـرة عـن
رؤية ربها قاصرة
“Na nyuso
zingine siku hiyo zitakunjika hazitoweza kumuona Mola wake”. Au maneno kama haya yanayoleta kukabiliana kwa maana baina ya watu
hawa na wale.
Wale
waliosema kuwa Allah (Subhanahu Wataala) aonekana na wakatoa Aya hii kuwa
dalili yao wamesema kuwa النظر kama imeletwa kwa maana
ya (الانتظار) ‘kungojea’ basi haiunganishwi na إلى
lakini inaunganishwa na إلى
ikiwa katika maana ya kuona na khasa ikiwa imehusishwa na nyuso. Jawabu
kwa maneno hayo kuwa maneno ya waarabu yapinga hoja hiyo. Huyu Hassan bin
Thaabit asema:
وجوه
يوم بدر ناظرات
إلى الرحمن يأتى بالفلاح
‘Nyuso siku
ya Badri (yaani wenye nyuso) zamngojea Rahmani Alete ushindi’
Na je
walikuwa wakuu wa Waumini katika siku ya Badr wamtizama (wamuone) Allah (Subhanahu
Wataala) wakati mwanashairi aliposema hayo juu yao :
(
و إذا نظرت إليك من ملك و البحر دونك
زدتني نعما )
‘Na ninapokutaraji nawe ni mfalme, na bahari haikufikii kwa
ukarimu, wewe huniongeza neema’
Na asema
mwingine:
(
كل الخلائق ينظرون سجاله نظر الحجيج إلى
طلوع هلال )
‘Viumbe wote wanangoja zawadi zake, kama
mahujaji wanavyongoja kuandama kwa mwezi’
ﭽ ﯭ ﯮ ﯯ
ﯰ ﯱ ﯲ ﯳ ﯴ ﯵ
ﯶ ﯷ ﯸ
ﯹ ﯺ ﯻ
ﯼ ﯽ ﯾ
ﯿ ﰀ ﰁ
ﰂ ﰃ ﰄ
ﰅ ﰆ ﰇ ﭼ
آل عمران: ٧٧
“Hakika wale wanaouza ahadi ya Allah na viapo vyao kwa ajili ya
thamani ndogo ya kilimwengu hao ndio hawatakuwa na sehemu ya kheri katika
Akhera wala Allah hatasema nao (maneno mazuri) wala hatawatazama (jicho la
rehema) siku hiyo ya Kiyama. Wala
hatawatakasa (na madhambi yao )
nao watapata adhabu iumizayo”.
Je makusudi
ya kauli yake Subhanahu Wataala:
ولا ينظر إليهم يوم القيامة ni
kuwa hawaoni (hao watu waovu Siku ya Kiyama) basi atakuwa anawaona baadhi ya
viumbe wake na hawaoni baadhi nyingine? Allah ametukuka na hayo wanayosema juu
yake kutukuka kukubwa. Na hakika makusudio ya kauli yake Subhanahu Wataala hiyo
ni kuwa hao Allah (Subhanahu Wataala) hatawaenezea Rehema Yake Siku ya Kiyama.
Kwa hivyo نظر الله تعالى إلى عبده
ikija kwa njia hii maana yake huwa “Allah kumuenezea Rehema Yake mja
wake” na نظرالعبد إلى ربه و maana yake “Mja kungojea
Rehema ya Mola wake”. Juu ya hivyo kitendo cha kuona hufanyika kwa macho sio
kwa nyuso, basi vipi hapa kinahusishwa na nyuso na kuhusishwa huko na nyuso ni
matumizi ya asli (“Hakika”) au ya kimethali (“Majaaz”)? Na kwa nini
zikahusishwa na nyuso bila ya kuhusishwa na viungo vingine vya mwili juu ya
kuwa kutazama kitu cha kupendeza kwasababisha moyo ufurahike kabla ya uso, na
athari ya kufurahika huku (kwa moyo) inarudisha (furaha hiyo) kwa mwili mzima.
Kwa nini basi nyuso ndizo zinazohusishwa na kutazama? Yote haya yatuonesha kuwa
النظر
katika Aya hii ni kwa maana ya الانتظار
yaani kungojea (sio kutazama au kuona).
Vile vile
wametumia hadithi za Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) dalili ya kuonekana kwa
Allah (Subhanahu Wataala). Zimetolewa hadithi hizi katika Sahihi Bukhari,
Sahihi Muslim na venginevyo zinaonesha kuwa Allah (Subhanahu Wataala)
ataonekana Siku ya Kiyama katika hizo:
Kuwa Mtume
(Salallahu Alayhi Wasalam) amesema: “Mtamuona Mola wenu kama
mnavyouona mwezi usiku wa Badri (mwezi unapokamilika)”.
Nami nataka
kujibu juu ya kutumia hadithi hizi kama dalili
ya kumuona Subhanahu Wataala kuwa kwanza hadithi hizi ni “hadithi Ahaadiya”
(yaani hadithi zilizopokewa kwa njia ya Sahaba mmoja mmoja kutoka kwa Mtume
(Salallahu Alayhi Wasalam). Na hadithi kama
hizi zawajibisha vitendo lakini hazithibitishi elimu. Kwa hiyo mambo ya Itikadi
hayawezi yakajengwa juu ya msingi wa (hadithi hizo za Ahaadiya) kwa sababu
Itikadi inajengwa na hoja zilizo na yakini na hakika wala haijengwi na hoja za
dhana, mbali tena ikiwa hadithi hizo zapingana na hoja za hakika kutokana na
Qur'an na Sunna zilizo na nguvu na makubaliano ya watu wema waliopita. Na licha
ya yote hayo zikichukuliwa hadithi hizi kuthibitisha kuonekana kwa Allah (Subhanahu
Wataala) zitasababisha mpingamano wa hatari na mkubwa sana . Kwani hadithi wanayoitumia sana :
( وإنكم سترون ربكم يوم
القيامة كما ترون القمر ليلة البدر )
“Na hakika mtamuona Mola wenu Siku ya Kiyama kama
mnavyouona mwezi usiku wa Badri (mwezi unapokamilika)”
Wameitoa hadithi hii mashekhe wawili (Al-Bukhari na Muslim) kwa njia ya
Abi Huraira na Abi Saeed Al-Khudry RA. Na
naleta hapa hadithi iliokuwa karibu zaidi na hadithi ya Abi Huraira kimatamko kama ilivyokuja katika Sahihi Muslim: Imekuja katika
hadithi hii kuwa Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) aliulizwa: Je tutamuona Mola
wetu Siku ya Kiyama? Akasema: Je mnakusanyana kuliona jua (kulitizama) wakati
wa mchana bila ya kuwa na kizuizi cho chote (kama
mawingu n.k). Wakasema: Hapana Ewe Mtume wa Allah, Akasema: Kama
hivyo Mtamuona. Watafufuliwa watu Siku ya Kiyama katika sehemu moja kisha
wataambiwa na wafuate kila Umma kile walichokuwa wakikiabudu. Basi kuna katika
wao watakaofuata Jua na wengine wao watakaofuata Mwezi na miongoni mwao
watakaofuata viongozi wa upotofu, na utabakia Umma huu na ndani yake mna
wanafiki wake na atawajia mola wao katika sura sio ile wanayoijua awambie mimi
mola wenu, basi hapo watamjibu twajikinga kwa Allah nawe! Hatuondoki mahala
petu hapa mpaka atujie mola wetu. Basi hapo atawajia (mola wao) katika sura
wanayoijua... mpaka mwisho wa hadithi.
Hapa mimi
nataka kuwauliza kabla ya kitu chochote wale wanaosema kuwa watamuona Mola wao
Siku ya Kiyama wakiitegemea hadithi hii. Je kumuona Allah (Subhanahu Wataala)
kwa namna (mfano) au bila ya namna? Kwa sababu twawasikia wakisema kuwa
watamuona bila ya namna yoyote na wakati hadithi inasema: namna hiyo mtamuona
(kama hivyo) yaani kama mnavyouona Mwezi na
mnavyoliona Jua na kuliona Jua na kuona Mwezi ni kwa namna Fulani, vipi basi
wanadai kuwa watamuona bila ya namna.
Pili: Je waamini kuwa Allah (Subhanahu Wataala) anabadilika
kutoka sura fulani kwenda sura nyingine na kutoka hali kwenda hali nyingine? Na
hali inajulikana kuwa kila kinachobadilika kimeumbwa.
Tatu: Je wamewahi watu kumuona Duniani hata waijue sura
yake Subhanahu Wataala na wakati atakapowajia kwa sura tofauti na ile
wanayoijua waseme: Twajikinga kwa Allah nawe hatuondoki mahali petu hapa mpaka
atakapotujia Mola wetu. Nimeyafanya majadiliano haya na baadhi ya wale wanaodai
kuwa Allah (Subhanahu Wataala) ataonekana Siku ya Kiyama, na lilikuwa jawabu
lao kwa nukta hii ya mwisho ni kuwa Allah (Subhanahu Wataala) ameeleza juu ya
sifa zake na vile vile Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) amewaambia Umma wake
juu ya sifa za Allah (Subhanahu Wataala), kwa hiyo wakija kumuona Allah (Subhanahu
Wataala) kwa sifa tofauti na zile sifa walizoambiwa anazo itaingia shaka katika
nafsi zao na husema: Hatuondoki mahala petu mpaka atujie Mola wetu. Nikawajibu
kwa hayo: Ikiwa sifa za Allah zabadilika kutoka hali kwenda hali nyingine na
kutoka sifa kwenda sifa nyingine je isingekuwa hiyo dalili kuwa Yeye Allah (Subhanahu
Wataala) ni kiumbe (amekuwako baada ya kuwa hayupo) kwa sababu kila chenye
kubadilika kimeumbwa. Ametukuka Allah (Subhanahu Wataala) na hayo Utukufu
mkubwa. Na upande mwingine je inawezekana Allah (Subhanahu Wataala) kujisifu
Nafsi Yake kwa kitu asichokuwa nacho? Au Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam)
kusema juu ya Allah (Subhanahu Wataala) kitu asichokuwa nacho? Wakajibu juu ya
hayo: Hayo yanaweza (Ya kumsifu Allah sifa asiyokuwa nayo) yakafanywa kwa
makusudio ya mtihani na majaribio. Nikawajibu kama ingekuwa makusudio ni
mtihani na majaribio katika kusema juu ya sifa za Allah tofauti na Alivyo basi
ingewezekana kuwa kila Alichotwambia Allah (Subhanahu Wataala) ni kwa makusudio
ya mtihani na majaribio na sio ukweli ulivyo, kwa hiyo kusingekuwa na Pepo wala
Moto wala malipo kwa mema na maovu.
Na vile
vile wale wanaodai kuwa watamuona Mola wao Siku ya Kiyama kwa hiyo baada ya
kuwa wamekwisha kusoma Kitabu cha Allah na wamekwisha soma Sunna ya Mtume
(Salallahu Alayhi Wasalam) na wametizama zile sifa Alizojisifu nazo Allah (Subhanahu
Wataala) katika Kitabu (Qur'an) na zile sifa alizozisema Mtume (Salallahu
Alayhi Wasalam) juu ya Mola wake Je anaweza mmoja katika hao atusifie sura ambayo
anatarajia kumuona Allah (Subhanahu Wataala) nayo Siku ya Kiyama kutokana na
aliyeyajua katika Kitabu cha Allah na Sunna ya Mtume wake Salallahu Alayhi
Wasalam?
Hapana
shaka hakuna mmoja anaeweza kujibu suala hilo
yaani atujulishe sura ambayo atamuona nayo Allah Siku ya Kiyama kwa namna
alivyoijua kutokana na Qur'an na Sunna na wala hakuna mtu aweza kuzungumzia juu
ya Dhati Iliyotukuka kama ilivyo kwa sababu
Allah (Subhanahu Wataala) Peke yake ndiye anayeijua ilivyo. Naye husema Subhanahu
Wataala:
ﭽ ﯦ ﯧ
ﯨ ﯩ ﭼ طه: ١١٠
“Wala wao hawawezi kumjua
(Mungu) vilivyo”
Kwa hiyo
hawawezi kuijua Dhati Tukufu (Allah (Subhanahu Wataala)).
Na upande
mwingine dai hilo
halikubaliki, na hivyo kwa sababu katika Sahihi Muslim kuna hadithi ya Abi
Saeed inayohusika na jambo hili:
( سيأتيهم ربهم في غير الصورة التي رأوه فيها أول مرة )
“Atawajia
Mola wao katika sura tofauti na ile waliomuona nayo mara ya kwanza”.
Hapa ni
pahala pa mwanzo wanaposimama watu katika visimamo vya Siku ya Kiyama, mara ipi
hiyo ya mwanzo (waliomuona Mola wao) inayozungumziwa katika hadithi hii? Je
alionekana Allah (Subhanahu Wataala) kaburini, au kulikuweko kumuona Allah
kabla ya mauti hata isemwe kuwa watamuona Allah kama
walivyomuona mara ya kwanza na Akiwajia kwa sura tofauti na ile wanayoijua
husema: Twajikinga kwa Allah na wewe hatuondoki mahala petu hapa mpaka atujie
Mola wetu.
Vile vile
katika hadithi hii kuna kinachoirudi itikadi yao kwani wao wanaamini kuwa kumuona Allah (Subhanahu
Wataala) ni neema inayowahusu waja wa Mola Waumini tu siku hiyo, wakati hadithi
hii inasema:
فتبقى هـذه الأمة فيها منافـقـوها فيأتيهم ربهم فى غير
الصورة التى يعرفونه بها
"Na utabakia Umma huu wakiwemo wanafiki wao na atawajia
Mola wao katika sura tofauti na ile wanayoijua."
Kwa hiyo
kutokana na hadithi hii ni wazi kuwa Waumini na wanafiki wote watashirikiana
katika kumuona Allah (Subhanahu Wataala), na huku wao wanasema kuwa kumuona
Allah (Subhanahu Wataala) kutakuwa huko Akhera Peponi, na hapa wameitumia kauli
ya Allah (Subhanahu Wataala):
ﭽ ﭒ ﭓ
ﭔ ﭕ ﭼ يونس:
٢٦
“Wale waliofanya wema
watapata (jazaa yao ) wema wao na zaidi”
Wao
wakasema الحسنى kuingia Peponi na الزيادة kuutizama uso wa Allah (Subhanahu Wataala).
Na zimekuja hadithi vile vile zinazoonesha hayo (zinazotia nguvu tafsiri yao hiyo), kati yake ni
hadithi ya Suheib: Kuwa Allah (Subhanahu Wataala) Atawaambia waja wake Waumini
Siku ya Kiyama: Je nisiwazidishie? (nisiwaongezee kitu juu ya haya niliowapa?).
Hapo watamwambia: Je hukuzifanya nyuso zetu zikiwa nyeupe na ukatuingiza
Peponi? Hapo Atafunua hijabu (Sitara). Ni wazi kabisa kuwa kumuona Allah katika
hadithi hii ni baada ya kutulia huko Peponi na hali hadithi ya Abi Huraira
ambayo wanaitolea hoja sana juu ya kuonekana kwa Subhanahu Wataala na hadithi
ya Abi Saeed hizi mbili zinaonesha kuonekana kwake Subhanahu Wataala ni katika
msimamo wa Siku ya Kiyama (sio Peponi), kwa hiyo hapa kuna mpingamano (hadithi
ya kwanza inatwambia kuonekana kwa Subhanahu Wataala ni Peponi na hali hadithi
mbili za mwisho ni katika msimamo wa Siku ya Kiyama). Kwa hiyo hakuna njia ya
kuepukana na mpingamano huu isipokuwa kutambua kuwa makusudio ya الرؤية ni
kuongezewa maarifa ya sifa zake Allah (Subhanahu Wataala) Siku ya Kiyama, ama
vinginevyo haiwezekani kabisa.
Dalili
nyingine walioitumia ni hadithi ya Ibn Abbas RA kuwa amesema: Hakika Mtume
(Salallahu Alayhi Wasalam) amemuona Mola wake usiku aliopelekwa “Israa”.
Na jawabu
lake kuwa maneno hayo hayakuthibiti kuwa yamesemwa na mtarajimu wa Qur'an Karim
ambaye ni Ibn Abbas Alimu wa Umma huu R.A, bali imethibiti kutoka kwake kinyume
cha hayo kama ilivyokuja katika Musnad ya mhifadhifu aliye hoja Al-Rabii Ibn
Habiib, bali vile vile ameitoa Imam Muslim katika Sahihi yake kutokana na Ibn
Abbas R.A kuhusu kuona kwa Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) usiku aliopelekwa
“Israa” Amesema:
Umemuona
moyo wake mara mbili رآه فؤاده مرتين na makusudio ya kuona moyo wake ni kuzidi kupata
maarifa ya Sifa zake Subhanahu Wataala na siyo vinginevyo. Na kama
imesihi hadithi iliyofunguliwa (مطلق) na ikiwa ipo hadithi
nyingine iliyofungwa (مقيد) basi hurudishwa ile
hadithi iliyofunguliwa kwenye hadithi iliyofungwa. Wanazo vile vile wanatoa
dalili kwa Aya nyingi za Qur'an ambazo hazioneshi kabisa kuonekana kwa Allah
sio kwa mbali wala karibu kama :
ﭽ ﮄ ﮅ
ﮆ ﮇ ﮈ
ﮉ ﭼ
المطففين: ١٥
“Hakika watazuiliwa, siku
hiyo na (Rehema) za Mola wao”.
Na kuitolea
kwao dalili Aya hii ni katika mlango wa kutoa dalili kwa kinyume cha andiko (مفهوم
المخالفة) , jambo
ambalo wamehitilafiana wanavyuoni juu ya hoja yake katika mambo ya dhana licha
mambo ya yakini (Imani). Na vile vile maana ya kuzuiliwa na Allah (Subhanahu
Wataala) ni kuzuiliwa na Rehema yake.
Pia wametoa
dalili kwa ombi la Nabii Musa A.S. kwa Mola wake Subhanahu Wataala:
ﭽ ﯖ ﯗ
ﯘ ﯙ ﯚ ﭼ الأعراف:
١٤٣
“Akasema: Mola wangu!
Nioneshe (Nafsi yako) ili nikuone”
Lakini Musa
AS hakuomba hilo kwa ajili ya nafsi yake, lakini
kwa hakika ameomba hilo
kwa ajili ya kuwanyamazisha watu wake. Na kama inavyosemwa juu ya suala la
Nabii Ibrahim AS ;
kwani Ibrahim AS sio alikuwa hajui kuwa Allah (Subhanahu
Wataala) Ahitilafiana na viumbe vyake na juu ya hivyo alivyoiona Nyota akasema:
Huyu mungu wangu, na vile vile alivyoliona Jua akasema: Huyu mungu wangu huyu
mkubwa. Lakini hakika amesema hivyo kwa kutaka kuwanyamazisha watu wake
(kuwashinda kwa hoja) ambao walikuwa wakiabudu nyota na wakiyatukuza maumbile
(Nature) na kutaka kuwasimamisha katika uhakika mmoja kuwa kila kitu kinatoweka
isipokuwa Dhati Yake Subhanahu Wataala. Kwa hiyo jawabu ni moja kutokana na
maneno ya Musa na maneno ya Ibrahim Salamu na Amani za Allah ziwe juu yao .
Kwa hiyo inabainika
kuwa kauli ya haki isiyokuwa na shaka kuwa Dhati ya Allah (Subhanahu Wataala)
(Yeye Mwenyewe (Subhanahu Wataala)) haionekani katika Dunia wala Akhera. Allah
(Subhanahu Wataala) Ametukuka na hayo Utukufu Mkubwa.
Na jawabu
kuhusu لن katika kauli yake Subhanahu
Wataala لن تراني ni
kwamba hiyo ni dalili ya kuwa muhali kuonekana kwake Subhanahu Wataala yaani
hawezekani kuonekana.
Wao
(wanaosema kuwa Allah Ataonekana) wasema kuwa لن
haina maana ya milele na jawabu lake kuwa kukanusha kwa لن
kunamaanisha milele mara na mara nyingine kunamaanisha sio milele lakini
uhakika ulioko ni kuwa katika kukanusha kwa “Lan” (لن)
linatizamwa lile jambo lililokanushwa na likiwa katika mambo
yanayolazimika kukanushwa milele huchukuliwa hivyo na ikiwa sio hivyo
huchukuliwa kinyume chake. Na katika mahala iliyotumika “Lan” (لن) kwa
maana ya kukanushwa milele kauli yake Subhanahu Wataala:
ﭽ ﭘ ﭙ ﭚ
ﭛ ﭜ ﭝ ﭞ ﭟ
ﭠ ﭡ ﭢ ﭣ
ﭼ الحج: ٧٣
“Hakika ya wale mnaowaabudu badala ya Allah hawawezi
kuumba nzi hata wakikusanyika kwa kumuumba”
Hapa kwa
hakika ni muhali wao kuumba nzi katika wakati wo wote ule na sio kukanushwa
huku kwa wakati fulani bila ya wakati mwingine. Na Allah (Subhanahu Wataala) ni
Mjuzi zaidi.
Na mimi
niko tayari kufanya mdahalo (debate) kwa yule anayesema juu ya kuonekana kwa
Allah (Subhanahu Wataala) aje nijadiliane nae mpaka nimrudishe kwenye haki au
yeye anirudishe mimi kwenye rai yake akinishinda kwa hoja, na akitaka tufanye
“Mubahala” (1) tutafanya. Allah (Subhanahu Wataala) ndie mwenye kutoa Tawfiiq.
Haya ni
maneno ya Sheikh Ahmed bin Hamed Al-Khalily Mufti wa Oman .
No comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.