Tuesday, 19 January 2016

Juzuu 6 Saumu---Kujenga uongofu katika nyoyo za vijana-----JUZUU 6 Saumu




          

                                                                                                         القدر: ١ - ٥

“Hakika tumeiteremsha (Qur'an) katika usiku wenye heshima kubwa (usiku wa mwezi wa Ramadhani). Na nini kitakachokujulisha hata ukajuwa nini huo usiku wa Heshima kubwa? Usiku wa heshima, huo ni bora kuliko miezi elfu. Huteremka Malaika na Al-Ruuh( Jibril A.S ) katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao kwa kila jambo. Amani (usiku) huo mpaka mapambazuko ya Al-Fajiri”.



Saumu ni nguzo ya nne katika nguzo za Uislamu, nayo ni miongoni mwa ibada za kiwiliwili zinazomfanya mtu ajisafishe na Riyaa (kuabudu kwa kutaka watu wakuone kuwa hodari sio kwa ajili ya Allah (Subhanahu Wataala) pekee na kutaka radhi yake). Inamuwajibikia kila mtu aliye baleghe kufunga mwezi wa Ramadhani kila mwaka, nao ni mwezi wenye baraka nyingi sana.


Saumu imehusiwa jambo muhimu ambalo halipo katika ibada nyinginezo, nalo ni kuwa ukweli wa hiyo Saumu kwa mwenye kufunga hakuna anaoujua isipokuwa Allah (Subhanahu Wataala), kwa ajili hiyo Amesema Subhanahu Wataala:

( الصوم لي وأنا أجازي به الجنة )

“Saumu ni yangu mimi na mimi namlipa (huyo anaefunga) kwa hiyo (Saumu) Pepo”.


Na juu ya kuwa Ibada zote ni zake yeye tu Allah (Subhanahu Wataala) (lakini imesisitiziwa kwa daraja kubwa iliyopewa kwani mtu aweza kudai amefunga lakini akiwa peke yake huenda akala au akanywa kwa hivyo ukweli wake anaujua Subhanahu Wataala pekee). Na katika hekima zake kuwa inaondoa maradhi na inasafisha akili na hutia nuru katika undani wa mwili (yaani moyo ukipata nuru anaepukana mtu na riyaa, hasadi, chuki, kibri n.k) na humpa mtu nguvu ya kufanya ibada na huizowesha nafsi kuhimili njaa ili iweze kusubiria mashaka ya maisha, na kadhalika. Saumu humfanya mtu aweze kupigana vita na magonjwa ya nafsi na kumtakasa nayo na kumfanya awe na huruma juu ya mafakiri na wenye shida.


Kuhusishwa Saumu na Mwezi wa Ramadhani ni kwa ajili ya kuhuisha kumbu kumbu ya kuteremka kwa Qur'an ili iwe uongozi kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongozi na upambanuzi (wa baina ya haki na batili) na ni kitu cha tabia kwa watu wa Qur'an kuisherehekea kumbu kumbu hii na kujikaribisha kwa Allah kwa kuishukuru neema hii yenye kulinda mabaya.


Saumu maana yake katika lugha ni kujizuia, na maana yake katika Sheria ni kuzuia yafikayo ndani ya mwili kutoka nje yake na kujizuia na jimaa na madhambi makubwa kwa kutia nia kutoka Al-Fajiri mpaka kuzama jua (Magharibi) kwa kauli ya Allah (Subhanahu Wataala) :


                                             ﭳﭴ                              ﭿﮀ                 ﮆﮇ                ﮍﮎ         ﮒﮓ                                            ﮣﮤ           ﮩﮪ                           ﯕﯖ                                                    ﯮﯯ          ﯴﯵ                                ﭗﭘ             ﭞﭟ                                ﭩﭪ                ﭱﭲ                            ﭾﭿ              ﮄﮅ            ﮋﮌ           ﮑﮒ                        البقرة: ١٨٣ - ١٨٧

“Enyi Mlioamini mmelazimishwa kufunga (Saumu) kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu (183) Siku chache tu (kufunga huko). Na atakayekuwa mgonjwa au katika safari basi atimize hisabu katika siku nyingine. Na wale wasioweza, watoe fidia kwa kumlisha masikini. Na atakayefanya wema kwa radhi ya nafsi yake, binafsi ni bora kwake. Na huku kufunga ni bora kwenu ikiwa mnajua. (Haya sasa basi fuateni) (184) (Mwezi huo mlioambiwa mfunge) ni Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa katika (mwezi) huo hii Qur'an ili iwe uongozi kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongozi na upambanuzi (wa baina ya haki na batili). Atakayekuwepo kwake katika huu mwezi (wa Ramadhani) afunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi (atimize) hisabu (ya siku alizowacha kufunga) katika siku nyingine. Allah anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na pia (anakutakieni) kumtukuza Allah kwa kuwa amekuongozeni, ili mpate kushukuru (185) Na waja wangu watakapo kuuliza hakika yangu (waambie kuwa) Mimi niko karibu nao. Naitika maombi ya mwombaji anaponiomba. Basi na waniitikie na waniamini, ili wapate kuongoka (186) Mmehalalishiwa usiku wa Saumu kuingiliana na wake zenu. Wao ni (kama) nguo kwenu (zilizokugandeni mwilini) na nyinyi ni (kama) nguo kwao. Allah anajua kwamba mlikuwa mkizikhini nafsi zenu. Kwa hivyo amekukubalieni toba yenu na amekusameheni. Basi sasa changanyikeni nao na takeni aliyokuandikieni Allah. Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa Alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Saumu mpaka usiku. Wala msichanganyike nao, na hali mnakaa Itikafu msikitini. Hiyo ni mipaka ya Allah, basi msiikaribie. Namna hivi Allah anabainisha hoja zake kwa watu ili wapate kumcha (187).” (Aya ya 183 – 187 ya sura Al-Baqarah)


Na anasema Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) :

( من صام رمضان إيمانا واحتسابا غفر له ما تقدم من ذنبه ومن قام رمضان إيمانا واحتسابا ومن قام ليلة القدر غفر له ما تقدم من ذنبه)

 “Anaefunga Ramadhani hali yakuwa anaamini (wajibu wa kufunga Mwezi huu na kuwa ni faradhi juu yake) na atarajia malipo mazuri (kwa Allah) basi hughufiriwa madhambi yake (yote) yaliyopita, na anaesimama (kusali Sala za usiku katika mwezi wa) Ramadhani hali ya kuwa anaamini na atarajia malipo mazuri na anaesimama (kufanya ibada) usiku wa Al-Qadri (Laylatul Qadri) hughufiriwa madhambi yake ( yote ) yaliyopita.”


Maana ya إيمانا  yaani anaamini kuwajibika kwa kitendo hicho alichokifanya (hapa ni Saumu).

Maana ya  احتسابا yaani atiye niya kuwa anafanya kitendo hichi kwa ajili ya Allah tu, atarajia kwa kitendo hicho thawabu yake tu bila ya kuwa na lengo lingine.

Na iwapo atachanganya niya hiyo pamoja na niya nyingine haitakuwa احتسابا  kwa mujibu ya kauli yake Subhanahu Wataala katika hadithi Qudusiy:

 ( من عمل عملا أشرك فيه غيري فهو له، وأنا أغنى الشركاء )

“Mwenye kufanya jambo akamshirikisha ndani yake mwengine asiye Mimi (Allah (Subhanahu Wataala)) basi hilo (jambo) ni lake yeye (huyo aliyeshirikishwa), na mimi sina haja na washirika.”


Hili ni sharti la kwanza. Sharti la pili la kughufiriwa (anayefunga na anaye simama usiku mwezi wa Ramadhani madhambi yake yote aliyoyafanya kabla) ni kuwa mwenye kufunga na mwenye kusali usiku asiwe anaendelea kufanya dhambi kubwa katika haki za Allah (Subhanahu Wataala) (kama kuacha kusali, kutoa Zaka au kunywa pombe n.k) au kuwadhulumu waja wake kwani wako wanaofunga na kusali Qiyamul-Leyl na hali bado wameshikilia kufanya madhambi makubwa na kuwadhulumu waja wa Allah (binaadamu wenzao). Basi hadithi hiyo ya kughufuriwa madhambi haimkhusu yeye kwa sababu hadithi hii siyo kwa kila anayefunga na kufanya ibada usiku, kwani ikiwa hivyo itakuwa kinyume na itikadi ya Kiislamu iliyo sahihi. Basi hili lizingatiwe.


Na katika hadithi nyingine inayotoa dalili ya kuwajibika kwa Saumu ya Ramadhani ni ile hadithi aliyoitoa Salman Al-Faarisiy R.A. amesema: Ametuhutubia Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) katika siku ya mwisho wa Mwezi wa Shaabani akasema:

(يا أيها الناس قد أظلكم شهر عظيم شهر مبارك شهر فيه ليلة خير من ألف شهر جعل الله صيامه فريضة وقيام ليله تطوعا ومن تقرب فيه بخصلة من الخير كان كمن أدى فريضة ومن أدى فريضة فيه كان كمن أدى سبعين فريضة فيما سواه، وهو شهر الصبر، والصبر ثوابه الجنة، وشهر المواساة وشهر يزاد فيه رزق المؤمن، من فطر فيه صائما كان له مغفرة لذنوبه وعتق رقبته من النار، وكان له مثل أجره من غير أن ينتقص من أجره شيء، قلنا يا رسول الله ليس كلنا يجد ما يفطر به الصائم فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم يعطي الله هذا الثواب من فطر صائماً على مذقة لبن أو تمرة أو شرب من ماء، ومن أشبع صائما سقاه الله من حوضي شربة لا يظمأ حتى يدخل الجنة وهو شهر أوله رحمة وأوسطه مغفرة وآخره عتق من النار ومن خفف عن مملوكه فيه غفر الله له وأعتقه من النار )

 “Enyi watu umekukaribieni mwezi mtukufu, mwezi wenye baraka, mwezi ndani yake kuna usiku ulio bora kuliko miezi elfu (yaani “Laiylatul Qadri”), Allah amejaalia kuufunga (huo mwezi) ni faradhi na kusali Sala za usiku (Qiyamul-Leyl) jambo la kujitolea kulifanya (lina malipo mazuri). Na anaejikaribisha kwa jambo la kheri ni kama aliefanya faradhi. Na aliyefanya faradhi katika mwezi huu ni kama aliyefanya faradhi sabiini katika miezi mingine. Nao ni mwezi wa subira, na subira thawabu yake ni Al-Jannah (Pepo) na ni mwezi wa maliwazo, mwezi inaongezwa ndani yake riziki ya Muumini. Anaemfuturisha ndani yake mwenye kufunga hughufiriwa madhambi yake na hukombolewa shingo yake (yaani yeye mwenyewe) kutoka Motoni na hupata malipo kama malipo yake (huyo aliyefuturishwa) bila ya kupungua kitu katika malipo yake. Tukasema ewe Mtume wa Allah sio kila mmoja wetu anacho cha kumfuturishia aliyefunga. Akasema Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam): Allah anampa thawabu hii anaemfuturisha aliyefunga kwa chubuo moja la maziwa au tembe ya tende au kinywaji cha maji na anaemshibisha aliyefunga Allah atamnywesha katika Hodhi langu kinywaji ambacho (kitamfanya) hatapata kiu mpaka aingie Peponi. Na ni  mwezi ambao mwanzo wake ni Rehema na kati kati yake ni Maghufira na mwisho wake ni kukombolewa na Moto na yule anaempunguzia mtumwa wake (kazi), Allah humghufiria na kumkomboa na Moto”.


Sababu ya kuileta hadithi kwa kirefu ni kupata faida na huenda Allah (Subhanahu Wataala) akajaalia (miongoni mwa wasomaji) atakayetekeleza yaliyomo humo na nitapata mimi sehemu katika hayo malipo kwa sababu anayeionesha kheri ni kama yule aliyeifanya kheri hiyo.




Amesema Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) :

( إن الله يباهي ملائكته بالشاب العابد فيقول : أيها الشاب التارك شهوته من أجلي المبذل شبابه لي  أنت عندي كبعض ملائكتي )

“Hakika Allah huwasifia Malaika wake kijana mwenye kufanya Ibada husema: Ewe kijana, aliyeacha matamanio yake kwa ajili yangu, anaeutumia ujana wake kwangu mimi, wewe kwangu mimi ni kama baadhi ya Malaika wangu”.


Unakutosha ufahari ewe unaefunga kuwa mstari mmoja na Malaika. Sababu ya kuhusishwa vijana katika kutajwa bila ya wazee kwa kuwa mzee yuko karibu zaidi na utiifu (hana matamanio makubwa yanayomzuia kufanya Ibada kama kijana) na inasemekana anayefika miaka arubaini na yungali hajaacha maasi basi huyo yuko karibu na ghadhabu ya Allah ndio maana unaona kuhimizwa kwa kijana ni zaidi kuliko mzee kwani yeye ndio sasa anayakabili maisha ama mzee anayapa mgongo. Allah (Subhanahu Wataala) asema:


              الزمر: ١٠

“Bila shaka wafanyao subira (wakajizuilia na maasi na wakaendelea na taa) watapewa ujira wao bila ya hisabu”.


Yaani wafanyao subira katika kumtii Allah na kujizuia na kumuasi na kusubiri katika misukosuko na mitihani anayoipata mja. Na anasema Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam):

(الصبر نصف الإيمان)

        “Subira ni nusu ya Imani”


Na amesema Salallahu Alayhi Wasalam: 

(لكل شيء باب وباب العبادة الصوم)

“Kila kitu kina mlango na mlango wa Ibada ni Saumu”


Na katika hadithi Qudusiy:

 (كل حسنة بعشرة أمثالها إلى سبعمائة ضعف إلا الصيام فإنه لي وأنا أجزي به إنما يذر شهوته وطعامه وشرابه لأجلي ، الصوم لي وأنا أجزي به)

“Kila jambo jema hulipwa (ujira) mara kumi hadi mara mia saba isipokuwa Saumu kwani hiyo ni yangu na mimi nitailipia. Bila ya shaka yeye huacha matamanio yake na chakula chake na kinywaji chake kwa ajili yangu Mimi. Saumu ni yangu na mimi nitailipia.”


Amesema Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) :

 (إذا دخل رمضان فتحت أبواب الجنة وغلقت أبواب جهنم وسلسلت الشياطين)

“Ikiingia Ramadhani inafunguliwa milango ya Pepo (Al-Jannah) na yafungwa milango ya Moto (Jahannam) na mashetani hufungwa kwa minyororo.”


Amesema Salallahu Alayhi Wasalam:

 ( للصائم فرحتان فرحة عند فطره وفرحة عند لقاء ربه ولخلوف في الصائم  أطيب عند الله من ريح المسك والصيام جنة فإذا كان يوم صوم أحدكم فلا يرفث، و لا يصخب، فإن سابه أحد أو قاتله فليقل إني امرؤ صائم )

“Anaefunga ana furaha mbili: furaha wakati anapofuturu na furaha wakati anapo kutana na Mola wake. Na harufu ya mdomo wa mwenye kufunga inanukia zaidi kwa Allah kuliko harufu ya miski. Na Saumu ni kinga, basi siku akiwa mmoja wenu amefunga asiseme maneno mabaya wala asipige makelele na akimtukana mtu yeyote au akapigana naye basi na aseme mimi nimefunga.”


Yamekuja mahadharisho (maonyo) kwa aharibuye Saumu yake katika Aya chungu nzima na katika hadithi nyingi. Kati ya hadithi hizo kauli ya Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) :

 (من لم يدع قول الزور والعمل به فليس لله حاجة في أن يدع طعامه وشرابه)

“Asiewacha kusema uwongo na kuutumia (uwongo) basi Allah hana haja kwa mtu huyo kuacha chakula chake na kinywaji chake.”

           

Unaona kwa uhakika kuwa Allah hataki mja wake akae na njaa na kiu bila ya sababu bali analolitaka kwake ni kuzuia matamanio ya viungo vyake.



Saumu imegawika vifungu vinne:

Saumu iliyo wajibu (faradhi).

Saumu iliyo haramu.

Saumu iliyo himizwa.

Saumu iliyo makruhu.



Saumu ya Mwezi wa Ramadhani, Saumu ya nadhiri, Saumu ya kaffara, nazo ni: kaffara ya kuuwa, kaffara ya “Dhihar” (mume kumwambia mkewe: wewe kwangu ni kama mgongo wa mama yangu basi anaharimika kwake mpaka atoe kaffara), Kaffara ya “Iilaau” yaani mwanamme kuapa kuwa hatamwingilia mkewe basi hatoweza kumuingilia mpaka atoe kaffara, kaffara ya kwenda kinyume na kiapo chake, vile vile Saumu ya (anayehiji) Attamatuu kwa yule asieweza kumiliki kuchinja. Kirefu cha haya kitapatikana katika vitabu vya Fiqhi.



Kufunga katika Idi mbili (Al-Fitri na Al-Adh-haa), kufunga kwa aliye katika hedhi na ujusi (kwa mwanamke) na kufunga siku ya shaka, nayo ni tarehe 30 thelathini Shaabani haifungiwi siku hii ili isiongezeke siku katika Ramadhani kutoka mwezi mwengine. Kama ilivyosemwa kutokana na Ikrima R.A. na Ammar R.A. wamesema: Aliyefunga siku inayotiliwa shaka basi amemuasi Aba Al-Qasim (Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie-) bali anapendelewa ajizuie na vinavyofunguza siku hiyo mpaka katikati ya mchana huenda ikaja habari ya kuonekana mwezi aendelee na funga yake, lakini juu ya hivyo hapana budi kuilipa siku hiyo kwa sababu hakuiamkia kuwa ana hakika kamili kuwa ni Ramadhani, na katika sharti ya Saumu kuwa atiye niya ya uhakika tokea usiku.


Saumu ya Ashuraa (siku ya kumi ya Muharram) na aongeze kufunga siku moja kabla yake au siku baada yake ili kuwahalifu (kwenda kinyume) mayahudi na manasara kwa sababu wao waitukuza siku hii kwa kuifunga, vile vile inahimizwa kufunga siku ya Arafa kwa mujibu wa kauli ya Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) :

 (صوم يوم عرفة يكفر سنتين ماضية ومستقبلة وصوم يوم عاشوراء يكفر سنة ماضية)

“Saumu katika siku ya Arafa hufuta (madhambi ya) miaka miwili uliopita na unaokuja, na Saumu katika siku ya Aashuraa hufuta madhambi ya mwaka uliopita.”


Inapendelewa vile vile kufunga siku tatu, “Ayyaam Beiydh” nazo ni tarehe 13, 14 na 15 katika kila mwezi wa Hijri (mwezi wa Kiislamu) isipokuwa tarehe 13 katika mwezi Dhul Al-Hijja kwa sababu ni katika siku za “Attashriq”. Amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam:

 ( من صام في كل شهر ثلاثة أيام فكأنه صام الدهر كله )

“Anaefunga katika kila mwezi siku tatu basi kama aliyefunga zama zote (milele).”


Pia inapendelewa kufunga siku sita katika Shawwaal kwa mujibu wa kauli yake Mtume Salallahu Alayhi Wasalam:

( من صام رمضان ثم أتبعه بستة أيام من شوال فكأنه صام الدهر كله )

“Anaefunga Ramadhani kisha akaifuatiliza kwa (kufunga) siku sita katika Shawwaal basi kama kwamba amefunga milele”.


Inahimizwa kufanya Itikaaf mwisho wa Ramadhani. Na ifanywavyo ni kuingia msikiti unaosaliwa jamaa kabla ya kutuwa jua usiku wa tarehe 21 Ramadhani, afanye hivyo kwa ajili ya kutaka radhi ya Allah Subhanahu Wataala na kutarajia malipo yake bila ya kuwa na kusudio lingine na ajifunge nafsi yake msikitini humo kwa kufanya ibada na asitoke humo isipokuwa kwa kwenda kusali Sala ya Idi. Hivi ndivyo ilivyokuwa Sunna. Anaetaka kufanya Itikaaf chini ya muda huo na atiye niya  kwa mujibu wa siku anazotaka kukaa Iitikaaf, na haitakiwi kubadilisha niya hiyo wakati yuko msikitini katika Itikaaf wala asijishughulishe na mambo ya Dunia isipokuwa yaliyo dharura kama kwenda kukidhi haja au kwenda kula ikiwa hawezi kula msikitini.


Akifanya Itikaaf katika wakati usiokuwa Ramadhani basi ni sharti afunge. Na kufanya Itikaaf katika Ramadhani na hasa katika kumi la mwisho kuna mambo ya kheri Allah huyaleta katika wakati huu na asaa (huenda) akafanikiwa kuipata Laiylatul Qadri. Mtume Salallahu Alayhi Wasalam alifanya Itikaaf katika mwanzo wa mwezi wa Ramadhani na katikati yake na mwisho wake na hii ndio ilikuwa amali yake ya mwisho Salallahu Alayhi Wasalam. Na Masahaba walikuwa wakichukuwa kwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam vitendo vyake vya mwisho mwisho (hawachukuwi vya zamani bali wachukuwa vipya). Na alikuwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam akifunga zaidi katika mwezi wa Shaabani (mbali na mwezi wa Ramadhani) lakini ni lazima afungue siku mbili za mwisho wa Shaabani asiziunganishe na Ramadhani kutokana na kukataza kwake Salallahu Alayhi Wasalam kuiunganisha Ramadhani na mwezi mwengine.



Saumu iliyo makruhu:

Ni Saumu ya siku za “Attashriq” nazo ni siku tatu zinazofuatia Idi Al-adh-ha (Idi kubwa) kwa sababu hizo ni siku ambazo Allah Subhanahu Wataala anawafanyia “dhiyafa” (anawakaribisha na kuwakirimu) waja wake kwa hiyo haifai kuikataa dhiyafa yake. Na zimeitwa ayyam “attashriiq” kwa sababu huanikwa nyama juani siku hizo. Na vile vile ni makruhu kufunga siku moja au mbili kabla ya Ramadhani ili zisiungane nayo, na pia kufunga siku ya Ijumaa peke yake isipokuwa kama ikitanguliwa na siku au ikifuatiliwa na siku kwa sababu wamesema kuwa Ijumaa ni Idi na haifai kufunga siku ya Idi.


Amesema Shekhe wetu Noor Diin Allah Amrehemu kuwa tofauti iliopo baina ya Idi na siku ya Ijumaa kuwa imekubaliwa na wote kwamba ni haramu kufunga siku ya Idi hata ikatanguliwa kufungwa siku moja au ikafatiliwa na siku moja, ambalo ni kinyume ya siku ya Ijumaa, kwani imekubaliwa na wote kwamba inaruhusiwa kufunga siku ya Ijumaa ikiwa itatanguliwa au ikafatiliwa na kufunga siku moja. Vile vile katika Saumu iliyo makruhu kufunga milele.


Amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam:

 (لا صام من صام الأبد)

“Hajafunga mwenye kufunga milele”


Na kauli yake aliyomwambia Abdullah bin Omar:

 (صم صيام داود : كان يصوم يوما ويفـطر يوماً، ولا يفـر إذا لاقى)

“Funga Saumu ya Dawood alikuwa afunga siku na afungua siku, na hakuwa akikimbia akutanapo (na adui).”


Aliambiwa hivyo wakati aliposhikilia ombi lake la kutaka kufunga milele akamnasihi Salallahu Alayhi Wasalam asifanye hivyo na akamwambia:

 ( صم وأفطر وقم ونم، فإن لعينيك عليك حقا وإن لنفسك وأهلك عليك حقا )

“Funga na ufungue (siku nyingine funga siku nyingine usifunge), usimame (kwa kufanya Ibada) na ulale, kwani jicho lako lina haki juu yako na nafsi yako na watu wako (mke na watoto wako) wana haki juu yako”


Na katika hadithi nyingine “wana fungu kwako”.


Vile vile katika Saumu iliyo makruhu ni Saumu ya msafiri akiwa amedhoofika hata akawa hawezi kufanya yale yaliyomuwajibikia kuyafanya, kama alivyofanya Mtume Salallahu Alayhi Wasallam katika baadhi ya vita vyake alipoona uchofu umedhihiri kwa masahaba zake kutokana na kufunga basi akawaamrisha wafungue kwa kuwaonea huruma. Kwa hiyo msafiri amepewa ruhusa ya kufungua na hiyo ni Rehema ya Allah Subhanahu Wataala juu ya waja wake.

Saumu kwa ujumla ni kheri na ina fadhila kubwa isipokuwa kwa zile siku zilizokatazwa kufunga kwa mujibu wa kauli yake Salallahu Alayhi Wasalam:

(لكل شيء  زكاة  وزكاة الجسد الصوم)

“Kila kitu kina Zaka na Zaka ya kiwiliwili ni Saumu.”


Na katika kauli yake Salallahu Alayhi Wasalam:

 ( من صام يوماً ابتغاء وجه الله أبعده الله من جهنم كبعد غراب طائر وهو فرخ حتى مات هرما )

“Anaefunga siku moja kwa kutaka kumridhisha Allah (tu peke yake) basi Mola humuweka mbali na Jahannam kama umbali wa kunguru anaeanza kuruka yu hali kinda mpaka anapokufa naye amekonga”.


Hadithi mbili hizi zimetolewa na Abu Huraira. Na katika hadithi:

 (الشتاء ربيع المؤمن طال ليله فقام وقصر نهاره فصام)

“Msimu wa baridi ni faida kwa mwenye kuamini: usiku wake ni mrefu na kwa hiyo hupata kusimama (usiku kufanya ibada) na mchana wake ni mfupi na kwa hiyo hufunga.”



Imefaridhishwa Saumu ya Ramadhani katika mwaka wa pili wa Al-Hijra na zikafutwa faradhi zote za Saumu zilizokuwepo kabla ya hapo. Na haisihi Saumu isipokuwa kwa kutia niya tokea usiku kuamkia ile siku atakayofunga. Kwa hiyo mwenye kumtokea Al-Fajiri kisha akatia niya ya kufunga asubuhi basi huyo atakuwa hana Saumu. Na mwenye kumtokea Al-Fajiri na ana janaba tokea usiku naye hakuoga janaba basi huyo hana Saumu kwa mujibu wa kauli yake Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :

)من أصبح جنبا أصبح مفطرا(

“Anaeamka asubuhi na hali ya kuwa ana janaba ameamka amefungua”


Na hadithi nyingine:

 ( كان رسول الله صلى الله عليه وسلم يصبح جنبا من جماع غير احتلام )

“Alikuwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam anaamka asubuhi na hali yakuwa ana janaba ya jimai wala sio (janaba) ya kuota.”

Hii ni Sunna ya kitendo na ile hadithi ya kwanza ni sunna ya kauli. Na sunna ya kauli inatangulizwa kabla ya sunna ya kitendo kwa uwezekano wa kuwa sunna ya kitendo ni katika mambo yanayomhusu yeye Mtume Salallahu Alayhi Wasalam peke yake.


Na katika mambo yanayopasa kuyajua kuwa wakati zikutanapo tupu mbili  basi imekwisha patikana janaba na inapasa kujiosha nayo, iwapo imetoka manii au haikutoka wala mtu asilifanyie jambo hilo upuuzi akafikiria madamu haikumtoka manii basi haimlazimikii kuoga janaba sivyo hivyo imekuja sunna ya Mtume Salallahu Alayhi Wasalam kuamrisha kuoga:

 ( إذا التقى الختانان وجب الغسل أنزل أو لم ينزل )

“Zikiingiana tupu mbili hadi zikakutana sehemu zao zinazotahiriwa, kuoga kwawajibika iwapo yametoka manii au hayakutoka”


Na anaepata janaba usingizini na asijuwe mpaka mchana huyu Saumu yake sahihi ikiwa ataharakisha kwenda kuoga wakati atakapotanabahi na wala asifanye kitu cho chote kabla ya kuoga, lakini akijichelewesha na kufanya mambo mengine kuna wasiwasi ya kuharibika Saumu yake.

Saumu iliyo sahihi ni ile iliyofanywa kwa mujibu inavyotakiwa katika sheria.


Na inavyotakiwa ni ifuatavyo:

Ni kuwa na adabu na kutekeleza amri za Dini tukufu na hivyo ni kuizuia nafsi na matamanio yaliyo dhahiri na yaliyofichika. Kuuzuiya ulimi usiudhi wengine kama kuwasengenya, kuwafitinisha, kuwatukana na maneno machafu yanayokera watu bila ya haki. Na vile vile kuzuia macho yake yasitizame yaliokuwa hayafai kutazama na atie niya ya kufunga tokea usiku kabla ya kutoka Al-Fajiri. Wala asiseme kama wasemavyo wasiojuwa kuwa Al-Fajiri ni ile Al-Fajiri iingiayo majumbani; hilo ni kosa kubwa kwani huo ni katika wakati wa mchana na aendelee kuwa na niya yake ya kufunga mpaka kuzama jua (kutua) kuzama kwa kweli siyo likizama jua nyuma ya mlima au likifunikwa na wingu au kiza. Na katika kipindi hichi ajizuie na kula, kunywa na kuingiliana na kufanya maasi na awe anajishughulisha na kumtaja Allah Subhanahu Wataala huku akifanya yaliyomuwajibikia katika mambo ya faradhi, asiingize tumboni kitu cho chote kikiwa chakula au kingine, yote hayo ayafanye kwa kutaka radhi ya Mola Subhanahu Wataala peke yake sio kwa lengo lingine.


Awe na Imani kuwa hii ni fardhi amemuamrisha Allah Subhanahu Wataala kuifanya na yeye huifanya bila ya kuuliza kwa nini ameamrishwa kufunga kwani yeye ni mja anafuata aliyoamrishwa na Mola wake kwa utiifu mkubwa ikiwa amependa au hakupenda. Na akipenda (akiridhia) atapewa thawabu na hatahasirika kwa aliyoyafanya na ataadhibiwa kwa kutoridhia amri ya Allah Subhanahu Wataala :


                                        ﭠﭡ                       الأحزاب: ٣٦

“Haiwi kwa mwanamme aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini, Allah na Mtume wake wanapokata shauri, wawe na hiari katika shauri yao, na mwenye kumuasi Allah na Mtume wake, hakika amepotea upotofu ulio wazi (kabisa).”


Na Allah Subhanahu Wataala hana haja ya kuwakalifisha waja wake na wala hana haja ya vitendo vyao bali amewakalifisha kufanya vitendo hivyo kwa maslaha yao wenyewe na hakuna ajuaye maslaha hayo isipokuwa yeye Subhanahu Wataala.


                           ﭿ                            الذاريات: ٥٦ - ٥٨

“Si kuwaumba Majini na Watu ila wapate kuniabudu. Sitaki kwao riziki wala sitaki wanilishe. Kwa yakini Allah ndiye mtoaji wa riziki, Mwenye nguvu, Madhubuti”.


Na hakutaka Allah Subhanahu Wataala kwa kuwaamrisha waja wake wafunge ili wapate njaa na kiu tu bali ametaka waingiwe na adabu na wapate faragha ya kumkumbuka yeye Subhanahu Wataala wakati wanapokuwa na njaa na kiu na wajue kuwa hawakupata njaa na kiu isipokuwa kwa kutaka radhi za Allah na malipo mema kutoka kwake. Anaetaka radhi za Allah basi na aitafute katika kila kitu iwapo katika kutekeleza amri zake au kuacha kufanya aliyoyakataza.


Kama ilivyosemwa ikihisi njaa nafsi vyashiba viungo na ikishiba basi viungo vyote hupata njaa. Saumu yasafisha moyo na uchafu chafu (kwa hiyo unasafika moyo na maradhi yake kama kiburi, kujiona, hasadi, chuki n.k.). Akionja anaefunga maumivu ya njaa huwakumbuka masikini wenye njaa siku zote basi huwahurumia kwa kadiri awezavyo. Walikuwa miongoni mwa waliofahamu wakisema kila wanapokula chakula: Ewe Allah usinichukulie kwa haki ya wenye njaa.


Na katika kufunga ni kufuata mfano wa Malaika AS kwani wao hawali wala hawanywi. Na inavyotakiwa mwenye kufunga usichoke ulimi wake kumtaja Allah Subhanahu Wataala na kusoma Qur’ani, na Muumini akimdhukuru sana Allah kwenye neema basi humsaidia akiwa na shida.

Kama inavyosemwa kuwa Nabii Yunus AS alipomezwa na nyangumi Allah Subhanahu Wataala amesema juu yake:


                                  الأنبياء: ٨٧

 “Basi (alipozongwa) aliita katika kiza (akasema): ‘Hakuna aabudiwaye isipokuwa wewe, mtakatifu, hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu nafsi zao’.”


Na hicho kiza ni kiza cha tumbo la nyangumi, kiza cha bahari na kiza cha usiku, basi wakasikia Malaika AS sauti yake na jinsi walivyokuwa wameizoea sauti yake waliitambua. Wakasema: Ewe Mola wetu twaisikia sauti ijulikanayo katika mahala pageni. Akawambia Mola wao Subhanahu Wataala sauti hiyo ni ya mja wangu Yunus, basi hapo Malaika wakamuombea msamaha na uokozi na Allah Subhanahu Wataala akamuokoa.


          ﮪﮫ           الأنبياء: ٨٨

 “Basi tukampokelea na tukamuokoa katika huzuni ile. Na namna hivyo ndivyo tuwaokoavyo walioamini”.


Inasemekana kuwa alitoka bila ya ngozi na akaudhiwa na nzi basi Allah Subhanahu Wataala akamuoteshea mti wa “Al-yaqtiin” ambao una siri fulani, hausogelewi na nzi. Katika hadithi Al-Qudsiy:

 ( من دعاني في الرخاء أجبته في الشدة )

“Anaeniomba katika neema (raha) basi humpokelea (anaponiomba) katika shida”


Na ibada zote zamfaa mtu katika shida kama ilivyozungumzwa juu ya watu wa Arraqiim (wenye habari zile zilizoandikwa vitabuni) ambao Allah amewataja katika sura ya Al-Kahf kuwa wao watatu waliingia pangoni katika mlima basi likaanguka jiwe na kuliziba hilo pango waliokuweko na kwa hivyo hawakuweza kutoka wakajiogopea wasiangamie humo. Wakazikimbilia amali zao nzuri walizozifanya kabla ya hapo (ziwafae katika shida hiyo). Wakaambiana wenyewe kwa wenyewe: kila mmoja wenu aitaje amali yake njema ili ajikaribishe nayo kwa Allah Subhanahu Wataala na huenda akatupa faraja. Hapo akasema mmoja wao: Ndio nilikuwa na binti ammi yangu na nikamtaka afanye zina nami na baada ya kumuomba sana na yeye kutoa ahadi nyingi sana mwisho nikafanikiwa kumpata na wakati nilipomkalia mkao wa mwanamme anapotaka kumjamii mwanamke nikamuacha (nisizini naye) kwa kumuogopa Allah. Ewe Mola ikiwa unajua kuwa niliacha kufanya yale machafu kwa ajili yako wewe basi tuokoe (na hilaki hii) basi hapo lile jiwe likasogea kadiri ya kuwa waliweza kuona muangaza.


Akasema wa pili: Ndio nilikuwa na wazee wangu wawili wamekonga (umri wao mkubwa) na nilikuwa nawanywesha maziwa ukifika usiku, lakini usiku mmoja nilichelewa kuja kuwaletea maziwa nipate kuwanywesha nikawakuta wamekwisha lala nikaona tabu kuwaamsha basi nikakaa nawangojea kando yao na huku maziwa nimeyashika mkononi, kwa sababu niliogopa kuwa nikiondoka hapo wakiamka hawataniona, nikiwa katika hali hiyo mpaka kukapambazuka Ewe Mola ikiwa unajua kuwa sikufanya kitendo hichi isipokuwa kwa ajili yako wewe tu basi tuokoe na janga hili. Na hapo, lile jiwe likasogea kidogo lakini bado wakawa hawawezi kutoka kwenye huo upenyu.


Akasema yule wa tatu: Ndio nilikuwa na vibarua wakinifanyia kazi na mmoja wao aligoma kuchukua ujira wake akenda zake basi nikaukuza huo ujira mpaka ukawa mali nyingi halafu baada ya kupita muda mrefu akanijia naye kashikwa na haja akanitaka nimpe ule ujira wake aliougomea kuuchukua hapo nikampa ile mali nyingi (nilioikuza) nikamwambia: haya ni maendeleo ya mali yako ichukue basi hakusadiki mpaka nikamhakikishia ukweli wa hayo. Ewe Mola ikiwa unajua kuwa amali hii nimeifanya kwa ajili yako tu basi tuokoe na balaa hii, likasogea lile jiwe kisha wakatoka. Basi hii ndio siri (faida) ya utiifu. Na Kitabu cha Allah kinahakikisha hayo katika kauli yake:


                  الطلاق: ٢

“Na anayemwogopa Allah, (Allah) humtengenezea njia ya kuokoka (katika kila balaa)”


                    الطلاق: ٤

“Na anayemwogopa Allah, (Allah) humfanyia mambo yake kuwa mepesi.”

Na ni katika sunna kusali “Qiyamul-layl” nayo ni sala ya “taraweeh” na sala ya usiku wa manane (Sahar) katika mwezi wa Ramadhani. Na juu ya “Qiyamul-layl” na fadhila yake zimekuja hadithi nyingi na zikatiliwa nguvu na Qurani Tukufu kwa kauli Yake Taala:


                            الذاريات: ١٧ - ١٨

“Walikuwa wakilala kidogo tu usiku. Na wakiomba maghufira (msamaha) nyakati za kabla ya Al-Fajiri”.


Anasema Al-Baidhaawiy: Kama kwamba wamekesha wajikumbusha makosa yao (na kuomba maghufira). Na kauli yake Subhanahu Wataala:


                                                                     السجدة: ١٦ - ١٧

 “Huinuka mbavu zao kutoka vitandani wakati wa usiku ili kumuabudu Mola wao kwa kuogopa Moto na kutaraji Pepo; na hutoa (Zaka na Sadaka) katika yale tuliyowapa. Nafsi yoyote haijuwi waliyofichiwa katika hayo yanayofurahisha macho huko Peponi ni malipo ya yale waliyokuwa wakiyafanya”.


Na alikuwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam asimama usiku (kusali) mpaka miguu yake yavimba, akaambiwa: unafanya hayo na Allah amekwisha kughufiria madhambi yako yaliyopita na yajayo. Akajibu : Je nisiwe mja mwenye kushukuru. Na akahimiza Salallahu Alayhi Wasalam kusali usiku akasema:

( عليكم بقيام الليل فإنه دأب الصالحين قبلكم ومقربة إلى ربكم ومكفرة للسيئات ومنهاة عن الإثم ومطردة للداء من الجسد )

“Shikilieni kusali Sala za usiku kwani hiyo ni tabia (ada) ya watu wema walio kabla yenu na kikurubisho kwa Mola wenu na kifutio cha madhambi yenu na kizuio cha makosa na kinafukuza maradhi mwilini”.


Na amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :

 ( أقرب ما يكون الرب من العبد في جوف الليل الأخير فإن استطعت أن تكون ممن يذكر الله في تلك الساعة فكن )

“Wakati anaokuwa Mola karibu sana na mja wake ni katika sehemu ya mwisho ya usiku (theluthi ya mwisho ya usiku) basi ukiweza kuwa miongoni mwa wanaomtaja Allah katika wakati huo basi kuwa (katika hao).”


Na alikuwa Salallahu Alayhi Wasalam anasema akiamka usiku (kufanya Ibada):

 ( اللهم لك الحمد أنت نور السموات والأرض ولك الحمد أنت قيوم السموات والأرض ولك الحمد أنت رب السموات والأرض ومن فيهن أنت الحق وقولك الحق ووعدك الحق ولقاؤك الحق والجنة حق والنار حق والساعة حق والنبيون حق ومحمد صلى الله عليه وسلم حق اللهم لك أسلمت وبك آمنت وعليك توكلت وفيك خاصمت وإليك حاكمت فاغفر لي ما قدمت وأخرت وما أسررت وأعلنت أنت المقدم وأنت المؤخر وأنت على كل شيء قدير لا إله إلا أنت ولا حول ولا قوة إلا بالله )


Na baada ya kusoma Dua hii hupangusa macho yake na kutizama mbinguni huku akisoma Aya kumi za mwisho za sura ya Al-Imraan.


Amefuzu mwenye kumuiga Mtume Salallahu Alayhi Wasalam katika harakati zake na kutulia kwake na maneno yake na vitendo vyake. Na uongofu wote uko katika kumfuata Muhammad Salallahu Alayhi Wasalam.



            Vile vile huitwa “Fitrat Al-abdaan” na “Zakaat Al-abdaan” na ni sunna iliyotiliwa mkazo kwa kauli yake Mtume Salallahu Alayhi Wasalam:

( زكاة الفطر على الغني والفقير من المسلمين أما الغني فيزكيه الله وأما الفقير فيرد الله عليه أكثر مما أعطى)

“Ni juu ya tajiri na fakiri katika Waislamu kutoa Zakaa ya Fitri, ama tajiri Allah humsafisha na ama fakiri Allah humrudishia zaidi kuliko alivyotoa.”


Na mafakiri miongoni mwa Masahaba RA walikuwa wakiipokea kisha hutoa kwa niaba ya nafsi zao.


Na alikuwa Imam Al-Khalily Radhi ya Allah iwe juu yake, alikuwa akiwaamrisha wanafunzi waipokee kisha waitoe kwa niaba ya nafsi zao na alikuwa mmoja wao aipokea kutoka kwa ndugu yake kisha humpa mwingine na huenda akapewa mara nyingine na ikabakia kwake.


Na ulimjia mwaka Imam Salim bin Rashid Al-Kharusiy, Radhi ya Allah iwe juu yake, akawa hana kitu cha kutoa Zakaa ya Fitri kwa hiyo akapeleka nguo yake sokoni kuuzwa na ikanunuliwa thamani yake chakula cha Fitri na akabakia yeye ataabika kwa baridi (alikuwa hana nguo nyingine ya kuvaa). Kisa hichi kimefanana mno na jinsi alivofanya Mtume Salallahu Alayhi Wasalam wakati alipotoa nguo yake kumpa aliekuja kuomba akabakia nyumbani hana nguo nyingine ya kutokea.


Na Zaka Al-Fitri inamlazimu Muislamu kujitolea nafsi yake na kuwatolea wote walio chini ya maangalizi yake kama mtoto, mke na mtumwa. Anamtolea kwa kila mmoja pishi ya chakula alichokuwa akila katika Ramadhani (na pishi inakadiriwa uzito wa kilo 2.05 [mbili na gramu 50]). Na wakati unaotolewa hiyo Zakaa ni baina ya Sala ya Al-Fajiri na Sala ya Idi kwa mujibu wa kauli yake Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :

 (أغـنوهم هذا اليوم عن السؤال)

“Watoshelezeni siku hii wasiombe”


Na imehimizwa kutoa sadaka kwa wingi na hasa katika mwezi wa Ramadhani na bora kuwapa jamaa zako wa karibu na jirani zako.

Alikuwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam ukiingia mwezi wa Ramadhani huzidi kuwa karimu kuliko upepo uliotumwa. Na kumpa sadaka ndugu yako katika Dini ni bora kuliko mwingine (kumpa sadaka Muislamu mcha Mungu ni bora kuliko kumpa mwengineo).



 (سبحان الله والحمد لله والملك لله والعظمة لله والكبرياء لله ولا إله إلا الله والله أكبر عدد خلقه وزنة عرشه ومداد كلماته ورضا نفسه وكما ينبغي له وكما هو له أهل لا ينقطع ولا ينفد من أزل الأزل إلى أبد الأبد وصلى الله على سيدنا محمد وعلى آله وصحبه وسلم )


Dua ya kwanza:

( اللهم إنا لك نعبد ولك نركع ونسجد وإياك ندعو ونحمد آمنا بك نرجو رحمتك ونخشى عذابك إن عذابك كان محذوراً  اللهم يا فارق الفرقان ومنزل القرآن خالق الإنسان عالم السر والإعلان بارك اللهم لنا وللمسلمين في صوم شهر رمضان وأعنا فيه وفي غيره على الصلاة والصيام والقيام وعلى تلاوة القرآن واقطع عنا حزب الشيطان وزحزحنا عن النيران وامنن علينا بالتوبة والغفران والقبول والرضوان وحبب اللهم إلينا الإيمان وزينه في قلوبنا وكره إلينا الكفر والفسوق والعصيان وأسكنا اللهم الجنان وزوجنا فيها من الحور العين الحسان وآتنا من كل فاكهة زوجين في دار السلام بمنك وفضلك وجودك وكرمك وإحسانك ولطفك يا ذا الجلال والإكرام )


Dua ya pili:

 ( اللهم اقسم لنا من خشيتك ما تحول به بيننا وبين معصيتك ومن طاعتك ما يبلغنا رحمتك ومن اليقين بك ما يهون علينا مصائب الدنيا ومتعنا بأسماعنا وأبصارنا واجعل ذلك الوارث منا وانصرنا على من ظلمنا وعادانا ولا تجعل مصيبتنا في ديننا ولا تجعل الدنيا أكثر همنا ولا مبلغ علمنا اللهم إنا نسألك فعل الخيرات وترك المنكرات وحب الصالحات ورحمة المساكين فإذا أردت بعبادك فتنة فاقبضنا غير مفتونين )

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.