Tuesday, 19 January 2016

Jezuu 9 Ndoa ----Kujenga uongofu katika nyoyo za vijana----



  

الروم: ٢١

"Na katika Ishara Zake(za kuonyesha ihsani zake juu yenu) ni kuwa Amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mupate utulivu kwao, naye Amejaalia baina yenu mapenzi na kuoneana huruma. Bila shaka katika haya zimo ishara kwa watu wanaofikiri". Aya ya 21 katika Sura Ar-Rum.


Ndoa ni Sunna iliyomo katika sharia ambayo imesisitizwa na Qurani Takatifu na Sunna ya Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- Amesema Allah Subhanahu Wataala katika aya ya 3 Sura An-Nisaa:

النساء: ٣

“Basi oeni mnaowapenda katika wanawake,(maadamu mtawafanyia insafu) wawili au watatu au wane. Na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu basi oeni mmoja tu. Au wekeni masuria wale ambao mikono yenu ya  kuume imewamilika”.

Sunna imekuja katika kauli na vitendo vyake Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie. Kitendo ni kuowa kwake -rehema za Allah na amani zimshukie- tokea alipokuwa umri wake miaka ishirini na tano mpaka kufa wake. Alioa wake wengi. Amemhalalishia Allah Subhanahu Wataala wake aliotaka kuoa bila ya kumuwekea kikomo(idadi ya wake)  fulani na amekufa na hali ana wake tisa.  Amehimiza Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- umma wake kuowa katika kauli yake:

 ( إذا خطب إليكم الكفء فلا تردوه فنعوذ بالله من بوار البنات )

"Akija kuposa kwenu aliokuwa kufuu yake basi msimrudishe. Kwani twajikinga kwa Allah na kudoda kwa watoto wa kike”.


Katika hadithi hii wahimizwa wazazi kuharakisha kuwaoza watoto wao wa kike na wale wanaume waliokuwa sawa nao (Akiffaa) wale aliowabainisha Mtume wetu -rehema za Allah na amani zimshukie- katika kauli yake-:

 (الأحرار من أهل التوحيد كلهم أكفاء إلا أربعة : المولى والحجام والنساج والبقال )

 “Waliokuwa huru katika watu wa tawheed wote "Akiffaa" isipokuwa wane:- Mtumwa, anaepiga chuku (al-hajjaam), mfumaji (annassaaj) na ajitwikae kapu kichwani akiuza mboga au nafaka (al-baqqaal).”


Imepokewa kutoka na Anas bin Malik radhi ya Allah Subhanahu Wataala iwe juu yake,  amesema:-

 ( كان رسول الله صلى الله عليه وسلم يأمر بالباءة وينهى عن التبتل نهيا شديدا فيقول تزوجوا الودود الولود فإني مكاثر بكم الأنبياء يوم القيامة )

  "Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- alikuwa anaamrisha kuoa na anakataza kwa ukali sana kukaa bila ya kuoa, na akisema :- "Oeni wanaopendeka katika wanawake, wanaozaa kwani mimi nitajisifu kwa wingi wenu kwa Manabii siku ya kiyama."


Amesema Abu Saeed: Amesema Mtume  wa Allah -rehema za Allah na amani zimshukie:

 ( تنكح المرأة لدينها ولمالها ولجمالها ، خذ ذات الدين والخلق تربت يداك ) وفي رواية : ( فاظفر بذات الدين تربت يداك)                                                                                 

"Aolewa mwanamke kwa dini yake, kwa mali yake na kwa uzuri wake mchague yule mwenye dini na tabia nzuri kusibu kheri mikono yako."


Maana yake anaeoa mwanamke kwa uzuri wake huwa baada ya muda huisha hamu nae kwani kawaida kila kinachotumiwa huisha hamu. Kwa hiyo utaona wale mafasiki huwa na mke mzuri lakini akija akiona mwanamke wa nje njiani husema: - Leo nimeona mwanamke sivyo alivyokuwa mzuri kama paa (ghazaal) kwa uzuri au maneno kama haya hata akiwa sura yake mbaya lakini huwa anampambia shetani akawa hashughuliki kumtizama mkewe halali yake kwa sababu kishachoka nae.


Kadhalika anaemuoa mwanamke kwa mali yake huenda akafukarika au kikatokea kitu katika hiyo mali kuizuia isifike kwa huyo mwanamme, au yeye mwanamke akakataa kumpa mali yake, basi hapo hutoweka ile sababu iliyomfanya avutike kumuoa huyo mwanamke, hapo ndipo anapomchukia au kitu cha mwisho huacha kumpenda basi kutakuwa wapi kushikamana?


Na katika hadithi iliyomo katika Musnad Imam Ar-Rabii:

Anaolewa mwanamke kwa mambo manne …” na hilo la nne ni kwa ukoo na heshima yake. Na anaeoa kwa sababu hii huenda huyo mwanamke akajifakharisha na akatakabari juu yake na kumdharau, basi hayatadumu mashikamano baina yao ikiwa mume pia ni mwenye heshima.  Amma kama akimuoa kwa dini yake basi dini ndio inayobakia na kwa kubakia kwake yabaki mazoea na mapenzi baina yao.  Kwa sababu kufikiria akhera kwa wote wawili ni zaidi kuliko dunia na khasa ikiwa mume kama yeye (mkewe) katika kukamata dini, kwani kikitokea kitu chochote baina yao upesi watafikiria kauli ya Allah Subhanahu Wataala:


النساء: ١٩

“Na kama mkiwachukia basi (msiwaache) kwani huenda mkakichukia kitu na Allah ametia kheri nyingi ndani yake.”  Aya 19 sura Al-Nisaa na kauli yake Allah Subhanahu Wataala:


الطلاق: ٦

"Na shaurianeni kwa wema" Aya 6 Sura At-Talaaq


Na kauli yake:


البقرة: ٢٢٩

"Kisha ni kumweka kwa vizuri au Kumwacha kwa Ihsani."

Aya 229 Sura Al-Baqarah

                            

Na nyinginezo katika aya zinazofundisha vipi kushikana baina ya mume na mke.

Na kauli yake Mtume wa Allah –rehema za Allah na amani zimshukie:

 ( لا يفرك مؤمن مؤمنة إن كره منها خلقا سره منها آخر )

“Asimbughudhi Muumin (mwanamme) Muumin (Mwanamke), akichukia tabia moja yake atapendezewa na nyingine.”


Hadithi zinazovutia katika ndoa ni nyingi na inakutosha kuwa mwislamu anahifadhi kwa ndoa heshima na dini yake:

 (ومن تزوج فقد أحرز نصف دينه فليتق الله في النصف الآخر )

(Na anaeoa amepata nusu moja ya dini yake basi amche Allah katika nusu iliyobakia).


Amesema Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie:

 (النكاح سنتي فمن رغب عن سنتي فقد رغب عني )

"Ndoa ni Sunna yangu basi yule anaekataa sunna yangu hakunitaka mimi".


Na amesema:

( النكاح سنتي فمن أحب فطرتي فليستن بسنتي )

"Ndoa ni Sunna yangu basi anaependa fitra yangu (maumbile aliyomuumbia Allah Subhanahu Wataala binaadamu ambayo ni ya Kiislamu) basi ashikamane na sunna yangu (Ya ndoa)”, ameitoa Ibn Abbas.


Vile vile amesema :

 ( تناكحوا تكاثروا فإني أباهي بكم الأمم يوم القيامة حتى بالسقط )

“Oaneni, mjifanye muwe wengi kwani mimi nitajisifu kwa ajili yenu mbele ya umma nyengine siku ya kiyama hata kwa kilichoharibika (kutokana na mimba)”


Na amesema:

 ( إذا أتاكم من ترضون دينه وخلقه فزوجوه ، إلا تفعلوا تكن فتنة في الأرض وفساد كبير)

"Akiwajia yule mnayeridhia dini yake na tabia zake basi muozesheni, ikiwa hamkufanya hivyo itakuwa fitna katika ardhi na uharibifu mkubwa".


Hapa waamrishwa wazee wa watoto wa kike  wasighalishe mahari. Mtastaajabu nikiwaambia kuwa katika wakti huu wako wanaofuata hadithi hii tukufu. Ameniomba kijana mmoja nimposee mwanamke kutoka kwa mmoja katika watu wema tunaejuana kabla. Basi nilipomuendea na nikamzungumzia jambo hili akanijibu bila ya kusita:- Muoze na kile anachotaka kumpa mkewe (mahari) na ampe. Je anaweza mtu kuamini kuwa haya yametokea katika wakti wetu huu?!


Na katika kutimia Imani yake kasema: Niwambie kitu nimeogopea nisije nikawaghishi ambacho ni ila ilikuweko katika mtoto wa kike. Huyu mtoto wa kike amefanyiwa operasheni wa wengu labda imeacha athari katika mwili wake.  Lakini juu ya yote hayo yeye hivi sasa mzima. Tizama hii amana, kisha tukawa peke yetu mimi na yeye tu nikamuuliza kwa nini ukatufanyia uzuri wote huu?  Akasema Je! Inawezekana wewe unijie kumposea mtu wamjua kisha nikurudishe? Basi itakuwa mimi nimeipinga hiyo hadithi (iliyotajwa hapo nyuma). Hapa tena ndio akauliza juu ya mtoto wa kiume na juu ya ukoo wake, na tabia zake? Allah Subhanahu Wataala amjaze kheri.


Kinashabihiyana na kisa kama hichi kisa kilichotolewa juu ya Saeed bin Al-Musayyab katika Mataabiina wakubwa kuwa mwanafunzi wake alifiwa na mkewe, basi akaacha kwenda kusoma kwake kwa masiku kisha aliporejea akamuuliza Shekhe sababu ya kuacha kwenda kusoma akajibu mke wangu amefariki. Akamuuliza bado hujaoa baada yake? Akajibu bado.  Akamwambia njoo nikuozeshe mtoto wangu wa kike, basi akamuozesha na ilipofika usiku akamwambia mama yake mtoto mtayarishe, akamtayarisha akamuamrisha ende nyuma yake. Akamgongea mwanafunzi wake mlangoni na hakuwa na khabari yoyote wala hakujitayarisha kumpokea arusi wake.  Akamwambia mchukuwe mkeo usilale bila ya mke.  Basi katika visa viwili hivi kuna mfano mzuri wa kuchukuliwa.

Na vile vile  amesema Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie:

 ( من نكح لله وأنكح لله استحق ولاية الله )

"Anaeoa kwa ajili ya Allah na kuozesha kwa ajili ya Allah amestahiki mapenzi ya Allah." Ameitoa Muaadh.


Na amesema:

(كل عمل ابن آدم ينقطع بعد موته إلا من ثلاث ولد صالح يدعو له ..)

"Kila kitendo cha binadamu kinakatika baada ya mauti yake isipokuwa---" kutokana na mambo matatu hayo mtoto mwema anamuombea dua”

Na hili halipatikani isipokuwa kwa ndoa.


Asema Ibn Abbas: "Na hayatimii manasik ya anaekwenda kuhiji isipokuwa kwa ndoa." Alikuwa akiwakusanya vijana wake na kuwaambia "Mkitaka kuoa basi nitawaozesha kwani mja akizini hutolewa Imani kutoka moyoni mwake."


Ametoa Al-ghazali katika "Al-Ihyaa":- kuwa Bishr Ibin Al-Harith ameonekana katika ndoto baada ya kufa kwake, akaulizwa amekufanya nini Allah akasema: zimepandishwa daraja zangu katika al-Janna, na sikufikia daraja za watu waliooa.  Tukamuuliza amefanya nini Abu Nasser Attammaar? Akajibu amepandishwa juu yangu kwa daraja sabiini, tukamwambia kwa nini tulikuwa tunakuona juu yake kwa amali, akajibu kwa subra yake juu ya watoto wake wa kike na familia yake kwa ujumla.  Na sababu yake na imesemwa kuwa :  Fadhli ya aliyeoa juu ya mjane ni kama fadhli ya mujaahid juu ya yule aliebakia nyuma hakwenda kupigana vita katika njia ya Allah Subhanahu Wataala, na vile vile rakaa moja ya mwenye kuoa ni bora kuliko rakaa sabiini za yule mjane.


Juu ya kuhimiza kwetu vijana waoe bila shaka twaelewa hali zao ngumu za kipesa na ughali wa mahari, lakini Muislamu akikusudia kufanya kitu kwa kutaka radhi ya Allah basi humrahisishia na kumsaidia.  Kwani aliyemiliki vilivyomilikiwa asema:


الطلاق: ٢ - ٣                       

"Anaemuogopa Allah, humtengenezea njia ya kuokoka (na kila balaa).  Na humpa riziki kwa namna asiyoitazamia” . Aya ya 2-3 Sura ya At-Talaaq.           

الطلاق: ٤

“Na anayemuogopa Allah humfanyia mambo yake huwa mepesi" Aya ya 4 sura ya At-Talaaq.


Kama ingekuwa vijana wangetia moyoni haya na wakaziamini hizi aya za Qurani basi yangekuwa mambo yao mepesi lakini yasikitisha kuwa wao wasema:-

Twaeka katika usalama uhai (maisha) wetu na twamaliza masomo yetu nini maana ya maneno haya isipokuwa kutokuwa na yakini kuwa Allah ndio mwenye kugawa riziki wafikiria kuwa wakipata kazi basi wamekwisha garantii uhai wao anaweza kiumbe chochote kudhamini riziki ya mwengineye? Na yeye mwenyewe riziki yake imedhaminiwa na Allah Subhanahu Wataala:


الذاريات: ٥٨

“Kwa yakini Allah ndiye Mtoaji wa riziki Mwenye nguvu, Madhubuti.”


Inasemekana kuwa mtu mmoja mwema alikuwa afikiriya juu ya riziki basi likampasukia jiwe gumu akaona ndani yake mdudu na ndani ya mdomo wake kuna jani la kijani(bichi). Basi Ametakasika Aliyeumba na Ametakasika Mtoaji wa riziki.

Amesema Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie:

(من ترك التزويج مخافة العيلة فليس منا )

“Anayeacha kuoa kwa kuogopa kufukarika si katika sisi”

Ameitoa Abu Saeed.


Amma aseme maneno haya kijana kisha afanye vitendo vibaya huyu mwisho wake si mzuri na ajifanyia ubaya nafsi yake na mujitamaa wake.


Amma juu ya vijana wa wakti wetu wa sasa naizuia kalamu yangu kuandika juu yao na nasema: "La hawla wala Quwata Illa Billahi" na namuomba Allah Subhanahu Wataala anihidi mimi na wao.

Amesema Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie:

 ( الدنيا كلها متاع وخير متاع المؤمن الزوجة الصالحة )

“Dunia yote ni manufaiko ya kupita na bora ya manufaiko ya Muumini ni mke mwema (aliyeshika dini yake).”


Na alishtaki mtu mmoja kwa Mtume wa Allah -rehema za Allah na amani zimshukie- juu ya ufakiri aliokuwa nao, basi akamuamrisha aowe kwa hiyo katika sharia ya Allah mke huwa msaada kwa mumewe kutokana na ufakiri. Amma katika maoni ya vijana wa leo na kwa yale waliyoshawishiwa na mashetani wao mke huwa ndie anayesababisha ufakiri kwao, nani basi katika wao ana haki ya kufuatwa. Amesema Mtume wa Allah -rehema za Allah na amani zimshukie:

 ( شرار أمتي عزابها )

"Wabaya wa umma wangu ni wale walio wajane (waliokuwa hawana wake au hawana waume).”


Alitamani Imamu wetu Jabir Bin Zayd (Radhi za Allah ziwe juu yake) afe mtoto wake kabla yake na afe yeye kabla ya mkewe. Akaulizwa juu ya matamanio haya akasema: "Nimetamani afe mtoto wangu wa kike kabla yangu hata awe katika mizani yangu siku ya kiyama na nife mimi kabla ya mke wangu ili nisiishi mjane (bila ya mke)”. Na katika haya twaona fadhila ya kufiwa mtu na mtoto mdogo.


Yasemekana kuwa mmoja katika watu wema alitakiwa aowe akakataa. Basi siku moja akaamka usingizini asema: Niozesheni, niozesheni akaulizwa juu ya hayo akasema: nimeota kuwa kiyama kimeshasimama nami nina kiu kali ilio karibu ya kukata koo langu, basi tulivyokuwa sisi tuko katika hali hii wakatokea watoto wakiuka huu mkusanyiko wa watu katika mikono yao mabirika ya fedha nao wawapa maji ya kunywa baadhi ya watu na wawaacha kuwapa maji wengi wao. Basi nikanyoosha mkono kwa mmoja kati yao kumwambia nipe maji kwani nina kiu kali sana, akanijibu huna mtoto kati yetu kwani sisi twawanywesha baba zetu. Nikamuuliza nani nyie, akanijibu sisi ni katika waliokufa katika watoto wa waislamu.


Basi anaeruzukiwa mke katika waislamu amshukuru Allah Subhanahu Wataala kwa fadhli zake, na ajuwe kuwa Allah Subhanahu Wataala ndie Bwana wake aliemhifadhi kutoka na kila michezo na mitelezo (mianguko), na ni wajibu juu yake kuchukulia umuhimu haki ya hii neema na asione kuwa ni ndogo kwani kwa hakika ni kubwa, na kila neema za Allah Subhanahu Wataala ni kubwa.

Na atie nia kwa ndoa hii kufuata sunna na kuhifadhi sharafu na kutotizama yaliyoharamishwa, basi akiingia kwa mkewe na wakaachwa peke yao afanye kama vile sharia inavyoamrisha.


Na wakati unapokuwa peke yako na mkeo na ukatumaini kuwa hakuna mtu mwengine pamoja na nyie na mkajifungia mlango, msogeleane na mkamate mkono wake huku ukimuuliza hali yake na hali ya baba yake na mama yake na kila kinachokuhudhurikia katika maneno ya upole na ulaini.


Mwanamwari ni bora kwa mwenye uwezo kutokana na mahimizo ya Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- juu yake.

حديث عبد الرحمن بن عوف لما جاء وعليه أثر عرس فسأله النبي صلى الله عليه وسلم ، قال تزوجت ، قال له : أبكرا أم ثيبا ، قال بل ثيب ، قال له : هلا بكرا تعضها وتعضك ، وقال عليه الصلاة والسلام ؟ عليكم بالأبكار فإنهن أطيب أفواها وأنتق أرحاما

Katika hadithi ya Abdurrahman bin Awf wakati alipokuja na athari ya kuoa imedhihirika juu yake. Akamuuliza Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- akamjibu nimeoa. Akamuuliza: Ni bikra au aliyekwishaolewa akamjibu: aliyekwishaolewa. Akamwambia si bora bikra umng’ate naye akung’ate?.

Na akasema sala na salamu ziwe juu yake:

(عليكم بالأبكار فإنهن أطيب أفواها وأنتق أرحاما )

"Shikilieni kuoa wanawari kwa hakika harufu za midomo yao ni nzuri na rahimu  zao ni safi zaidi".


Na kila ukikithirisha utangulizi(mipapaso) wa jimai ni bora hata ikikuchukulia muda mrefu, usiharakishe na hata kama ukakhainiwa na kuteremsha (kwa manii) katika wakti huu basi nenda ukajioshe najasa, sukutua na jitie maji puani (kama katika kutawadha) na mrudie mkeo uendelee kazi yako hata ujione kuwa umehisi raha na mkeo amezidi hamu yake juu yako basi hapa  ndio ukidhi haja inayotakiwa.

Kisha sema:

"أعوذ بالله من الشيطان الرجيم بسم الله الرحمن الرحيم "                          

 "Audhu Billahi Mina Shaytani Rajiim, Bismillahi Rrahmani Rrahiim.”


Basi shetani katika hali hii akisikia jina la Allah hukimbia na amma sivyo akaa pamoja na nyie na anaingilia katika mambo yenu kama anavyoweza kuingilia na kuharibu.  Na vile vile katika kutaja Allah ni kufuata sunna na kumshinda shetani na ukisahau kusema hapo mwanzo sema utapokumbuka.

" بسم الله على أوله وآخره "                                                

Bismillahi Ala Awalihi Wa Akhirihi, kama ilivyokuja katika sunna .


Baadhi ya Mashekhe (Ulamaa) wasema: Ukiwa peke yako na arusi wako usali rakaa mbili kabla ya kumfanya chochote kama shukrani kwa Allah Subhanahu Wataala. Kwa hakika jambo hili sio kila mtu anaweza kulifanya, na akajikalifisha mtu kulifanya hatajuwa nini la kusema katika sala yake, kwa sababu moyo wake umeshughulishwa na kitu kingine, basi si lazima kufanya hivyo walakini hana budi kumtaja Allah kwa hali yeyote ile.


Katika mambo nadra kutokea lile alilolitaja Al-Ghazaaliy katika kitabu chake "Al-Ihyaa": Ameingia mtu katika watu wema kwa bibi arusi wake akamwambia nasali rakaa mbili kumshukuru Allah, alipoingia katika sala akamsahau bi arusi wake akangojea mkewe mpaka asubuhi. Na katika usiku wa pili, wa tatu na wa kumi hivyo hivyo mpaka ikiwapitia miaka arubaini bado haja muingilia mkewe.  Tuseme huyu mtu alitokea kweli kufanya haya basi subra ya huyu mwanamke vile vile ilikuwa ya ajabu.


Tulikuwa twamjua mtu ambaye ameoa mwanamke wangali bado wadogo na wamekufa wamekwisha pindukia umri wao miaka sabiini na wakti wote huu hakuwahi huyu mwanamme kufunua nguo ya mkewe. Na hakuna aliyejua habari hii isipokuwa ilipokuwa karibu ya mauti yao, siku moja ukaanguka ushungi wake mbele ya mumewe basi akasema: Mungu wangu nakuomba sitara yako imeanguka hijabu yangu mbele ya Mohammed kukusudia mumewe. Akaulizwa vipi wasema hivyo naye ni mumeo?  Akajibu nimeona haya kwani ni mara ya kwanza yeye kuona kichwa changu na shingo yangu.  Na alikuwa mwanamke mwema wamesalimika watu na ulimi wake, akisali sala za usiku basi si ajabu kusubiri na kujistiri (kusitiri).


Basi ukishamaliza haja yako na bi arusi wako bado hajatosheka usifanye haraka ya kunyanyuka, kwani hiyo katika tabia njema ya kumfikiria mkeo. Hebu fikiria kama yeye angetosheka na wewe bado hujatosheka kisha akasimama akakuwacha vipi ungeridhika?  Shika kwa mkono wako wa kushoto kitambaa au tissue (karatasi) na yeye vile vile akamate tissue yake basi ukinyanyuka kutokana naye ifute hiyo najasa kwa hicho kitambaa na  yeye vile vile afanye hivyo hivyo ama sivyo itawaingia katika nguo zenu au katika godoro (mahala mnapolala) ambapo itahitajia kuiosha kwani ni najisi.  Wala msijifutie kitambaa kimoja (baina ya mume na mke) kwani kitendo kama hichi kinasababisha kuchukiana. Na inapendelewa usipite mchana au usiku wa Ijumaa umjaamii mkeo kwa fadhila anaeoga usiku wa kuamkia Ijumaa au mchana kua anaghufiriwa dhambi zake.


Na kumuingilia mkeo kwa mkao wowote ule inajuzu.

Aya 223 – Suratul Baqarah.


البقرة: ٢٢٣

"Wake zenu ni kama konde zenu, basi ziendeeni konde zenu mpendavyo."


Na ukitaka kurudia tena nenda ukaoshe najasa kisha usukutue na kustanshiq (kutia maji mdomoni na puani na uyapeleke ndani kama iwezekanavyo kisha uyatoe )  na unywe maji vinywa vitatu halafu umrudie mkeo. Vivyo hivyo ukitaka kurudia mara ya tatu na ya nne, na haikulazimu kuoga janaba kwa kila unavyofanya kitendo hicho, bali uoge mara moja mwisho baada ya kutimiza haja zetu wakti wote unapotaka mwanzo wa usiku au mwisho wake, lakini usilale nawe una najasa. Imetolewa kuwa Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- amewapitia wake zake wote usiku mmoja na hakuoga ila baada ya kuwapitia wote.  Na tumebainisha namna ya kuoga janaba katika juzuu ya kwanza ya kitabu hiki, na ikiwa wewe wajua kuoga janaba na mkeo hajui basi ni wajibu wako kumfundisha.


Surat Tahriim Aya 6:


التحريم: ٦

"Enyi Mlioamini! Jiokoeni nafsi zenu na watu wenu na moto"


Tumetaja huko nyuma kuwa inamlazimu mwanamume akitaka kuoga janaba kwanza akojoe hata yatoke yaliyobakia katika dhakar yaani manii. Vile vile inamlazimu mwanamke kutia vidole vyake katika faraji yake ili atoe manii ya mwanamme iliyoganda hapo aitoe nje ya rahim kwa sababu mwanamke akikojoa havitoki kwa huo mkojo vile vilivyokuwa katika faraji (kama katika hali ya mwanamme) kwani mahala pa kutokea mkojo sio pale pa jimai na hedhi. Lazima azingatie kitu hichi kwa sababu ikiwa hakuyatoa hayo masalio ya manii kwa vidole vyake, yatatoka baadaye na kunajisi nguo zake.


Wako baadhi waliokuwa hawataki mtoto basi humwaga nje manii (nje ya mkewe).  Wanasema Maulamaa:- Mwanamke aliyekuwa huru hamwagiwi nje (na mumewe) isipokuwa kwa Idhini yake na kitendo hicho kinakuwa wakati anapokaribia mwanamme kukojoa (kutoa manii) aitoa dhakar yake akamwaga nje ya faraji ya mwanamke.

Hukumu yake inajuzu wakikubaliana  mume na mke na haiwi isipokuwa kwa jambo lililokuwa dharura sana kama kwa kuogopea siha ya mwanamke isiharibike kwa sababu ya kushika mimba na kuzaa.


Amma watumwa wanawake (masuria) inajuzu kuwamwagia nje bila idhini yao na walimshauri masahaba radhi za Mola Subhanahu Wataala ziwe juu yao Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- katika jambo hili la kumwaga nje ulipokuwa ujane umewazidia.


Ametoa al-Rabii Rehema za Allah Subhanahu Wataala ziwe juu yake katika Musnadi wake kutokana na Jabir bin Zayd kutokana na Abi Saeed Al-Khudry amesema:

 (خرجنا مع رسول الله صلى الله عليه وسلم في غزوة بني المصطلق فأصبنا سبايا فاشتهينا النساء واشتدت علينا العزبة فأردنا أن نعزل فقلنا نعزل وفينا رسول الله قبل أن نسأله عن ذلك ، قال فسألناه فقال : ما عليكم أن لا تفعلوا ، فما من نسمة كائنة إلا وهي كائنة إلى يوم القيامة )                                                                         "Tumetoka pamoja na Mtume wa Allah -rehema za Allah na amani zimshukie- katika vita vya Banii Mustalaq tukapata mateka (ya wanawake) tukatamani wanawake na ukatuzidia ujane na tukataka  kutoa nje tukasema tutatoa nje na baina yetu Mtume wa Allah kabla hatujamuuliza suala hilo, akasema basi tukamuuliza akasema: "Si juu yenu ikiwa hamtafanya kwani hakuna nafsi iliyoandikiwa kuweko ila itakuweko mpaka siku ya kiyama."


Imetolewa na Anas kuwa mtu mmoja amemuuliza Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie:

 ( لو أن الماء الذي يكون منه الولد أفرغته على صخرة لأخرج الله منها ولدا أو يخرج الله منها ولدا ، وليخلقن الله نفسا وهو خالقها )

“Kama ingelikuwa yale maji yaliyoandikiwa kutoka ndani yake kiumbe (mtoto) ungeyamwaga juu ya jabali basi Allah Subhanahu Wataala angetoa kutokana nalo (hilo jabali) mtoto na hakika ataumba Allah Subhanahu Wataala nafsi naye ndiye Muumbaji wake.”


Na katika "Muslim", imetokana na Jabir

 (أن رجلا أتى النبي صلى الله عليه وسلم فقال : إن لي جارية هي خادمنا وسانيتنا ، وأنا أطوف عليها ، وأنا أكره أن تحمل ، فقال : اعزل عنها إن شئت فإنه سيأتيها ما قدر لها فلبث الرجل ثم أتاه فقال : إن الجارية قد حملت ، فقال : " قد أخبرتك أنه سيأتيها ما قدر لها ".                                                        

kuwa mtu mmoja alimjia Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- akasema hakika nina kijakazi (mtumwa mwanamke) (page 156) naye ni mfanya kazi wetu nampitia (kwa kumwingilia) na nachukia ashike mimba, akamjibu jitenge naye (yaani mwaga nje) ukitaka kwani kwa hakika  kitamjia kile alichoandikiwa kumjia. Kisha akakaa yule mtu muda halafu akamjia Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- akamwambia : yule kijakazi amepata mimba, akamjibu: “Nimekwambia kuwa kitamjia tu kile alichoandikiwa.”


Kama huwezi kuowa na huwezi kusubiria jimai (kuingilia mwanamke) basi jisaidie kwa kufunga kama alivyotufundisha mwalimu wetu -rehema za Allah na amani zimshukie- hayo kwa kauli yake:

 (من خاف من شدة الميعة فليصم فإن الصوم له وجاء )

"Yule anayeogopa hamu kubwa ya jimai ( na kungilia) basi afunge kwani funga humchokesha kwa hivyo inavunjika hamu yake  ya jimai."


Amesema Allah Subhanahu Wataala katika Aya ya 69 Sura Al-Ankabut:

العنكبوت: ٦٩

"Na wale wanaojitahidi kwa ajili yetu kwa yakini tunawaongoza kwenye njia zetu.   Na bila shaka Allah yu pamoja na wafanyao mema."


Allah amewapa mtihani wanawake katika hedhi (vipindi vya mwezi) na nifasi (ujusi – baada yakuzaa) na katika hali mbili hizi imeharimishwa kumwingilia mwanamke. Ama kustarehe nae katika sehemu zilizobakia haikukatazwa isipokuwa ajiepushe na utupu na aweke juu yake kitambaa. Na ameruhusiwa amruhusu mumewe sehemu yoyote nyengine isipokuwa duburi (nyuma) kwani hiyo ni haramu wakti wote, napo ni mahala pa uchafu si mahala pa uzalishaji, basi pakimbie mahala hapo mkimbio wa kondoo kutokana na chui. Na ajifundishe mwanamke vipi ajioshe na hedhi na nifasi nako kama kujiosha na janaba vile vile. Isipokuwa inamlazimikia kuzifungua nywele zake katika hedhi na nifasi lakini haimpasi hivyo katika janaba isipokuwa anazichovya nyewele zake mpaka ziingie maji. Vile vile inampasa kutia vidole vyake katika utupu wake ili aisafishe kutokana na damu kama anavyojisafisha na janaba kwani njia yao ni moja.


Na wanawake wako makundi mawili katika kujua tohara kutokana na hedhi na nifasi (ujusi), baadhi yao watoharika kwa kutoka maji meupe na yaitwa maji ya tohara nayo ni maji meupe, mepesi na yafanana na chokaa hutoka baada ya kukatika damu, na baadhi yao watoharika kwa ukavu, nayo ni kukatika kwa damu na huyu si kawaida yake kutoka maji meupe. Basi aliyokuwa kawaida kutoharika kwa maji meupe asijitoharishe kwa ukavu, na hapana budi ayaone hayo maji meupe na ikiwa hakuyaona na  hali damu imekwishakatika basi angojee siku mbili kisha aoge. Ikiwa litarudia jambo hili mara tatu (kutoyaona maji meupe) basi abadilishe kawaida yake kuwa baada ya kujitoharisha kwa kuona maji ajitoharishe kwa ukavu.


Na muda wa tohara hauwi chini ya siku kumi na pindi akiona damu kabla ya siku kumi basi asiichukulie kuwa hedhi isipokuwa hiyo ni istihaadha na hawachi kwa hiyo sala wala saumu mpaka afike ule wakti wa kawaida kupata hedhi, hapo inakuwa hukmu yake ya hedhi badala ya istihaadha,  basi anawacha sala na saumu. Na mambo ya hedhi na tohara yako mengi sana hayatoshi kuzungumziwa katika mukhtasari (ufupi wa maelezo) huu, lakini juu yake mwanamke kuuliza juu ya dini yake wala asipuuze au kuona haya kwani Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- amewasifu wanawake wa ki-Ansaar wakati alipouliza mmoja wao basi akasema :

 (رحم الله نساء الأنصار لم يمنعهن الحياء أن يتفقهن في الدين )

 "Allah Amewarehemu wanawake wa ki-Ansaar haikuwakataza haya kujifundisha mambo ya dini yao"

Na sababu ya hadithi hii ni kuwa mwanamke mmoja amemuuliza Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- akasema:

 (برح الخفاء يا رسول الله ، ترى المرأة في النوم ما يرى الرجل ، أعليها الغسل ؟ فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم : عليها الغسل إذا أنزلت ) وفي رواية ( أن أم سليم امرأة أبي طلحة الأنصاري جاءت إلى رسول الله صلى الله عليه وسلم فقالت : يا رسول الله : إن الله لا يستحي من الحق ، هل على المرأة غسل إذا هي احتلمت ؟ قال نعم : إذا رأت الماء )                                                

"Kimedhihiri kilichostirika ewe Mtume Wa Allah, anaona mwanamke katika usingizi kile anachokiona mwaname, Je! ni juu yake kuoga ? Basi akasema Mtume wa Allah ni juu yake kuoga akiteremsha (yaani akikojoa)"


Na katika hadithi moja: kuwa Um Saliim mke wa Abi Talha Al-Ansaariy alikuwa kwa Mtume wa Allah -rehema za Allah na amani zimshukie- akasema: "Ewe Mtume Wa Allah hakika Allah haoni haya kutokana na haki, Je inampasa mwanamke kuoga ikiwa akiota? Akasema: Ndio kama akiona maji (akikojoa).”


Amesema Jabir: Imekuja juu ya suala hili  kutokana na masahaba wengi kuwa haimlazimu kuoga kama mwanamume bali inamtosha tu kutia udhu.


Hapa kuna jambo ambalo linatakiwa kuzingatiwa nalo: Ikiwa mwanamme ataka kumuingilia mkewe na ukagusa utupu wake utupu wa mwanamke pamoja na kuingiza mbele ya dhakari kisha akarudi pasi na kuendelea na jimai na lau kwamba hakukojoa basi inawapasa waoge janaba, na pengine watu wengine watasema kuwa haipasi kuoga janaba isipokuwa baada ya kutoka manii nalo ni kosa kwani imekuja kutokana na sunna kinyume na hivyo.


Na imetokana na Rabii rehema za Allah ziwe juu yake – kutoka kwa Abu Ubaida kutoka kwa Jabir Bin Zayd kasema:

 ( سألت عائشة هل كان يغتسل رسول الله من جماع ولم ينزل ، قالت عائشة : كان رسول الله صلى الله عليه وسلم يصنع بنا ذلك ويغتسل ويأمرنا بالغسل ويقول الغسل واجب إذا التقى الختانان ) وقال جابر قالت عائشة رضي الله عنها (يقول النبي صلى الله عليه وسلم اذا قعد الرجل من المرأة بين شعبها وأجهدها وجب الغسل )

'Nimemuuliza Aisha Radhi za Allah Subhanahu Wataala ziwe juu yake Je! Alikuwa akioga Mtume wa Allah -rehema za Allah na amani zimshukie- kwa jimai ambayo hakutoka manii, akasema Aisha alikuwa Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- afanya na sisi kama hivyo kisha huoga na atuamrisha sisi kuoga (janaba) na anasema: “Kuoga ni wajibu zikiingiana tupu mbili hadi zikakutana sehemu zao zinazotahiriwa" na akasema Jabir amesema Aisha Radhi za Mola ziwe juu yake amesema Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie: “Pindi mwanamme atakapomkalia mwanamke juu ya mapaja yake na akatia dhakari katika utupu wake basi wanawajibika kuoga (wote wawili)”.'


Ni haramu kwa mume na mke kutoa habari juu ya yale yanayotendeka baina yao katika usiri wao, kwani anaefanya hivyo ni kama anaemjamii mke wake sokoni au barabarani na hakuna tofauti yoyote.


Asimwingilie mkewe naye amelala kwani yatokea mambo yanahusiana na kitu hichi :

1)             Inampita ile ladha ambayo inapatikana kutokana na kitendo hicho.

2)             Pengine ameingia katika kipindi chake cha mwezi (hedhi).

3)             Pengine asijue kuwa ana janaba na huenda akasali  na janaba yake.

4)             Inalazimika kwa mume kumfundisha mkewe mambo ya dini ikiwa yeye ni mjuzi zaidi.


المائدة: ٢

"Na saidianeni katika wema na utawa (Ucha Mungu)"


Allah Subhanahu Wataala amemsifu Nabii wake Ismaeel (A.S.) kwa kauli yake:


 مريم: ٥٥

"Na alikuwa akiwaamrisha watu wake sala na zaka na alikuwa mridhiwa mbele ya Mola wake"


Na Mola amemuamrisha Mtume wake -rehema za Allah na amani zimshukie:


 طه: ١٣٢

"Na waamrishe watu wako kusali, na uendelee mwenyewe kwa hayo, hatukuombi riziki bali sisi ndio tunakuruzuku.  Na mwisho mwema utawathubutikia wamchao Mungu."

                                                                            

Na yaungamana na Sala na Zaka mambo yote ya dini lakini sababu ya kutajwa makhsusi ni kuwa ndio nguzo mbili za msingi katika nguzo za Kiislamu kwani ni wajibu wa Muislamu kuzihifadhi hizo nguzo mbili kutokana na mambo ambayo hayajuzu bali hata kutokana na yale yaliokuwa hayapendezi.


النساء: ٣٤

"Wanaume (wawe) ni walinzi wa wanawake, kwa sababu Allah amewafadhilisha baadhi yao kuliko wengine, na kwa sababu ya mali zao wanazozitoa."


Katika wakati wetu huu imefunguka milango ya shari ambayo wengi miongoni mwa wanawake wameingia ndani yake, hawakuchunga heshima zao wala hawakuhifadhi dini zao. Nimetangulia kusema kuwa hakuna aliyemharibu mwanamke isipokuwa mwanamme: na zilipoanguka haiba zao na ukaondoka wivu wao juu ya wake zao wakawa kama wanyama bali baadhi ya wanyama bora kuliko wao, kwa sababu wako katika wao wawaonea wivu majike yao.  Walipofika katika daraja hii ( ya kutokuona wivu) basi wakatoka wanawake zao kutokana na lile umbo ambalo Allah Subhanahu Wataala amewaumba, ukaharibika mwelekeo wao na kutawanyika. Wengine wakakamata kazi pamoja na wanaume wageni (sio maharimu wao), wengine wakatoka mabarabarani bila ya kujihifadhi miili na uchi wao, baadhi yao wanahudhuria mikutano na afungua mmoja wao mdomo wake mbele ya jamhuri atoa mashairi au ahutubia. Sisemi isipokuwa  إنا لله وإنا إليه راجعون  .


Wamekhitalifiana maulamaa juu ya mwanamke Je! Akataze mabaya? Wakasema baadhi yao sio asifanye hivyo kwa sababu itabidi anyanyue sauti yake, na kuwa malaika hakika wanalaani mwanamke ambaye sauti yake inatoka nje ya ukuta wa nyumba yake, vipi basi wale ambao wanawataabisha malaika wao kuwalaani kula wakati. Na wako miongoni mwao ambao wamejivua na uhuru (wa kikweli anayestahiki mwanamke wa Kiislamu) wakatoka kwenda kwa kawafeer (Hair Saloon or Beauty Saloon) na kitu gani kinachokujuulisha nini kawafeer imetoka jina lake kutokana na kufr.


Mwanamke anapoingia tu katika mahala hapa anakufuru, na huyo mtu anaefanya kazi hapo mahali akimgusa nywele zake amekufuru mara ya pili,  akimpunguza nywele zake amekufuru mara ya tatu. Hatimaye anatoka hapo mahali haikubakia kitu katika dini yake, na hurma (kukatazwa) ya kukata nywele za mwanammke ni kama mkatazo wa kukata ndevu za mwanamume sawasawa. Dalili ya nguvu ya hurma ya nywele za mwanamke kuwa anaempiga mwanamke katika kichwa chake ikaanguka nywele yake na ikiwa haikuota mahala pake nyingine basi lazima amlipe huyo mwanamke dia(faini), na kama hivyo kwa ndevu za mwanamme. Basi inakutosha kuwa sharia ya Kiislamu imeeka kwa mambo mawili haya diya ya muislamu mwanamme na akavipa daraja. Leo utakuta mwanamme asalimisha ndevu zake kwa kinyozi azikate au kuzinyoa na kadhalika mwanamke asalimisha nywele zake kwa kinyozi (yoyote yule akiwa mwanamke au mwanamme) azinyoe bila ya thamani bali wao walipa ujira wa kunyolewa. Basi inakutosha ile shari ya kusikia haya mambo bila ya wewe kuyafanya vipi hali ya yule anaepata riziki yake kwa pesa kama hizi na wala hajali shari yake.  Anasema: Anaewaita watu kumkosoa (kwa vile alivyojieka katika hali mbaya) basi watamkosoa katika yaliyo haki na yaliyo si haki na amesema vile vile: "Na haifai asili ya mtu kuwa ni Bani Hashim ikiwa yeye mwenyewe nafsi yake ya ovyo"


Umeona yale wanayoyafanya watu leo, utaona wanasoma sunna iliyotoharika lakini wanafanya kinyume ya hiyo sunna (mpango unaostaajabisha). Imeamrisha sharia kukata kucha na wao utawaona wazifuga, na kama hizo kucha hazioti kwa kawaida yake utawaona wazinunua madukani kisha wazipachika vidoleni mwao zikiwa kama kucha za tai (aina fulani ya ndege).  Imeamrisha sharia kufuga ndevu kubwa (kama ilivyokuja katika hadithi ya Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- na wao wazinyoa, na imeamrisha kukata sharubu na wao wazifuga, na Imeamrisha mwanamke kukaa nyumbani kwake naye katoka nje.


Azungumza mmoja katika Maulamaa wa Kiislamu asema: Kuwa siku moja alikuwa amepanda treni pamoja na binti yake na karibu yake kakaa mwanamke wa kizungu. Huyu mzungu akamzungumzia yule mtoto wa kike wa kimasri juu ya Omar Bin Al-Khatab, Radhi ya Allah iwe juu yake, na mwendo wake mzuri wa kusifika. Basi alipoondoka yule mwanamke, akamwambia baba yake: Nataka kitabu katika tarehe ya Omar bin Al-Khattab akamuuliza baba yake kwa nini? Akasema kwa sababu huyu mwanamke wa kizungu kanizungumzia juu ya Omar kwa hiyo kanitia hamu ya kujua tarehe yake. Akamwambia ewe binti yangu nimekuzungumzia yafika mara kumi juu ya Omar haikufaa kitu lakini wakati alipokuzungumzia huyu mzungu mara ukamsikiliza, je! Inataka tusiitie kufanya mazuri ila baada ya kuwaona wageni (waliokuwa si waislamu) wayafanya ndio sisi tuwaige?


Basi ndio hivi wajidai Waislamu kuwa wamepata uhuru kutokana na ukoloni, nchi zimepata uhuru lakini sio nyoyo zao, zimebakia chini ya ukoloni zinafanya kama wanavyoamrisha na kupenda vitendo vyao.


Tumetembea Ulaya, Umarikani, Mashariki ya Asia, China na Japan hatukuona mwandiko wa Kiarabu, kila mmoja aandika kwa lugha yake tu. Lakini tizama katika nchi za Kiarabu vipi wameitukuza lugha ya Kiiengereza na Kifaransa, hata yule anayeuza vinywaji baridi anaandika juu ya duka lake kwa Kiingereza ili kupata heshima kwa hiyo lugha. Basi Waarabu bado wameshikamana na maadui zao, na wao (maadui) wameshikamana na wengine (si waarabu). Kama ilivyosemwa:


Nimeshikana naye (mwanamke) naye kashikana na mwengine (mwanamme mwingine pasi yangu) na huyo mwanamme kashikana na mwanamke mwengine.


Basi mpaka lini tutakuwa katika hali kama hii. Wala usiulize juu ya kukata nyusi za wanawake na mengineo katika mambo ambayo sharia imekataza wazi wazi, kama ilivyotolewa na Ar-Rabii katika Musnadi wake amesema Abu Ubaidah kutokana na Jabir bin Zayd kutokana na Ibn Abbas Radhi za Allah ziwe juu yake  kuwa Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- amesema :

( لعن الله النامصة والمتنمصة ، والواصلة والمستوصلة ، والواشمة والمستوشمة ، والمتفلجات للحسن )

“Allah amemlaani mwanamke anaekata nyusi zake na yule anayempunguza huyo mwanamke nyusi na yule anayeongezea nywele zake ili ziwe ndefu na yule anayefanya kitendo hicho cha kuongeza nywele na yule anayejichora juu ya uso wake na mkono wake (mchoro ule maarufu uliokuwa hautoki) na yule anayechorwa. Na yule anayechonga meno yake ili awe na mwanya apate kuwa mzuri.”


Na ametoa Ar-Rabii kutokana na Abu Obaidah kutokana na Jabir bin Zayd amesema:

 (بلغني عن معاوية بن أبي سفيان قال وهو على المنبر عام حج : فتناول قصة من يد حرسي فقال : يا أهل المدينة : أين علماؤكم : سمعت رسول الله صلىالله عليه وسلم يقول : " إنما هلكت بنو إسرائيل حين اتخذت مثل هذه نساؤهم ")                                                                  

(Imenifikia kutoka kwa Muawiya bin Abi Sufyan amesema naye yuko katika membari ya Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- katika musimu wa Hija akachukua kifurushi cha nywele kilichokuwa katika mkono wa askari wake kisha akasema enyi watu wa Madina wako wapi Maulamaa wenu nimemsikia Mtume wa Allah -rehema za Allah na amani zimshukie- asema: “Hakika wamehilikika Bani Israeel wakati wanawake zao walikuwa wakivaa kama hichi”)


Nimesoma katika jarida kuwa bi arusi mmoja alivaa "wig" (Baarookah) kisha akapelekwa kwa mumewe siku ya arusi, basi wakati mumewe alipoingia akamkuta amekwisha kufa. Wakati lilipoondolewa hilo wig akakutwa nyoka ndani yake naye ndiye aliyekuwa sababu ya kifo chake. Basi laiti kila anayevaa wig amtokee ndani yake nyoka kama huyo (kwa sababu amekwenda kinyume na sharia ya kiislamu), isipokuwa Allah Subhanahu Wataala anatoa fursa ya wakati (kwa yule anaefanya maasi na mwenginewe mpaka wakati maalum), lakini hapuuzi kitu (kila kitu chaandikwa katika kitabu chake na siku ya kiyama atayakuta yote aliyoyafanya). Na ikiwa huyo nyoka hatomng'ata duniani atamng'ata katika moto wa Akhera ikiwa hakutubu, na sifikiri yule anayefanya makusudi kumuasi Allah Subhanahu Wataala na akaendelea hivyo, huyo hapati tawfiiq ya kutubu.  Na nimemsikia Imam Al-Khalily, Allah Amrehemu, anasema anaingia motoni yule anayekusudia na hajali nini anatenda (afanya maovu bila ya kujali).


Tumekwisha jua yale mambo mabaya aliyokuwa akifanyiwa mwanamke kabla ya Uislamu na ukosefu wa heshima na adabu uliokuwa ukimpata. Kila msomaji anayajua haya hata wale wanawake wanaojidai kuwa wao ni wasomi na kuwa wamestaarabika, wanajua kuwa Uislamu umewatukuza (umenyanyua cheo chao) na umewapa heshima. Kwa hiyo waliwajibikiwa waushukuru Uislamu kwa hayo na wafate amri zake, na kuwa maasi yanaondoa zile neema tulizopewa, na katika kutomtii Allah Subhanahu Wataala sio maendeleo ya Dunia wala Akhera.

                                                                  

Nastaajabu uhai gani huu unaomfanya mtu adanganyike nao  na atopee katika kumuasi Allah Subhanahu Wataala bila ya kujali wapi anaelekea, na sote twajua kuwa uhai huu haudumu. Hatusikii isipokuwa baina ya kula wakti mchache mtu Fulani kaondokana nao na kuelekea kule ambako ametanguliza vitendo vyake, basi tizama kitu gani wakitanguliza mbele yako na wapenda kukiendea.


Mfano uliokuwa karibu na haya ni kuwa wakati unapojenga nyumba mpya wataka kukaa ndani yake, jee utaikalia nayo ni mbovu? Je! Utaikalia nayo haijakamilika? Utaihamia bila ya kuwa na samani (fanicha)? Basi mfano kama huu katika kuelekea kwenda akhera nao ndio uhai wa hakika (ukweli).


العنكبوت: ٦٤

"Na hayakuwa haya maisha ya dunia ila upuuzi  na mchezo, na nyumba ya akhera ndio maisha hasa laiti wangalijua."


Yaani maisha  ya akhera ndio ya kudumu basi mcheni Allah Subhanahu Wataala enyi waja wa Allah naye haridhii kwa waja wake kumkufuru (ukafiri), na pindi wakimkufuru basi yeye hawahitajii wao lakini wao ndio waliokuwa mafakiri kwake.


Amesema Mtume wa Mola -rehema za Allah na amani zimshukie- katika hadithi Qudsiy:

 (يا عبادي لو أن أولكم وآخركم وجنكم وإنسكم كانوا على أتقى قلب رجل منكم ما زاد في ملكي شيئا ، ولو أن أولكم وآخركم وجنكم وإنسكم كانوا على أفجر قلب رجل واحد ، ما نقص ذلك من ملكي شيئا)                                                                                            

“Enyi waja wangu lau kama wa kwanza wenu na wa mwisho wenu na majini wenu na mainsi wenu walikuwa kama mtu miongoni mwenu mwenye moyo unaemcha Allah kuliko wote isingezidisha katika mulki yangu kitu cho chote. Na lau kama wa kwanza wenu na wa mwisho wenu na majini wenu na mainsi wenu walikuwa kama mtu miongoni mwenu  mwenye moyo wa uasi kuliko wote isingepunguza kitu katika mulki yangu.”


Na nawaambia wanawake wa kiislamu, mcheni Allah Subhanahu Wataala na wala msidanganyike na maneno ya wanaopenda kusema (bila ya ilimu) na vitendo vya Dajjaliin (wapotezaji) kwani ni raha chache inayopita (na haiko mbali kutoweka).


النساء: ٨٩

"Wanataka (makafiri) lau mngekufuru kama walivyokufuru wao ili muwe sawa".


Na Mtume wa Allah -rehema za Allah na amani zimshukie- asema:

 (أقرب ما تكون المرأة من وجه ربها إذا كانت في قعر بيتها وإن صلاتها في صحن دارها أفضل من صلاتها في المسجد ، وصلاتها في بيتها أفضل من صلاتها في صحن دارها وصلاتها في مخدعها أفضل من صلاتها في بيتها )

“Mahala anapokuwa mwanamke karibu kabisa na Mola wake ni pale akiwa ndani ya nyumba yake, na hakika sala yake katika ua wa nyumba yake ni bora kuliko sala yake msikitini, na sala yake nyumbani kwake bora kuliko sala yake katika ua wa nyumba yake, na sala yake chumbani mwake ni bora kuliko sala yake nyumbani mwake.”


Na asema Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie:

 ( المرأة عورة فإذا خرجت استشرفها الشيطان )

“Mwanamke yapasa ajistiri kwani akitoka, shetani huwa pamoja nae (kumpambia).”


Basi haya ikiwa katika salaa ambayo bila shaka yoyote ni taa (kumtii Allah Subhanahu Wataala) vipi ikiwa katika mchanganyiko na wanaume katika vikao vyao, mikutano yao na michezo yao na mengineyo? Walikuwa wanawake waliopita akitoka mume wa mmoja wao amwambia: Usije ukachuma haramu kwani sisi twasubiria njaa na shida lakini hatusubirii moto (Jahannam).


Na kauli iliyojumuisha adabu za mwanamke :

-          Awe amekaa nyumbani kwake hakithirishi kupanda kwake na kutoka kwake(hatoki isipokuwa kwa dharura).

-          Mwenye maneno kidogo na jirani zake.

-          Amhifadhi mumewe akiwa hayupo.

-          Amfurahishe katika kuwepo kwake .

-          Ajiepushe kusikika Sauti yake na mtu wa mbali.

-          Hamu yake iwe kutengeneza hali yake na kuipanga nyumba (kuishughulikia) yake.

-          Mwenye  kumuabudu Mola wake.

-          Akinai kwa kile alichoruzukiwa mumewe na Allah Subhanahu Wataala.

-          Atangulize haki ya mumewe mbele ya haki yake.

-          Asifanye haraka kwenda mlangoni kwa yule anayegonga kutaka idhni ya kuingia.

-          Awe tayari katika hali yoyote kumsikiliza mumewe.

-          Awe msafi na ajitie manukato na atahadhari asinuse mumewe harufu itayomkera kutoka kwake au aone kwake mandhari ambayo itamkirihisha .

-          Awaonee huruma watoto wake na watoto wa mumewe kwa mke mwingine.

-          Ahifadhi sitara yao (yaani hawatolei hawa watoto aibu zao).

-          Ulimi wake uwe mfupi hauna maudhi .


Imetolewa kutokana na Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie :

 ( حرم الله على كل آدمي الجنة يدخلها قبلي، غير أني نظرت إلى يميني فإذا امرأة تبادرني إلى باب الجنة فأقول : ما لهذه تبادرني ؟ فيقال لي يا محمد : هذه امرأة كانت حسناء جميلة، وكان عندها يتامى لها فصبرت عليهن حتى بلغ أمرهن الذي بلغ ، فشكر الله لها ذلك )

“Allah Subhanahu Wataala amemharimisha mtu yeyote kuingia Janna (Peponi) kabla yangu, isipokuwa nnapotizama  kuliani kwangu kuna mwanamke ambaye ananiwahi kufika katika mlango wa pepo basi husema : Ana nini huyu aniwahi? Ndipo hujibiwa : Ewe Muhammad: Huyu mwanamke alikuwa mzuri wa kuvutia na alikuwa ana mayatima  (watoto wake wanawake) basi akawasubiria mpaka likafika jambo lao pale lilipofika, basi Allah Subhanahu Wataala akashukuru (akamjazi) kwa hayo aliyoyatenda.”


Imetolewa kutoka kwa Asmaa bint Abu Bakar Allah Subhanahu Wataala amridhie:  Amenioa Azzubeir na hali hana kitu katika ardhi yake kama mali au mtumwa wala chochote isipokuwa farasi  na ngamia. Nilikuwa nikimlisha huyo farasi  na kumsaidia (mume wangu) kumtosholezea huyo farasi mahitajio yake na nikimtwangia nafaka (chembe za mimea) ngamia wake na kumlisha na kumnywesha na nikiteka maji kisimani kwa ndoo na nikiponda unga, na nilikuwa nikibeba mbegu juu ya kichwa changu kutoka umbali wa theluthi mbili ya farsakh (farsakh = maili tatu) mpaka aliponiletea Abu Bakar kijakazi (mfanya kazi au mtumwa wa kike) basi akanitosheleza kumshughulikia huyo farasi basi ikawa kama kanikomboa .


Basi hizi ni katika sifa za wanawake wema ambao ndio wanaotakiwa kuwa mfano kwa wengine. Wale waitao watu kwenye batili(wapotezaji) katika wakati huu wanapigia mifano wanawake kama hawa ili wawadanganye watu wa kawaida wasiokuwa na maarifa katika dini yao wapate kuchanganyikana (baina ya wanaume na wanawake) na watokane na mipaka ya dini yao, kwani umefanywa Uislamu na watu wake  walioongoka lengo la kuwavutia watu kufanya mabaya (wanawaita watu kufanya mabaya kisha wasema hivi ndivyo Uislamu unavyohimiza), na Uislamu uko mbali na yale wanayousingizia. Makusudio yao ni kupoteza watu kwani hakika Uislamu ni wenye nguvu na kila mmoja ataka awe mwenye nguvu, basi wakishawapoteza wawakimbia kama alivyosema Allah Subhanahu Wataala katika kitabu chake juu ya sheitani amesema:


الحشر: ١٦ - ١٧

"Ni kama shetani anapomwambia mtu: "kufuru" na anapokufuru akamwambia: "Mimi si pamoja nawe, hakika namuogopa Allah, Mola wa walimwengu". Basi mwisho wa wote wawili hao ukawa waingie motoni kukaa humo daima na hiyo ndiyo jazaa ya madhalimu".


إبراهيم: ٢٢

"Na shetani atasema itapokatwa hukumu (ya wema kwenda peponi na wabaya kwenda motoni atawaambia  wale maasi wataomng'ang'ania): Allah alikuahidini ahadi ya kweli (na leo ameitimiza), nami nilikuahidini lakini sikukutimizieni. Wala sikuwa na mamlaka juu yenu (ya kukulazimisheni kunifuata), isipokuwa nilikwiteni tu nanyi mkaniitika .  Basi msinilaumu bali jilaumuni wenyewe: siwezi kukusaidieni wala nyinyi hamuwezi kunisaidia.  Hakika mimi nilikataa kunishirikisha kwenu toka zamani."  Kwa yakini madhalimu watakuwa na adhabu iumizayo."


Na madhalimu ni wale wanaoasi amri za Allah Subhanahu Wataala na Mtume wake -rehema za Allah na amani zimshukie.


Hapa kuna jambo ambalo lazima kujitahadharisha nalo nakuwa watu wanalichukulia wepesi nalo ni zito sana.  Kama ndugu wanaishi katika nyumba moja na wanao wake zao au mmoja katika wao ana mke na mwingine hana basi utawaona hao wanawake hawajistiri na ndugu za waume zao bali wajifungua mbele yao ( wazionyesha zile sehemu ambazo wajibu kustiriwa) na vile vile wanakula nao pamoja.  


Na hawatofautishi baina ya mume na shemegi yake isipokuwa katika unyumba(wakati wa kulala) na hii ni hatari kubwa kwani hakuna tofauti baina ya ndugu wa kiume wa mume na mwanamme mwengine (aliekuwa si mahram) katika makatazo. 


Mwanamke yeyote yule ambaye mwanamume anasihi kumuowa  basi ni haramu kwake (huyo mwanamume) kuona sehemu yoyote katika mwili wake au nywele zake , hapana shaka kuwa mke wa ndugu akimuacha mumewe basi anaweza yule ndugu kumuoa.

النبي صلى الله عليه وسلم قال لرجل سأله عن الدخول على النساء ، فنهاه عن ذلك فقال ما تقول في الحمو ؟ قال النبي صلى الله عليه وسلم : ( الحمو الموت )                                        

Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- amehadhirisha sana mambo haya, akamwambia mtu fulani aliyemuuliza juu ya kuingia kwa wanawake kuwa asifanye hivyo yaani kamkataza kuingia walipo wanawake waliokuwa sio mahrim wake. Akamuuliza tena jee vipi shemegi (yaani ndugu wa mume) akasema Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- "Shemegi ni mauti". Kamwita mauti basi kuna kitu baada ya mauti? Twamuomba Allah Subhanahu Wataala afya na tawfiiq ya kufuata amri zake na kujizuia na makatazo yake na atujaalie katika wale wanaosikiliza kauli kisha wakaitekeleza vizuri kabisa.




Ameitoa Mufti Mkuu wa Sultanate ya Oman Sheikh Ahmed Bin Hamed Al-Khaliliy.


Uislamu ni dini ya fitra (kimaumbile) ameiteremsha Allah Subhanahu Wataala hii dini kuliongoza hilo umbile (fitra) katika njia yake iliokuwa ya kweli kwa hivyo zimekuja hukumu zawafikiana na mahitajio yake (hilo umbile) na zinatekeleza mahitajio yake. 


Na katika mambo yaliyokuwa wazi kabisa kuwa kila mmoja katika mwanamme na mwanamke anazo sifa makhsusi za kimaumbile zinazolazimisha kutofautiana kwa hali zao kinafsi, kimwili na kijamii basi ndio hivyo utaona Uislamu umeharamisha kwa kila mmoja katika wao asijivalishe sifa za kimaumbile za jinsi nyingine kama tunavyoona katika kauli yake -rehema za Allah na amani zimshukie:

( لعن الله المتشبهين من الرجال بالنساء والمتشبهات من النساء بالرجال )

“Allah amewalaani wale wanaojishabihisha na wanawake katika wanaume na wale wanaojishabihisha na wanaume katika wanawake”.


Kwa sababu katika kufanya hivyo ni kutokana na fitra (maumbile aliyojaalia Allah Subhanahu Wataala katika viumbe vyake) na kugongana na sunna za uhai na kuingilia zile sifa za wengine. 


Na hapana shaka mwanamme aliekuwa maumbile yake yamebakia katika usalama inamkataza haiba yake ya kiume kuvaa dhahabu kwa sababu hiyo inapingamana na alama za kiume na ugumu wa hiyo jinsi ya kiume na kuwa hiyo inaambatana na ulaini wa kike. Kisha tunaona katika athari za sunna za Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- makatazo ya nguvu na mahadharisho ya adhabu ya Allah Subhanahu Wataala kwa wale wanaume wanaovaa dhahabu kitu ambacho hakimuachii mtu nafasi ya kusita kuikubali hukumu, na nyingi katika hizi athari zimezungumzia juu ya pete. 


Ifuatayo ni mifano itakayokuangazia katika njia ya maarifa.

1- روى إلامام الربيع رحمه الله عن الإمام علي بن أبي طالب –كرم الله وجهه – قال : نهاني الرسول  صلى الله عليه وسلم عن لبس القسي وعن لبس المعصفر وعن خاتم الذهب وعن قراءة القرآن في الركوع والسجود .. أخرجه النسائي وكذلك الترمذي ما عدا ذكر القراءة في الركوع والسجود                                                                     

1.. Ametoa Imam Al-Rabii Rehema za Allah ziwe juu yake kutokana na Imam Ali Bin Abii Taalib - Allah aukirimu uso wake -  amesema:-  Amenikataza Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- kuvaa aina ya nguo fulani kutoka Misri ambayo imechanganywa na hariri (Al-Qasiy) na pia kuvaa nguo yenye rangi ya zaafarani (Al-Ma'safir) na pete ya dhahabu na kusoma Qurani katika rukuu na sujuudu.  Ameitoa vile vile Annasai na Attirmidhi isipokuwa kutajwa kusoma katika rukuu na sujuud na akasema hadithi hasan na sahiih.


2- أخرج البخاري ومسلم والنسائي عن أبي هريرة أن رسول الله صلى الله عليه وسلم نهى عن خاتم الذهب وفي رواية للنسائي أن النبي صلى الله عليه وسلم نهاني عن تختم الذهب                                                                                       

2.. Ametoa Al-Bukhari na Muslim na Annisai kutokana na Abu Huraira kuwa Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- amekataza kuvaa pete ya dhahabu na katika hadithi ya Annasaai kuwa Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- kanikataza kuvaa pete ya dhahabu.


3- روى الترمذي عن عمران بن حصين –رضي الله عنه – قال ( نهى رسول صلى الله عليه وسلم عن التختم بالذهب )                                                                   

3.. Ametoa Attirmidhi kutokana na Imraan Bin Hussein amridhie Allah Subhanahu Wataala, amesema – amekataza Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- kuvaa pete ya dhahabu.


4- روى مسلم عن ابن عباس –رضي الله عنهما – أن رسول الله صلى الله عليه وسلم رأى خاتما من ذهب في يد رجل فنزعه وطرحه وقال ( يعمد أحدكم إلى جمرة من نار فيطرحها في يده ) فقيل للرجل بعدما ذهب رسول الله صلى الله عليه وسلم خذ خاتمك انتفع به فقال لا آخذه أبدا وقد طرحه رسول الله صلى الله عليه وسلم                                  

4..  Ametoa Muslim kutokana na Ibn Abbas Allah Subhanahu Wataala amridhie yeye na baba yake kuwa Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- ameona pete ya dhahabu katika mkono wa mwanamme akaipopotoa kisha akaitupa na akasema:- Anakusudia mmoja wenu jinga la moto na kulitupa mkononi mwake. Akaambiwa yule mtu baada ya kuondoka Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- chukua pete yako ujinufaishe nayo akasema siichukui abadan (milele) baada ya kuitupa Mtume wa Allah -rehema za Allah na amani zimshukie.


5- روى النسائي عن أبي سعيد الخدري – رضي الله عنه – أن رجلا قدم من نجران إلى رسول الله صلى الله عليه وسلم وفي يده خاتم من ذهب فأعرض عنه رسول الله صلى الله عليه وسلم وقال ( إنك جئتني وفي يدك جمرة من نار )                                                                

5.. Ametoa Annasai kutokana na Abi Saeed Al-Khudriy amridhie Allah Subhanahu Wataala kuwa mtu mmoja alikuja kwa Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- kutoka Najraan na katika mkono wake pete ya dhahabu basi akageuka upande mwingine (kuepukana nae) akasema "Hakika wewe umenijia na katika mkono wako jinga la moto".


6 – روى النسائي عن البراء بن عازب –رضي الله عنه – أن رجلا كان جالسا عند النبي صلى الله عليه وسلم وعليه خاتم من ذهب وفي يد النبي صلى الله عليه وسلم مخصرة فضرب بها أصبع الرجل فقال: مالي يا رسول الله ؟ قال ( ألا تطرح هذا الذي في أصبعك ) فأخذه الرجل فرمى به فرآه النبي صلى الله عليه وسلم بعد ذلك فقال ( ما فعلت بالخاتم ) قال رميت به قال (ما بهذا أمرتك إنما أمرتك أن تبيعه فتستعين بثمنه ) ...                                                                      

6.. Ametoa Annasai kutokana na Al-Barraa bin Aazib amridhie Allah Subhanahu Wataala kuwa mtu mmoja alikuwa amekaa kwa Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- na amevaa pete ya dhahabu na katika mkono wa Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- ana fimbo akampiga kwayo vidole vya huyo mtu, akasema nimefanya nini Mtume wa Allah? Akasema : "Hukitupi hicho kilichokuwa katika kidole chako akaichukua yule mtu akaitupa kisha Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- akamuona baadaye akamwambia umeifanya nini ile pete akamwambia nimeitupa akamwambia "sikukuamrisha kufanya hivyo lakini nimekuamrisha uiuze na ufaidike na thamani yake".  Na yote yatakayosemwa katika hadithi hii lakini yatiwa mkazo na hadithi nyinginezo sahihi.


7- روى الثعلبي عن أبي ثعلبة الخشني – رضي الله عنه – أن النبي صلى الله عليه وسلم أبصر في يده خاتما من ذهب فجعل يقرعه بقضيب معه فلما غفل النبي صلى الله عليه وسلم ألقاه قال ( ما أرانا إلا قد أوجعناك وأغرمناك )                                                                       

7.. Imetolewa na Thaalabiy kutokana na baba wa Thaalaba Al-Khasheniy – Allah Subhanahu Wataala awe radhi naye kuwa Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- ameona katika kiganja chake pete ya dhahabu akawa anaipiga ile pete (anaigonga) kwa kigongo alichokuwa nacho na wakati alipoghafilika Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- akaitupa akasema "Sioni isipokuwa tumekuumiza na kukutia gharama.”


Zinatosha hadithi hizi kwa yule mwenye moyo au akatega masikio yake naye ni shahidi. Zinatosha kumzuia asivae pete ya dhahabu wala kuitumia na hakuwa muumini wa kiume au wa kike baada ya kupitisha Allah na Mtume wake amri wakawa na khiari ya jambo hilo (isipokuwa kufuata amri iliyopitishwa na Allah Subhanahu Wataala na Mtume wake) na yule anayemuasi Allah na Mtume wake  basi amepotea upotevu wa uwazi. 


Na ilivyothibiti kuwa pete ya dhahabu haramu kwa mwanamume kwa dalili hizo zilizokuwa wazi kabisa katika sunna ya Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie, basi pete ile wanayovalishana bwana na bi arusi umezidi ule uharimisho wake kwa kuwaiga washirikina na kuwafanya mfano wetu, na hayo hayatokani isipokuwa kwa wale zilizougua nyonyo zao na kutikisika nafsi zao na kupungua imani yao. Kwani kujishabihisha nao ni kudhihirisha yale yaliyo ndani ya nyoyo zao (kuwapenda washirikina na Muislamu wa kweli hawi hivyo)  ya kuwatukuza na kupenda adaati zao na kufuata njia zao na haya yote yamehadhirishwa na Allah Subhanahu Wataala kwa waja wake waumini kuwafanya makafiri marafiki zao.


Je! Niwaambie nini asili ya Dabla ( pete wanayovalishana mume na mke katika arusi)?.


Hakika asili yake ni upotevu wa Kirumi wa hali ya chini kabisa.  Walikuwa Warumi wanaamini kuwa mwanamume akimvalisha mwanamke pete ya chuma katika kidole cha kati cha mkono wa kushoto na kinyume chake pia yaani mwanamume akimvalisha mwanamke  katika munasaba wa posa kufanya hivyo kuna athari katika kuhifadhi mapenzi kwa imani yao kuwa kuna mawasiliano baina ya hicho kidole na moyo kama kwamba kwa hivyo kila mmoja katika wao anauteka moyo wa mwenziwe. Kisha ikaendelea mila hiyo kupiga hatuwa zaidi huko ulaya wakawa wavalishana pete ya dhahabu badala ya chuma.


Basi mila hii ikawavutia wengi wenye maradhi katika nyoyo zao katika nchi za Kiislamu, ikachukuliwa kuwa katika alama za maendeleo na ustaarabu na ukweli sio isipokuwa katika dalili za kuchelewa na kushuka chini.


Watakia nini waislamu kuiga mambo yaliyokuwa hayana msingi wowote yaliyoletwa na ujahiliya wa kirumi na ukarithiwa na ujahiliya wa kiuropa.  Na haya yameonekana na kuwa hayana msingi wowote kutokana na majaribio ya kimaisha.  Ndoa ngapi zilizofanywa katika msingi huu (wa kuvalishana pete) zikapindukia kuingia katika taabu na joto la moyo na kugombana kusikokwisha wala kuwezekana.  Na raha gani waliyopata wengi waliokuwa hawakuifata hii hii mila ya kijahiliya. Laiti ningejua mpaka lini hawa wanaohisabika katika idadi ya Waislamu watakuwa ni mikia ya wengine wanaiga kila mila zao za kipuuzi na kila mambo yao ya ovyo.


Na watu leo wengi katika kuvaa pete wanafuata njia tofauti na muongozo wa Mtume wa Allah -rehema za Allah na amani zimshukie-, kwani wao wanavaa pete kidole cha kati kufuata mila za wengine na ilihali hadithi za Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- zaonesha kuwa yeye alikuwa akivaa pete kidole cha mwisho.


روى مسلم عن علي – كرم الله وجهه – قال : نهاني رسول الله صلى الله عليه وسلم أن أجعل خاتمي في هذه أو التي تليها ، وأشار إلى الوسطى والتي تليها ونحوه عند أبي داود والنسائي والترمذي                                                                          

Ametoa Muslim Kutokana na Ali – Allah Subhanahu Wataala aukirimu uso wake – Kasema amenikataza Mtume wa Allah -rehema za Allah na amani zimshukie- kuijaalia (kuivaa) pete yangu katika hichi au kinachofuatia na akaonyesha kidole cha kati na kinachofuatia na imetolewa kama hivyo kwa Abi Dawood na Annassai na Attirmidhi. Basi na agutuke Muislamu na mambo kama haya madogo madogo na atahadhari na mtelezo wa miguu na wa fahamu (akili) na Allah SUBHANAHU WATAALA ndio mwenye kutoa tawfiiq.  Na Rehema za Allah na Amani yake ziwe juu ya bwana wetu Muhammad na juu ya watu wake na Masahaba zake wote!

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.