Tuesday, 19 January 2016

Jezuu 15 Jicho ----- Kujenga Uongofu katika nyoyo za Vijana




Katika maradhi yanayomganda Muislamu ni maradhi ya jicho.


Jicho ndio kiongozi wa viungo katika heri na shari. Na maradhi ya kutazama ni maradhi makubwa, inataka Muislamu ajihifadhi na ubaya wake (fitina yake) juu ya uzito wa kujihifadhi nayo, lakini inawezekana kuwa mwepesi wa kujihifadhi nayo kwa kutanabahi na hayo. Maradhi yote (ya nafsi) asili yake ni kutazama. Kuna methali inayosema:-

“Kutazamana (kwanza) kisha kuchekeana halafu kuamkiana kisha kuzungumza kisha kupeana miadi na  kukutana”. Kwa hiyo kitu cha kwanza ni kutazama. Lakini mja hahisabiwi kwa mtazamo wa mwanzo kwa mujibu wa kauli yake Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-

( لك الأولى وعليك الثانية )

 “Mtazamo wa kwanza ni wako (huhisabiwi nao kuwa ni kosa) na wa pili ni juu yako (wahisabiwa nao)”.


Ukifuatilia mtazamo mtazamo mwengine unazidi katika jicho lake uzuri wa huyo anaetazamwa hata ikiwa si mzuri kwani sheitani anampambia aliye mbaya na pengine asifanikiwe kupata kile alichokitaka kutokana na huyo aliyemtaka. Na juu ya hivyo amekuwa kisha pambiwa (na shaitani) na kila akikaa humfikiria basi hiyo ndiyo khasara kubwa Siku ya Kiyama. Na Allah Subhanahu Wataala peke yake ndiye anayejua ukubwa wa khasara hiyo. Basi inatakiwa wakati anapotazama kilichoharamishwa na ikaifatilia nafsi yake hicho kitu hapo anavutika kurudia kutazama (mtazamo wa pili) basi na aizuie nafsi yake asifanye hivyo kwani mtazamo wa pili ndio ujinga wenyewe unaosababisha maradhi mengi katika moyo wake. Na akilihifadhi jicho lake kutazama basi ni njia ya kuponesha hayo maradhi yaliyo katika moyo wake. Ikiwa halihifadhi jicho lake basi hataweza kuvihifadhi viungo vyake vingine na huenda akaingia katika balaa kubwa haiwezi. Amesema Nabii wa Allah Issa AS:-

 ( إياكم والنظرة  فإنها تزرع في القلب شهوة وكفى بها من فتنة )

 “Jiepushe na kutazama (vilivyoharimishwa) kwani hupanda katika moyo matamanio yatosha peke yake hayo kuwa ni fitina (upotofu).”


Amesema Nabii wa Allah Dawood AS kumwambia mtoto wake Suleiman AS:-

( يا بني امش خلف الأسد  والأسود ولا تمش خلف المرأة )

 “Ewe mwanangu tembea nyuma ya simba na simba wengi wala usitembee nyuma ya mwanamke.”

Aliulizwa Nabii Yahya AS:- Kitu gani kinachotangulia zinaa? Akajibu:-  Kutazama na kutamani.


Amesema Ibliis: Kutazama ni upinde wangu wa zamani na mshare wangu ambavyo sikosei nikipiga kwavyo.

Imetolewa kutokana na Mtume Salallahu Alayhi Wasalam amesema:-

( النظرة سهم مسموم من سهام إبليس فمن تركها خوفاً من الله تعالى أعطاه الله تعالى إيماناً يجد حلاوته في قلبه )

“Kutazama ni mshare wa sumu miongoni mwa mishare ya Ibliis mwenye kuacha kwa kumuogopa Allah Subhanahu Wataala anampa Allah Subhanahu Wataala Imani anaupata utamu wake katika moyo wake”.


Na anasema Salallahu Alayhi Wasalam:-

 ( ما تركت بعدي فتنة أضر على الرجال من النساء )

 “Sikuacha baada yangu fitina iliyo na madhara kwa wanaume zaidi kuliko (fitina ya) wanawake.”


Na amesema Salallahu Alayhi Wasalam:-

( اتقوا فتنة الدنيا وفتنة النساء فإن أول فتنة بني إسرائيل كانت من قبل النساء )

“Ogopeni fitina ya Dunia na fitina ya wanawake kwani fitina ya kwanza ya Bani Israeel ilikuwa kutokana na wanawake.”


Ameitoa Abu Saeed. Amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-

( لكل ابن آدم حظ من الزنا فالعينان تزنيان وزناهما النظر واليدان تزنيان وزناهما البطش والرجلان تزنيان وزناهما المشي والفم يزني وزناه القبلة والقلب يهم أو يتمنى ويصدق ذلك الفرج أو يكذبه )

 “Kila binadamu ana sehemu yake katika zinaa kwani macho yazini na zinaa yake ni kutazama na mikono yazini na zinaa yake ni kushika na miguu yazini na zinaa yake ni kwenda na mdomo wazini na zina yake ni kubusu na moyo wawa na hamu au watamani na utupu unakubali hayo (kwa kufuata amri na matamanio ya moyo) au wakadhibisha (yaani wakataa).” Ameitoa hadithi hii Abu Huraira.


Amesema Ummu Salamah ametaka idhini Ibn Ummu Maktoum ‘kipofu’ kwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam kuingia nyumbani na mimi na Maimuna tumekaa akasema AS: Jifunikeni! Tukasema kwani yeye si kipofu, haoni? Akasema AS: Je nyinyi hamuoni? Na katika hadithi ya Arrabii Allah Subhanahu Wataala Amrehemu: Je nyinyi vipofu?

Kwa hiyo hadithi hii ni dalili ya kuwakataza wanawake wasiwatizame wanaume hata vipofu.


Yasemekana kulikuwa na mtu mwema anaadhini katika msikiti fulani miaka mingi alikuwa hafarikiani na adhana na watu walikuwa wakimuona katika miongoni mwa watu bora zaidi wa zama zake. Siku moja akapanda katika mnara wa msikiti akatazama chini yake akamuona binti wa kinasara yuko nyumbani mwake akarudisha mtazamo(wa pili), akawa  hawezi kuondoka hapo mnarani, yule binti wa kinasara akamuona wakawa watupiana macho yule binti akamuashiria apindukie ukuta ili amfikie basi katika kupindukia ukuta akaanguka na akafa nyumbani mwake (yule binti) kabla ya kupata haja yake, twamuomba Allah Subhanahu Wataala atuepushie vitangulizi vya maangamivu.

           

Yasemekana kuwa mtu mmoja miongoni mwa taabiina alikuwa amehifadhi Qur’ani kamili na amehifadhi hadithi nyingi katika hadithi za Mtume Salallahu Alayhi Wasalam basi akatokea kumuona mwanamke wa kinasara akauchukua moyo wake (kampenda sana) akamfuata na huyo mwanamke akamridhia kwa mapendekezo yake lakini kwa sharti atoke  katika  Uislamu akakubali kutoka. Allah Subhanahu Wataala atuepushie hayo; akaishi naye muda katika mji wa Antakiya. Na siku hiyo baadhi ya marafiki zake walipita Antakiya wakauliza juu yake wakaambiwa yuko mahali fulani wakamuendea wakamkuta achunga nguruwe wakamuuliza juu ya hali yake akawajibu muombeni Allah awaepushe na kila maovu. Wakamwambia ulikuwa umehifadhi Qur’ani na umehifadhi nyingi miongoni mwa hadithi za Mtume Salallahu Alayhi Wasalam akawajibu haikubakia Qur’ani kwangu isipokuwa Aya mbili:-

                           

 آل عمران: ٨٥

“Na anayetaka Dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye khasara (kubwa kabisa).”


                           ﮥﮦ      ﮩﮪ         البقرة: ٢١٧

“Na watakaotoka katika Dini yao katika nyinyi kisha wakafa hali ya kuwa makafiri, basi hao ndio ambao amali zao zimeharibika katika Dunia na Akhera. Nao ndio watu wa Motoni, humo watakaa milele”.


Na katika hadithi imebakia kwangu hadithi moja nayo:  من بدل دينه فاقتلوه   Anaebadili Dini yake basi muuweni (Anayetoka katika Dini ya Uislamu auliwe). Hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kwa Allah Subhanahu Wataala.

Na miongoni mwa mitizamo inayosababisha kuhiliki ni kuitizama Muislamu Dunia kwa kuishughulikia sana na kuitukuza na kutoishughulikia Akhera yenye kubakia na ndio mwisho wa kila mtu huko kwani anaependelea kinachopita (kisichodumu) juu ya kinachobakia huyo hana akili na inataka mtu aijalie Dunia kama kipando (anachokipanda mtu kama gari, ndege, meli au mnyama kusafiri) kinachomchukua kumpeleka katika nchi anayoikusudia kwenda. Kwa hiyo Dunia haistahiki kupewa heshima ila kwa kadiri ya kukufikisha huko kwenye haja yako (Al-Janna) na kwa sababu kipando chahifadhiwa na kutunzwa ili kipate kukufikisha mahala unapopataka kadhalika Dunia yahifadhiwa na kuheshimiwa kwa ajili ya kukufikisha Akhera kwani Dunia ni sababu na Akhera ndio lengo la mja.


Amesema Allah Subhanahu Wataala :-


                           ﮧﮨ                    المنافقون: ٩

“Enyi Mlioamini! Yasikusahaulisheni mali yenu wala watoto wenu kumkumbuka Allah; Na wafanyao hayo, hao ndio wenye kukhasirika.”


Na amesema Allah Subhanahu Wataala :-


       ﮠﮡ                  التغابن: ١٥

“Bila shaka mali zenu na watoto wenu ni jaribio (kwenu, mtihani kutazamwa mtakhalifu amri za Allah kwa ajili yao au mtafuata amri zake). Na kwa Allah kuna ujira mkubwa kabisa.”


Na amesema Allah Subhanahu Wataala :-


                     هود: ١٥

“Wanaotaka maisha ya Dunia na mapambo yake.”


Na amesema Subhanahu Wataala:-

                       العلق: ٦ - ٧

“Sivyo hivi (we binaadamu)! Kwa hakika binaadamu hutakabari (6) Akijiona amepata utajiri(7).


Na amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-

)حب المال والشرف ينبتان النفاق في القلب كما ينبت الماء البقل(

 “Kupenda mali na utukufu kwaotesha unafiki katika moyo kama maji yanavyootesha mimea”.


Na amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-

)ما ذئبان ضاريان أرسلا في زريبة غنم بأكثر إفسادا فيها من حب الشرف والمال والجاه في دين الرجل المسلم(

“Mbwa mwitu wawili wanaopelekwa katika kikundi cha mbuzi hawawi waharibifu kwao zaidi kuliko (uharibifu unaofanywa) na kupenda utukufu na mali na cheo katika Dini ya mtu Muislamu.”


Amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-

( يهلك المكثرون إلا من قال به في عباد الله هكذا هكذا وقليل ما هم )

 “Wanahiliki wanaopenda mali nyingi isipokuwa wale wanaozitoa pesa zao katika waja wa Allah kwa njia hii na njia hii (kwa njia mbali mbali kama kuwapa watoto wao, kuwapa masikini) na hao ni kidogo”.


Na amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-

(سيأتي بعدكم قوم يأكلون أطايب اللذائذ  وألوانها ويركبون فره الخيل وألوانها  وينكحون أجمل النساء وألوانها ويلبسون أجمل الثياب وألوانها لهم بطون من القليل لا تشبع وأنفس بالكثير لا تقنع عاكفون على الدنيا يغدون ويروحون إليها اتخذوها آلهة من دون إلههم وربا دون ربهم إلى أمرها ينتهون ولهواهم يتبعون فعزيمة من محمد بن عبد الله لمن أدركه ذلك الزمان من عقب عقبكم وخلف خلفكم أن لا يسلم عليهم ولا يعود مرضاهم ولا يتبع جنائزهم ولا يوقر كبيرهم فمن فعل ذلك فقد أعان على هدم الإسلام)

 “Watakuja watu baada yenu wanakula vyakula vyenye ladha na rangi mbali mbali (aina tofauti) na wapanda farasi wazuri wa starehe na wenye rangi tofauti na wanaoa wanawake wenye wingi wa uzuri na rangi mbali mbali na wavaa mavazi mazuri yalioje na yenye rangi mbali mbali hao wana matumbo hayashibi na kidogo na nafsi hazikinai wamejishughulisha na Dunia wenda na warudi kwa ajili yake (Dunia) wameifanya kuwa ni Mungu hali ya kuwa wamemuacha Allah wao na wameifanya kuwa ni mola pasi ya Mola wao Subhanahu Wataala wafuata amri yake na wafuata matamanio yao basi Muhammad bin Abdullah anamlazimisha yeyote utakaemfikia wakati huo miongoni mwa watoto wenu na watoto wa watoto wenu watakaokuja baada yenu na vizazi vyenu vitakavyofuatia baada yenu asiwaamkie hao (sifa zao zilizotajwa hapo juu) wala asiwatizame wagonjwa wao wala asishindikize majeneza yao (asiwazike) wala asimheshimu mkubwa wao na atakaefanya hivyo basi amesaidia katika kuuvunja Uislamu. Ameitoa Abu Amamah.


Na Amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-

( يقول ابن آدم مالي مالي وهل لك من مالك إلا ما أكلت فأفنيت أو لبست فأبليت أو تصدقت فأمضيت )

 “Binaadamu asema mali yangu mali yangu, Je unayo mali wewe ila kile ulichokula ukakiondoa au ulichokivaa ukakichakaza au umekitoa sadaka ukakipeleka (mbele yako kikiwa katika ujira wako Siku ya Kiyama).”


Na amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-

( أخلاء ابن آدم ثلاثة واحد يتبعه إلى قبض روحه والثاني إلى قبره والثالث إلى محشره فالأول ماله والثاني أهله والثالث عمله )

 “Marafiki wa binadamu watatu mmoja anakuwa pamoja nae mpaka anapochukuliwa roho yake na wa pili (amfata) mpaka kaburini na watatu mpaka Siku ya Kiyama wa kwanza ni mali yake, wa pili ahli wake na watatu vitendo vyake.”


Inasemekana kuwa zilivyotengezwa dinari na darhamu Ibliis akazinyanyua juu ya kichwa chake kisha akazieka juu ya kipaji chake kisha akazibusu akasema anaekupendeni basi huyo mtumwa wangu wa kweli, na watu kidogo wanaomiliki nafsi zao mbele ya dinari au dirham kuna methali inasema:- “Muoneshe dirhamu ujue vipi kujiepusha kwake na mambo ya haramu”. Vile vile inasema methali nyingine:- Usidanganyike na mtu kwa kuitia kiraka kanzu yake au kwa kunyanyua nguo yake juu ya vifundo vyake viwili au kwa mn’garo wa kipaji chake cha uso muoneshe dirhamu utajua utiifu wake au kujitenga kwake na maharimisho ya Allah Subhanahu Wataala .

           

Inasemekana kuwa Musallamah bin Abdul Malik aliingia kwa Omar bin Abdul Aziz, Allah Amrehemu, wakati wa mauti yake akasema: Ewe Amir Almuminiin umefanya jambo hakufanya mtu kabla yako, umewaacha watoto wako hawana dirham wala dinari. Na alikuwa na watoto kumi na tatu, basi akasema Omar nikalisheni wakamkalisha hapo akasema:- Ama kauli yako kuwa sikuwaachia dinari wala dirhamu kwani sikuwazuia mimi kwenda mashambani wala sikuwapa wao haki ya watu wengine ama ukweli ni kuwa watoto wangu ni moja katika watu wawili: Awe mtiifu kwa Allah Subhanahu Wataala basi Yeye atamtosheleza haja zake kwani Allah Subhanahu Wataala awatizamia watu wema mambo yao au awe (mtoto wangu) asi kwa Allah na sijali hayo yatakayompata.


Na kwa ujumla utajiri ni bora kuliko umasikini kwa sababu Mtume Salallahu Alayhi Wasalam amemuomba Allah Subhanahu Wataala amkinge na ufakiri na akauwita ukosefu ulioje, amma utajiri watumiliwa katika kumtii Allah Subhanahu Wataala zaidi kuliko ufakiri, na vile vile utajiri unafaida nyingi za Kidunia na Kidini amma za Kidunia zajulikana na amma faida za Kidini na za Akhera ni kufanya ibada zinazoambatana na kutoa pesa kama kutoa matumizi ya nyumbani (chakula, nguo na mengineyo), kuwapa mafakiri, kutoa sadaka katika mambo ya hija na jihadi, kutoa pesa za kujengea maskani, kuoa, na kipando (mnyama, pikipiki au gari) ambayo hakuna budi kuyafanya na matumizi mengineyo ambayo hawezi mtu akafikia kumwabudu Allah Subhanahu Wataala isipokuwa kwayo. Hizo ni katika ibada ambazo apata thawabu ikiwa atatia niya nzuri ya kujikaribisha na Allah Subhanahu Wataala. Vile vile kama kuhifadhi sharafu yake na ya watoto wake, kuwapa ujira wafanya kazi au kujenga misikiti, madaraja na nyumba za kufikia wageni na mengineyo kama kueka mali wakfu ili kufanya mambo ya kheri na mambo haya yote ni kheri yanayofikisha katika radhi ya Allah Subhanahu Wataala. Upande mwingine mali hiyo hiyo inayotolewa kufanya mambo yote hayo mazuri inaweza ikamletea shari na ubaya mkubwa huyo mwenyewe ikiwa niya yake ya kutumia mali hiyo ni matamanio ya uasi, ufahari, kujiona nafsi yake kuwa ni bora na kuwa ana mali nyingi kuliko watu wengine na kufanya uroho mkubwa kunakomfanya mtu achume mali kihalali halafu aitumie palipokuwa si halali au yamshughulishe mali na njia ya kuyachuma kwake hata asifanye wajibu wa Dini yake na kuwa akija msikitini kwa mfano kusali basi huwa kama yuko juu ya jinga la Moto mpaka atakapotoka humo, mwili wake upo ndani msikitini na roho yake na moyo wake inafuwata kazi zake nje ya msikiti, wakati ikichelewa adhana kwa mfano au ikama wamuona atizama saa yake na kumpigia kelele muadhini umekwisha pita wakati, umekwisha pita wakati haya kimu Sala, kazi zetu zitaharibika na kama hivyo. Basi wafikiri itakuwa vipi Sala ya mtu kama huyu isipokuwa usumbufu tu wa hofu na huzuni na kukesha usiku na kutopata usingizi bila ya kula vidonge vya usingizi na hapati faragha hata ya kula basi nini faida ya mali kama hii? Basi yeyote yule aliyekuwa haikumstarehesha mali yake, yeye na masikini ni sawa. Kitu muhimu cha kuzingatia kuwa mwanadamu amezungukwa na mitihani kutoka upande wa ufakiri na utajiri na anahitajia subira na jihadi ili kupasi mitihani hii.


ﯿ      الأنبياء: ٣٥

“Na tutakufanyieni mitihani kwa (mambo ya) shari na ya kheri.”


Twamuomba Allah Mtukufu Atusalimishe na Atusaidie kwa tawfiiqi yake na ulinzi wake na ukarimu wake kwani Yeye ni Muweza wa hayo. Amin.


Zimekuja hadithi za Mtume Salallahu Alayhi Wasalam katika kusifu kukinai na kuikosoa tamaa ya vilivyo katika mikono ya watu.


Amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-

( لو كان لابن آدم واديان من ذهب لابتغى لهما ثالثا ولا يملأ جوف ابن آدم إلا التراب ويتوب الله على من تاب)

 Kama angelikuwa binaadamu ana mabonde mawili ya dhahabu basi angelitaka la tatu na wala tumbo la binaadamu halijai(hatosheki) isipokuwa na udongo na Allah Apokea toba ya aliyetubu.”


Na Asema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-

 ( منهومان لا يشبعان منهوم العلم ومنهوم المال )

“Waroho wawili hawashibi, mroho wa elimu na mroho wa mali.”


Na asema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-

 ( يهرم بن آدم ويشب معه اثنتان الأمل وحب المال )

“Anazeeka binaadamu na viwili vyabakia nae katika ujana matumaini na kupenda mali” au kama alivyosema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam.


Na anasema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :

 (طوبى لمن هدي للإسلام وكان عيشه كفافاً وقنع  به )

“Ana malipo makubwa (mazuri) alieongozwa katika Uislamu na yakawa maisha yake kiasi ya kumtosheleza bila ya kuhitajia watu na kuwaomba akakinaika nayo.”


Na anasema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-

( ما من أحد فقير ولا غني  إلا ويوم القيامة يتمني أنه كان أوتي قوتا في الدنيا )

 “Hakuna mtu yoyote Siku ya Kiyama akiwa tajiri au fakiri isipokuwa atamani kuwa Duniani alipewa chakula kiasi ya kutosheleza siku moja.”


Na anasema Salallahu Alayhi Wasalam:-

 ( ليس الغنى عن كثرة العرض إنما الغنى غنى النفس )

 “Sio utajiri kuwa na mali nyingi lakini utajiri (wa kweli) ni utajiri wa nafsi”.


Na anasema Salallahu Alayhi Wasalam:-

 ( أيها الناس أجملوا في الطلب فإنه ليس لعبد إلا ما كتب له ولن يذهب عبد من الدنيا حتى يأتيه ما كتب له من الدنيا وهي راغمة )

 “Enyi watu ufanyeni uchumi wenu uwe mzuri (bila ya kutaka haramu au kufanya tamaa na ghishi na kupoteza ibada kwa kushughulika na maisha) kwani hapati mja isipokuwa kile alichoandikiwa (kukipata) na haondoki mja Duniani isipokuwa kitamjia alichoandikiwa chataka au hakitaki.”


Na amesema Ibn Masood amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-

 ( إن روح القدس نفث في روعي أن نفسا لن تموت حتى تستكمل رزقها فاتقوا الله وأجملو في الطلب)

 “Hakika Roho mtakatifu (Jibriil) amepuliza katika moyo wangu kuwa nafsi haifi mpaka imalize riziki yake (iliyoandikiwa) basi mcheni Allah na ufanyeni uchumi wenu uwe mzuri.”


Amesema Abu Ayoub RA kuwa alikuja mbedui kwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam akasema ewe Mtume wa Allah nipe mauidha na uyafupishe akasema Salallahu Alayhi Wasalam:-

 (إذا صليت فصل صلاة مودع ولا تحدث بحديث تعتذر منه غدا واجمع اليأس مما في يد الناس )

 “Ukisali sali Sala ya mwenye kuaga (kama ni Sala yako ya mwisho na huwahi kusali Sala ijayo) na usizungumze mazungumzo ambayo kesho itabidi uyatolee udhuru (yaani uyapime yawe mazuri sio kuteta watu au kufitinisha n.k) na ukate tamaa kwa kilichoko katika mikono ya watu (usitamani kilichokuwa kwa mwenzako).”


Aliulizwa mwenye hekima nini mali yako akajibu kujipamba katika umadhihari wangu (nje) kwa makusudio ya kujitengeza undani wangu (amali ya mtu anayoifanya ina athari kubwa katika nafsi yake, kama kusema ukweli, kutokughishi, kutoteta watu. Tabia nzuri kwa ujumla yatengeza undani wa mtu kama kuondoa hasadi, chuki, kujiona bora, kiburi) na kukata tamaa na kilicho katika mikono ya watu.


Inasemekana kuwa kuna mtu alikamata ndege (mdogo) akamuambia wanitakia nini? Nataka nikuchinje halafu nikule, akamjibu wallahi haitamtosheleza (nyama yangu) mtu kwa kuwa haina ladha, wala kama ana njaa haitamshibisha lakini nitakufundisha mambo matatu ni bora kwako kuliko kunila mimi. Ama la kwanza nitakufundisha ningali niko katika mkono wako na la pili nikiwa juu ya mti ama la tatu nikiwa juu ya jabali. Akamwambia haya lete la kwanza. Akamwambia usisikitike juu ya kitu kilichokupita. Halafu akamwachia, alipokwenda mtini akamwambia lete la pili. Akamwambia usisadiki kitu kilichokuwa hakiwezekani, kuwa kitakuwa. Kisha akapuruka kwenda juu ya jabali akasema:- Ewe mtu wa tabu (mwenye bahati mbaya) kama ungenichinja ungetoa katika tumbo langu lulu mbili uzito wa kila moja katika hizo ni mithkala ishirini akajin’gata kwa kusikitika (juu ya kuzikosa hizo lulu) akamwambia haya lete hilo la tatu akamwambia wewe umeyasahau hayo mawili (ya mwanzo) vipi nikwambie la tatu. Sikukwambia usilisikitikie lililokupita na usisadiki kitu kisichowezekana kuwa kitakuwa. Mimi nyama yangu, damu yangu na magoya yangu vyote havifiki mithkala ishirini vipi basi zitatoka katika tumbo langu lulu mbili kila moja uzito wake mithkala ishirini  kisha akapuruka akenda zake.


Amesema Abu Attayib:- Anaetumia saa nyingi kwa kukusanya mali kuogopa usimpate ufakiri basi huo ndio ufakiri wenyewe.


Nami nimesema yenye maana hii:-

“Kila kilichokuwa katika ardhi kimeumbwa kwa ajili yetu hiyo ni heshima na neema kwetu. Amegawanya (Allah Subhanahu Wataala) riziki baina ya viumbe vyake na wala haumzidishii mtu uhodari wake isipokuwa kile alichoandikiwa na tabu yake ya kutafuta riziki iliokuwa haikuandikwa katika lawhi Al Mahfudhi ni bure. Na kinyume ya hivyo anaipata (riziki alioandikiwa) ijapokuwa hakuitafuta lakini kuacha kutafuta riziki iliyo halali ni ajizi kwani riziki haina mabawa bali hiyo ni kama wajibu inayotakiwa kufanywa na usiwe mzigo (juu ya wenzako) lakini tafuta riziki bila ya kunyan’ganya na kutumia nguvu na uitafute polepole na kwa uzuri. Kwani kila kilichokujia kwa unyan’ganyifu (na kugombana) kinakwenda katika kupotea na kuhiliki. Na kukusanya kwako mali umri wako wote kwa kuchelea ufakiri basi huo ndio ufakiri wenyewe, Ewe Mola nakuomba maghufira na maisha ya kunitosheleza, ewe Mola nijalie riziki yangu iwe ya kutosheleza haja yangu na iniepushe kuomba watu”.

Imesemwa kuwa baadhi ya watu wazuri wamesema:- “Ajabu kwa anaenunua watumwa kwa mali yake na hanunui watu huru kwa wema wake”. Kaulizwa mmoja wao juu ya ukarimu akasema:- “Utoe mali yako kwa ajili ya Allah Subhanahu Wataala”. Akaulizwa nini udhibitifu wa jambo akasema:- “Uizuie mali yako kwa ajili Yake(Allah)”. Akaulizwa nini israfu akasema:- “Kutumia mali kwa kutaka cheo”. Amesema katika wao:-  Wewe ni wa mali (imekumiliki) ukiizuia (kwa ubakhili usiitumie katika kheri) na ukiitumia basi mali ni yako (umeimiliki) Amesema mwingine:- “Bora ya mali ni ile iliyotumiwa kwa kuhifadhi heshima na sharafu”.

Amesema mwingine:- “Kufanya jitihada katika kutumia ulichonacho ni ukarimu wa juu kabisa (wa mwisho)”.

Amesema mwingine:- Sijapata kunyoosha mguu wangu mbele ya niliekaa naye.


Na katika visa vya mabakhili: Alikuwa katika mji wa Basra mtu mmoja tajiri lakini bakhili. Basi mmoja katika majirani zake akamwalika chakula akamletea chakula kizuri kinaitwa “tabahijah bibeidh” chapikwa na mayai akawa anakula yule mgeni (tajiri bakhili). Akala sana na huku anywa maji mpaka akavimbiwa na akayaona mauti mbele ya macho yake na akawa ajipindua kwa maumivu mwisho akenda kwa daktari kumuelezea hali yake akamwambia si tatizo kubwa lakini fanya utapike hicho ulichokula na utakuwa mzima akajibu:- Hah nitapike “tabahijah bibeidh”!! Bora kufa kuliko kufanya hivyo.

           

Kuna kisa kingine kinasema: Amekuja mbedui kwa mtu fulani ambaye mbele yake kuna tini (matunda fulani) basi alivyomuona yule mbedui akazifunika na nguo yake akakaa yule mbedui, yule mtu akamwambia Je unajua kusoma sura yoyote ya Qur’ani? Akajibu naam basi akasoma .........والزيتون وطور سينين yule mtu akamsahihisha(kama kumuuliza) والتين yule mmbedui akasema tini iko chini ya nguo yako.


Mmoja akamwita (kamkaribisha) mwenzake nyumbani kwake bila ya kumpa chakula akamfunga katika hali hiyo mpaka Al asiri na ikamshika njaa sana mpaka akawa kama kichaa na yule mwenye nyumba akachukua uudi (gitar- chombo maarufu cha kupiga muziki) akamuuliza mgeni wake sauti gani unayoitamani nikupigie akamjibu sauti ya karai (likikaanga nyama au samaki).


Kimetolewa kisa juu ya mtu bakhili. Umepindukia mpaka ubakhili wake. Akaulizwa mkwewe juu yake:- hebu tusifie meza yake ya chakula inakuwa vipi? Akajibu:- (jawabu lenye maana kama hii) Chakula kidogo sana na si kizuri (hakiliki). Na akaulizwa nani ahudhuria chakula hicho? Akajibu:- Malaika karimu wanaoandika amali za waja. Akaulizwa basi hapana anaekula nae? Akajibu:- Bali kuna nzi wala pamoja nae. Akaambiwa (huyu mkwe) twaona utupu wako waonekana na nguo yako imetoboka si bora ungelimuomba kitu akusaidie? Akasema mimi Wallahi nashindwa kumiliki sindano kushona hii nguo. Na kama mkwe wangu huyu angekuwa ana nyumba kutoka Baghdad mpaka Nuba (nchi katika Africa) imejaa sindano kisha akamjia Jibriil na Mikaiil na pamoja nao Yaaqoub Nabii wa Allah Subhanahu Wataala Salamu ya Allah iwe juu yao wakamuomba sindano moja awaazime ili waishonee kanzu ya Nabii Yusuf AS ambayo ilipasuliwa kwa nyuma basi asingewaazima hiyo sindano.


Na mmoja wao (katika mabakhili) alikuwa hali nyama kwa kuona ubakhili mpaka umjie uchu (kupenda sana) hapo ndipo humtuma kijana wake ili amnunulie kichwa cha mnyama, akaulizwa, twaona huli isipokuwa vichwa katika kaskazi (siku za joto) na kipupwe (siku za baridi) kwa nini wafanya hivyo? Akasema:- Ndio kwa sababu kichwa naijua bei yake kwa hiyo nasalimika na hiyana ya huyo kijana, na yeye vile vile kichwa sio nyama yake anayoipika (anayo nyama yake nyingine anayoipika) kwa hiyo hawezi akanilia nyama yangu akitaka kula jicho, sikio au funda humsimamisha na kuichukua mimi nikaila kwa hiyo huninunulia na kunipikia bila ya kuweza kula kitu cho chote kilichokuwa haki yangu. Siku moja alikuwa atoka nyumbani kwake enda zake kwa khalifa (kiongozi wa nchi) mkewe akamwambia Je utanipa nini ukirudi umepewa zawadi? Akamwambia nikipewa dirham 100,000 elfu mia nitakupa dirham moja na akapewa dirham 60,000 elfu sitini akampa dawnaq 4 nne (kasoro ya dirham moja).


Wako wapi hawa (mabakhili vilivyotajwa visa vyao hapo juu) ukiwafananisha na yule ansari alieingia kwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam akamkuta ana mgeni hana chakula cha kumpa (cha usiku) basi akamchukua yule ansari nyumbani kwake kisha kikaletwa chakula kikaekwa mbele yao akamuamrisha mkewe azime taa na akanyoosha mkono wake kama kwamba ataka kula kile chakula lakini hali, akala yule mgeni na alipoamka asubuhi Mtume Salallahu Alayhi Wasalam akamwambia Allah Subhanahu Wataala kafurahika na kitendo chenu mlichokifanya usiku kwa mgeni wenu na Allah Subhanahu Wataala Akateremsha Aya:-


                  الحشر: ٩

“Na wanawapendelea kuliko nafsi zao ingawa wenyewe wana hali ndogo”.


Inasemekana kuwa Abdullah bin Jaafar alitoka kwenda shambani kwake akapitia shamba la mitende la watu fulani akamkuta kijana mweusi anafanya kazi humo naye alikuwa (huyo kijana) ameleta chakula chake akaingia humo shambani mbwa akaja karibu yake yule kijana akamtupia kipande cha mkate kisha akamtupia cha pili na cha tatu akavila yule mbwa na Abdullah amtizama akamwambia: ewe kijana kiasi gani chakula chako (unachokula) kwa siku akamjibu hicho ulichokiona akamwambia kwa nini umempendelea mbwa? Akamjibu hii ardhi hakuna mbwa kwa hiyo huyu amekuja kutoka umbali mkubwa ana njaa basi nimeona vibaya nishibe mimi na yeye akae na njaa. Akamwambia wewe utafanya nini leo (utapata wapi chakula?) akamjibu mimi nimekwisha ifunga siku yangu hii (sili tena wala sina pa kupata chakula) akasema Abdullah bin Jaafar:- Kijana huyu ni karimu zaidi kuliko mimi basi akalinunua hilo shamba na kila kilicho ndani yake pamoja na huyo kijana na kisha akamkomboa huyo kijana na akampa sehemu ya hilo shamba.


Tunatoa hapa kisa cha Thaalaba bin Haatib kwa ajili ya kuhadhirisha na fitina ya mali. Amesema Thaalaba: Ewe Mtume wa Allah muombe Allah aniruzuku mali akasema:-

 ( يا ثعلبة قليل تؤدي شكره خير من كثير لا تطيقه )

Ewe Thaalaba kidogo unachoweza kutoa shukrani yake bora kuliko kingi (mali nyingi) ambacho hukiwezi. Akasema: Ewe Mtume wa Allah niombee kwa Allah Aniruzuku mali, akasema:-

 ( يا ثعلبة أما ترضى أن تكون مثل نبي الله تعالى أما والذي نفسي بيده لو شئت أن تسير معي الجبال ذهباً وفضة لسارت )

 “Ewe Thaalabah huridhiki kuwa mfano wa Mtume wa Allah Mtukufu, kwa kweli naapa kwa Aliye nafsi yangu katika mikono yake kama ningelitaka majabali (milima) kuwa dhahabu na fedha yangelikuwa”.

Akamwambia:- Naapa kwa Aliye kuleta kwa haki Mtume kama ukimuomba Allah aniruzuku mali hakika nitampa kila mwenye haki, haki yake na nitafanya na nitafanya....

akasema Mtume wa Allah Salallahu Alayhi Wasalam:-

“Allah mruzuku Thaalabah mali  اللهم ارزق ثعلبة مالا  Akafuga mbuzi wakazaana kama wanavyozaana wadudu mpaka Madina ikawa ndogo kwao (jinsi walivyokuwa wengi) basi akahama katika bonde katika mabonde yake mpaka ikawa asali ِAdhuhuri na Alasiri jamaa tu na sala nyingine akawacha kusali jamaa na wakazidi kuongezeka hao mbuzi mpaka ikabidi ahame mbali zaidi hadi akaacha kusali sala ya jamaa isipokuwa sala ya Ijumaa nao bado wangali wakaongezeka kama wanavyoongezeka wadudu mpaka hatimaye akaacha kusali Ijumaa mpaka ikawa habari za Madina awauliza wanaokwenda huko siku ya Ijumaa. Hapa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam akauliza juu yake: 

ما فعل ثعلبة بن حاطب

Je nini amefanya Thaalabah bin Haatib. Akaambiwa Ewe Mtume wa Allah amefuga mbuzi wakawa wengi mpaka ukadhikika mji wa Madina nao, na wakamuelezea habari yake yote akasema:-

 ( يا ويح ثعلبة بن حاطب يا ويح ثعلبة يا ويح ثعلبة )

 “Ewe Thaalaba bin Haatib ole wako, ewe Thaalaba ole wako, ewe Thaalaba ole wako”.

Allah akateremsha Aya hii:-


                ﮢﮣ             التوبة: ١٠٣

“Chukua sadaka katika; mali zao, uwasafishe kwa ajili ya hizo (sadaka zao) na kuwataja kwa vizuri (mbele yangu) na uwaombee dua. Hakika kuwaombea kwako kutawapa utulivu (watengenekewe)”


Baada ya kuteremka Aya hii ya kufaridhisha Zakaa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam akawatuma watu wawili na akawaandikia barua ili kwenda kwa Waislamu kukusanya sadaka mmoja wao katika kabila la Juhainah na wapili kabila yake ni Bani Saliim, akawaambia Salallahu Alayhi Wasalam:-

 ( مر بثعلبة بن حاطب وفلان رجل من بني سليم )

Mpitieni Thaalabah bin Haatib na fulani, mtu mmoja katika Bani Saliim. Akawaambia wachukue kutoka kwao Sadaka iliyo haki kwao kuitoa. Wakenda mpaka wakafika kwa Thaalabah wakamwambia atoe Sadaka na wakamsomea barua ya Mtume Salallahu Alayhi Wasalam akasema hiki si kingine isipokuwa kodi (twatozwa) hii si kingine isipokuwa mwenzake kodi nendeni mpaka mkishamaliza rudini kwangu. Wakenda zao kwa yule Assalimiy akawakaribisha na akenda kuwatolea bora wa ngamia aliekuwa nao akawatenga kisha akaja nao kuwakabidhi hao wajumbe (hakika hii ni taufiki kutoka kwa Mola Subhanahu Wataala). Walipowaona wale ngamia na hali yao ilivyokuwa nzuri kabisa wakamwambia Assalimiy haina haja ya kutupa katika bora ya ngamia uliokuwa nao inatosha utupe walio hali ya wastani lakini akawaambia hapana chukueni hawa. Walipomaliza kuchukua sadaka kwa Assalimiy wakarejea kwa Thaalabah bin Haatib wakamtaka awape sadaka akawambia hebu nionesheni barua yenu (iliyotoka kwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam) akaitazama kisha akasema hii ni mwenzake (mfano wa) kodi nendeni zenuni mpaka nitazame nini rai yangu juu ya jambo hili wakaondoka mpaka wakamjia Mtume Salallahu Alayhi Wasalam na alipowaona akasema Salallahu Alayhi Wasalam:-   يا ويح  ثعلبة  “Ole wako Thaalabah” kabla wao hawajamwambia kitu na akamuombea Assalimiy halafu wakamwambia alivyowafanyia Thaalabah na alivyowafanyia Assalimiy.

Akateremsha Allah Subhanahu Wataala juu ya Thaalabah Aya ifuatayo:


                                                                                      التوبة: ٧٥ - ٧٧

“Na miongoni mwao (hao wanafiki) wako waliomuahidi Allah kuwa: Akitupa katika fadhila zake tutatoa sadaka na tutakuwa miongoni mwa wanaotenda mema (75) Lakini alipowapa hizo fadhila zake walizifanyia ubakhili na wakakengeuka, nao (mpaka hivi sasa) wanakengeuka (76) Kwa hiyo akawalipa unafiki (kutia) nyoyoni mwao mpaka siku ya kukutana naye (Allah), kwa sababu ya kukhalifu kwao waliomuahidi Allah na kwa sababu ya kusema kwao uwongo”(77).


Wakati ilipoteremka Aya hii kwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam alikuwepo hapo mtu miongoni mwa jamaa zake Thaalaba akasikia kitu gani Allah Subhanahu Wataala ameteremsha juu yake (Thaalaba) akatoka kumuendea Thaalaba alipofika kwake akamuambia:- Huna mama ewe Thaalaba Allah Ameteremsha juu yako kadha wa kadha. Akatoka (Thaalaba) mpaka akafika kwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam akamuomba amkubalie sadaka yake akasema Salallahu Alayhi Wasalam:-

إن الله منعني أن أقبل منك صدقتك

“Hakika Allah amenikataza kuipokea sadaka yako”. Hapo akawa ajimwagia udongo juu ya kichwa chake basi Mtume Salallahu Alayhi Wasalam akamwambia:-

هذا عملك أمرتك فلم تطعني

“Hii ni kazi yako (malipo ya kitendo chako) nimekuamrisha nawe hukunitii (hukunifuata maneno yangu)” Basi alipoona amekataa (Salallahu Alayhi Wasalam) kupokea kitu cho chote kutoka kwake akarudi nyumbani kwake na alipofariki Mtume wa Allah Salallahu Alayhi Wasalam akaja na sadaka yake kwa Abu Bakar Siddiq RA na vile vile akakataa kuipokea kisha akaja nayo kwa Omar RA naye kadhalika hakuipokea na akafa Thaalabah katika khilafah ya Othman bin Affan. Kama ilivyotolewa kutokana na Nabii wa Allah Subhanahu Wataala  Isa AS kuwa alikuwa apita njiani akamfuata mtu na huku akimwambia napenda kuwa katika usuhuba wako basi ndio hivyo wakawa pamoja na wakaondoka katika safari yao na wakaishia katika ukingo wa mto na wakakaa hapo kula chakula cha mchana na wao wana vipande vitatu vya mkate wakavila vipande viwili kikabakia kipande kimoja halafu akasimama Nabii Isa AS kwenda kunywa maji mtoni kisha akarudi. Aliporudi hakukikuta kile kipande kilichobakia cha mkate akamuuliza yule mtu: Nani aliechukua kipande cha mkate? Akamjibu: Sijui. Kisha akaendelea na safari yake pamoja na sahibu yake akaona paa na watoto wake wawili akamwita mmoja wao akamchinja kisha akamchoma halafu akamla pamoja na sahibu yake baadaye akamsemesha yule mtoto wa paa (aliekwisha chinjwa na kupikwa na kuliwa) simama kwa idhini ya Allah Subhanahu Wataala hapo akasimama na kumuendea mama yake. Akamwambia yule mtu nakuuliza kwa jina la yule aliekuonesha Aya hii nani aliechukua kile kipande cha mkate akajibu : “Sijui” kisha akaishia katika bonde la maji akauchukua Nabii Isa AS mkono wa yule mtu kisha akatembea nae juu ya yale maji alipovuka upande wa pili akamwambia:- Nakuuliza kwa jina la Yule aliekuonesha Aya hii nani aliekula kile kipande cha mkate akamjibu: Sijui kisha wakenda mpaka wakafika mahala penye amani. Hapo akakaa Isa AS na akawa akusanya mchanga mpaka ukawa kichuguu halafu akakiambia kuwa dhahabu kwa Idhini ya Allah Subhanahu Wataala kikawa dhahabu. Na akakigawa vifungu vitatu kisha akasema theluthi moja yangu na moja yako na moja ya aliekula kipande cha mkate. Basi hapo upesi akasema mimi ndio niliekula kile kipande cha mkate. Na baada ya kusikia haya Mtume wa Allah AS akasema chukua wewe mafungu yote matatu. Kisha akamwacha hapo naye akenda zake akabakia kainamia ile dhahabu ajaribu kuibeba lakini hawezi kwa uzito wake mkubwa na huku hawezi kwenda zake akaiwacha. Hatimaye wakaja watu wawili wakataka kumuuwa ili wapate kuichukua hiyo dhahabu, akafikiria ujanja kisha akawambia tuigawe sawasawa baina yetu na mmoja wenu ende mjini akatuchukulie chakula tupate kula. Akenda mmoja katika wao na huku afikiria katika nafsi yake kuwa awatilie wale wenzake sumu ili wafe halafu ile dhahabu yote aichukue yeye. Na kweli akafanya hivyo na huku wale waliobakia kuilinda ile dhahabu wakashauriana kumuua yule aliekwenda kuchukua chakula baadaye wagawane mali. Aliporudi wakamuua na wakakila kile chakula chenye sumu wakafa wote wawili na ikabakia ile mali na wenyewe wote wamekufa kando yake. Akapita Mtume wa Allah Isa AS nao wako katika hali hiyo akawaambia masahibu zake hii ndio Dunia na jinsi inavyowafanyia wale wanayoipenda basi tahadharini nayo. Hakuna kitu kibaya kama kuhadaika (kudanganyika) na Dunia kwani matokeo yake ni mabaya sana kwa mwenye kudanganyika nayo na kufikiria kuwa yuko katika maisha ya raha na wasaa Allah Subhanahu Wataala ametutolea mfano katika kitabu chake kitukufu:-


                                        ﭿ                     ﮈﮉ                                               ﮚﮛ                           ﮥﮦ                               النور: ٣٩ - ٤٠

 “Na wale waliokufuru, vitendo vyao (wanavyoviona vizuri) ni kama mazigazi, (mangati - sura ya maji) jangwani, mwenye kiu huyadhani ni maji, akiyaendea hayaoni chochote (na wao watakapoziendea amali zao Siku ya Kiyama. Hawatapata chochote kwani waliupinga Uislamu, na hali ya kuwa wanajua kuwa ndio Dini ya haki); Wamkute Allah hapo, awalipe hisabu yao sawa sawa; na Allah ni Mwepesi wa kuhisabu. (39) Au (amali zao zile mbaya) ni kama giza katika bahari yenye maji mengi; inayofunikwa na mawimbi juu ya mawimbi; na juu yake kuna mawingu, giza hili juu ya hili; anapoutoa mkono wake anakaribia asiuone (kwa kiza kilivyoshtadi); na ambaye Allah Hakumjaalia nuru hawi na nuru”.


Basi hivyo hakika kuhadaika na Dunia kunapoteza. Na sawasawa ikiwa kuhadaika huko ni kwa elimu au cheo au mali au heshima au ushujaa au ukarimu au mengineyo yanayomfanya mwanadamu ajione nafsi yake bora kuliko wengine.

Allah Subhanahu Wataala Ametuhadhirisha katika Qurani wakati Aliposema:-


                 لقمان: ٣٣

“Basi yasikudanganyeni maisha ya (hii) Dunia, wala asikudanganyeni yule mdanganyi mkubwa, (Ibliis) katika (mambo ya) Allah”.


Na amesema Allah Subhanahu Wataala :-


                         الحديد: ١٤

“Walakini nyinyi mlijitia wenyewe katika ukafiri (baada ya kuwa Waislamu) na mkangojea (mabaya yawafike Waislamu), mkajitia shaka (zisizokuwa na sababu), na matamanio ya nafsi (zenu) yakakudanganyeni”.


Mtume Salallahu Alayhi Wasalam amesema[1]:-

(حبذا نوم الأكياس وفطرهم كيف يغبنون سهر الحمقى واجتهادهم ولمثقال ذرة من صاحب تقوى ويقين أفضل من ملئى الأرض من المغترين)

“Ni bora usingizi (kulala) wa wenye akili na kula kwao (bila ya kuwa wamefunga kuliko ibada ya wajinga) na vipi (hao wenye akili) wanatamani kukesha kwa wajinga na jitihada yao (katika kufanya ibada) na hakika uzito wa punje (uzito mdogo sana wa kitendo) wa mwenye kumcha Mungu na mwenye yakini ni bora kuliko (vitendo) vya wanaojivuna waliojaa katika Dunia (kwa wingi wao)” Ameitoa hadithi hii Abu Addardaa.


Amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-

 ( الكيس من دان نفسه وعمل لما بعد الموت والأحمق من أتبع نفسه هواها وتمنى على الله الأماني )

 “Mwenye akili ni yule anayeifanyia hisabu nafsi yake (akafanya mema) na akatenda kwa ajili ya (usalama wake) baada ya mauti na mjinga ni mwenye kufuata matamanio ya nafsi yake (akafanya maasi na akatarajia kwa Allah malipo mazuri”. Ameitoa Shaddaad bin Aws.

Baadhi ya wanavyuoni wamefasiri maana ya “ghuruur” ni “kuipa mtu nafsi yake mambo yanayowafiki matamanio”. Huyu haipingi nafsi yake na anaifuata moja kwa moja (nafsi mara nyingi inaamrisha mabaya) na inavyotaka kuifanyia jihadi (kupigana nayo jihadi). Na mfano wa watu hawa kama wale wanaosema kulipwa keshi (tasliimu) ni bora kuliko kuakhirishwa yaani kulipwa baadaye. Na Dunia ni keshi na Akhera ni kuakhirishwa. Yakini ni bora kuliko shaka na ladha za Dunia ni yakini ama ladha za Akhera ni shaka na kipimo kama hichi kibovu kinafanana na kipimo cha Ibliis katika kauli yake Allah Subhanahu Wataala  Akizungumzia habari yake (Ibliis):


                     الأعراف: ١٢

“Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. (mimi) umeniumba kwa Moto, naye umemuumba kwa udongo”.


Na anasema huyu mwenye kughurika na Dunia kama ingekuwa mimi sie bora na mpendwa kwa Allah Subhanahu Wataala asingenipa neema zote hizi na ihsani zote hizi kwa hivyo amekosea wakati anapofikiria kuwa kila aliejaziwa ihsani amependwa anapofikiria kuwa kila neema za Dunia zafuatia baadaye neema za Akhera:


                  الكهف: ٣٦

“Na kama (kitatokea hicho kiama) nikarudishwa kwa Mola wangu, bila shaka nitakuta kikao chema kuliko hiki.”


Watu wema wakikabiliwa na Dunia huogopa na hufikiria kuwa hii ni fitina (mtihani) imewajia kinyume ya walioghurika (na Dunia) ikiwakabilia hufikiria kuwa ni heshima kutoka kwa Allah na ikiondoka Dunia kutoka kwao huona kuwa wamepuuzwa, kama Alivyosema Allah Subhanahu Wataala :


                                                     الفجر: ١٥ - ١٦

“Lakini mwanadamu, Mola wake Anapomfanyia mtihani Akamtukuza na kumneemesha, basi husema: Mola Wangu Amenitukuza (wala hashughuliki kufanya mema ili kutengeneza Akhera yake) (15) Na Anapomfanyia mtihani Akampunguzia riziki yake husema: Mola wangu Amenidhalilisha (nikifanya mema au mabaya ni sawa sawa, hatayashughulikia basi naendelea kufanya mabaya)(16)”.

Akamjibu Allah Subhanahu Wataala kumwambia huyo mtu sivyo hivyo (كلا) bali nyinyi hamuwatizami mayatima wala hamuwalishi masikini.


Wakati mtu anapofanya maasi na  akiambiwa awache kufanya hayo maasi husema:- Hakika Allah Karimu (Atanisamehe madhambi). Amesema Al-Ghazaliy:- Ukisema kuwa makosa wanayo wale waasi wanaosema kuwa Allah Karimu na sisi twatarajia rehema zake na maghufira kwani Yeye Amesema Mimi niko katika dhana ya mja wangu kwangu basi anidhanie mja wangu anavyotaka. Basi jua kuwa sheitani hampotezi binadamu isipokuwa kwa maneno yanayokubalika katika dhahiri yake na yakatalika katika undani wake kwani ingekuwa sio kwa uzuri wa dhahiri yake zisingehadaika nyoyo kwao, lakini Mtume Salallahu Alayhi Wasalam ametufunulia hayo akasema:-

 ( الكيس من دان نفسه وعمل لما بعد الموت و الأحمق من أتبع نفسه هواها ويتمنى على الله )

 “Mwenye akili ni yule anayeifanyia hisabu nafsi yake (akafanya mema na kuacha mabaya) na akatenda kwa ajili ya (usalama wake) baada ya mauti. Na mjinga ni mwenye kufuata matamanio ya nafsi yake (akafanya maasi) na akatarajia kwa Allah malipo mazuri.”


Akasema (Al-Ghazaliy) na hii ndio kutamani (bila ya kufanya vitendo) ambako shaitani amekuita kutaraji  (رجاء) (huku ni kutumai na kutaraji rehema ya Allah baada ya kutekeleza amri zake) ambako amewahadaa wajinga wakafikiria kuwa inawezekana kupata rehema na maghufira bila ya kumtii Allah Subhanahu Wataala.

Allah Subhanahu Wataala ametoa sherehe ya kutaraji (رجاء)  Akasema:-


                          البقرة: ٢١٨

 “Hakika wale walioamini na wale waliohajiri (wakahama kwenda Madina) na wakapigania njia ya Allah, hao ndio wanaotumai rehema za Allah”.


Basi hao ndio hakika watumai rehema ya Allah Subhanahu Wataala baada ya kuamini na kutenda wanayowajibika kuyafanya. Kuna tofauti kubwa baina ya Aliyesema Allah juu yao:-


                  المؤمنون: ٦٠

“Na hao ambao watoa (Zaka na sadaka katika mali) waliyopewa, na hali nyoyo zao zinaogopa kwa kuwa watarejea kwa Mola wao.”


Wajiangusha katika kumuabudu Mola wao nao wanalia kwa kumuogopa (Mola wao).

          الذاريات: ١٨

“Na wakiomba maghufira (msamaha) nyakati za kabla ya alfajiri.”


Kuna tofauti kubwa sana baina ya hawa na baina ya waliojizamisha katika matamanio yao na juu ya hivyo wacheka wasema Allah Karimu basi nani mwenye akili asema hawa wawili mbele ya Allah ni sawa. Au kauli yake Allah Karimu inamtosha yaani hana haja tena ya toba na kurejea kwa Mola wake.

Basi mbona yule wa mwanzo vile vile kasema Allah Karimu, mwenye rehema na mwenye kughufuru lakini hakutosheka bali akafatilia na vitendo vizuri.

                  القلم: ٣٥

“Je! Tuwafanye wanaotii sawa na waasi?”


                                      ﯭﯮ         الجاثية: ٢١

“Je! Wanafikiri wale waliofanya maovu kuwa tutawafanya kama wale walioamini na kutenda mema kwamba maisha yao na mauti yao yawe sawa? Ni hukumu mbaya wanayoihukumu (ya kuwa wote watakuwa sawa).”


Na ghururi (kuhadaika na kudanganyika kwa kujiona kuwa neema alizokuwa nazo ni kwa uhodari wake mwenyewe kama elimu, mali, uzuri, cheo n.k) iliokuwa mbaya sana ni ile inayowapata wenye elimu (wanavyuoni) kujiona na kujivunia na elimu yao na kufikiria kuwa wao ni bora kuliko wengine na kuwa Allah Subhanahu Wataala Hakuwapa elimu isipokuwa Kawachagua na kuwapenda na wamesahau nini Allah Amesema juu yao:-


                            الأعراف: ١٧٥

“Na wasomee habari za wale tuliowapa Aya zetu (kuzijua), kisha wakajivua nazo (wasizifuate). Na shetani akawaandama, wakawa miongoni mwa waliopotea (wasomee habari za wabaya pia wazijue wajiepushe nazo)”.


Na wengineo wengi aina kama hii na hasa wenye kutoa mawaidha wakati wanaposimama juu ya majukwaa wafikiria katika nafsi zao kuwa kipaji hichi hawakupewa isipokuwa wao tu na Allah Subhanahu Wataala na kuwa wao tu ndio wanaoinusuru Dini ya Allah na wanao waongoza Waislamu. Na ikiwa wao wanajiona kama hivyo basi wao sio isipokuwa kama taa yamulika kwa ajili ya watu nayo yenyewe (hio taa) yaungua na vile vile kama mfano wa nyumba iliyo giza na taa ipo lakini imewekwa juu ya sakafu yake. Wao katika dhahiri yao wawaita watu ili kumuabudu Allah na hali wao wenyewe wamkimbia na kadhalika watia katika nyoyo za watu hofu ya Allah Subhanahu Wataala na hali wao wenyewe nyoyo zao ziko katika amani na adhabu yake Subhanahu Wataala.

Allah ameshabihisha mfano wa hao ni kama mbwa na punda basi kudhalilishwa na kupuuzwa gani kukubwa zaidi kuliko huko. Na hao wako vikundi viwili kikundi kimoja kimejiepusha na maasi ya dhahiri na waonekana kuwa watu wema lakini undani wao umeingiliwa na kujiona nafsi zao bora kuliko wengine na wawaona watu wengine ni mzigo juu yao na kuwa wawategemea wao katika mambo yao na kuwa wana fadhila kubwa kwa sababu ya uwezo wa kuzungumza waliopewa. Na kikundi cha pili vile vile waonekana watu wazuri kwa mujibu wa madh-hari yao (udhahiri) lakini hawaoni mambo ya matamanio isipokuwa huyafanya, wala tamaa isipokuwa huigeuza ndio mungu wao basi unawaona kama simba juu ya majukwaa lakini huwa kama nzi (hawawezi kujizuia kwa udhaifu wao) mbele ya tamaa ama katika upweke wao wanakuwa majahili hawafanyi yale wanayowahimiza watu kuyafanya (katika amri za Allah Subhanahu Wataala) na husema mambo yahukumiwa kwa mwisho wake, na mengineyo katika mielekeo inayowadhuru.

Anasema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-

)من ازداد علما ولم يزدد هدى لم يزدد من الله إلا بعدا(

 “Mwenye kuzidi elimu bila ya kuzidi uongofu hazidi isipokuwa kuwa mbali zaidi na Allah Subhanahu Wataala”.


Na amesema Salallahu Alayhi Wasalam:

 ( يلقى العالم في النار فتندلق أقتابه فيدور بها في النار كما يدور الحمار في الرحى )

 “Hutupwa Mwanachuoni Motoni mpaka yatoka matumbo yake na huzunguka nayo Motoni (hayo matumbo) kama anavyokizunguka punda kinu (cha kusagia nafaka kama ngano n.k)”.


Na anasema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-

 ( ويل لمن لم يعلم مرة وويل لمن يعلم ولم يعمل مرتين )

 “Ole wake aliekuwa hajui (mjinga) mara moja na ole wake aliekuwa anajua na hakutenda (kwa mujibu wa elimu yake) mara mbili”. Yaani elimu yake inakuwa hoja juu yake Siku ya Kiyama.


Na anasema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-

 ( أشد الناس عذابا يوم القيامة عالم لم ينفعه الله بعلمه )

 “Watu watakaoadhibiwa zaidi Siku ya Kiyama ni Mwanachuoni ambaye Allah hakumjaalia kufaliwa na elimu yake”.


Amesema Ibn Masood RA:-

( كفى بخشية الله علما وكفى بالاغترار بالله جهلا )

“Kumuogopa Allah kunatosha kuwa elimu na kuhadaika na Allah kunatosha kuwa ujinga’.


Omar bin Al-Khattab RA alimuona mmoja katika Masahaba azunguka Al-Kaaba (afanya tawaf) na nyuma yake wanafunzi wake akampiga (Omar RA yule Sahaba) fimbo yule sahaba akamuuliza ubaya gani ulioniona nimeufanya? Akamjibu sikuona ubaya wowote lakini ni kumbusho kwani watu kidogo tu ambao hayaingii katika nyoyo zao majivuno vikipigapiga viatu nyuma yao watembeapo. Tizama hadhari yao iko namna gani watu walioridhiwa na Allah Subhanahu Wataala na wamechaguliwa basi walinganishe hao na watu wa siku zetu hizi utamuona mmoja wao anajigamba (anasema) nani kama mimi kwa uhodari na ufasaha na ndie mimi nilioihami Dini hii ya Allah Subhanahu Wataala na nikiwafundisha waja wake hii Dini na nikapata radhi ya Allah Subhanahu Wataala kwa kufanya hivyo. Hajui maskini huyu kuwa amepata ghadhabu ya Allah Subhanahu Wataala na amejiweka mbali nae wakati anapojifikiria kuwa anajikaribisha nae.

Ewe unaemtaka Allah (radhi yake) muendee katika njia yake ama sivyo kunyimwa (radhi ya Allah Subhanahu Wataala ) ndio matokeo yake.

Kwa ujumla Muislamu yuko katika hatari ambayo imemzunguka kutoka kila upande lakini iwapo ataichunga nafsi yake kwa makini sana na kuifanyia hisabu basi matokeo yake ni kupewa tawfiiq na Allah Subhanahu Wataala ya kufikia radhi yake.

         التغابن: ١٦

“Mcheni Allah muwezavyo (mwisho wa jitihada yenu).”


Kinazungumziwa kisa katika kuihisabu nafsi hisabu iliyo ngumu:-

Kuwa kuna mtu alikuja kwa Bishr bin Al-Haarith kumuaga akamuambia nimeazimia kutoka kwenda kuhiji je kuna utumwa wowote? Akamuuliza kiasi gani ulichotayarisha kwa matumizi yako? Akamjibu dirham elfu mbili. Akasema Bishr wakusudia kwa hija yako hii nini? Kwa ajili ya kuabudu (kufuata amri zake Allah Subhanahu Wataala) au kwa kutamani kuiona Al-Kaaba au kwa ajili ya kutaka ridha ya Allah Subhanahu Wataala? Akajibu ni kwa ajili ya ridha ya Allah Subhanahu Wataala. Akamwambia jee ukipata ridha ya Allah Subhanahu Wataala nawe uko nyumbani kwako kwa kuzitumia hizo dirham elfu mbili utakaa nyumbani kwako? Akamuambia ndio nitakaa. Akamuambia nenda ukawape hizo pesa watu kumi walio na madeni wapate kulipa madeni yao na umpe fakiri umuondolee mashaka yake na umpe mwenye watoto masikini awatosheleze watoto wake na umpe anaelea mayatima umfurahishe na moyo wako ukiwa una nguvu ya kuweza kumpa mtu mmoja (pesa zote hizo) basi mpe kwani kuingiza kwako furaha katika moyo wa Muislamu na kumwokoa alie na shida na kumuondolea mtu madhara na kumsaidia aliye dhaifu ni bora kuliko hija mia baada ya hija ya faridha (ya Uislamu) basi simama nenda kazitoe kama nilivyokuamrisha na kama sivyo basi nambie kitu gani kilichokuwa katika moyo wako. Akasema Ewe Aba Nasr safari yangu kwenda kuhiji ndio yenye nguvu zaidi moyoni mwangu. Akacheka Bishr na akamwambia:- mali ikikusanywa mnamo uchafu wa biashara na shubuha inalazimika nafsi itumie (hiyo mali) katika haja yoyote ile na hapo inajidhihirisha kuwa inafanya vitendo vizuri (kama kwenda kuhiji “tatawuu”(sunna) na hali ziko njia nyingine ambazo ukiitumia humo unapata ridhaa yake Subhanahu Wataala na ujira mkubwa) na Allah Subhanahu Wataala Ameapa kwa Nafsi yake kuwa hakubali vitendo isipokuwa kutoka kwa wacha Mungu.

           

Katika miongoni mwa adabu za waliotangulia ni walikuwa wapole kwa ndugu zao (wa Kiislamu) na kuamkiana kwa kupeana mikono na katika hayo kuna hadithi nyingi zilizokuja moja wapo kauli yake Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-

)قبلة المسلم أخاه المصافحة(

“Kumuamkia Muislamu ndugu yake ni kumpa mkono”.

Na imetolewa na Anas bin Malik kuwa amesema: Aliambiwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam kuwa mtu akutana na ndugu yake na rafiki yake amuinamie? Akasema: Hapana. Akaambiwa amkumbatie na ambusu akasema: Hapana. Akaulizwa ampe mkono Akasema : Ndio.


Vile vile katika adabu zao kumsimamia anaekuja nayo ni sunna yake Salallahu Alayhi Wasalam imetolewa habari kuwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam alimsimamia Jaafar bin Abi Taalib wakati alipomjia na akasema Salallahu Alayhi Wasalam:-

( ما أنا بفتح خيبر أسر مني بقدوم جعفر )

 “Furaha yangu ya kufunguliwa (kushinda vita vya) Kheiybar si zaidi kuliko ya kuja kwa Jaafar.”


Akawaambia Salallahu Alayhi Wasalam Ansari wakati alipokuja Saad bin Muadh RA:

( قوموا لسيدكم )

“Msimamieni bwana wenu”

Basi ada ya watu wa Oman ya kumsimamia anaekuja kwao iko katika msingi wa sunna ya Mtume Salallahu Alayhi Wasalam.


Katika sunna kumletea chakula mgeni wake (anaemtembelea) kama alivyotoa kisa Laqiit bin Sabrah akasema tumekwenda kwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam lakini hatukumkuta nyumbani kwake tukamkuta Aisha RA akaamrisha tufanyiwe harisa (chakula chatengezwa kwa unga na maziwa) tukafanyiwa na vile vile tukaletewa sahani ya tende tukala kisha akaja Mtume Salallahu Alayhi Wasalam akasema: Je mmepata chochote (chakula) هل أصبتم شيئا Tukajibu ndio ewe Mtume wa Allah.


Vile vile katika sunna kwa mtu anaerudi safarini awaletee chakula wanaokuja kumwamkia kama ilivyokuja kuwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam alirudi kutoka safari akachinja ngamia.

Haitakiwi kurudi mtu nyumbani kwake usiku kutoka safarini kwa makatazo ya Mtume Salallahu Alayhi Wasalam kuwagongea watu wa nyumbani kwako usiku akasema Salallahu Alayhi Wasalam:-

)إذا قدم أحدكم من سفر فلا يطرقن أهله ليلا(

“Akija mtu kutoka safarini asiwagongee watu wa nyumbani kwake usiku”.


Nasema katika wakati huu ambao mtu hana hiari katika kufika nyumbani kwake (kwa sababu taratibu za nyakati za misafara imekwisha pangwa na makampuni ya ndege, train na mabasi n.k. haiko katika mikono ya mtu binafsi kuchagua wakati anaotaka kusafiri na kurudi nyumbani kwake pengine wakati wa kurudi kwake usiku basi ikiwa hapana budi isipokuwa hivyo na awapigie simu nyumbani kwake awajulishe kuwa anarejea wakati huo wa usiku na akifanya amekuwa kama kwamba amerejea mchana kwani inakuwa imeondoka ile sababu ambayo kwa ajili yake amekatazwa na Mtume Salallahu Alayhi Wasalam. Amesema Kaab bin Maalik kuwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam harudi kutoka safarini isipokuwa mchana katika wakati wa dhuhaa.


Vile vile katika adabu za anaerudi safarini asali rakaa mbili katika msikiti ulio jirani na nyumba yake na hichi kitu kimependelewa na wanavyuoni kwa fadhila kubwa kwa mwenye kuweza kukifanya.


Katika wasiya wa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam uliojumuisha mengi ni wasiya wake kwa Muadh bin Jabal wakati alipomwambia:

 ( يا معاذ أوصيك بتقوى الله وصدق الحديث والوفاء بالعهد وأداء الأمانة وترك الخيانة وحفظ الجوار ورحمة اليتيم ولين الكلام وبذل السلام وحسن العمل وقصر الأمل ولزوم الإيمان والتفقه في القرآن وحب الآخرة والجزع من الحساب وخفض الجناح وإياك أن تسب حليما أو تكذب صادقا أو تطيع آثما أو تعصي إماما عادلا أو تفسد أرضا . أوصيك باتقاء الله عند كل حجر وشجر ومدر وأن تحدث لكل ذنب توبة السر بالسر والعلانية بالعلانية بذلك أدب الله عباده ودعاهم إلى مكارم الأخلاق ومحاسن الأدب )

“Ewe Muaadh nakuusia katika kumcha Allah Subhanahu Wataala na ukweli katika kuzungumza, na kutimiza ahadi na kutekeleza amana na kuacha khiyana na kuhifadhi ujirani na kurehemu yatima na kuzungumza kwa upole na kutoa Salamu (kuamkiana kwa Kiislamu) na kufanya vitendo vyema na kufupisha mategemeo (ya kuishi) na kujifungamanisha na Imani na kusoma (na kuielewa) fiqhi ya Qur’ani na kupenda Akhera na kuiogopa hesabu na kuwa mpole na usije ukamtukana mtu mwenye subira (subira kubwa na mpole) na usimkadhibishe mkweli na usimtii mfisadi na usimuasi Imamu (kiongozi) muadilifu au usiharibu ardhi. Nakuusia umche Allah panapo kila mawe na miti na  kijiji. Na utubu kwa kila dhambi (unalolifanya) siri kwa siri na uwazi kwa uwazi (dhambi la siri ulifanyie toba kisirisiri na la uwazi vile vile toba yake iwe uwazi) hivyo ndivyo Allah alivyowafunza adabu waja wake na akawaita kufanya tabia njema na adabu nzuri”.


Ametoa Muadh vile vile kutokana na Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-

( خذ الإسلام بمكارم الأخلاق ومحاسن الأدب )

“Uchukue Uislamu kwa tabia njema na adabu nzuri”.



Inasemekana kuwa hakuvaa mja vazi lililo bora kuliko unyenyekevu na anaeruzukiwa unyenyekevu basi amepumzika na amepumzisha (watu wengine).

Na ametoa (hadithi) Anas RA kuwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam amesema:-

( إن الله أوحى إلي أن تواضعوا ولا يتباهى بعضكم على بعض )

“Hakika Allah ameniletea wahyi kuwa Muwe wanyenyekevu na msiringiane baadhi yenu kwa baadhi”.


Na amesema Salallahu Alayhi Wasalam kuwa katika kauli ya Allah Subhanahu Wataala :-

                        آل عمران: ٣١

“Sema (ewe Muhammad)ikiwa mnadai  mnampenda Allah basi nifuateni mimi”


Kasema:

)على البر والتقوى والرهبة وذل النفس(

 “Kuwa kumfuata katika mambo mazuri (ukiyafanya wapata thawabu na radhi ya Allah) na kumcha Mungu na kumuogopa (kumuabudu Allah) na kujidhalilisha nafsi”.


Na alikuwa Salallahu Alayhi Wasalam kwa unyenyekevu wake anakubali mwito wa aliye huru na mtumwa na akubali zawadi ijapokuwa ni chubuo moja la maziwa (kwa udogo wake) au paja la sungura na alikuwa akiilipa (hiyo zawadi kwa kutowa kitu kingine kwa yule aliempa zawadi) na akiila (hiyo zawadi) na hatakabari katika kuitikia mwito wa kijakazi (mtumwa mwanamke) na wa masikini na husema:

( إن من رأس التواضع أن تبدأ بالسلام من لقيت وترد على من سلم عليك وأن ترضى بالدون من المجلس وأن لا تحب المدحة والتزكية والبر )

 Hakika miongoni mwa kiini cha unyenyekevu ni kuanza kumsalimia (kuamkiana kwa Kiislamu) unaemkuta na kumjibu Salamu anaekuamkia na kuridhika na kikao cha duni(chini kabisa) katika majlisi na usipende kusifiwa na kuonekana kuwa wewe ni bora kuliko wengine kwa imani na vitendo.”


Na anasema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-

)طوبى لمن تواضع من غير منقصة وذل في نفسه من غير مسكنة(

“Malipo makubwa (mazuri na inasemekana kuwa  طوبي  ni jina la mti katika Al-Jannah) kwa mtu aliye mnyenyekevu bila ya kuwa ana upungufu wowote (yaani hana upungufu wa mali au cheo au ukoo mzuri) na aliyejidhalilisha nafsi yake bila ya haja (hahitajii kwa mtu kitu chochote).”


Na aliulizwa mmoja katika watu wema juu ya unyenyekevu akasema kuikubali haki na kuifuata na kuikubali kwa alieisema na umsikilize na vile vile kasema anaeiona nafsi yake ina thamani basi huyo hana sehemu katika unyenyekevu. Inasemekana kuwa imeandikwa katika vitabu vya Allah: “Hakika Nimetoa vizazi (vya binaadamu) kutoka mgongo wa Adam (AS) na sikupata moyo ulio na unyenyekevu zaidi kwangu kuliko moyo wa Musa (AS) ndio kwa hivyo Nimemchagua na Nimezungumza nae”. Na yasemekana anaetambua yaliyofichika katika nafsi yake basi hafanyi tamaa ya kupata makubwa na heshima na huenda njia ya unyenyekevu wala hagombani (hamkasirikii) na anaemtukana. Na humshukuru Allah Subhanahu Wataala kwa yule atakaemsema yeye kwa vizuri. Na amesema Luqman AS: “Kila kitu kina kipando na kipando cha elimu ni unyenyekevu”. Hakuna kitu kinachomletea mtu unyenyekevu kama kusuhubiana na watu wema. Mmoja wao aliulizwa nini kikomo cha unyenyekevu akasema:- Uwe unapotoka nyumbani kwako humkuti mtu isipokuwa unamuona bora kuliko wewe.

Aliulizwa mmoja katika watu wenye hekima: Je unajua neema ambayo hahusudiwi mwenye kuwa nayo wala balaa ambayo hahurumiwi mwenye kuwa nayo. Akasema ndio. Akasema amma neema ambayo hahusudiwi aliye nayo hiyo ni unyenyekevu na balaa ambayo hahurumiwi mwenye kuwa nayo ni kiburi. Na unyenyekevu ni sifa yenye nguvu inakuwa katikati baina ya kiburi na kujiteremsha mtu kadari yake (kupindukia kiasi) amma kiburi ni kujipandisha mtu nafsi yake zaidi ya kadari yake amma sifa inayokabili hii ni kujiteremsha mtu nafsi yake kufika daraja ya kujipuuza na kujidharau na inafikisha kupoteza haki yake. Na katika sifa ya waumini kuwa baina ya sifa mbili hizi (daraja mbili hizi) mbaya (ovu) kwani kiburi bila ya shaka chanzo chake ni ujinga kama ilivyosemwa na mmoja wa walioghurika:- “Nimemvisha (farasi wangu tandiko lake) na nimejifunika uso wangu nikazunguka sehemu zote za ardhi na nikasema je yuko aliye tayari kutoka kupigana na mie basi hakutoka mtu kunijia”. Kiburi kinamtia mtu ukubwa aliekuwa hakuufikia.

Allah Subhanahu Wataala amewatoa maanani wenye kiburi Amesema Subhanahu Wataala:-

              النحل: ٢٣

“Kwa hakika Yeye hawapendi wanaotakabari”


Na akasema:-

     ﭿ      الزمر: ٦٠

“Je, si katika Jahannamu makazi ya wale wanaotakabari”


Amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam katika hadithi Qudusiy:

 ( الكبرياء ردائي والعظمة إزاري فمن نازعني واحدا منها قذفته في نار جهنم )

 “Kiburi ni shati langu na ukubwa ni kikoi changu atakaenyan’ganyiana nami moja katika hayo basi nitamtumbukiza Motoni.”


Na Allah ametuonesha dawa kwa aliyepata maradhi hayo Akasema Subhanahu Wataala:-

                      الطارق: ٥ - ٦

“Hebu naajitizame mtu, ameumbwa kwa kitu gani (5) Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa(manii)”(6).


Na kauli yake:


                                     

 عبس: ١٧ - ١٩

“Ameangamia binaadamu namna gani ulivyo kwendelea mno ukafiri wake (17) Kwa kitu gani Amemuumba (18) Kwa tone la manii; Amemuumba Akamuwezesha (Akampa uweza)”(19).


Amesema mwana hekima:

( كيف يزهو من رجيعه أبد الدهر ضجيعه )

“Vipi ajiona bora ambaye kwenye tumbo lake kumejaa uchafu na kila anapolala haumbanduki uchafu huo.”

Vipi anatakabari mtu hali ameumbwa kwa udongo. Milele yeye huwa mwenye kufanya makosa.


Mukabili wake ni kujiteremsha mtu chini ya kadiri yake kwani haitakiwi Muislamu kujiteremsha nafsi yake mahala pa kujidharaulisha na kufanyiwa masikhara na hasa waliosoma na wavaao vilemba vyeupe (amama) wanaojishabihisha na watu wema hao ndio wachukiza zaidi wakifanya hivyo. Basi na wawe katika msimamo wa mtu mwenye nguvu katika elimu yake na Dini yake na sio kusimama msimamo wa alie shindwa na kuwa dhalili na ajijue kuwa yeye yuko katika nguvu kubwa mazali ameshikamana na kumtii Allah Subhanahu Wataala kwani Asema:-


          المنافقون: ٨

“Na utukufu hasa ni wa Allah na Mtume wake na wa Waumini”.


Hakuwaambia maneno haya matajiri na wanaojikaribisha na viongozi basi ijue kadiri yako ewe uliesoma na uiweke pale alipoiweka Allah. Wala usijidhili kwa kuwafuata wanaopenda Dunia na kujifanya una haja mbele yao kwani wewe ni bora zaidi kuliko wao. Kisha baada ya hivyo muweke kila mtu katika daraja yake bila kumdharau. Ameitwa Al-Hassan bin Aliy “mdhalilishaji wa Waumini” wakati alipojiteremsha (daraja) na kumpa Muawiya haki bila ya kuwa na haki nayo. Hakika katika mambo yanaosikitisha sana kuwa baadhi ya waliosoma au wanaojifananisha na watu wema wajitenga na kujidhalilisha mbele ya wenye vyeo au matajiri basi kwa hivyo waliharibu jina la haki na watu wake (wa haki) kwani wawafanyia sababu watu wajeuri kurefusha ndimi zao juu ya watu wa fadhila (wa Dini, wema).


Mara nyingi wasikia watu wajeuri (wahuni) wakiwasema watawaa (walioshika Dini) kwa kujitakia na kujiharibia wenyewe watawaa hata wakawapa fursa hao wahuni kuwaudhi. Yasemekana hapo zamani kulikuwa na kadhi ambaye ameimbiwa na muimbaji mpaka akastarehe kisha akajivalisha kamba shingoni akasema nivuteni nipate kuwa zawadi (hadyi) ya Al-Kaaba kwani mie n’gombe, kwani kajidharaulisha mwenyewe na huu ni mfano kwa wengine vile vile.

Omar bin Khattaab RA alimuona mtu anakwenda kajiinamia akamwambia nyanyua kichwa chako usituharibie Dini yetu. Sheikh Saleh bin Aliy Al-Haarthy alimuona mtu amejitenga naye kajiinamia akamwambia una nini? Akamjibu nimevaa amama (kilemba cheupe ambacho ukikivaa umefuata sunna ya Mtume Salallahu Alayhi Wasalam) nimekuwa mutawaa. Akamwambia kazana kwani wafikiria anaekuwa mutawaa anapooza na kuwa mnyonge. Akamvua amama yake na kuitupa chini. Mtu anaekamata Dini lazima awe mfano mzuri kwa wengine kwa tabia nzuri na ushujaa na kukazana. Amesema Abu Nasr Al-Maghribiy katika shairi lake kwa maana yake:-

Nampenda kijana anaetafuta maendeleo (elimu na kazi na mengineyo) na amekazana kwa ajili ya Dunia na Akhera. Amma ndugu yake usingizi hakaribishwi kwangu wala alielegea na kupooza asiependa maendeleo.


Kuingiliana na watu pamoja na kushika amri za sheria ya Dini (zinazohusiana na haki za watu) ni bora kuliko kujitenga ijapokuwa imekuja katika hadithi ya Mtume Salallahu Alayhi Wasalam ishara ya kupendelea kujitenga na mtu kukimbia na Dini yake. Basi hivyo ni wakati hawezi muumini kusimamisha Dini yake na aogopa kuwa atawacha kufanya yaliyomuwajibikia kuyafanya au kufanya maasi (ikiwa atachanganyika na watu) kama ilivyokuja (hadithi) kutokana na Abdullah ibn Masood RA amesema:-

Amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-

 ( ليأتين على الناس زمان لا يسلم لذي دين دينه إلا من فر بدينه من قرية إلى قرية ومن شاهق إلى شاهق ومن جحر إلى جحر  كالثعلب الذي يروغ قالوا ومتى ذلك يا رسول الله قال إذا لم تنل المعيشة إلا بمعاصي الله فإذا كان ذلك الزمان حلت  العزوبة) . قالوا وكيف ذلك يا رسول الله وقد أمرتنا بالتزويج قال (إنه إذا كان ذلك الزمان كان هلاك الرجل على يد أبويه فإن لم يكن له أبوان فعلى يد زوجته وولده فإن لم يكن له زوجة ولا ولد فعلى يد قرابته) قالوا وكيف يا رسول الله قال (يعيرونه بضيق المعيشة فيتكلف ما لا يطيق حتى يوردوه موارد الهلكة)

 “Utawajia watu wakati hasalimiki mwenye Dini na Dini yake isipokuwa ataekimbia na Dini yake kutoka mji kwenda mji mwingine na kutoka mlima (mrefu) kwenda mlima mwingine na kutoka shimo kwenda shimo jingine kama mbweha anayechenga. Wakasema na lini yatakuwa hayo ewe Mtume wa Allah, Akasema: wakati maisha yatakuwa hayapatikani isipokuwa kwa maasi ya Allah. Basi ukifika wakati huo unahalalika ujane. Wakasema na vipi hivyo ewe Mtume wa Allah na hali wewe umetuamrisha kuoa. Akasema : Hakika unapokuja wakati huo kunakuwa kuangamia kwa mtu katika mikono ya wazazi wake na akiwa hana wazazi basi katika mikono ya mkewe na watoto wake na akiwa hana mke wala watoto basi katika mikono ya jamaa zake. Wakasema vipi hivyo ewe Mtume wa Allah. Akasema wanamnyanyasa kwa ajili ya udhiki wa maisha yake basi hapo ndipo anapojikalifisha zaidi ya uwezo wake mpaka wanamwingiza katika mambo ya kuangamiza”.


Basi kama hivyo amebainisha Mtume Salallahu Alayhi Wasalam wakati gani kujitenga (na watu) kwapendelewa bali ni wajibu ikiwa kuchanganyika na watu kutamharibia mtu Dini yake.


Ama ikiwa aweza kusema haki hata ikiwa hasikilizwi na ikiwa aweza kumuongoza anaetaka kuongozwa na kumuelekeza aliepotea basi kama huyu kukaa kwake katika jamii ni bora kuliko kuondoka kama ilivyotolewa kuwa Allah Subhanahu Wataala amemteremshia wahyi Dawud AS : Ewe Dawud vipi Nakuona umejitenga uko peke yako. Akajibu: Mola wangu nimewaacha watu kwa ajili Yako. Basi Allah Akamletea wahyi; Ewe Dawud kuwa mwenye kuzinduka ujichukulie marafiki na kila rafiki aliyekuwa haniridhishi Mimi usifuatane nae kwani huyo moyo wako utaingia ugumu kwake na atakupeleka mbali na mimi. Imekuja katika habari: Hakika aliye na daraja bora miongoni mwenu mbele ya Allah ni wale wanaozoea na kuzoewa (na watu) kwani muumini anazoea na anazoewa (azoeleka). Amesema Ubadat bin Assaamit RA kuwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam amesema:-

 ( يقول الله عز وجل حقت محبتي للمتحابين في والمتزاورين في والمتباذلين في والمتصادقين في )

 “Asema Allah Mwenye nguvu Aliyetukuka yamewajibika mapenzi yangu kwa wanaopendana kwa ajili Yangu na wanaotembeleana kwa ajili Yangu na wanaopeana kwa ajili Yangu na wanaofanyiana ukweli kwa ajili Yangu.”


Vile vile imetokana na Mtume wa Allah:

( المؤمن كثير بأخيه )

“Muumini ni mwingi kwa ndugu yake”.


Kuyafanyia umuhimu mambo ya Wailamu ni wajibu na asiyeyafanyia umuhimu mambo ya Waislamu basi sio miongoni mwao na aliekuwa hana rafiki hana maisha (mazuri) na amesema Allah azungumzia hali ya makafiri katika Akhera:-

                       الشعراء: ١٠٠ - ١٠١

“Basi hatuna waombezi (100) Wala rafiki khalisi (101)”


 الحميم   katika asili yake ni  الهميم    ikabadilishwa harufu  هـ  ikawekwa badala yake  ح   na  الهميم   imechukuliwa kutokana na  الاهتمام  yaani kufanya umuhimu mambo ya ndugu yake (rafiki yake awe naye).


Amesema Omar RA:- Akiona mmoja wenu mapenzi kutoka kwa ndugu yake (rafiki yake) basi amkamate (huyo rafiki awe naye).


Tunamuomba Allah Subhanahu Wataala Atupe taufiki (ya kushika Dini yake) na mwisho mwema na kufa katika uongofu na tufanye kwa mujibu wa elimu yetu na hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kwa Allah na rehema na Salamu ziwe juu ya mbora wa viumbe vya Allah Muhammad bin Abdullah na juu ya watu wake na Masahaba wake na kila aliyemfuata.




[1]  Inavoonesha, mtungaji amechukua hadithi hii kutoka kitabu cha Imam Al-Ghazali kiitwacho (Ihyaau Uluumi 'Diin), nayo ni miongoni mwa hadithi za humo ambazo Maulama wa Hadithi wamesema hazikuthibiti kutoka kwa Mtume – rehma za Allah na amani zimshukie. Bali imesemwa kuwa ni maneno ya Abu Addardaa mwenyewe, kama alivoitoa Imam Ahmad katika kitabu chake (A'zuhd) na Alhaafidh Al-Iraaqiy katika (Takhriiju Ahaadithi Al-Ihya).

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.