Alitoka
-rehema za Allah na amani zimshukie- kwenda Shaam pamoja na ami yake Abu Talib
ambaye alisimama pamoja naye katika misukosuko iliyompata, alimnusuru na
kumgombea bila ya yeye mwenyewe kuingia katika Uislamu juu ya kuwa Mtume
-rehema za Allah na amani zimshukie- alimtaka afanye hivyo katika kauli yake:
قل كلمة أحاج بها لك
عند الله maana yake: “Sema neno nitakugombea kwalo
mbele ya Allah”. Badili yake wakati alipozidiwa na
uangamiaji wake alisema: “Siwezi kuacha dini ya mashekhe(wazee)”.
Lakini kwa sababu ya msimamo wake mzuri (wa kumhami
Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie-) amepunguziwa adhabu kama ilivyokuja kutokana na Mtume -rehema za Allah na
amani zimshukie- kuwa adhabu yake itakuwa katika kina cha chini cha moto wa
Jahannam(“Dhahdhah”). Laiti ningejua nini hii “Dhahdhah”.
Watu wa Oman
husema katika methali: “Hakuna katika moto jinga lililo baridi”.
Twajikinga kwa Allah na moto wa Jahannam, ufupi wake wa
kina au urefu wake.
Aloposafiri na ami yake umri wake ulikuwa
miaka tisa, na alimuowa Bibi Khadija bint Khuwailid wakati umri wake ulipokuwa
miaka ishirini na tano na umri wa Bibi Khadija miaka arubaini na watoto wake
Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- wote amezaa na Bi Khadija
isipokuwa Ibrahim amezaa na Maria Al-Qibtiya. Alipokufa Ibrahim alikuwa mwenye
umri wa miaka miwili na alilia Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- kwa
huzuni ya kufa kwake, alipoambiwa wewe walia na watukataza sisi kulia akasema:
إنما أبكي شفقة
ورحمة له ولا أقول ما يسخط الرب
“Hakika mimi nalia kwa
kumuonea huruma na sisemi lile linalomghadhibisha Mola wangu.
Alisafiri Mtume
-rehema za Allah na amani zimshukie-, kabla ya kumuowa Bibi Khadija, kwenda
kufanya biashara huko Shaam pamoja na mfanya kazi wa Bibi Khadija, Maysara,
basi aliporudi kutoka Shaam akamuelezea bibi yake juu ya Mtume -rehema za Allah
na amani zimshukie, tabia zake nzuri na ishara zioneshazo Utume wake (hapa
kabla ya kupewa Utume) baada ya kusikia
hayo Bibi Khadija alimtaka Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie-
amuoe na akampelekea posa yeye mwenyewe, akakubali -rehema za Allah na amani
zimshukie- kisha akamuoa. Basi akapata hadhi kubwa Duniani na akafuzu huko
Akhera kwa kuingizwa Janna kwani amembashiria Jibril A.S kuwa ana Nyumba ya
Jawhar huko Peponi yasiyokuwemo makelele humo(ugomvi) wala machofu. Alikufa
Bibi Khadija mwaka ule ule aliokufa ammi yake Mtume -rehema za Allah na amani
zimshukie, Abu Talib, kwa hivyo ukaitwa mwaka huo “mwaka wa huzuni” baada ya
Utume kwa miaka kumi na mbili.
Alipokuwa umri wake miaka
thelathini na sita Makureshi waligombana wakati wa kulijenga Al-Kaaba juu ya
nani aliweke “Al-Hajar Al-Aswadi”(Jiwe lijulikanalo katika pembe moja ya
Al-Kaaba) na kila kabila liliona lina haki ya kuliweka. Hapo wakamchagua Mtume
awe hakimu wao na kuwa watakuwa radhi na hukumu atakayoitoa kwani walikuwa
wakimwita Al-Amiin(mwaminifu). Basi alileta -rehema za Allah na amani
zimshukie- kitambaa na kuliweka hilo
jiwe juu yake kisha akaita kila kabila lilete mbele mtu mmoja akamate hicho
kitambaa kisha walinyanyue na kuliweka mahali pake maalumu kwenye pembe ya
Al-Kaaba.
Alipokuwa umri wake miaka arubaini na moja
aliletewa “Wahyi” alipokuwa katika pango lijulikanalo kwa “Ghaar Hiraa”.Wakati
huu alikuwa apenda kujitenga na kuwa pekee kwa ajili ya kuabudu katika pango hilo . Akaja Jibriil A.S
kumletea Wahyi kutoka kwa Mola wake akamuambia:
اقرأ yaani soma akajibu siwezi kusoma basi
akambana huku akimwambia soma akajibu siwezi kusoma akamfanyia hivyo mara tatu
kisha akamsomea:
اقرأ باسم ربك الذي خلق “Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba”, aya ya
kwanza ya sura Al-Alaq. Basi akahofu na akenda kwa Bibi Khadija akamwambia:دثريني دثريني yaani nifunike nifunike, alifahamu Bi Khadija
kuwa ana hofu akamuliza sababu yake akamwambia
aliyoyaona akamwambia: Tumaini Allah Subhanahu Wataala hawezi akakuwacha kwani wewe
unawasili Rahimu na unawasaidia wenye kupata misiba.Na ikamteremkia: يأيها المدثر “Ewe
uliyejifunika maguo”.
Walipojua tu
Maqureshi juu ya jambo hili, na baada ya Mtume -rehema za Allah na amani
zimshukie- kuwadhihirishia huu mwito wa kufuata Dini ya Allah Subhanahu Wataala wakamgeukia na kumfanyia maudhi mbali mbali
tokea kumtukana mpaka kumpiga na kumkadhibisha na mengineyo yaliotajwa katika
vitabu vya sira. Na mwishowe wakamfunga pamoja na ahli ya nyumba yake na kabila
lake, Waumini na makafiri wao miongoni mwa kabila la Abdil Muttalib.
Wakawafunga katika bonde, baina ya milima miwili, lisilokuwa na uwazi wa
kutokeya upande wa pili. Wakawazuilia kupewa chakula, maji, kufanya biashara na
hata kutembeleana, msuso haujatokea bado
kama huo na wakaunganika makabila yote ya Qureshi juu ya msuso huo,
wakaandikiana mkataba kuwa asitoke Muhammad na watu wa nyumba yake katika bonde
hilo mpaka wafe
humo. Wakabakia humo miaka mitatu kama
ingekuwa si kwa maangalizi ya Allah Subhanahu Wataala na hifadhi yake kwao hakika wangekufa.
Kinatosha kisa
kilichowatokea kuwa zingatio la kuonesha
hali gani ngumu na mashaka iliyowapata. Alisimulia mmoja wao: Niliamka usiku
kwenda haja ndogo basi nikakojolea kitu kitoacho sauti chini yangu nikakichukua
kumbe ngozi ya ngamia,nikaiosha na kuichoma kisha nikaila. Jee kuna kitu tena
zaidi ya hicho?.
Baada ya kupita miaka
mitatu Allah Subhanahu Wataala akajaalia watu
fulani kwenda kuuharibu huo mkataba wakaukuta wote umeliwa na mchwa
isipokuwa اللهم باسمك
na hiyo ilikuwa ndiyo sababu ya kutolewa kifungoni. Akaelekea Mtume
-rehema za Allah na amani zimshukie- kwenda Taaif kwa kudhania labda huko
atawapata watakaosikiliza mwito wake lakini ukweli ulikuwa kinyume cha hayo,
kwani alipata maudhi makubwa hayana mfano kutoka Thaqiif kama ilivyozungumziwa
katika vitabu vya Sira (hakika mukhtasari huu ni kwa ajili ya kuhimiza
kutafuta-elimu).
Basi akarejea kutoka
Taaif hali ana uzito katika moyo wake kwa mambo yaliyompata huko na hali
ikazidi kuwa mbaya kwa kufiwa na mkewe
mtiifu na ammi yake mwenye huruma naye. Akataka Mola wake kumuondolea uzito huo
na kumliwaza kwa kumchukua katika mwendo wa usiku wa Israa kutoka Masjid
A-Haraam kwenda Masjid Al-Aqsa kisha kumpaza Mbinguni kwenda “Sidrat
Al-Muntahaa”. Allah Aliye Karimu
Amempa
heshima -rehema za Allah na amani zimshukie- kwa muujiza huu mtukufu hata
asifikirie kuwa amemwakilishia mambo yake juu ya mmoja katika viumbe vyake.
Akamuamini mwenye kuamini (baada ya kuelezea watu kisa chake hicho) na
akamkadhibisha mwenye kukadhibisha na hakuna
aliyetokea katika sura nzuri zaidi kwenye jambo hili kama Abu Bakar
Assiddiq,hakuna mwingine aliyewafikiwa kama
yeye. Wakati alipoambiwa juu ya madai ya sahibu yake (Mtume -rehema za Allah na
amani zimshukie- kuwa amefika Masjid Al-Aqsa kisha akapazwa kwenda Mbinguni
katika sehemu ndogo ya usiku huo) alisemaكان قال فقد
صدق: إن
maana yake “Ikiwa amesema hivyo basi
usemi huo ni kweli”. Kwa hiyo
Allah Subhanahu Wataala akamwita Siddiiq na
akapata heshima kubwa kwa sifa hiyo.
Akaendelea Mtume
-rehema za Allah na amani zimshukie- pamoja na Waumini wenye kudhalilishwa waliyonae
kupata kila maudhi kwa washirikina. Mpaka alipotoa idhini Allah Subhanahu Wataala kwa kila anayetaka katika hao
waumini kuhajiri kwenda Uhabeshi ili kuwapunguzia mateso wanayoyapata. Allah Subhanahu Wataala akawatiishia mfalme wa Uhabeshi aitwaye Annajaashiy, akawaangalia
vizuri na kuwaonea huruma. Aliingia Uislamu kisirisiri na alipokufa, alisaliwa
na Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- huko madina sala ya maiti
“ghaiib”(maiti asiyekuwepo). Kisha yakawa matayarisho yanafanywa kwa Hijra
kubwa ya kwenda Madina. Ukafanyika muahada wa mwanzo wa kujitolea na Maansari
“Beiy’at Al-Aqaba” katika musimu wa Hija.
Muahada wa pili ukafanyika katika mwaka
uliofatia na ambao ulifatiwa na hijra ya Mtume -rehema za Allah na amani
zimshukie- baada ya kuhajiri wengi katika Masahaba kwenda Madina, pahala penye
amani ambapo imepelekwa Da’awa iliyotahirika.
Visa vingi vilitokea vinavyoambatana na tukio
hili la Hijra ,
ama Abubakar Siddiq alifuzu kuupata
Usuhuba wa Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- ambaye ndiye pekee
aliyehajiri nae kutoka Makka kwenda Madina. Waislamu wote walihajiri kisirisiri
isipokuwa Omar bin Khattab Al-Faaruuq alihajiri wazi wazi bila ya kificho,
aliwaita Maqureshi baada ya kuiaga Al-Kaaba akasema: Mimi nahajiri basi
anaetaka mama yake amkose anifuate na
hakuna aliyejasiri kumfuata. Nguvu ni kitu kisifiwacho kwani kinaweza kufanya
mengi.
Alipofika Mtume -rehema za Allah na amani
zimshukie- Madina kitu cha kwanza alichokifanya ni kujenga Msikiti wake -rehema
za Allah na amani zimshukie. Ikawa ni Sunna kwa kila anaehamia mahala,kitu cha
kwanza ajue sehemu atakaposalia, na hata nyumbani kwake Muislamu inapendelewa aweke mahala maalumu pa kusalia. Kadhalika ukijengwa mji mpya kitu cha kwanza kinachowekwa katika plani na kujengwa ni
Msikiti. Waliafikiana Waislamu waifanye Tarehe yao kutokana na tukio la Hijra na wakaufuta ule
mvunjiko ulioko baina ya Muharram na Rabiil-Awal (Mtume -rehema za Allah na
amani zimshukie- alihajiri katika Rabiil-Awal lakini Muharram ndio uliojaaliwa
mwanzo wa mwaka). Hapo mwanzo tarehe ilikuwa juu ya msingi wa matukio yaliokuwa
yakipita. Kama kusema miaka fulani imepita
baada ya tukio fulani. Kwa mfano wamesema Mtume -rehema za Allah na amani
zimshukie- amezaliwa katika mwaka wa Al-Fiil na kadhalika.
Yasikitisha leo kuwa Waislamu
wamejisahaulisha tarehe yao
ya Hijra baada ya kuijua na kuifuata wakaiwacha na kukamata tarehe ya Miladi
(A.D). Nadhani kwa sababu mishahara yao
inaambatana nayo. Kuna mithali ya Ki-Omani inayosema ‘Mwezi ambao huna matumizi
ndani yake huhisabu siku zake’. Imebakia Serikali ya Suudiya imehifadhi Tarehe
ya Hijra, Allah aijazi kheri.
Katika mwaka wa pili wa Hijra imefaridhiwa
funga ya mwezi wa Ramadhani na katika mwaka huo huo vilikuwa vita vya Badri
vilivyotenganisha baina ya Haki na batili kwa hivyo ikanyanyuka shani ya
Uislamu na wakauliwa humo waliouliwa miongoni mwa majabbari wakubwa wa
Kiqureshi. Na katika mwaka wa tatu wa Hijra vilikuwa vita vya Uhud ambavyo waliuliwa
humo Waislamu wengi kwa sababu ya
kuihalifu amri ya Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- na dhana
nzuri waliokuwa nayo Masahaba (ya
matumaini ya kushinda vita) kisha wakashindwa washirikina. Mtume -rehema za
Allah na amani zimshukie- aliwaamrisha watupa mishare na upinde wakamate sehemu
zao bila ya kuziacha hata wakiona washirikina washindwa, wao wakenda kinyume ya
amri yake -rehema za Allah na amani zimshukie- wakaziwacha hizo sehemu
kukimbilia ngawira. Hapo ndipo wapiganaji wakishirikina wakazikimbilia hizo
sehemu na kusababisha kushindwa kwa Waislamu mara ya pili. Wakauliwa wengi
katika Waislamu kisha Allah Subhanahu Wataala akawapa nguvu na kurejea katika
mpambano ndipo waliposhindwa washirikina kama
alivyosimulia Allah Subhanahu Wataala katika Kitabu chake kitukufu.
Kutokana na vita hivi kuna zingatio muhimu la
kuchukuliwa nalo kwa ajili ya kupinga amri moja tu katika amri zake Mtume
-rehema za Allah na amani zimshukie- kumesababisha kushindwa Waislamu vipi leo
itakuwa hali yao
Waislamu na wamekwenda kinyume cha amri
zake zote Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie? Lini kushindwa na maadui
zao kutawabanduka? Leo umebainika ukweli wa hadithi ya Mtume -rehema za Allah
na amani zimshukie- juu ya hali Waislamu-:
يوشك أن تتداعى
عليكم الأمم كما تتداعى الأكلة على قصعتها قالوا : أومن قلة يومئذ نحن يا رسول الله؟ قال : بل أنتم كثير
ولكنكم غثاء كغثاء السيل ولينزعن الله الهيبة من قلوب أعدائكم وليقذفن الوهن في
قلوبكم قالوا : وما الوهن يارسول الله ؟ قال : حب الدنيا وكراهية الموت
“Uko karibu wakati ambao umma zote zitaitana
kuwakusanyikia (Waislamu) kama wanavyoitana walaji kukikusanyikia chakula chao.
Wakasema: Je ni kutokana na uchache wetu
siku hiyo ewe Mtume wa Allah? Akasema: Bali nyie wengi lakini nyie ni takataka kama takataka za (maji ya)
mvua, kwa hakika Allah ataondoa katika nyoyo za maadui zenu kuwaogopeni na
hakika atawatia katika nyoyo zenu udhaifu wakamuuliza na ni udhaifu gani ewe
Mtume wa Allah, akajibu kupenda Dunia na kuchukia mauti.”
Amesema shekhe Abu
Muslim Allah Amrehemu katika shairi: “Mtengano katika Uislamu haukusababishwa
na upanga wa adui yake zaidi ya ulivyo baina ya watu wake(Waislamu wenyewe kwa
wenyewe).”
Katika mwaka wa sita
wa Hijra alielekea Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- kwenda kufanya
Umra kwa mara ya kwanza tokea kuihajiri Makka lakini washirikina walimzuia
kuingia kwa hivyo alirejea kutoka Hudeibiya. Na humo ukafanyika muahada wa 'Arridhwaan'
na ikashuka sura ya Al-Fat-h. Ikawa ndio mara ya kwanza Maqureshi kumtambua
Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- na Dola yake, kwa hivyo ukawa ndio
Ushindi wa mwanzo wa Waislamu na utangulizi wa kuifungua kwao Makka (kuichukua
kutoka kwa washirikina) na kudhihirika kwao. Na katika mwaka wa nane
ilifunguliwa Makka ihishimiwayo na ndio ikawa mwisho wa nguvu ya washirikina
wakadhihirika katika hali ya udhalilifu na utiifu kwa Waislamu wakasema
(kumwambia Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie : “Ndugu mheshimiwa na
mtoto wa ndugu mheshimiwa umemiliki basi samehe,” akasema Mtume -rehema za
Allah na amani zimshukie:اذهبوا فأنتم الطلقاء “Nendeni kwani mko huru”. Basi akawaachia na
kuwakomboa baada kuwa umewamiliki mkono wake wa kuume na hii ndio shaani ya
watu wakarimu.
Katika mwaka wa tisa
Abu Bakar - Allah amridhie- alikwenda kuwapeleka watu kuhiji na ikateremka sura
ya Bara’ah (Tawba). Basi Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- alimtuma
Ali bin Abi Talib kwenda kuwasomea watu (hiyo sura) na awafukuze washirikina
wasiingie Al-Haram kwa hiyo ikawa mwisho wao kuitufu Kaaba. Walikuwa
wanawalazimisha watu kutufu uchi isipokuwa akikodi nguo kwao ili atufu eti
wadai haifai mtu kutufu Kaaba na nguo aliyomuasi nayo Allah Subhanahu Wataala wakijisahau nafsi zao kuwa wametopea katika
najasa na maasi, methali inasema: “Unaliona vumbi katika jicho la ndugu yako
lakini hulioni gogo katika jicho lako”.
Katika mwaka wa kumi alihiji Mtume -rehema za
Allah na amani zimshukie- hija ya “Al-Wida’a (Muagano)na akawafundisha watu
namna ya kuhiji na akasema:خذوا عني مناسككم “Chukueni kutoka kwangu Ibada zenu”. Kila
alichofanya Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- katika Hija hiyo
wanawajibika Waislamu wakifanye na kinyume chake ni kuhalifu Sunna yake. Na
katika mwaka wa kumi na moja ilikamatwa roho yake Mtume -rehema za Allah na
amani zimshukie- na akajiunga na Rafiki zake waliyotukuka(Watu wa Peponi).
ﭽ ﰁ
ﰂ ﰃ ﰄ ﭼ الزمر: ٣٠
“Kwa yakini wewe utakufa na
wao pia watakufa”
Akasimamia
jambo hili (la Uislamu )
Abu Bakar Siddiq baada ya kufa Mtume -rehema za Allah na amani
zimshukie- usimamizi ulio barabara kwa muda wa miaka miwili na miezi
kadha. Kisha akasimamia Omar bin Khattab -Al-Farooq- kwa muda wa miaka
kumi kisha baada yake Othman bin Affan kwa muda wa miaka kumi na mbili,
walimsifu watu mwanzo wa Khilafa yake kisha baada ya hapo wakachukizwa na mambo
yake mwishowe akafa kwa kuuliwa. Akasimamia baada yake Ali bin Abi Talib kwa
muda wa miaka mitano na miezi kadha akafa hali ya kuwa ameuliwa. Kisha Khilafa
(utawala wa Kiislamu) ukabadilika kuwa ufalme wakawa Maumawiy wanapasiana baina
yao ufalme kisha baada yao
Maabasiy kisha waliokuja baada yao .
Na mwenye kutaka kujua zaidi basi arejee kwenye vitabu vya sira na tarehe.
Baada
ya mwaka arubaini wa Hijri haukubakiya
tena mwendo (sira)wa kweli wa Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- na wa
Makhalifa wake wenye kufuata muongozo wa sawasawa (Arraashidiin) isipokuwa
baada ya kuuhuisha mwendo huu Waislamu waitwao kwa jina la Maibadhi (Al-Ibaadhiya)
katika mwaka wa mia na ishirini na nane Hijri. Katika Oman walimsimamisha Al-Julanda bin Masood
ahukumu kwa sheria ya Allah na katika nchi za Magharibi ya Arabuni
walimsimamisha Abu Al-Khattab Al-Maafriy na ama katika Hadhramaut na Yemen
walimweka Taalib Al-haq Abdallah bin Yahya Al-kindiy. Na hii ni neema kutoka
kwa Allah Subhanahu Wataala juu ya Maibadhi kwani Sunna hii haikupatikana
isipokuwa kwao tu, hakika hakuna wengine waliyosimamisha Maimamu wakahukumu
katika msingi wa Makhalifa waliongoka tokea wakati ule mpaka wakati wa mwisho
tuliokuwa nao sasa hivi isipokuwa wao. Tutaelezea akitaka Allah Subhanahu
Wataala kisa cha kufa kwake Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- kwa
kirefu.
Na kaapa juu ya Ujumbe wake:-
يس: ١ - ٣
“Yaa
Siyn(1) Naapa kwa (hii) Qur’ani yenye kutengenezwa vizuri(2) Kuwa hakika wewe
ni miongoni mwa Mitume (wa Allah)(3)”
Na kaapa juu ya mapenzi yake:-
الضحى: ١ - ٣
“Naapa
kwa mchana(1) Na
kwa usiku unapotanda(2) Hakukuacha Mola wako wala hakukasirika (nawe Ewe Nabii
Muhammad)”
Na kaapa juu ya utukufu wa tabia yake:-
القلم: ١ - ٤
“Nuun(Naapa kwa) Kalamu na yale wayaandikayo
(kwa kalamu hizo)(1) Kwa neema ya Mola wako wewe si mwendawazimu. (Makafiri
wakimwambia Mtume-kwa ajili ya kumtukana tu-kuwa yeye ni mwendawazimu)(2) Na
kwa hakika una malipo yasiyokatika (yataendelea maisha)(3) Na bila shaka una
tabia njema kabisa(4)”
Na kaapa juu ya kusalimika kwake na upungufu:-
الحاقة: ٣٨ - ٤٣
“Basi naapa kwa mnavyoviona(38) Na
msivyoviona(39) Kwa hakika ni kauli iliyoletwa na Mjumbe(wa Allah ) mwenye heshima
(kubwa)(40) Wala si kauli ya mtunga mashairi (kama mnavyosema). Ni machache sana mnayoyaamini(41) Wala si kauli ya mchawi (kama mnavyodai). Ni kidogo kuwaidhika kwenu(42) Ni
uteremsho utokao kwa Mola wa viumbe vyote(43)”
Na kaapa kuwa Allah amlipiza kisasi anayemuudhi
Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie:-
ﭼ العلق: ١٥ - ١٦
“Sivyo hivyo (anavyofanya!). Kama
haachi, Tutamkokota kwa nywele za utosi (wake tumtie motoni)(15) Utosi muongo,
wenye madhambi(16)”
Na kaapa kwa Uhai wake -rehema za Allah na
amani zimshukie:-
الحجر: ٧٢
“Naapa kwa umri wako! Hakika wao walikuwa katika ulevi wao (wa maovu) wanahangaika ovyo.”
Na kaapa juu ya umbali wa maadui zake kutokana
naye:-
المطففين: ١٥
“Sivyo hivyo! Hakika
watazuiliwa, siku hiyo na (neema za) Mola wao.”
Na kamhusisha kuwa tofauti na watu wengine:-
النور: ٦٣
“Msifanye
wito wa Mtume baina yenu kama wito wa nyinyi
kwa nyinyi”
Na kamhusisha kupunguzwa sauti mbele yake na
kuwa kunyanyanyua sauti kwabomoa vitendo (thawabu):-
الحجرات: ٢
“Enyi mlioamini! Msipaze sauti zenu kuliko sauti ya
Mtume wala msiseme naye kwa sauti ya
nguvu kama mnavyosemezana nyinyi kwa nyinyi,
visije vitendo vyenu vikakosa thawabu, na hali hamtambui”
Na kamhusisha kwa kutajwa jina lake pamoja
na jina la Allah
kwani kila zinapotolewa shahada mbili ikiwa katika Adhana, Ikama, hotuba au
kushahadia hatajwi Allah isipokuwa hutajwa naye Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie.
Kamhusisha kwa kuwaamrisha Malaika wake na waja
wake Waumini wamsalie:-
الأحزاب: ٥٦
“Hakika Allah anamteremshia rehema Mtume;
na Malaika wake (wanamuombea dua kwa
vile vitendo vizuri alivyovifanya). Basi enyi Waislamu (mliopata neema hii ya
kufindishwa haya na Mtume) msalieni (Mtume, muombeeni rehema) na muombeeni
amani.”
Na Allah Subhanahu
Wataala amemtaja Mtume
-rehema za Allah na amani zimshukie- pamoja naye mara nyingi katika Qurani:-
التوبة: ٧٤
“Na hawakuona baya (kwa kuja
Uislamu) ila ya kuwa Allah na Mtume wake amewatajirisha kwa fadhila zake”
Na katika kauli yake :-
النساء: ٨٠
“Mwenye kumtii Mtume amemtii Allah
(kwani anayoyaamrisha Mtume yametoka kwa Allah”
Na wakati alipomlaumu alimtangulizia msamaha
kabla ya lawama :-
التوبة: ٤٣
“Allah
amekuwia radhi (amekusamehe). Kwa nini umewapa ruhusa? (Ungengoja) mpaka wanaosema
kweli wakupambanukie, na uwajue waongo.”
Na kamhusisha kwa kumghufiria madhambi yake
yaliyopita na yajayo:-
الفتح: ٢
“Ili Allah akusamehe makosa yako yaliyotangulia
na yanayokuja, na kukutimizia neema zake na kukuongoa katika njia iliyonyooka”
Na amemhusisha kuwa hakumwita kwa jina lake kama
Manabii wengine bali alimwita kwa kauli yake:-
( يأيها النبي ، يأيها الرسول ، يأيها المزمل ، يأيها
المدثر )
Ewe Nabii, ewe Mtume, ewe Uliyejifunika maguo, ewe Uliyejifunika maguo.
Na pia amemhusisha
kwa kuwajibishia Waislamu wamsalie na kuifanya
Ibada juu yao .
Ziko hadithi nyingi zithibitishazo hayo kama kauli yake Mtume -rehema za Allah
na amani zimshukie:-
( من ذكرت عنده فليصل علي وإن صلاتكم علي إجابة لدعائكم
وزكاة لأعمالكم ومرضاة لربكم )
“Ninaetajwa mbele yake basi na
anisalie kwani kunisalia kwenu ndio kukubaliwa dua zenu na ndio kuvitakasa
vitendo vyenu na ndio kumridhisha Mola
wenu”.
Na hii ni amri ambayo
tunawajibika kuitekeleza.
حين دخلنا على رسول الله في بيت أمنا عائشة رضي الله
عنها حين دنا الفراق فنظر إلينا فدمعت عيناه صلى الله عليه وسلم ثم قال :(مرحبا
بكم حياكم الله آواكم الله نصركم الله وأوصيكم بتقوى الله وأوصي بكم الله إني لكم
منه نذير مبين ألا تعلوا على الله في عباده وبلاده وقد دنا الأجل والمنقلب إلى
الله وإلى سدرة المنتهى وإلى جنة المأوى وإلى الكأس الأوفى فاقرؤا على أنفسكم وعلى
من دخل في دينكم بعدي مني السلام ورحمة الله )
“Wakati tulipoingia kwa Mtume wa Allah -rehema za
Allah na amani zimshukie- katika nyumba ya mama yetu Aisha R.A wakati wa
kufariki kwake dunia kumekaribia, basi akatutizama kisha yakamtoka machozi
-rehema za Allah na amani zimshukie- akasema: Karibuni Allah awape uhai, Allah
awape pa kufikilia (pa kukimbilia) Allah awape ushindi, nawausia mumche Allah na namuomba Allah awahifadhi na
kuwa kanileta mimi kwenu muonyaji wa uwazi kabisa kwa adhabu yake. Basi
msifanye dhuluma na ufisadi kwa waja wake na ardhi yake Subhanahu Wataala na kuwa ajali yangu imekurubia na kurudi kwangu ni kwa Allah kwenye
Sidratul Muntaha na Jannat Al Maawa. Na kwenye nasibu yangu (malipo) kubwa
kabisa, basi jitoleeni juu ya nafsi zenu na wale watakaoingia katika dini yenu baada yangu, jitoleeni kutoka kwangu
salamu na rehema ya Allah Subhanahu Wataala”
Inasemekana
kuwa Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- amemwambia Jibril A.S kwenye
mauti yake:
( من لأمتي
بعدي )
“Nani atakaowatizama Umma wangu kwa kuwaongoza
baada yangu”, basi Allah akamteremshia
wahyi Jibril kuwa:
( أن بشر حبيبي أني لا أخذله في أمته وبشره بأنه أسرع الناس خروجا
من الأرض إذا بعثوا وسيدهم إذا جمعوا وأن الجنة محرمة على الأمم حتى تدخلها أمته )
فقال( الآن قرت عيني )
“Mbashirie
Mpenzi wangu kuwa mimi sitamuacha (kumkatisha tamaa) kwa kuwa Umma wake wako
chini ya hifadhi yangu na mbashirie kuwa yeye ni wa kwanza kutoka ardhini siku
watakaofufuliwa watu na bwana wao siku watapokusanywa watu na kuwa pepo
imeharimishwa kwa umma nyingine mpaka uingie umma wake”. Basi hapo akasema
Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie:
“Sasa limeburudika jicho langu”.
Amesema Bibi Aisha R.A ametuamrisha Mtume wa Allah
-rehema za Allah na amani zimshukie- tumuoshe kwa makanda ya ngozi saba(ya
maji) kutoka visima saba, tukafanya hivyo akahisi raha basi akatoka na
akasalisha watu na kuwaombea maghufira watu wa Uhud na kuwaombea dua kisha
akawausia Muhaajiriin juu ya Maansaar akawaambia:
(أما بعد يا معشر
المهاجرين فإنكم تزيدون وأصبحت الأنصار لا تزيد على التي هي عليها اليوم وأن
الأنصار عيبتني التي آويت عليها فأكرموا كريمهم – يعني محسنهم – وتجاوزوا عن
مسيئهم ) ثم قال إن عبدا خير بين الدنيا وبين ما عند الله فاختار ما عند الله )
فبكى أبو بكر رضي الله عنه وظن أنه يريد نفسه فقال النبي صلى الله عليه وسلم : على
رسلك يا أبا بكر ( سدوا هذه الأبواب الشوارع في المسجد إلا باب أبي بكر فإني لا
أعلم امرءا أفضل عندي في الصحبة من أبي بكر )
“Amma
baad, enyi wana wa Muhaajiriin hakika nyie mwaongezeka (yaani yazidi idadi yao
kwani wanahajiri kutoka Makka) na Maansaar wao hawaongezeki zaidi ya vile
walivyokuwa na hakika Maansaar ni wahifadhi wangu niliofikilia kwao basi
mkirimuni aliokuwa mwema wao na msameheni aliokuwa mbaya wao, kisha akasema:
Hakika kuna mja aliekhiarishwa baina ya Dunia na baina ya kile kilichokuwa kwa
Allah Subhanahu Wataala basi akachagua kilichokuwa kwa Allah. Hapo akalia Abu Bakr R.A. kwani alitambua kuwa huyo mja
aliekhiyarishwa ni yeye Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie. Basi akasema
Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie: Pole pole ewe Abu-Bakr! Fungeni hii
milango ya njiani ilioko katika msikiti
isipokuwa mlango wa Abu Bakr kwani sijui mtu aliyekuwa bora kwangu katika
usuhuba kuliko Abu Bakr.
Kasema Bibi
Aisha R.A. akachukuliwa (akafa) Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie-
katika nyumba yangu na katika siku yangu na baina ya kifua changu na shingo
yangu (yaani katika mikono yangu) na akakutanisha Allah baina ya mate yangu na
mate yake katika mauti yake. Kaingia
kwangu ndugu yangu Abdur-Rahman na amekamata katika mkono wake mswaki basi
ikawa Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- autizama ule mswaki nikajua
kuwa autaka nikambwambia jee nikuletee? Akanifanyia ishara kwa kichwa chake
kuwa naam basi nikampa akauchukua kisha akautia katika mdomo wake ukawa ule
mswaki mgumu kwake nikamwuuliza je nikulainishie? Akanifanyia ishara kwa kichwa
chake kuwa naam. Basi nikaulainisha na kulikuwa mbele yake chombo kina maji
akawa aingiza mkono wake ndani ya hicho chombo na huku akisema laa ilaaha illa Allah hakika
mauti yana maumivu makubwa. Kisha akausimamisha mkono wake akisema “Ar-Rafiq Al
Aalaa” yaani kuwa wakati ule akihiarishwa na yeye anachagua usuhuba wa walioko
Peponi basi hapo nikasema Wallahi
hakutuchagua sisi.
Walipoona
Maansar kuwa Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- azidi kuwa mzito
wakauzunguka Msikiti na alipoambiwa hayo Mtume -rehema za Allah na amani
zimshukie, akatoka na huku amewaegemea Al Fadhl na Aliy na mbele yake yuko Al
Abbas na kichwa chake Mtume -rehema za
Allah na amani zimshukie- kimefungwa na miguu yake aiburuza mpaka akakaa katika
kidato cha chini cha minbari, wakamsimamia watu akamshukuru Allah Subhanahu Wataala na kumsifu akasema:-
( أيها الناس إنه بلغني
أنكم تخافون عليَ الموت كأنه استنكار منكم للموت وما تنكرون من موت نبيكم ألم أنع
إليكم وتنعى إليكم أنفسكم هل خلد نبي قبلي فيمن بعث فأخلد فيكم ألا إني لاحق بربي
وإنكم لاحقون به وإني أوصيكم بالمهاجرين الأولين خيرا وأوصي المهاجرين فيما بينهم
فإن الله عزَ وجل قال :
وإن الأمور تجري بإذن الله فلا يحملنكم استبطاء أمر على
استعجاله فإن الله عزَ وجل لا يعجل بعجلة أحد ومن غالب الله غلبه ومن خادع الله
خدعه – فهل عسيتم إن توليتم أن تفسدوا في الأرض وتقطعوا أرحامكم – وأوصيكم
بالأنصار خيرا فإنهم الذين تبوءوا الدار والإيمان من قبلكم – أن تحسنوا إليهم ألم
يشاطروكم الثمار ، ألم يوسعوا عليكم في الديار ، ألم يؤثروكم على أنفسهم وبهم
الخصاصة ألا فمن ولي أن يحكم بين رجلين فليقبل من محسنهم وليتجاوز عن مسيئهم ألا
ولا تستأثروا عليهم ألا وأني فرط لكم وأنتم لاحقون بي ألا وأن موعدكم الحوض ألا
ومن أحب أن يرد علي الحوض غدا فليكفف لسانه ويده إلا مما ينبغي ) فقال العباس يا
نبي الله أوص بقريش فقال ( إنما أوصي بهذا قريشا والناس تبع لقريش برهم لبرهم
وفاجرهم لفاجرهم فاستوصوا آل قريش بالناس خيرا يا أيها الناس إن الذنوب تغير النعم
وتبدل القسم فإذا بر الناس تبرهم أئمتهم وإذا فجر الناس عقوهم –
“Enyi watu imenifikia habari kuwa mwaniogopea kufa kama kwamba kwa hayo mnapinga mauti na ni kitu gani
kinachowafanya mpinge mauti ya Mtume
wenu. Jee hamkuarifiwa kifo changu na mkaarifiwa vifo vyenu wenyenu? Je
alipata kuisha milele Nabii kabla yangu katika manabii waliotumwa hata mkataka
mimi niishi kwenu milele? Basi nawahakikishia kuwa mimi napelekwa kwa Mola
wangu nanyi vile vile mwapelekwa kwake na kuwa mimi nawausia juu ya Muhaajiriin
wa kwanza kheri (mkae nao vizuri) na
wausia Muhaajirin baina yao
wenyewe kwa wenyewe kwani Allah Subhanahu Wataala amesema
“Naapa kwa zama (zako ewe
Nabii Muhammad)(1) Kuwa Binadamu yuko katika hasara (2) Isipokuwa wale
walioamini na wakafanya vitendo vizuri, na wakausiana (kufuata) haki na
wakausiana (kushikamana) na subira (kustahamiliana)”.
“Na
hakika kuwa mambo yanakwenda kwa idhni yake Allah basi isiwapelekee kuharakisha
kitu mnachokiona kinakwenda pole pole kwani Allah Subhanahu
Wataala
haharakishi kitu kwa ajili ya haraka ya mtu fulani na atakaye kushindana na
Allah humshinda na anaemkhadaa Allah naye vile vile humkhadaa (hampi hidaya
kwenye njia ilionyooka). Pengine huenda mkapotea na mkafisidi katika ardhi na
kuwakata jamaa zenu, na nawausieni juu ya Maansaar Kheri kwani wao ndio
waliofanya maskani yao hapo Madina kabla yenu na
ndio walioutakasa Uislamu wao barabara kabla yenu nawausia muwafanyie wema.Jee,
hawakuwagawia nusu ya mazao yao ? Jee, hawakuwafanyieni nafasi katika nyumba zao?
Jee, hawakuwapendeleeni nyie juu ya nafsi zao japokuwa wao wenyewe wahitaji
sana? Basi mjue kwa hakika aliyepewa wilaya ya kuhukumu baina ya watu wawili
(katika wao Maansari) amkubalie mwema wao na amsemehe mbaya wao, basi msije
mkapendelea (nafsi zenu) juu yao ,
hakika mie ndie nitakaowatangulia na nyie mtanifuatilia, hakika miadi yenu ni
Hodhi. Hakika anayetaka kungia kwangu katika hodhi langu kesho (siku ya kiyama)
basi azuiye ulimi wake na mkono wake isipokuwa kwa kilicho lazima. Akasema Al
Abbas ewe Mtume wa Allah toa usia kwa Maqureish. Akasema Mtume -rehema za Allah
na amani zimshukie: Hakika mimi huu usia
(wa kuwafanyia mema Maansaar na Muhajiriin)
nawausia Maqureish wao ndio wanaofuatwa na watu, mwema (wa watu)
anafuata mwema wao (Maqureish) na mbaya (wa watu) anafuata mbaya wao
(Maqureish) (wao ndio viongozi wa kiwa wazuri na raia zao watakuwa wazuri na wakiwa wabaya raia watakuwa hivyo
hivyo). Basi nawausieni enyi Maqureish
kuwafanyia watu kheri. Enyi watu hakika
madhambi yabadilisha mema na mgawanyo wa riziki, wakifanya mazuri watu (kumtii
Mola) na viongozi wao watawafanyia mazuri na wakifanya watu maasi basi nao
watataabishwa na viongozi wao na kutofanyiwa uadilifu.”
وروى ابن مسعود رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه
وسلم قال لأبي بكر رضي الله عنه سل يا أبا بكر فقال يا رسول الله دنا الأجل فقال
دنا الأجل وتدلى فقال : ليهنئك يا نبي الله ما عند الله فليت شعري عن منقلبنا فقال
" إلى الله وإلى سدرة المنتهى ثم إلى جنة المأوى والفردوس الأعلى والكأس
الأوفى والرفيق الأعلى والحظ والعيش المهنا فقال يا نبي الله من يغسلك قال رجل من
أهل بيتي الأدنى فالأدنى قال ففيم نكفنك قال في ثيابي هذه وفي حلة يمانية وفي بياض
مصر" فقال كيف الصلاة عليك منا وبكينا وبكى ثم قال " مهلا غفر الله لكم
وجزاكم عن نبيكم خيرا إذا غسلتموني وكفنتموني فضعوني على سريري وفي بيتي هذا على شفيري
قبري ثم اخرجوا عني ساعة فإن أول من يصلي علي الله عزَ وجل ثم يأذن للملائكة في
الصلاة علي فأول من يدخل علي من خلق الله ويصلي عليَ جبريل ثم ميكائيل ثم إسرافيل
ثم ملك الموت مع جنود كثيرة ثم الملائكة بأجمعها عليهم السلام ثم أنتم فادخلوا علي
أفواجا فصلوا علي أفواجا زمرة زمرة وسلموا تسليما ولا تؤذوني بتزكية ولا صيحة ولا
رنة وليبدأ منكم الإمام وأهل بيتي الأدنى فالأدنى ثم زمر النساء ثم زمر الصبيان
قال فمن يدخلك في قبرك قال " زمر من أهل بيتي الأدنى فالأدنى مع ملائكة كثيرة
لا ترونهم وهم يرونكم قوموا فأدوا عني إلى من بعدي ")
Imetolewa
na Ibn Masood zimshukie Radhi za
Allah kuwa Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie-
amesema kumwambia Abu Bakr R.A.: Uliza ewe Abu Bakr. Akasema Ewe Mjumbe wa Allah
imekaribia ajali yako? Akasema imekaribia ajali na kuteremka. Akasema (Abu Bakr
R.A.) hakika nakupongeza na utafurahishwa kwa kile utakachokipata kwa Allah
na laiti ningejua nini utakuwa mwisho
wetu. Akasema Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie: Ni kwenda kwa Allah na Sidratu Al Muntahaa
kisha kwenye Pepo ya Maawaa na Firdaws ya Juu kabisa na malipo makubwa sana na
rafiki wa Juu kabisa na hadhi na maisha ya raha. Akasema Jee Mjumbe wa Allah
nani atakaekuosha akasema mwanamme
katika Ahli Al-Beit (katika familia yangu au jamaa yangu) aliyenikaribia zaidi
kisha aliyenikaribia zaidi. Akamuuliza Jee tukuvike sanda (tukufunge sanda)
kwa kitu gani? Akasema katika nguo zangu hizi na katika shuka za Kiyamani na
weupe wa Masri. Akamuuliza jee vipi tukusalie ? Hapo tukalia naye akalia
kisha akasema : Polepoleni Allah Subhanahu Wataala awaghufiriye na awajazi kheri kutokana na Mtume
wenu. Mkisha niosha na kunifunga sanda
niekeni juu ya kitanda changu katika nyumba yangu hii katika ukingo wa kaburi
langu kisha tokeni nje muda mdogo kwani wa kwanza atakaye nisalia ni Allah Subhanahu Wataala kisha atawapa idhini
Malaika kunisalia basi wa kwanza katika viumbe vya Allah Subhanahu Wataala atakayeingia kunisalia
ni Jibriil A.S kisha Mikaaiil kisha Israafiil kisha Malaika wa Mauti pamoja na askari wake wengi halafu Malaika
wote wengine A.S. kisha nyie ingieni vikundi na munisalie vikundi mkusanyiko
mkusanyiko na nisalimieni (niamkieni) mwamkio wala msiniudhi kwa kunisifu au
kulia kwa makelele au kuomboleza. Na aanze miongoni wenu Imamu na watu wa
nyumba yangu aliekaribu zaidi kisha anaefuatia kisha vikundi vya wanawake kisha
vikundi vya watoto. Akauliza nani atakaekuingiza kaburini mwako ?
Akajibu mikusanyiko katika watu wa
nyumba yangu aliye karibu zaidi kisha anaefuatia pamoja na malaika wengi
hamuwaoni na wao wanawaona fikisheni ujumbe kwa niaba yangu kwa wale watakao
kuwa baada yangu.
Kasema Abdullah bin Zamaa :-
جاء بلال في أول شهر ربيع الأول
فأذن بالصلاة فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم (مروا أبا بكر يصلي بالناس )
فخرجت فلم أر بحضرة الباب إلا عمر في رجال ليس فيهم أبو بكر فقلت قم يا عمر فصل
بالناس فقام عمر فلما كبر – وكان رجلا صيتا – سمع رسول الله صلى الله عليه وسلم
صوته بالتكبير فقال ( أين أبو بكر يأبى الله ذلك والمسلمون ) قالها ثلاث مرات (
مروا أبا بكر فليصل بالناس) فقالت عائشة
رضي الله عنها يا رسول الله إن أبا بكر
رجل رقيق القلب إذا قام في مقامك غلبه البكاء فقال (إنكن صويحبات يوسف مروا أبا بكرفليصل بالناس
)
Amekuja Bilal katika
mwanzo wa mwezi wa Rabee Al Awwal akaadhini akasema Mtume wa Allah Subhanahu Wataala Muamrishe Abu Bakr
awasalishe watu. Basi nikatoka na sikumuona hapo mlangoni miongoni mwa watu
ispokuwa Omar, na Abu Bakr alikuwa hayupo pamoja nao nikasema simama Ewe Omar
uwasalishe watu akasimama alipopiga takbira ya Ihram – alikuwa mtu mwenye sauti
kubwa akamsikia Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- katika kupiga takbira akasema – Yuko wapi Abu
Bakr, Allah pamoja na Waislamu wakataa hivyo
(kusalisha mwingine ila Abu Bakr) kasema maneno hayo mara tatu Mwamrisheni Abu Bakr awasalishe watu akasema Aisha R.A. Ewe Mjumbe wa Allah
hakika Abu Bakr moyo wake mwepesi akisimama mahali pako hataweza kujizuia
kulia. Akasema : hakika nyie (wanawake) ni masahib wa Yusuf (wale wanawake
waliomfanyia Yusuf A.S kila aina ya
vitimbi) muamrisheni Abu Bakr awasalishe watu. Akasema, basi Abu Bakr akawasalisha
watu baada ya ile sala aliowasalisha Omar. Alikuwa Omar akimwambia Abdullah bin
Zamaa baada ya hapo vipi mambo gani ulionifanyia wallahi kama ningejua kuwa
Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- amekuamrisha (umwambie Abu Bakr)
basi nisingelifanya (kusalisha) akajibu Abdullah bin Zamaa hakika sikumpata mtu
aliyekuwa wa mbele kufanya hivyo kuliko wewe. Kasema Aisha R.A sikusema hayo
(niliomwambia Mtume –rehema za Allah na
amani zimshukie) wala sikumuepushia nalo jambo hilo Abu Bakr isipokuwa kumtakia
ajiweke mbali na dunia na vile vile nimefanya
hivyo kwa kuona hatari na hilaki iliokuwepo katika uongozi wa nchi (ukubwa)
isipokuwa aliesalimishwa na Allah Subhanahu Wataala, vile vile nimeogopa kuwa watu wasije kuwa hawatampenda
milele mtu atakaesimama kusalisha mahali pa Mtume -rehema za Allah na amani
zimshukie- naye bado yuko hai isipokuwa akitaka Allah, kwa hivyo watamhusudu na
kumfanyia ubaya na wakipata mkosi itakuwa yeye ndiye sababu na hali jambo hilo
ni jambo la Allah
na lilipitishwa kwa Kadhaa yake. Juu ya hivyo Allah akamuepusha na kila
nilichomuogopea kuwa kitampata katika mambo ya Dunia na Dini. Akasema Aisha –
Ile siku aliokufa Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- walipoona watu
amepata nafuu katika maradhi yake mwanzo wa mchana wakamuaga kwenda majumbani
mwao na kufanya haja zao huku wana matumaini wakawa pamoja na wake zao. Basi
tulivyokuwa sisi tuko katika hali hiyo ambayo hatujawahi kabla ya hapo kuwa
katika hali kama hiyo ya matarajio na furaha
hapo akasema Mtume -rehema za
Allah na amani zimshukie- tokeni (kuwambia wake zake) huyu Malaika aomba idhini
ya kuingia kwangu wakatoka wote waliokuwa nyumbani isipokuwa mimi (Aisha R.A.) na kichwa chake
kiko juu ya kipakatio changu akakaa na mimi nikajitenga kwenye upande mwingine
wa nyumba akawa anazungumza (kwa sauti ndogo) na Malaika muda mrefu kisha
akanita na kurudisha kichwa chake kwenye sehemu yangu mahali pa kupakatia
akasema kuwaambia wake zake na watoto wake ingieni. Nikasema hii sio sauti ya
Jibriil A.S. akajibu Mtume –rehema za Allah na amani zimshukie: Kweli ewe
Aisha, huyu ni Malaika wa mauti (wa kutoa roho za watu ) amenijia akaniambia kuwa Allah SWT amenileta
na ameniamrisha kuwa nisingie kwako isipokuwa kwa idhini na ikiwa hukunipa
idhini nirudi na ukinipa idhini niingie na akaniamrisha nisikamate roho yako mpaka
uniamrishe basi nini amri yako ? Nikamjibu nisubirie mpaka anijie Jibriil
A.S. kwani hii ni saa yake Jibriil. Akasema Aisha R.A. tukawa tumekabiliwa na
jambo hatuna jawabu lake wala rai juu yake.
Basi tukapigwa na mshangao
(mduwao) kama tumepigwa na umeme hatujui nini la kufanya wala hakuna
anaezungumza katika watu wa nyumba ya Mtume -rehema za Allah na amani
zimshukie- kwa kulitukuza kulioje hilo jambo na vipi haiba ilivyojaa katika
nyoyo zetu akasema (Aisha R.A) akaja Jibriil (A.S) katika saa yake akaamkia
nikaitambua sauti yake na hapo wakatoka watu wa nyumba yake (-rehema za Allah
na amani zimshukie-) naye akaingia akasema hakika Allah aliyekuwa na nguvu na
kutukuka akupa salamu na akwambia wajihisi vipi ? Naye ni Mjuzi zaidi wa
hali yako kuliko yoyote mwingine lakini ametaka kukuzidishia heshima na sharafu
na atimize heshima yako na sharafu juu
ya viumbe vyote vingine na uwe sunna katika Umma wako (yaani mfano). Akamwambia
nahisi maumivu akamjibu jibashirie kwani
Allah Subhanahu Wataala ametaka akufikishe
kule alipokuahidi (yaani daraja kubwa kwani mtu hupewa mtihani na Allah Subhanahu Wataala akasubiri ikawa sababu
ya kupandishwa daraja yake). Akamwambia Ewe Jibril Malaika wa mauti ametaka
idhini yangu kisha akamuelezea ile habari yote. Akasema Jibriil wewe Muhammad
hakika Mola wako ana shauku na wewe kwani hakukujulisha kitu gani amekutakia?
(amekutakia daraja Kubwa). Akamjibu kumwabia usiondoke sasa mpaka atakapokuja
(Malaika wa mauti) hapo ndipo alipowaruhusu wake zake na watoto wake kuingia nyumbani.
Akasema Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- « Ewe Fatima
nisogelee karibu yangu » akaja akamuinamia, akamnong’oneza, akanyanyua kichwa chake (Fatma) huku machozi
yamtoka na hawezi kuzungumza kisha akamwambia “sogeza kichwa chako karibu yangu”
akamuinamia na (Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie-) akamnong’oneza
akanyanyua kichwa chake huku hawezi kuzungumza kwa kucheka na hakika tuliyoyaona
(mzungumzaji ni Aisha) kwake (Fatma R.A) yalikuwa maajabu nikamuuliza baada ya
hapo akanijibu kuwa mara ya kwanza alinambia (Mtume -rehema za Allah na amani
zimshukie-) kuwa mimi nitakufa leo basi hapo nikalia kisha akasema nimemuomba
Allah SWT uwe wewe wa kwanza katika watu wangu watakaonifatia na tuwe pamoja na
ndipo nilipocheka,halafu akamsogezea watoto wake wawili (Hassan Na Hussein
R.A.) akawanusa. Akasema (Aisha R.A.)
halafu akaja malaika wa mauti akaomba
idhini ya kungia akapewa idhini akasema watuamrisha nini ewe Muhammad akasema “
Nifikishe kwa Mola wangu hivi sasa”
akasema (Malaika wa mauti ) ‘Ndio katika siku yako hii, ama hakika Mola
wako ana shauku ya kukutana na wewe na hakusita kwa mtu yeyote mwingine kama
alivyosita (kuchukua roho yako) kwako wewe na hakunikataza kuingia kwa mtu
yoyote mwingine bila ya idhini isipokuwa
kwako wewe lakini saa yako iko mbele yako’ kisha akatoka (Nasema kauli yake
« Hakusita kwa mtu yoyote kama alivyosita kwako” maneno haya sivyo yanavyoonekana katika
udhahiri wake kwani Allah Subhanahu
Wataala halibadiliki neno kwake lakini yametokea hayo kwa kuonewa huruma na
kuzidishwa heshima yake -rehema za Allah na amani zimshukie- » maneno ya
mtungaji).
Akasema Bibi Aisha R.A. akaja Jibril akasema ‘Amani iwe juu yako Ewe Mtume wa Allah
hii ni mara yangu ya mwisho kuteremka ardhini umekwisha fungwa wahyi na
imekwisha fungwa Dunia na sikuwa na haja yoyote ardhini isipokuwa wewe na wala
sikuwa na haja ardhini isipokuwa kuweko kwako ( yaani Mtume –rehema za Allah na
amani zimshukie-) kisha baada ya kufa kwako nikae huko niliko bila ya kuteremka
tena ardhini’. Hapana naapa kwa yule aliyemleta Muhammad kwa haki hakuna
mtu nyumbani alieweza kumrudishia neno lolote kwa hayo aliyoyasema wala
kumtumia mtu katika watu wake ( kumueleza juu ya hali ya Mtume –rehema za Allah
na amani zimshukie-) kwa utukufu wa yale yanayosikika katika mazungumzo yake
(Jibril A.S.) na kwa kumuonea kwetu huzuni
na huruma ( Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie). Akasema basi nikasimama kwenda kwa Mtume –rehema
za Allah na amani zimshukie- ili nikieke kichwa chake katika kifua changu na
nikamkamata kifuani na akawa azimia mpaka apoteza fahamu na huku kipaji chake
chatoka jasho sijawahi kuliona (jasho) kama hilo katu kabla kwa mtu yeyote basi
nikiwa nalipangusa hilo jasho na sikupata kunusa harufu ya kitu cho chote nzuri
kuliko hilo jasho na nilikuwa namwambia anaporudisha fahamu “Wewe niliyejitolea
mhanga kwa baba yangu na mama yangu na
nafsi yangu na watu wangu aina gani hii ya jasho linalotolewa na kipaji
chako? Akasema ewe Aisha hakika Muumin
yatoka roho yake na jasho zuri lamtoka na kafiri yatoka roho yake baina ya tama
zake mbili kama roho ya punda (inavyotoka).
Nilivyosikia hayo nikaogopa tukawatumia jamaa zetu waje. Na mwanamme wa
mwanzo aliefika ni ndugu yangu tukamtuma kwenda kumwita baba – Abu Bakr akaja
lakini alipoona hali ya Mtume –rehema za Allah na amani zimshukie- imekuwa ya
nafuu akamuomba ruhusa ili ende nyumbani kwake huko As-Sanh nje ya Madina
akamwambia Ewe Mtume wa Allah nakuona hujambo na usiku huu ni usiku wa fulani
(mmoja katika wake zake) basi nipe ruhusa nimweendee hapo akampa ruhusa Mtume –rehema
za Allah na amani zimshukie- kwa hivyo akafa wakati Abu Bakr hayupo akenda
mjumbe wake Mtume –rehema za Allah na amani zimshukie- kwenda kumwita akaja (
Abu Bakr R.A.) na huku amsalia Mtume –rehema za Allah na amani zimshukie- na
macho yake yapukutika machozi na huku duku duku limemshika kwa huzuni yake
ilivyokuwa kubwa naye juu ya yote hayo ni mshupavu katika vitendo vyake na
maneno yake Akamwinamia kisha akamfunua uso wake na kumbusu kipajini na
mafundani na akampangusa usoni, akawa analia na huku asema “wewe ninayejitolea
muhanga kwa baba yangu na mama yangu na nafsi yangu na watu wangu umependeza
(umzuri) katika uhai na mauti, kimekatika katika kufa kwako kile kilicho kuwa
hakikukatika kwa mauti ya Nabii ye yote mwingine wala kukatika kwa Unabii wo
wote mwingine, sifa yako ni juu zaidi kuliko vile tunavyoweza kuisifu, msiba
wako ni mkubwa zaidi kuliko vilio vyetu na majonzi yetu. Umekhusiwa (kufanywa
mambo yako tafauti na watu wengine) mpaka ikawa hafi mtu isipokuwa ukawa msiba
wa kufa kwako sababu ya nafuu ya huo
msiba ikiwa Mtume –rehema za Allah na amani zimshukie- amekufa basi msiba wangu
ni nafuu,na ukafanywa kama watu wengine mpaka tukawa sisi na wewe sawasawa.
Kama ingekuwa mauti yako sio kwa khiari yako mwenyewe basi nafsi zetu
zingekuhuzunikia huzuni kubwa kabisa na kama usingetukataza kulia basi
tungelikulilia mpaka machozi yetu yakakauka. Ama kile tulichokuwa hatuwezi
kujizuia nacho ni majonzi juu yako na kukukumbuka vitu viwili
hivi viko pamoja (havibandukani)
na wala haviondoki. Ewe Mola wetu tufikishie hisia zetu kwake (Mtume –rehema za
Allah na amani zimshukie-). Tutaje Ewe
Muhammed –rehema za Allah na amani zimshukie- kwa Mola wako na iwe katika moyo
wako basi kama ingekuwa sio kwa ule utulivu uliotuachia asingeweza mmoja katika
sisi kusimama kwa sababau ya upweke tulioupata kwa kifo chako. Ewe Mola tufikishie kwa Mtume wako haya
tuliyo yapata kwa ajili yake (kifo chake)
na umhifadhi katika nyoyo zetu (tuwe twamkumbuka wakati wote na kufuata
aliyotufundisha)
Akasema Aisha R.A. akawa kila akizimia (na kufufuka) asema “Bali Rafiki
alie wa Juu” kama kwamba arudishiwa kuhiarishwa naye achagua hicho alicho
kitaja. Akiweza kusema husema “Salaa
Salaa kwani nyie mtaendelea kukamatana ikiwa mtasali pamoja Salaa, Salaa” Akawa aendelea kuusia hivyo mpaka kufa kwake –rehema
za Allah na amani zimshukie- katika wakati baina ya kupanda kwa dhuhaa na
katikati ya mchana siku ya jumatatu. Baada ya kufa wakaja watu (kwa wingi
kuingia nyumba yake Mtume –rehema za Allah na amani zimshukie-) baada ya
kusikia vilio na maombolezi ya kumsikitikia Mtume wa Allah Subhanahu Wataala wakahitilifiana watu
katika mauti yake wengine hawakusadiki (wakaifanya hii habari uongo) wengine
wakaduwaa (wakawa hawasemi kama mabubu) na wengine wakachanganyikiwa na
wakasema maneno yaliyokuwa hayaeleweki, wakabakia wengine na akili zao timamu
na wengine wakawa kama viwete (hawawezi haraka yoyote) basi akawa Omar bin Al Khattab miongoni mwa
waliofanya uongo habari ya kufa kwake –rehema za Allah na amani zimshukie- na
Aliy miongoni mwa walioshindwa kufanya haraka yoyote wakawa wamekaa tu. Na
Othman miongoni mwa waliokuwa wamenyamaza hawawezi kusema kitu) na akatoka Omar
kwa watu akasema kuwa Mtume –rehema za Allah na amani zimshukie- hakufa na
Mwenyezi Mungu SWT atamrudisha kama alivyomuahidi Musa naye atawajia Wallahi
nisimsikie Mtu ataja kuwa Mtume –rehema za Allah na amani zimshukie- amekufa
isipokuwa nitamrukia na upanga wangu huu. Na hakuwa katika Waislamu mtu kama
Abu Bakr na Al Abbas kwani Allah SWT amewapa tawfiiq yake na muongozo wake na
alipo watokea watu Abu bakr baada ya kupata yakini ya kifo cha Mtume –rehema za
Allah na amani zimshukie- akasema “Enyi watu yule aliekuwa amuabudu Muhammad
basi Muhammad amekwisha kufa na aliekuwa amuabudu Mola wake Muhammad basi yeye Mola ni Hai hafi. Amesema Allah SWT:
آل عمران: ١٤٤
« Na hakuwa Muhammad ila ni Mtume tu. Wamepita kabla yake
Mitume (wengi kabisa). Akifa au akiuwawa ndiyo mtarudi nyuma (kwa visigino
vyenu muwe makafiri kama zamani?) Na
atakayerudi nyuma kwa visigino vyake hatamdhuru Allah cho chote. Na Allah
atawalipa wanaomshukuru.”
Basi
ikawa kama watu hawakuisikia Aya hii isipokuwa
siku hiyo. Hapo wakalia kwa makelele
ahliya yake Mtume –rehema za Allah na amani zimshukie- pamoja na wale wote
waliohudhuria. Hayakusita makelele haya
ya vilio isipokuwa kwa mwamkio wa mtu kwa sauti kubwa hapo mlangoni akasema
Assalaam Alayku enyi watu wa nyumba ya Mtume –rehema za Allah na
amani zimshukie-
( كل نفس ذائقة الموت )
“Kila nafsi haina budi kuonja mauti”. Hakika kwa Allah kuna mabakio kwa kila
anaendoka (ukipatikana msiba huwalipa Allah SWT wale wenye msiba badala yake
kitu kinachowapumbazisha ukawa nafuu) na kwake yeye hupata mtu kila
anachokitaka na kwake yeye SWT huokoka mwanadamu kutokana na kila anachokiogopa
basi Allah ndio mumuombe na yeye mumtumainie, wakawa wamsikiliza bila ya
kumuona na wakanyamaza kulia, waliponyamaza ikakatika sauti yake akatoka mmoja
wao kumchungulia bila ya kumuona yeyote. Kisha wakarudia tena kulia na hapo
tena akaita muitaji mwingine wasiyeitambua sauti yake, Enyi watu wa nyumba ya
Mtume –rehema za Allah na amani zimshukie- mdhukuruni Allah SWT na
mshukuruni katika kila hali mtakuwa wenye Ikhlasi. Hakika kwa Allah kuna nafuu kwa kila msiba na
malipo kwa kila kinachotakiwa basi mtiini yeye Allah SWT na kwa mujibu wa
amri yake mutende. Akasema Abu
Bakr hawa ni Al Khadr AS na Al Yasaa A.S wamehudhuria kifo cha Mtume –rehema za Allah na
amani zimshukie.
Na
asiwashughulishe sheitani kwa kufa kwa Mtume wenu wala asiwapoteze kutokana na
dini yenu kwa kuwafanya msiweze kufanya kheri au kuchelewa kufanya kheri. Msipofanya kheri na kuchelewa kuifanya ndipo
atakapowajia na kuwapoteza (huyo sheitani)
Alipomaliza
kutoa hotuba yake akasema “Ewe Omar ndio juu yako wewe imenifikia habari kuwa
unasema Mtume wa Allah SWT hakufa kwani hujuwi
kuwa Mtume wa Allah SWT amesema siku kadha kadha wa kadha na siku kadha
kadha wa kadha na amesema Mola katika kitabu chake:
الزمر: ٣٠
“Kwa yakini wewe
utakufa na wao pia watakufa”
Akasema
(yaani Omar R.A) Wallahi kama kwamba sijaisikia aya hii katika kitabu cha Allah
SWT kabla ya sasa kwa yale yaliyotupata. Nashuhudia kuwa kitabu cha Mola kama
kilivyoteremshwa na kuwa hadithi za Mtume –rehema za Allah na
amani zimshukie-
kama zulivyozungumzwa na kuwa Allah SWT yuhai nae hafi.
البقرة: ١٥٦
“Hakika sisi ni wa
Allah na hakika kwake yeye tutarejea (atatupa jaza yake)”
Na
sala za Allah (Rehema zake) zimfikie Mtume wake na twatarajia ujira wetu kwa
Allah SWT kwa msiba huu wa kuondokewa na Mtume wake –rehema za Allah na amani
zimshukie.
Kisha
Abu Bakr akakaa, akasema Aisha R.A. walipokusanyika kumuosha wakasema wallahi
hatujui vipi tumuoshe Mtume wa Allah –rehema za Allah na
amani zimshukie,
tumvue nguo zake kama tunavyowafanyia
maiti zetu, au tumuoshe na nguo zake, akasema basi Allah akawapelekea
usingizi hata hakubakia miogoni mwao mtu isipokuwa kidevu chake kiko kifuani
kwake kwa usingizi kisha akasema msemaji - hajulikani nani- muosheni Mtume wa
Allah –rehema za Allah na amani zimshukie- na nguo zake (yaani bila ya kumvua nguo)
basi ndipo walipotanabahi na wakafanya hivyo mpaka walivyo maliza kumuosha
akavishwa sanda. Akasema Aliy tumetaka
kumvua kanzu yake tukaitwa kuambiwa msimvue Mtume wa Allah nguo zake basi
tukaitikia na tukamuosha na kanzu yake na tukamlaza kama tunavyoosha maiti zetu
na hatukutaka tugeuziwe kiungo cho chote katika viungo vyake tupate kukiosha
isipokuwa twageuziwa na twakiosha mpaka twamaliza na kukawa na harufu nyumbani
kama twapuliziwa upepo wenye harufu nzuri sana na huku twaisikia sauti yatwambia
muwe wapole (katika kumuosha) na Mtume wa Allah –rehema za Allah na
amani zimshukie-
kwani mtatoshelezwa ( yaani mtasaidiwa kumuosha).
Likatandikwa
kaburi lake –rehema za Allah na amani zimshukie- kwa kitandikio chake (shuka lake) na
kitambaa cha makhmeli (قطيفته) na zikatandikwa nguo zake
juu yake (kaburi lake ) zile alizokuwa kazivaa. Kisha akatiwa kaburini baada ya
kuvishwa sanda. Kwani hakuacha baada ya
kufa kwake mali wala hakujenga katika
uhai wake tofali juu ya tofali yaani hakujenga nyumba ya udongo wala hakuweka
boriti (قصبة
) juu ya boriti yaani hakujenga nyumba ya makuti na katika kifo chake –rehema za Allah na
amani zimshukie-
kuna zingatio kamilifu naye ni mfano mzuri kwa Waislamu.
Maneno yake
yalikuwa kidogo (hazungumzi isipokuwa kwenye haja) na mepesi kufahamika. Na
hazungumzi mambo ya kipuuzi na ayapangilia maneno yake kwa mpango mzuri
hayagongani katika maana yake. Amesema
Aisha R.A. alikuwa asoma Qur’ani upesi upesi lakini bila ya kukosea au kuacha
kitu sio kama kusoma kwenu huku kwa haraka (Alikuwa husoma Qur’ani kwa
mfuatilio wa maneno mzuri sana sio kama kusoma kwenu huku). Alikuwa mbora wa wafupishaji wa
maneno na kwa hivyo alivyokuwa anakuja Jibriil A.S. alikuwa Mtume -rehema za
Allah na amani zimshukie- pamoja na kufupisha kwake maneno akusanya maana ya yote aliyokuja nayo Jibriil
A.S. Alikuwa asema maneno kidogo yaliyochukua maana kubwa haongezi maneno bila
ya haja wala hapunguzi kusema kitu ambacho kitaleta kasoro katika maana kama
kwamba maneno yake yafuatiya baadhi yake baadhi. Na baina ya maneno yake kuna
kusimama hata kwa yule anayemsikiliza ahifadhi anayoyasema na kuyasikia vizuri.
Alikuwa mwenye sauti kubwa na nzuri kuliko sauti za watu wote. Hunyamaza muda
mrefu na hazungumzi palipokuwa hapana haja, hasemi isipokuwa haki katika hali
zote mbili za kuridhika na kughadhibika.
Hamsikilizi yule anayezungumza
maneno yaliyokuwa si mazuri.Ikiwa kalazimika kusema kitu ambacho sio cha
kusemwa basi husema kwa “kinaya” yaani dhahiri yake hufahamika vingine na vile
kinavyokusudiwa. Alikuwa asema
( لا تضربوا
القرآن بعضه ببعض فإنه نزل على وجوه )
“Msiipiganishe
Qur’ani baadhi yake na baadhi kwani imeteremka katika mielekeo mingi (rai
nyingi)"
Alikuwa
akitabasamu sana kwa masahaba zake hana mfano wake. Siku moja alikuja mbeduwi
akamkuta Mtume –rehema za Allah na amani zimshukie- amebadilika rangi yake hali
ambayo haikuwaridhisha masahaba zake, akataka yule mbedui kumuuliza wakamwambia
usifanye hivyo ewe mbeduwi kwani sisi hatupendezewi na hali ya rangi yake.
Akawajibu niachieni kwani naapa kwa yule aliemleta kwa haki Mtume sitamwacha
mpaka atabasamu. Akasema Ewe Mtume wa Allah imetufikia kuwa Masiih Dajjaal
atawajia watu na mkate hali ya kuwa wafa njaa jee unaona wewe nawatoa mhanga
kwako baba yangu na mama yangu nijizuie nisiule ule mkate wake kwa ajili ya
kujikataza kula haramu na kuitakasa nafsi yangu hadi nife njaa au niupige mkate
wake (niule) mpaka nikashiba (mbavu zangu zikajaa kwa shibe) hapo nimwaamini
Allah SWT na nitamkufuru yeye (Masiih Dajjaal). Wakasema (Masahaba) basi hapo
akacheka Mtume wa Allah -rehema za Allah na amani zimshukie- mpaka meno yake
magego yakaonekana kisha akasema! “Hapana bali Allah Subhanahu
Wataala
atakutosheleza kwa kile atakachowatosheleza Waumini.” Alikuwa mwenye kutabasamu
zaidi na mwenye nafsi safi
kuliko watu wote isipokuwa wakati wa kuteremka Qur’ani au akikumbuka kiyama au
akihutubu hutuba kubwa. Alikuwa akipatwa na jambo hujivua nafsi yake na uwezo
na nguvu (kuwa hana uwezo wala nguvu na hivyo ni vya Allah) na humtegemea Allah
SWT na kutawakali kwake katika jambo hilo .
Vile vile humuomba Allah SWT amuongoze katika njia iliyonyooka:
( اللهم أرني الحق حقا فأتبعه وأرني الباطل باطلا وارزقني اجتنابه وأعذني من أن يشتبه علي فأتبع هواي بغير
هدى منك واجعل هواي تبعا لطاعتك وخذ رضا نفسك من نفسي في عافية واهدني لما اختلف
فيه من الحق بإذنك إنك تهدي من تشاء إلى صراط مستقيم )
“Ewe
Mola wangu nioneshe haki niione kuwa ni haki ili niifuate na nioneshi upotofu na
niuone kuwa upotofu na nijaalie niepukane nao. Na niepushe na kuchanganyikiwa
nisije nikafata mapendekezo ya nafsi yangu bila ya muongozo wako nijaalie
mapendekezo yangu yende sambamba na amri zako (taa yako). Niridhie hata
unilinde kutokana na kila lililokuwa baya na uniongoze katika yale
yaliokhtalifiwa katika haki kwa idhini yako hakika wewe unamuongoza umtakaye
katika njia iliyonyooka.”
Mara nyingi wakati anapokula hukusanya magoti yake
mawili na miguu yake miwili kama anavyokaa anaesali (kikao cha Attahiyatu) na
husema:
( إنما أنا عبد آكل كما يأكل العبد وأجلس كما يجلس العبد )
“ Hakika mimi ni mja nala
kama anavyokula mja na nakaa kama anavyokaa mja”.
Na alikuwa ala kile kilicho mbele yake (katika
sahani). Akamjia Othman na ‘ faaludhaj’ ( aina ya chakula) akaila na
akasema:
( إن هذا الطعام طيب )
"Hakika chakula hichi
kizuri."
Na katika matunda ya majimaji aliyokuwa
ayapenda kuliko yote ni tikiti (Batteekh) na zabibu na siku moja alikula tende
mbichi (rattab) kwa mkono wake wa kulia na akashika kokwa kwa mkono wake wa
kushoto akapita mbuzi akamuashiria akawa (yule mbuzi) anakula katika mkono wake
wa kushoto na yeye anakula kwa mkono wake wa kulia mpaka alipomaliza na
akaondoka yule mbuzi. Na alikuwa pengine anakula zabibu kwa kukamata mkole wake
(mkole wa zabibu) halafu hula hizo
zabibu moja moja kutoka mkoleni
hata vipunje vyake huanguka na kuonekana katika ndevu zake. Alikuwa
-rehema za Allah na amani zimshukie- apenda maboga na alikuwa akisema hakika
huu ni mti wa ndugu yangu Yunus A.S.Na alikuwa asema:
( يا عائشة إذا طبختم قدرا فأكثروا
فيها من الدبأ فإنه يشد قلب الحزين )
"Ewe Aisha mkipika
chungu (cha mchuzi) kithirisheni mboga (mabamia, mabilingani upate kuwa mwingi) kwani huko kunatia nguvu moyo wa
mwenye huzuni (akipelekewa katika huo mchuzi)".
Alikuwa apenda katika nyama ya mbuzi miguu ya
mbele na mabega na katika viungo apenda siki na katika tende apenda aina fulani
inayoitwa « al-Ajwa » na alikuwa achukia mafigo kwa mahala pake
karibu na mkojo. Alikuwa hali thomu na vitunguu maji wala kiraathi (aina fulani
ya vitunguu ambayo vile vile yatoa harufu). Hakuwa kabisa akitia kasoro chakula
lakini kikimpendeza akila na ikiwa hakukipenda akiwacha hasemi cho chote cha
kufanya hicho chakula kichukiwe na wengine watakaosikia kasoro hiyo. Alikuwa
aramba vidole vyake baada ya kumaliza kula mpaka vyageuka vyekundu aramba
kimoja kimoja na huku akisema :( إنه لا يدري في أي الطعام
البركة ) « Hakika
mtu hajui katika chakula gani kilichokuwa na baraka. » Na akimaliza husema:
( الحمد
لله اللهم لك الحمد أطعمت فأشبعت وسقيت فأرويت لك الحمد غير مكفور ولا مودع ولا
مستغنى عنه )
« Sifa zote njema ni za Allah. Ewe Mola shukrani ni zako umelisha mpaka
ukashibisha na ukanywisha mpaka ukaitoa kiu.
Shukrani ni yako isiyokufuriwa wala isiokatika wala isiowezekana kuachwa
bila kushukuriwa ». Alikuwa akishakula mkate na nyama khasa huosha mikono
yake miwili vizuri kisha hupangusa yale maji yaliobakia mikononi katika uso
wake na alikuwa anywa katika michubuo mitatu kabla ya kila chubuo asema
‘Bismillahi’ na mwisho wake asema ‘Al Hamdulillah’ (Yaani husoma Bismillah mara
tatu na Al-Hamdulillah mara Tatu). Alikuwa akinywa maji huyafyonza hayabugii na
alikuwa hahemi mbele ya kile chombo anachonywea bali ahema kando yake na alikuwa
nyumbani kwake ana haya zaidi kuliko mwana mwali. Hawaulizi juu ya chakula
(wampe chakula) au kuwahimiza wampe chakula wakimpa chakula ala na cho chote
wanachompa akikubali na wanachomnywesha anywa na pengine husimama mwenyewe na
kuchukua kile anachotaka kula au
knywa(ajitumikia).
Alikuwa
Mtume -rehema za Allah na amani
zimshukie- avaa pete na pengine hutoka na katika pete yake kuna uzi umefungwa
ili akiuona akumbuke kitu fulani na
alikuwa avaa kofia chini ya kilemba (amama), na alikuwa ana kilemba chaitwa
“Assahaab” (wingu) akamgaia Aliy bin Abi Talib
na Ali wakati mwengine hutokea kakivaa na Mtume -rehema za Allah na amani
zimshukie- husema:
( أتاكم علي
في السحاب )
“Amewajia
Aliy katika wingu.”
Nasema
labda hadithi hii ndio iliyowafanya wale katika mashia wanaosema kuwa Aliy bin
Abi Talib yuko katika mawingu. Basi wakisikia radi wamwamkia Aliy. Alikuwa -rehema za Allah na amani zimshukie-
akivaa nguo huanza upande wa kulia na asema:
( الحمد لله الذي كساني ما أواري به عورتي وأتجمل به في الناس
)
‘Namshukuru Allah
aliyenivalisha ninachojistiria utupu wangu na ninachojipambia kwa watu.’ Na
akivua nguo huanza kwanza upande wa kushoto.
Alikuwa akivaa nguo mpya humpa nguo yake ya zamani maskini kisha husema
:-
( ما من مسلم يكسو مسلما من سمل ثيابه لا يكسوه إلا لله
إلا كان في ضمان الله وحرزه وخيره ما واراه حيا وميتا )
“Hampi Muislamu nguo yake ya zamani Muislamu mwenzake na
hamvalishi ila kwa ajili ya Allah (kutaka radhi yake) isipokuwa huwa katika
dhamana ya Allah Subhanahu Wataala
na kinga yake na kheri yake madamu ameivaa hiyo nguo wakati yu hai au
amekwishakufa.” Ilikuwa katika tabia
yake -rehema za Allah na amani zimshukie- kuwapa majina wanyama wake, silaha
zake na vitu vyake na lilikuwa jina la bendera yake “Al-uqaab” yaani “mwewe”.
Na jina la upanga wake anaokwenda nao vitani “Dhul-Faqaar” yaani “Wenye misingi” na anao upanga unaoitwa “Al-Mikhdham” (mkali) na upanga mwingine waitwa “Ar-Rasuub”
(unaozama) na mwingine waitwa “Al-Qadhiib” (unaopendeza) mshikio wake umepakwa kwa fedha na lilikuwa jina la upinde
wake “Al-Katuum” (usiovuma) na jina la podo lake (mfoko wa mishale) “Kaafuur”
na jina la ngamia wake “Al-Qaswaa” na mwingine “Al-Adhbaa” na jina la baghla wake (mnyama baina farasi
na punda kwa kimo) aitwa “Addaldal” na jina la punda wake “Yaafuur” na jina la
mbuzi wake aliekuwa akinywa maziwa yake “iyna” (
عينة ) .
Na
alipokwisha ondoka akasema -:
( ردوه علي
رويدا )
“mrudisheni kwangu polepole”
Alikuwa
-rehema za Allah na amani zimshukie- katika vita basi maadui wakawaona waislamu
wako katika ghafla, akaja mtu (katika washirikina) mpaka akasimama mbele ya
Mtume wa Allah huku ameshika upanga akamwambia nani anayekukinga na mie?
Akamwambia (-rehema za Allah na amani zimshukie-) "Allah". Na hapo
ukaanguka ule upanga kutoka mkononi mwake akauchukua Mtume wa Allah akamwabia
yule mtu “nani anaekukinga na mimi?”
Akamwabia kuwa wewe bora kuliko mimi ( katika kusamehe). Akamwambia Sema
Ash-hadu an laa ilaah Illa Allah wa Anniy Rasool Allah. Akasema hapana (yaani
sisemi hivyo) isipokuwa natoa ahadi kuwa sipigani vita na wewe wala siwi pamoja
na watu wanaopigana na wewe. Hapo akamwachia kwenda zake akenda kwa watu wake
akawaambia nimewajia kutoka kwa mbora wa watu.
Anazo
-rehema za Allah na amani zimshukie- habari nyingi namna kama hii alikuwa
asema:- Asiniletee mmoja wenu habari juu
ya mmoja katika masahibu zangu kwani napenda kuwajia na moyo wangu uko safi juu yenu. Akasema
Aliy bin Abi Taalib amenipeleka Mtume wa Allah -rehema za Allah na amani
zimshukie- mimi, Zubair na Al-Miqdaad
akasema “ Nendeni kwenye bustani ya “Khaakh” ndani yake kuna mwanamke (yumo
ndani ya kihema kidogo kinachoekwa juu ya ngamia yaani ‘Khaudaj’) ana barua
ichukueni kutoka kwake. Tukenda kisha tukamwambia yule mwanamke itoe hiyo barua
au tutakuvua nguo akaitoa katika mikia ya nywele zake tukaileta kwa Mtume
-rehema za Allah na amani zimshukie-. Ikajulikana kuwa inatoka kwa Haatib bin
Abi Balta’a (katika Masahaba) na inakwenda kwa washirikina wa Makka anawapasha
habari juu ya jambo katika mambo ya Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie-
ambayo hakutaka jambo hilo alijue mtu yo
yote nalo nafikiria ni juu ya kuiteka Makka wakati aliposema Mtume -rehema za
Allah na amani zimshukie:- “Ewe Mola tuzibie macho (tusionekane ulisitiri jambo
letu hili la kuteka Makka) mpaka tuwachukue Quraish kwa ghafla” au kama
ilivyokuwa katika maana ya hadithi. Akasema Mtume -rehema za Allah na amani
zimshukie- kitu gani Ewe Haatib kilichokusababisha ufanye hivyo? Akasema Ewe Mtume usiniharakishiye, mimi ni mtu niliokuwa
nimeshikana sana na watu wangu na katika Muhaajiriin uliokuwa nao wanao jamaa
zao Makka wanaohami watoto wao (hao Muhaajirin), kwa hiyo mimi nikataka msaada
kwa watu wengine (Mushrikiin) wawahami watoto wangu kwa sababu sina watu wangu
wa karibu kwa damu wa kunifanyia hivyo, si kufanya hivyo kukufuru au kuridhika
na ukafiri baada ya Uislamu au kurtadi kutokana na dini yangu. Akasema Mtume -rehema za Allah na amani
zimshukie:- Hakika aliyowaambia ni ukweli. Akasema Omar R.A niwache niikate
shingo ya munafiq huyu. Akajibu Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie,
hakika yeye amepigana vita vya Bader na kitu gani kitakacho kujulisha pengine
Allah Subhanahu Wataala amewatazama waliopigana vita vya Bader
akasema “Fanyeni mnayotaka kufanya mimi nimekwisha waghufiria madhambi yenu.”
Alikuwa
Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- mnyenyekevu zaidi kuliko watu wote
juu ya cheo chake kikubwa kabisa. Amesema Ibn Aamer: Nimemuona anapiga mawe
Jamara Al Aqaba kutoka juu ya ngamia mweupe mwenye weusi kidogo alikuwa akipiga
mawe pamoja na watu wa kawaida sio kuwapiga na kuwafukuza watu ili apite yeye
Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- (kama
wanavyofanyiwa wafalme). Alikuwa akipanda punda alietandikwa kwa kitambaa cha
makhameli na pamoja na hayo alikuwa akimpandisha mtu mwingine pamoja naye.
Aliletwa mtu kwa Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- alivyomuona akatetemeka kwa haiba yake (sura yenye
kumfanya mtu amuogope akimuona mara ya kwanza). Basi hapo Mtume -rehema za
Allah na amani zimshukie- akamwambia: "Pole pole kwani mimi si mfalme
isipokuwa ni mtoto wa mwanamke wa Kiqureish aliekuwa akila nyama ilyokaushwa
kwa jua". Alikuwa akikaa pamoja na masahaba zake huchanganyika nao akawa kama
mmoja katika wao hata akija mtu mwengine asiweze kumtambua Mtume -rehema za
Allah na amani zimshukie- baina yao
mpaka aulize.
Nasema
(maneno ni ya mtungaji) wamechukua mfano wake Maimamu wa Kibaadhi radhi ya
Allah SWT ziwe juu yao
(wakitawala kwa sharia ya Allah Subhanahu Wataala). Alikuwa mgeni aingiapo katika
mjumuiko wa watu hamjui nani kati yao
Imam mpaka aambiwe huyu ndiye Imam. Tizama kisa kilichokuwemo katika “Allulu
Arratb” (kitabu cha mtungaji) cha Imam Azzan bin Qais alipoingia mtu aliemkusudia yeye akenda
kumuamkia mtu mwingine badala ya kumwamkia
Imam kwa jinsi anavyo changanyika na masahibu zake.
Alikuwa
Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- haitwi na mmoja katika masahaba zake
isipokuwa kuitikia kwake huwa ni “Labbeik”, na alikuwa atabasamu nao wakati
wanapozungumza na wanapocheka na
hawakatazi isipokuwa kutokana na haramu.
Kughadhibika
na kuridhika kwake kulikuwa mara kwajulikana katika uso wake kwa usafi wa rangi
yake ya uso (mabadiliko yo yote katika uso wake mara yaonekana). Mmoja katika
waliomsifu kamshabihisha kama mwezi unavyoonekana usiku wa bader (usiku
unaokamilika mwezi). Amemsifu sahibu
wake Abu Bakr R.A:- Mwaminifu Al Mustafa anaita kwenye kheri kama kwamba ni
mwanga wa mwezi uliokamilika umebainika kizani, kilikuwa kipaji chake Mtume
-rehema za Allah na amani zimshukie- kipana na nyusi zake nyembamba na
zimekamilika (za kifungo) na baina ya nyusi zake kwametameta kama fedha
iliyosafi na yalikuwa macho yake mapana (makubwa) na vile vile yalikuwa meusi sana na
yemchanganyika na wekundu, kope za macho yake zilikuwa nyingi na pua yake
imenyanyuka na imenyooka na meno yake yana mwanya, na akifungua mdomo wake
kucheka kama kwamba amefungua mwanga wa umeme unavyometameta, midomo yake
miwili katika bora ya viumbe vya Allah Subhanahu
Wataala, akiufunga
mdomo wake honekana kuwa mdogo, mafunda yake yameingia ndani na magumu. Ana
ndevu nyingi aziwachia, achukua (apunguza au anyoa) masharubu, na ile sehemu ya
shingo yake inayopigwa na jua na upepo rangi yake ni kama birika la fedha
lililochanganyika na dhahabu inametameta katika weupe wa fedha na wekundu wa
dhahabu. Ni mwenye kifua kipana na nyama ya mwili wake imeshikana vizuri
(haikutebwereka) kama kiyoo katika kusimama kwake na kama
mwezi kwa weupe wake. Amewasilishiwa
baina ya mwanzo wa kifua chake (chini ya roho yake) mpaka kwenye kitovu chake
kwa nywele zilizotengezwa kama namna ya bomba (la maji), hapakuwa katika kifua
chake wala katika tumbo lake
nywele isipokuwa hizo na
vile vile alikuwa na mikunjo ya tumbo mitatu aifunika na kikoi katika hiyo
mitatu mmoja na miwili yaonekana. Ana mabega makubwa yenye nywele nyingi na
mwenye vifundo vya vidole vya mikono vikubwa. Ni mwenye mgongo ulio mpana,
baina ya mabega ya mawili kuna mhuri wa unabii (khaatam Annubuwa) umefuatia
(huo mhuri) bega lake la kulia ndani yake kuna doa jeusi (ndugu) limepiga
manjano, kando yake kuna nywele zimelizunguka hilo
doa kwa mfatilio kama ile alama iliyoko juu ya
uso wa farasi. Mikono yake mikubwa imejaza (tokea mabegani kwenda vifundoni
mpaka mwanzo wa viganja) na viganja
vyake virefu (sehemu ya kushikia ya mkono upande wa nje) na vile vile mikubwa yenye
wasaa (sehemu ya kushikia upande wa tumboni yaani ndani) vidole vyake virefu na
kama kwamba mabomba ya fedha. Kiganja chake kilaini kuliko aina fulani ya
kitambaa (hariri). Anukia ikiwa kajitia mafuta mazuri au hakujitia, akimwamkia
mtu hubakiliwa na harufu nzuri siku nzima. Huweka mkono wake juu ya kichwa cha
mtoto akawa hujulikana miongoni mwa watoto wengine kuwa ameshikwa na Mtume
-rehema za Allah na amani zimshukie- kwa jinsi anavyonukia. Ilikuwa miguu na
mapaja yake mikubwa na huonekana kuvimba kwake chini ya kikoi chake. Alikuwa
wastani katika umbo lake
alinenepa kidogo katika
siku zake za mwisho na ilikuwa nyama ya mwili wake imekamatana. Alikuwa Mtume
-rehema za Allah na amani zimshukie- katika kutembea kwake kama
vile ang’oka katika ardhi na khatua zake zakikaribiana na hutembea polepole
(kwa taratibu) bila ya maringo. Alikuwa
asema nina majina kumi kwa Mola wangu, mimi Muhammad na mimi Ahmad na mimi
Al-Maahiy na mimi Al Aaqib na mimi Al Haashir na mimi Rasool ar- Rahma na mimi Rasool at- Tawbah na Rasool- Al Malaahim
an Al Maqfiy na mimi Quthum (Aliye kamilisha, aliyejumuisha) Allah Amteremshie
Rahma na Amani nyingi sana. Twamuomba Mwenyezi Mungu Subhanahu
Wataala aturuzuku
tumfuate na wala tusipotee njia yake. Ukoo wake Mtume -rehema za Allah na amani
zimshukie- (Nasab Yake) Muhammad bin
Abdillah bin Abdel Al Muttalib bin Haashim bin Abd Manaaf bin Qusey bin Kinanah
bin Murrah bin Kaab bi Luay bin Ghaalib bin Fihr bin Maalik bin Annadhr bin
Kanaanat bin Khuzaymah bin Mudrikah bin Ilyaas bin Mudhar bin Nizaar bin Maaddi
bin Adnaan na mpaka hapa umehifadhiwa ukoo wake wenye sharafu kwa mujibu wa
kauli yake Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- kwani akiutaja ukoo wake na akafika Adnaan husema “wamesema
uwongo wanaoandika juu ya ukoo” kasema mara mbili au mara tatu kwa sababu baada
ya Adnaan kuna mpingamano mkubwa.
Amekufa
baba yake Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- naye bado yuko katika
tumbo la mama yake na amekufa mama yake Aminah bint Wahb na umri wake –rehema za Allah
na amani zimshukie- miaka sita, na amekufa babu yake
Abdul Muttalib na Mtume wa Allah -rehema za Allah na amani zimshukie- ana umri
wa miaka minane. Akamchukua kumlea baada yake mtoto wake huyo Abdul Muttalib
naye ni Abu Taalib ammi yake Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie.
Amemuowa Bi Khadija R.A. na umri wake miaka ishirini na tano na ukoo wake
wakutana na ukoo wa Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie- katika
Qusey. Amefanya sulhu baina ya Maquraish
katika ugomvi wao wa kulinyanyua Jiwe jeusi (حجر
الأسود)
wakati ana umri wa
miaka thelathini na tano. Amepewa Utume
wakati umri wake miaka arubaini (40) na alificha Mtume wa Allah kuteremshiwa kwake wahyi kwa muda wa miaka
mitatu mpaka ilipoteremka:
الحجر: ٩٤
“Basi (wewe)
yatangaze ulioamrishwa (wala usijali
upinzani wao) na ujitenge mbali na (vitendo vya ) washirikina”
Amepelekwa
katika safari ya Israa kwenda Bait Al-Maqdis kisha akapazwa kwenda mbinguni
katika safari ya Miiraji kabla ya Al Hijra kwa mwaka na huko ikafaridhishwa
sala.Akafa ammi yake Abu Taalib na mkewe Bi Khadija R.A. katika mwaka mmoja
kabla ya Al Hijra kwa miaka mitatu na ukaitwa mwaka huo mwaka wa huzuni.
Hijra
ya Mtume wa Allah -rehema za Allah na amani zimshukie- kwenda Madina ilikuwa
baada ya miaka kumi na tatu baada ya kupewa Utume.
Kubadilishwa
Kibla kutoka Beit Al Maqdis kwenda Al-Kaaba kulikuwa mwanzo wa miezi kumi na nane kutoka A-Hijra.
No comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.