Elimu yagawanyika katika
sehemu mbili:
Elimu yenye kufaa,
kushukuriwa, kusifiwa.
Elimu inayodhuru
inayokosolewa.
Ama elimu yenye kushukuriwa
nayo imegawanyika katika sehemu mbili nazo:-
“Fardha ein” yaani inampasa
kila Muislamu aijue (ajifundishe) na “Fardh kifaya” yaani aina hii ya
elimu wakiijuwa (wakijifundisha) baadhi ya Waislamu yawatosheleza wengine
waliobakia wasijue. Hakuna haja hapa kutaja fadhila za elimu kwani tayari huko
nyuma imeshatajwa baadhi ya fadhila zake na kama
inavyojulikana kuwa elimu ni uhai wa nyoyo unaozifanya zisiwe pofu na nuru ya
macho unaomfanya mtu asidhulumu na nguvu ya mwili inayomzuia mtu asiwe dhaifu
inayomfikisha cheo cha waja wema na daraja za juu. Kutumia mtu fikira yake
katika elimu ni sawa sawa na kufunga na kuisoma (elimu) ni sawa sawa na kusali
Sala za usiku na kwa ujumla Allah Subhanahu Wataala atiiwa kwa elimu amma
ujinga hauna kheri yoyote.
Elimu ya fardhi ein: Ni elimu ya kitabu
Qur'ani na Sunna, na dalili yake kauli ya Mtume wetu Salla- llahu Alayhi
Wasallam "Kutafuta elimu ni faridha (wajibu) kwa kila Muislamu", na
kwa tamko lengine ni kama ilivyokuja katika
hadithi:-
"Uislamu umejengwa juu ya
mambo matano, Shahada kuwa hakuna mwengine wa kuabudiwa isipokuwa Allah na kuwa
Muhammad ni Mtume wa Allah na kusimamisha Sala na kutoa Zakaa na kufunga
Ramadhani na kuhiji nyumba ya Allah Takatifu (Al-Kaaba) kwa mwenye uwezo wa
kwenda huko". Kila moja katika mambo matano hayo yawajibika kufanywa
katika wakati wake na inapowajibika kuifanya moja katika faridha zake hizo
anakuwa hana wakati wa kupoteza lazima akimbilize kuifanya katika wakati wake
ulioekewa au sivyo atahiliki kwa kuacha kuifanya hiyo faradhi. Kwa hiyo, ni
wajibu kujuwa haya kabla ya kufika wakati wake hiyo faridha.
Amma shahada mbili
zamwajibikia Muislamu akisha baleghe bila ya kuchelewa (akifika wakati wa
taklifu na kuna alama zake) na Sala inamwajibikia kadhalika ukafika wakati wake
na vile vile Saumu yamwajibikia ukiingia mwezi wa Ramadhani na Zakaa kadhalika
ikitimu mali kiwango maalumu (An-nisaab) na ukakamilika mwaka mmoja baada ya
kufika hiyo nisabu hapo ndipo huwekwa wakati maalumu wa kuitoa Zakaa na Hija
yawajibika kwenye uwezo na hivyo yale mambo yaliyo katazwa kuyafanya yawajibika
kuyajua Muislamu wakati yanapomkabili kwa mfano kama mtu amezini kisha akasema
kuwa sikujua kuwa zina haramu basi amehiliki na ujinga wake huo haumsaidii kitu
basi kadhalika mambo yote yaliyoharimishwa unaweza usiyajue kabla ya kuyafanya
lakini mara ukisha yafanya haikufai ujinga wako kwani waandikiwa madhambi ya
kosa hilo. Basi kwa hivyo wamewajibisha wanavyuoni kujifundisha mambo haya
kabla ya kufika wakti wake.
Na elimu ya “Fardhi kifaya”
ni kama elimu ya tiba (kuwaganga watu), hesabu
na elimu ya mirathi kwani akikosekana lau mwanachuoni mmoja wa elimu hizi
katika nchi basi wakazi wa nchi ile wote waingia makosani lakini akipatikana
mmoja tu anaejua elimu hizi wale wengine wote watoshelezwa na huyu mmoja na
watokana na dhima ya hiyo faradhi (elimu). Amma elimu inayodhuru inayokatazwa
ni kama ya uchawi na kutizamia na elimu yote inayowaletea watu madhara na
maudhi na yumo katika kikundi hichi yule
anaesoma elimu ya fiqhi ili apate kubishana na kujisifu na vile vile kujiingiza
sana katika elimu ya Qadar na elimu ya nyota kukusudia dunia (kupata uchumi).
Amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasallam "Ikitajwa Qadar basi zuieni na
ikitajwa nyota zuieni na wakitajwa Masahaba zangu zuieni (yaani msiseme kitu na
kuingiza lenu)". Ameitoa Ibn Masood.
Na kuna aina ya elimu iliyoruhusiwa
kama elimu ya mashairi shuruti isiwe ndani yake mambo ya upumbavu na elimu ya
Chemistry na Physics na nyinginezo katika elimu ambazo si wajibu kwa Muislamu
kuzijua kwa hiyo baada ya kujifundisha zile elimu zilizokuwa wajibu (zinazomfaa
Muislamu na zampasa azijue) hapana kitu bali vizuri kujifundisha hizi elimu
nyingine kwani kukijua kitu ni bora kuliko kutokijua. Lakini inampasa Muislamu
kuwa msingi au asili ya elimu yake iwe elimu ya Dini kisha asome mambo ya Dunia
kwani Dunia ni shamba la kuvunia Akhera. Na haikamiliki Dini isipokuwa kwa
Dunia na “Utawala na Dini ni pacha” kwani Dini ni asili na mtawala ni mlinzi na
kilichokuwa hakina mlinzi hupotea na vile vile hautimii umilikaji na udhibiti
wa kitu isipokuwa kwa mtawala na njia ya udhibiti haitimii isipokuwa kwa elimu
ya fiqhi na huu ni msingi anaeupuuza basi huhasirika. Katika mambo muhimu
yanayompasa mwanafunzi ayajue ikiwa ataka apate elimu ni kuwa elimu ni nuru
haiangazi isipokuwa katika mahali panapowafikiana nayo. Na vile vile aisafishe
nafsi yake kutokana na kila uchafu (asiwe na sifa mbaya au kufikiri mabaya) na
asionekane katika sehemu mbaya zinazowafanya watu wamtilie shaka wanaemuona
hapo, kama sinema au vikao vya watu ovyo na
mengineyo ya mambo yanayotiliwa shaka kwa sababu elimu ni nuru nayo haimuongozi
anaejichafua na mambo maovu. Amesema Al-Ghazaliy katika “Ihyaa”: “Ukisema naona
kikundi cha wanavyuoni na wanafiqhi wametokeza katika matawi na katika mashina
(elimu) na wamehisabika katika jumla ya watemi katika elimu lakini tabia zao mbaya
yaani hawajajisafisha nafsi zao kutokana na tabia mbovu hizo” basi hujibiwa
(huyo aliyesema maneno hayo juu) ikiwa wewe unajua vidato vya elimu mbali mbali
na wajua vidato vya elimu ya Akhera itabainika kwako kuwa hicho
walichojishughulisha nacho kina faida ndogo kwani elimu tu bila ya vitendo
(amali); ama faida yake (elimu) hupatikana inaposuhubiana na vitendo vilivyo na
ikhlasi ya kutaka radhi ya Allah Subhanahu Wataala sio kufanya kwa ajili ya
Dunia (kujionesha kwa watu kuwa una elimu). Allah Subhanahu Wataala amesema
katika Qur'ani:
الأحزاب:
٤
“Allah Hakumuwekea mwanadamu nyoyo mbili kifuani mwake”.
Na katika mithali (mfano) wa
ki Omani:-
“Haiwi kazi mbili katika kazi
moja”.
Na moyo ukigawanyika hauwezi
ukafika katika uhakika kwa hivyo imesemwa: “Elimu haikupi baadhi yake mpaka
uiipe (hiyo elimu) nafsi yako yote na ukiipa nafsi yako yote bado uko katika
hatari kuwa haitakupa baadhi yake.” Vile vile inampasa mwanafunzi amnyenyekee
(amheshimu) mwalimu wake amuachie yeye amuendeshee mambo yake na aone kuwa ni
heshima kubwa kumhudumia mwalimu wake ikiwajibika hali ya mambo kuwa hivyo,
kama ilivyohadithiwa kutokana na Zayd bin Thabit Radhi ya Allah iwe juu yake
alikuwa mazikoni basi akaletewa mnyama wake apate kumpanda. Akaja Ibn Abbas akashika
hatamu za yule mnyama kwa heshima ya Zayd bin Thabit R.A. Akamwambia mwachie
(hiyo hatamu) ewe mtoto wa ami yake (baba mdogo) Mtume wa Allah. Basi akamjibu
Ibn Abbas hivyo ndivyo alivyotuamrisha Mtume Salallahu Alayhi Wasalam
tuwafanyie wanavyuoni wetu. Hapo Zayd bin Thabit naye akambusu mkono wake (Ibn
Abbas) akasema na hivi ndivyo alivyotuamrisha tuwafanyie watu wa nyumba ya
Mtume wetu (Ahlu lbeit). Tizama unyenyekevu wa Ibn Abbas naye ni mtoto wa Ammi
wa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam na Zayd ni mtumwa katika watumwa wa Mtume
Salallahu Alayhi Wasalam pamoja na kuwa Ibn Abbas elimu yake si chini ya elimu
ya Zayd. Kujidhalilisha hakufai isipokuwa kwa mwanafunzi kumfanyia mwalimu
wake. Imetolewa hadithi kutokana na Mtume Salallahu Alayhi Wasalam : “Kujidhalilisha
sio katika tabia ya Muumini isipokuwa katika kutafuta elimu”. Imetolewa
kutokana na Shekhe Noor Diin Assalmy kuwa alikuwa akimfundisha mwanafunzi wake
Qaswarah bin Humood Arrashdiy akamwambia hii nafahamu basi hapo Shekhe
akanyamaza wala hakumjibu kitu lakini wakati aliporejea kutaka kufundishwa
akamwambia wewe mwenyewe wafahamu huhitajii mwalimu basi akamtia adabu kwa kosa
lake lile dogo, vipi basi kwa yule anaemjibu mwalimu wake majibu mabaya kabisa
mtu kama huyu anajiharimisha nafsi yake elimu. Na ilivyo sawa asione unyonge
kujifundisha kwa mtu yoyote na ikiwa yeye hataki kusoma isipokuwa kwa walimu
wakubwa wakubwa basi ni mjinga. Elimu ni sababu ya kuokoka na kupata raha na
imeandikwa katika kitabu cha “Ihyaa” : Amkimbiae mnyama mkali mwenye madhara,
ataka amle hatobagua nani amuonyeshe mahala pa kukimbia baina ya ajulikanaye na
watu au aliekuwa hajulikani na watu, kwa sababu yeye ataka kusalimisha maisha
yake, basi atakubali kuoneshwa pa kukimbilia na yoyote yule. Na moto ukali wake
na adhabu yake ni kubwa zaidi kuliko madhara na ukali wa mnyama yoyote, kwa
hiyo hekima ndiyo inayotafutwa na Muumini anaichukua popote atakapoipata na
kutoka kwa yeyote atakaemletea wamesema katika mfano walioutoa:-
“Elimu haimkubali kijana
mwenye kujitukuza kama maji ya mvua yasivyokubali pahala paliponyanyuka”.
Kwa ujumla wa maneno
mwanafunzi yeyote aliebakisha rai katika nafsi yake iliyo kinyume na rai ya
mwalimu wake basi mhukumie mwanafunzi huyo kutofuzu na kuwa atakhasirika.
Amejirudisha chini (kwa kujidhalilisha). Nabii wa Allah Subhanahu Wataala Musa
AS mbele ya Al-Khadhr AS wakati alipotaka kujifunza kwake akasema:
الكهف: ٦٦
“Je!
Nikufuate ili unifundishe katika ule uongofu (uongozi) uliofundishwa?”
Basi akaridhika kuwa mfuasi na
hali yeye ni Nabii wa Allah Subhanahu Wataala na Mtaalamu mkubwa kuliko wote
katika wakati wake. Imetolewa kutokana na Aliy bin Abi Talib kuwa amesema kweli
ni katika haki ya Mwanachuoni (Aalim) asikithirishiwe kuulizwa maswali wala
usimlazimishe kujibu maswali au ukimwuona ameingia uvivu usimrudishie swali au
akinyanyuka usimzuie kwa kumkamata nguo yake wala usimtolee siri yake wala
usimsengenye mtu mbele yake wala usimchunguze ili umtolee kasoro zake na hata
akikosea basi umkubalie udhuru wake na wajibu wako kumheshimu na kumtukuza kwa
kutaka radhi ya Allah Subhanahu Wataala madamu yeye afuata amri yake Subhanahu
Wataala. Usimtangulie kukaa na akihitajia kitu ukimbilie ili uwe wa kwanza
kumtimizia haja yake. Vile vile asiwache fani katika fani mbali mbali za elimu
ili ajaribu kujifundisha ijapokuwa kidogo kisha ikiwa Allah Subhanahu Wataala
atampa uwezo wa kuzielewa na kutamakani katika elimu hizi basi ajifundishe kwa
wasaa zaidi ama sivyo ajishughulishe kwa kile kilichokuwa muhimu na
ajitosheleze nacho na achukue katika fani nyinginezo kadiri ya kusalimika na
uadui wake kwani mtu ni adui wa kile alicho mjinga nacho (alichokuwa hakijui):
الأحقاف:
١١
“Na walipokosa kuongoka kwa haya basi wanasema: ‘Huu ni uongo wa
(watu wa) zamani’.”
Amesema Abu Attayib katika
shairi:
“Na aliekuwa mdomo wake
mchungu kwa ugonjwa, maji mazuri huyaona machungu”.
Kadhalika (mtafutaji elimu)
asiikusudie kwa maslahi ya Dunia bali aikusudie kwa kutaka radhi ya Mola
Subhanahu Wataala na kwa kutaka ipande daraja yake iwe sawa na Malaika na waliyekuwa
karibu katika waja wake Allah Subhanahu Wataala walio bora na waliochaguliwa
sio kwa kusudia ukubwa, mali, makazi, kubishana na wenye tabia mbaya na kutaka
kusifiwa na wanavyuoni. Kwani mwenye kujua na kutenda kwa mujibu wa elimu yake
kisha akafundisha basi huyo ndiye anaeitwa mtukufu katika ufalme wa Allah
Subhanahu Wataala huko mbinguni na kamathilishwa kama jua linaloangaza vitu
vingine nalo lina muangaza lenyewe na kama miski (aina ya mafuta mazuri) yatia
harufu vitu vingine na yenyewe ina harufu nzuri. Amma aliye na elimu na hatendi
kwa mujibu wa elimu yake kama daftari lampa faida mwengine nalo li tupu na kama
punda abebae vitabu (naye hafaidiki navyo hivyo vitabu) au kinoleo chanoa vitu
vingine (kisu ili kiwe kikali) lakini chenyewe hakikati au utambi wa fanusi
(kandili) waangazia vinginevyo lakini wenyewe waungua kama anavyotolewa mfano
mtu kama huyu kuwa yeye ni kama utambi wawashwa kuangazia watu nao waungua.
Basi mtu akijifunza na akafanya kwa mujibu wa hiyo elimu kisha akataka
kufundisha wengineo lazima awe na adabu ya mwalimu yaani awe na huruma na
wanafunzi wake na awafanye kama watoto wake kama katika hadithi aliyeitoa Abu
Huraira kutokana na Mtume Salallahu Alayhi Wasalam amesema: “Mimi kwenu nyinyi
ni kama baba na watoto wake”, akusudia kuwaokoa na moto wa Akhera nayo ni
muhimu zaidi kuliko wazee wawili kuwaokoa watoto wao na moto wa Dunia kwa hiyo
haki yake ni kubwa zaidi kuliko haki ya wazee wawili na juu ya mwalimu
asikusudie kufundisha kwake manufaa ya Dunia na yakapatikana hayo manufaa ya
Dunia basi yawe sababu yasiwe lengo ama lengo liwe kupata radhi ya Allah
Subhanahu Wataala. Wala asiwasumbulie wanafunzi wake kuwa yeye ana fadhila juu
yao ya kuwasomesha ijapokuwa kwa uhakika hii fadhila anayo juu ya wanafunzi
wake lakini asiwasumbulie bali aamini kuwa fadhila na utowaji wote ni wa Allah
Subhanahu Wataala ampa amtakaye na kuwa yeye kapewa na Allah hii neema ili
awafundishe waja katika waja wake waliojaaliwa wawe chini ya dhamana yake hata
awe yeye ndie sababu ya kutengeneza nyoyo zao ili wajikurubishe kwa Allah
Subhanahu Wataala. Mfano wake ni kama mtu
amekuazima ardhi ili uilime na uipande ikiwa wewe ndie uliofaidika kwa hivo
vipando basi fadhila yarudi kwa yule aliekuazima hiyo ardhi. Vile vile
wafananisha atafutae elimu kwa ajili ya Dunia mfano wake ni kama
asafishae soli ya viatu vyake kwa uso wake kwa hivyo kabadilisha mambo
amemfanya anaepasa kuhudumiwa kuwa ndie anaehudumu na anaehudumu kuwa ndie
anaehudumiwa. Inataka vile vile mwalimu kumkataza mwanafunzi wake mambo mabaya
kwa njia ya kificho ficho na hekima kadri iwezekanavyo bila kumtolea uwazi
hicho anachomkataza. Na vile vile kwa njia ya huruma.Kumfunulia wazi kwamfanya
huyo mwanafunzi ajasiri kukifanya hicho anachokatazwa na kupenda kuendelea
nacho. Amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam naye ni muongozi wa kila mwalimu
na kiongozi wa kila Muislamu “Lau kama wangalikatazwa watu kubanja kinyesi (cha
wanyama) basi wangekibanja na wakasema hatukukatazwa kufanya hivyo isipokuwa
kuna kitu ndani yake”. Ameitoa hadithi
hii Al-Ghazali katika kitabu chake “Ihyaa”. Alitangulia kufanya hivyo baba yetu
Adam pamoja na mkewe katika Al-Jannah kama alivyotwambia Allah Subhanahu
Wataala katika kitabu chake kitukufu.
Vile vile Mwalimu anaesomesha
somo fulani haitakiwi ayatie ubaya kwa mwanafunzi wake masomo mengine bali ampe
fursa ya kusoma lolote katika hayo analolitaka wala asimtumilie maneno magumu
asiyoyafahamu kwani hivyo kutamfanya alichukie hilo somo na kuvurugika akili yake. Mtume
Salallahu Alayhi Wasalam amesema “Hakuna mtu yeyote ataewazungumzia watu maneno
ambayo akili zao hazielewi isipokuwa huwa fitina kwa baadhi yao ”. Na katika shuruti la mwalimu awe afanya
(atenda) kwa mujibu wa elimu yake kisiwe kitendo chake kinyume na kauli yake.
Asema Al-Ghazaliy katika kitabu chake “Al-Ihyaa” “Elimu yapatikana kwa hoja ama
kitendo hupatikana kwa kuonekana na macho na wenye macho ni wengi zaidi (kuliko
wenye hoja) kwa hiyo yoyote anaekifanya kitu halafu akawakataza watu kukifanya
hicho kitu basi huwa sumu na hupotosha watu kwani wamfanyia maskhara watu na
wamtuhumu kisha hupata matamanio zaidi ya kufanya hicho alichowakataza na
husema kama si kitu kizuri asingekifanya.
Wanavyuoni wabaya ni katika
watu wanaoadhibiwa vikali sana
kuliko wote Siku ya Kiyama. Na wanaokusudiwa hapa ni wale wanaotumia elimu yao kwa kupata maslahi ya
Dunia na kupata ladha ya Dunia yoyote itakayokuwa hiyo ladha. Zimetolewa
hadithi nyingi kuhusika na jambo hili kama kauli yake Mtume Salallahu Alayhi
Wasalam :- “Hakika watu wenye adhabu kali sana
Siku ya Kiyama Mwanachuoni hakufaidika au Allah Subhanahu Wataala hakumfidi cho
chote na elimu yake”. Na asema vile vile : “Hawi mtu Mwanachuoni mpaka awe
afanya kwa mujibu wa elimu yake”. Na asema Elimu ni aina mbili elimu iko juu ya
ulimi basi hiyo hoja ya Allah Subhanahu Wataala kwa viumbe vyake na elimu iko
moyoni hiyo ndiyo elimu ifaayo. Asema: Katika wakati wa mwisho huwa watu
wanaoabudu ni wajinga na huwa wanavyuoni mafasiki” Asema Salallahu Alayhi
Wasalam:- “Msisome elimu ili mpate kuiringia kwa wanavyuoni au mpate kubishana
na watu wasio na tabia njema na mfanye nyuso za watu ziwatazame nyie kwa hiyo elimu basi anaefanya hivyo
ataingia Motoni”. Asema Salallahu Alayhi Wasalam:
(من كتم علماً عنده ألجمه الله بلجام من نار)
“Anaeficha elimu ikiwa kwake (haitoi kwa watu)
Allah Subhanahu Wataala atamfunga lijamu ya moto”
Na
Akasema Salallahu Alayhi Wasalam:-
( لأنا من غير الدجال أخوف
عليكم من الدجال فقيل وما ذاك فقال من الأئمة المضلين )
“Hakika mimi nawaogopea asiye Dajjal zaidi
kuliko Dajjal(mwenyewe) akaambiwa ni nani huyo? Akajibu Nawaogopea Maimamu
wapotezaji”
Na
akasema Salallahu Alayhi Wasalam:
(من ازداد علما ولم يزدد هدى لم يزد من الله
إلا بعدا )
“Anaezidi kuwa na elimu na
bila ya kuzidi uongofu hapati kitu
kutoka kwa Allah isipokuwa kuzidi kuwa mbali naye”(kuwa mbali na rehema zake)
Akasema
Al-Hassan: Usiwe katika wanaokusanya elimu ya wanavyuoni na hekima nzuri za
wenye hekima kisha watenda vitendo vya watu ovyo (wahuni). Mtu mmoja kamwambia
Abu Huraira:- Nataka kujifunza elimu lakini naogopa nisije nikaipoteza akasema
“inatosha kuacha kwako kufanya, kwa mujibu wa hiyo elimu, kuwa umeshaipoteza”.
Akasema Al-Khalil bin Ahmed: “Watu ni wanne, mtu ajua na ajua kuwa ajua basi
huyo ndie Mwanachuoni mfateni na mtu ajua na hajui kuwa ajua basi huyo amelala
mwamsheni, na mtu hajui na ajua kuwa hajui basi huyo ataka kuongozwa
muongozeni, na mtu hajui na hajui kuwa hajui basi huyo mjinga mkataeni”.
Amesema Sufyan Athowriy Elimu inaipigia makelele amali (kitendo) kuiita
ikiitikia ndio vizuri au sivyo inakwenda zake (elimu). Amesema Al-Hassan:- Rada
inayowapata Maulamaa (kuadhibiwa kwa sababu ya kuacha amali) ni kufa kwa moyo
na kufa kwa moyo ni kutaka Dunia kwa amali ya Akhera. Wamesema katika utenzi
wakimaanisha hayo kama ifuatavyo:-
Nimestaajabu
anaenunua upotevu kwa uongofu na ajabu zaidi anaenunua Dunia kwa Dini, na
anaestaajabisha zaidi kuliko hawa wawili anaeuza Dini yake kwa Dunia ya
mwengine.
Amesema
Usama bin Zayd radhi ya Allah iwe juu yake: “Nimemsikia Mtume Salallahu Alayhi
Wasalam akisema:-
( يؤتى بالعالم يوم القيامة فيلقي في النار
فتندلق أقتابه فيدور بها كما يدور الحمار بالرحى فيطيف به أهل النار فيقولون
مالك فيقول كنت آمر بالخير فلا آتيه وأنهى عن الشر وآتيه )
“Aletwa Mwanachuoni
Siku ya Kiyama kisha atupwa Motoni na yatatoka matumbo yake (yatamzongometa) na
atakuwa ayazunguka kama anavyokizunguka punda kinu (cha kusaga nafaka kama ngano nk.) na watampitia watu wa Motoni wakimuuliza
una nini? Basi atawajibu nilikuwa naamrisha kheri na mimi mwenyewe siifanyi na
nakataza shari na naifanya. Akasema Mtume wa Allah Subhanahu Wataala Eesa AS. Mfano wa wanavyuoni waovu ni kama
jiwe kubwa limeanguka kwenye mdomo wa mto halinywi maji wala haliachii maji
yende kwenye mimea, na mfano wa wanavyuoni wabaya ni kama mfereji (mchirizi) wa
maji watumiwa kunyweshea majani umejengwa na kubabiwa kwa jassi nje (wapendeza)
na ndani yake kuna uchafu, na kama makaburi nje yake au udhahiri wake ni jengo
na ndani yake mifupa ya wafu.
Katika
habari ya Nabii wa Allah Dawood AS anazungumzia alivyosema Allah Subhanahu
Wataala : “Kuwa kitu cha chini nitakachomfanyia Mwanachuoni ikiwa atatanguliza
mapendekezo yake kabla ya mahaba yangu (kunipenda mimi) ni kumharimishia
(kumnyima) ladha ya kuninon’goneza mimi. Ewe Dawood usimwuulize mwanachuoni
alieleweshwa na Dunia akupe habari yangu (Allah Subhanahu Wataala ) kwani
atakupotosha njia ya mapenzi yangu, hao ndio wakatao njia (kuwaibia watu)
wangu. Ewe Dawood ukimuona mtu anitaka Mimi basi kuwa (uwe) mtumwa wake, Ewe
Dawood alierudi kwangu huku akimbia nimemuandikia kuwa na ujuzi wa kuyapambanua
mambo (baina ya mazuri na maovu) na niliemuandikia hivyo (kuwa na ujuzi huo)
simuadhibu milele”. Amesema Saeed bin Al-Mussyab mkimuona Mwanachuoni
anawaendea maamiri (viongozi au wakubwa wa Dunia) basi huyo ni mwizi.
Amesema
mwanashairi:- Mchungaji mbuzi awalinda mbuzi wasiliwe na mbweha basi vipi ikiwa
hao wachungaji wenyewe ni mbweha.
Imesemwa
vile vile kuwa watu wote ni wafu isipokuwa wanavyuoni. Na wanavyuoni wote
wamelewa isipokuwa watendaji katika wao. Na watendaji wote wamedanganyika
isipokuwa wenye ikhlasi na mwenye ikhlasi yuko katika hofu mpaka ajue mwisho
wake (kifo) utakuwa nini.
Inapendeza
kwa Mwanachuoni asitoe fatwa mpaka aulizwe na asijibu ikiwa katika
waliohudhuria hapo yuko aliye na elimu zaidi kuliko yeye. Na mafundisho haya
kwa mwanafunzi ndiyo yampasa zaidi kuyafata kwani kujasiri kufanya hivyo
kunamletea kujihisi kuwa ni mtu mashuhuri basi inaogopewa kumletea hatari mtu
huyo. Baadhi ya Masahaba wamepita wakamkuta mtu awatolea watu muhadhara akasema
yule sahaba huyu awambia watu nijueni (yaani ataka umashuhuri). Na alikuwa Ibn
Omar RA asema: “Mwataka mutufanye sisi kuwa daraja mwavuuka juu yetu kwenda
Jahannam”. Alikuwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam mara nyingi akiulizwa ajibu
kwa kusema “Sijui” na Ibn Omar alikuwa akiulizwa maswali kumi hujibu moja na
huyanyamazia tisa. Nasema (maneno ya mtungaji) yameletwa maswali kwa Imam
Al-Khaliliy Allah Amrehemu akayajibu baadhi yake na akasema juu ya yaliobakia
“Allah ndie anaejua zaidi”.
Laletwa
suala kwa Sahaba nae humsukumia mwenzake na yeye vile vile humsukumia mwengine
na hivyo hivyo na pengine huenda likarudi kwa yule wa mwanzo na walikuwa
wakisukumiana mambo manne:-
Uimamu,
Wasiya, Amana na Kutoa fatwa na walikuwa wakijishughulisha na mambo matano:- Kusoma
Qur’ani, kuimarisha misikiti (kuishughulikia kwa jengo na kwenda kusali)
kumdhukuru Allah Subhanahu Wataala na kuamrishana mema na kukatazana mabaya kwa
mujibu walivyosikia kauli yake Mtume Salallahu Alayhi Wasalam “Kila maneno ya
binaadamu yana madhara naye hana faida nayo isipokuwa matatu kuamrisha mema,
kukataza mabaya na kumdhukuru Allah Subhanahu Wataala”. Kukaa kimya ndiyo rai
yao walioishikiliya na vile vile hali ya wenye elimu waliowafatilia isipokuwa
kwenye dharura na kwenye haja ya kuzungumza katika kuwaongoza na kuwafundisha
watu sio kwa kutaka umashuhuri Allah Awarehemu na Awaridhie.
Salman
Al-Farsiy amemuandikia Abi Addardaa awaridhie Allah Subhanahu Wataala na alikuwa Mtume Salallahu
Alayhi Wasalam ameunga udugu baina ya masahaba wawili hawa kamwandikia:- Ewe
ndugu yangu imenifikia habari kuwa umekuwa (umejiweka) mganga unawatibu
wagonjwa- amaanisha unawatolea fatwa
watu- basi tizama ikiwa ni mganga zungumza kwani maneno yako ni ponyo na ikiwa
unajifundisha uganga basi Allah Allah usije ukamuua Muislamu. Ikawa Abu Ddardaa
hajibu tena akiulizwa baada ya hapo. Uchaji Mungu ndio unaomiliki kila kitu na
kuihisabu nafsi ndiko kunakoizuia nafsi isende katika mambo ya upotofu. Na
kuipenda Dunia ndio kichwa cha kila kosa na kuchukua hadhari katika Dini ni
wajibu. Ameitoa (hadithi hii ifuatayo) Al-Haakim kutokana na Mtume wa Allah
Subhanahu Wataala :-
أن من خيارأمتي
قوما يضحكون جهرا من سعة رحمة الله ويبكون سرا من خوف عذابه أبدانهم في الأرض
وقلوبهم في السماء، أرواحهم في الدنيا وعقولهم في الآخرة يتمشون بالسكينة ويتقربون
بالوسيلة
"Hakika katika bora wa Umma
wangu, ni watu wachekao wazi wazi (waonekana na watu) kwa wingi wa rehema ya
Allah na walia kisirisiri kwa kuogopa adhabu yake, miili yao iko ardhini na
nyoyo zao ziko mbinguni, roho zao ziko Duniani na akili zao ziko Akhera
watembea kwa utulivu na wajikurubisha kwa kila njia za kheri".
Haitakiwi
Mwanachuoni akithirishe kucheka kwani huko kwaleta tabia ya kutokuwa na utulivu
(waqaar) na elimu lazima iandamane na tabia hii na Mwanachuoni haibebi elimu
isipokuwa mwenye tabia hii nzuri. Alikuwa Shekhe Noor Diin Assalmiy mara
nyingine chamjia kicheko sana
basi siku moja Mwanachuoni mkubwa Sheikh Muhammed bin Masoud Assaiidiy
akamwambia baada ya kumsikia kucheka:- “Mwanachuoni akicheka kicheko huitupa
elimu yake mtupo” yaani (humpotea) basi yasemekana alilia Sheikh alivyosikia
maneno hayo na hakuonekana tena baada ya hapo kucheka.
Inasemekana mambo matano
(tabia tano) ni katika alama za wanavyuoni wa Akhera na hizi zinaeleweka katika
Aya tano katika kitabu cha Allah Subhanahu Wataala ya kwanza ni kumuogopa Allah
Subhanahu Wataala na hii iko katika kauli yake:
فاطر:
٢٨
“Kwa hakika wanaomuogopa Allah miongoni mwa
waja wake ni wale wataalamu (wanavyuoni).
Na
alama ya pili ni unyenyekevu kutokana na kauli yake Mola Subhanahu Wataala:
آل
عمران: ١٩٩
“Kwa
kumnyenyekea Allah. Hawabadili Aya za Allah kwa thamani ndogo (ya Dunia).”
Alama
ya tatu ni kujidhalilisha kwa Waislamu (tawaadhuu) kutokana na kauli yake Allah
Subhanahu Wataala:
الحجر: ٨٨
“Na inamisha bawa lako kwa wanaoamini
(uwafunike kama kuku na ndege wengine
wanavyofunika watoto wao kwa kuwaonea huruma)”
Alama
ya nne ni tabia njema kutokana kauli yake:
آل عمران:
١٥٩
“Basi kwa sababu ya rehema itokayo kwa Allah umekuwa
laini kwao (Ewe Muhammad)”
Alama
ya tano ni kutokuipa mbele Dunia na kuishughulikia Akhera (Azzuhd)
القصص:
٨٠
“Na
wakasema wale waliopewa elimu: Ole wenu! Malipo ya Allah ni mazuri kwa yule
anayeamini na kufanya vitendo vizuri (kuliko aliyonayo huyu Karuni)”
الأنعام:
١٢٥
“Basi yule ambaye Allah anataka kumwongoza,
humfungulia kifua chake Uislamu. Na yule ambaye Allah anataka kumhukumu kupotea
hufanya kifua chake kuwa kizito kinaona tabu kubwa (kufuata huo Uislamu).” Aya 125
Al-Anaam.
Wakati
Mtume Salallahu Alayhi Wasalam aliposoma Aya hiyo hapo juu akaulizwa maana ya
tafsiri yake akasema “Hakika nuru ikitupwa moyoni basi kifua cha mtu huyo
chaifungukia nuru hiyo na kikapanuka.” Akaulizwa je kitu hicho huwa na alama
yoyote? Akasema “ndio kuipa mgongo nyumba idanganyayo (Dunia) na kuielekea
nyumba ya milele (Akhera), na kujitayarisha na mauti kabla ya kufika”. Na
anatakiwa mwanafunzi akusanye kila elimu ijapokuwa kidogo hata achukue kutokana
na vitabu vya Mayahudi na Manasara na waliotoka katika Dini hata aijue kheri
apate kuifuata na aijue shari apate kuiwacha.
Imesemwa:-
Nimetaka kuijua shari sio kwa kuifanya hiyo shari bali kujiepusha nayo na
aliekuwa hawezi kuifafanua shari kutokana na kheri basi huanguka ndani yake
(shari).
Amesema
Hudheifa bin Al-Yamani RA “Amenihusisha Mtume wa Allah Subhanahu Wataala kwa
kunipa elimu ambayo hakumwambia mtu yeyote mwingine isipokuwa mimi na hivyo kwa
sababu watu wamuuliza juu ya kheri na mimi namuuliza juu ya shari kwa kuogopa
nisije nikaifanya kwani kheri haiwezi ikanishinda kuijua”. Na mara moja
akasema: “Hakika nimejua kuwa aliekuwa haijui shari hawezi kuijua kheri. Na
alikuwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam amemkhusisha kuwajua Wanafiq na kujua
elimu ya Unafiqi na sababu zake na mambo yanayoleta fitina na alikuwa aitwa
“mwenye siri” (sahib Assir).
Elimu
haipatikani isipokuwa kwa akili na sharafu ya akili ni kubwa sana . Asema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam
“Enyi watu tieni akili hata muyaelewe yanayotoka kwa Mola wenu Subhanahu
Wataala, na usianeni kutumia akili ili muyajue mlioamrishwa na mliyokatazwa, na
jueni kuwa akili itawapa habari itokayo kwa Mola wenu. Na jueni mtu mwenye
akili ni mwenye kumtii Allah ijapokuwa sura yake mbaya, daraja yake ni ndogo na
ya chini na hajishughulikii madh-hari yake. Na mjinga ni yule anayemwasi Allah
ijapokuwa sura yake nzuri mwenye kujulikana sana daraja yake kwa watu ni kubwa, mtokeo
wake mzuri, fasihi katika kuzungumza kwani nyani na nguruwe wana akili zaidi
kwa Allah Subhanahu Wataala kuliko wanaomuasi. Wala usidanganyike kwa
kuwatukuza watu wa Dunia yeyote atakaekuwa kwani wao ni miongoni mwa
waliokhasirika”. Ameitoa Abu Huraira: Na Amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam
:- “Kitu cha kwanza Alichokiumba Allah Subhanahu Wataala ni akili Akaiambia
nikabili ikamkabili (ikamjia). Kisha Akaiambia rejea ikarejea kisha Akasema:
Naapa kwa shani yangu na kwa Utukufu wangu sikuumba kiumbe chenye heshima zaidi
kwangu kuliko wewe. Kwako nachukua na kwako natoa na kwako natoa malipo mazuri
na kwako natoa malipo mabaya” ameitoa hadithi hii Aisha RA. Na amesema Mtume
Salallahu Alayhi Wasalam :- “Hakika mjinga asibu (kwa kufanya uharibifu) kwa
ujinga wake zaidi kuliko fasiki anavyofanya kwa ufasiki. Na hakika watapanda
waja vyeo vya juu mbele ya Mola wao kesho kwa kadiri ya akili zao, ameitoa
Attirmidhiy. Akasema Salallahu Alayhi Wasalam: “Hakika mtu atafikia kwa tabia
yake njema daraja ya anaefunga, anaesali sala za usiku, na haitimu mtu tabia
yake njema mpaka kwanza itimu akili yake. Basi hapo itatimia imani yake na kuwa
mtiifu kwa Mola wake na kumuasi adui yake Ibliis, ameitoa Attirmidhiy kutokana
na Aisha. Amesimulia Ibn Abbas RA kuwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam amesema:
Kila kitu kina ala (ya kukihifadhi) na matayarisho makubwa ya Muumini ni akili
na kila kitu kina tandiko na tandiko la mtu ni akili na kila waja wana nguzo na
nguzo tukufu ya Dini ni akili na kila watu wana lengo na lengo la waja ni akili
na kila watu wana mwitaji na mwitaji wa
wanaoabudu ni akili na kila tajiri ana bidhaa na bidhaa ya wanaojitahidi ni
akili na kila wenye nyumba wana nidhamu na nidhamu ya nyumba za Masiddiqiin ni
akili na kila kilichoharibika chafanyiwa matengenezo na matengezo ya Akhera ni
akili na kila mtu huacha baada yake kitu anachonasibishiwa nacho, na
wanachonasibishwa Masiddiqiin na kuzungumziwa nacho ni akili, na kila safari
ina kituo chake (mahala inapoanzia) na kituo cha Waumini (umuhimu wao na ubora
wao) ni akili. Na akasema Salallahu Alayhi Wasalam vile vile :- “Aliekuwa
imetimia akili yake zaidi miongoni mwenu ni yule mwenye hofu zaidi na mbora
zaidi wenu katika kuyafikiria yale ninayowaamrisha na ninayowakataza ijapokuwa yeye ni mpungufu wenu katika
kufanya mambo ya utiifu (ya kujikaribisha kwa Allah Subhanahu Wataala”. Ameitoa
hadithi hii Abu Qatada. Na hadithi za Mtume na athari zake katika heshima ya
akili ni nyingi sana . Na amesema Bwana wa Maimamu Allah
amrehemu katika kitabu chake “Ad-Dhahab Al-khaalis”: Akili kwa wengi kati yetu
ni nguvu na hoja katika moyo na ni kama kuona katika jicho basi kwa hivyo ni
kitu kilichokuwa hakionekani wala hakihisiwi lakini kipo katika viungo vya mtu
(hakijulikani mahala pake maalumu) isipokuwa(hakipo) katika chini ya miguu
(nyayo) na utupu. Nimesema : Wametaja wenye elimu mambo ya akili waliyoyataja
na mja hana uhodari wa kuipata bali ni hadhi anayopewa mja na Bwana wa mabwana.
Hakuna
kitu bora baada ya elimu kuliko
kumdhukuru Allah Subhanahu Wataala na mahala wanapokutanika wampendao Allah ili
wamdhukuru. Na bora katika dhikiri ni kusoma Qur’ani na kumnyenyekea Allah
Subhanahu Wataala kwa kumuomba mahitajio yote kama
alivyotaka tufanye hivyo katika kauli yake:
غافر: ٦٠
“Niombeni nitakupeni”
Na
kauli yake:
البقرة:
١٨٦
“Basi Mimi niko karibu nao. Naitika maombi ya
muombaji anaponiomba”
Vile
vile ameonyesha fadhila ya kumdhukuru Allah Subhanahu Wataala:
البقرة:
١٥٢
“Basi nikumbukeni (kwa kunishukuru kwa hii
niliyokuneemesheni ya kukuleteeni Mtume) (Nami) nitakukumbukeni.”
Na
kauli yake:
الأحزاب:
٤١
“Mkumbukeni Allah kwa wingi.”
Na
kauli yake:
آل عمران:
١٩١
“Ambao humkumbuka Allah wakiwa wima na wakikaa
na wakilala.”
Na
kauli yake:
النساء:
١٠٣
“Mwishapo
kusali kuweni mnamkumbuka Allah Subhanahu Wataala (vile vile) msimamapo na
mkaapo na (mlalapo) ubavu.”
Amesema
Ibn Abbas Allah awaridhie (wote wawili) yaani (maana ya Aya hii) usiku na
mchana na bara na baharini na katika safari na ukiwa mjini kwako na katika
utajiri na ufakiri na maradhi na siha (afya) na siri na dhahiri.
Na
kauli yake:
الأعراف:
٢٠٥
“Na
mtaje Mola wako moyoni mwako kwa unyenyekevu na khofu na bila ya kupiga kelele
katika kauli yako hiyo (usemi wako huo; mkumbuke Mola wako umtaje) asubuhi na
jioni, wala usiwe miongoni mwa walioghafilika.”
Na
kauli yake:
العنكبوت:
٤٥
“Na kwa yakini kumbuko la Allah (lililomo ndani ya Sala)
ni (jambo) kubwa kabisa (la kumzuilia mtu na mabaya).”
Na
Allah Subhanahu Wataala amewakosoa wanafiki kuwa hawamtaji Allah Subhanahu
Wataala Aksema:
ﭽ
ﮆ ﮇ ﮈ
ﮉ ﮊ ﭼ
النساء:
١٤٢
“Wala hawamtaji Allah ila kidogo”.
Na
imetokana na Mtume Salallahu Alayhi Wasalam katika kuwahimiza watu kumkumbuka
(kumtaja) Allah kauli yake:- “Anaemtaja Allah kwenye watu walioghafilika nae ni
kama mti uliokuwa kati ya kuni (miti iliokauka
inayovunjikavunjika)”. Na asema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam kutokana na Allah
Subhanahu Wataala “Mimi niko pamoja na mja wangu madamu anitaja na aharakisha
midomo yake miwiwli (wa juu na wa chini) kunitaja ”. Akasema Mtume Salallahu
Alayhi Wasalam : “Hakufanya binadamu kitendo kinachomuepusha zaidi na adhabu ya
Allah kuliko kumtaja Allah Subhanahu Wataala. Wakasema (Masahaba) Ewe Mtume wa
Mungu hata jihadi katika njia ya Mungu, akasema (kujibu) hata jihadi katika
njia ya Mungu, isipokuwa upige kwa upanga wako mpaka uvunjike kisha upige kwa
upanga wako mpaka uvunjike”, ameitoa hadithi hii Attabaraniy. Kutokana na
Muaadh amesema Mtume -rehema za Allah na amani zimshukie:- “Anaependa
kupandishwa (daraja) katika mabustani ya Peponi basi akithiri kumtaja Allah
Mwenye nguvu na utukufu. Na akaulizwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam kitendo
gani kilicho bora akasema “Ufe na ulimi wako bado ungali maji maji kwa kumtaja
Allah”. Asema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam katika hadithi Qudusiy: Akinitaja
mja wangu katika nafsi yake Nami namtaja katika nafsi yangu na akinitaja katika
mkusanyiko Nami namtaja katika mkusanyiko bora zaidi kuliko mkusanyiko wake na
akijikaribisha kwangu shubiri Nami najikaribisha kwake dhiraa na akajikaribisha
kwangu dhiraa Nami najikaribisha kwake pima na akija kwangu
(atembea) Mimi namkimbilia” Imekubaliwa. Na katika hadithi ya Abu Huraira, na
maana ya kumkimbilia kumjibu maombi yake upesi kama
kusema na : مكر الله maana yake niqma yake, ومكروا ومكر الله na
hii kwa kiarabu inaitwa “Mushaakala”.
Na
hadithi : Saba
(watu) Allah awafunika katika kivuli chake siku iliokuwa hakuna kivuli
isipokuwa kivuli chake. Katika jumla ya hao saba mtu amemtaja Allah peke yake
(kando yaani mbali na watu) yakamtoka machozi kwa kumuogopa Allah. Na Asema:
Inayemshughulisha dhikiri yangu badala ya kuniomba mie nampa zaidi kuliko
ninavyowapa wanaoniomba. Na katika hadithi Qudusiy: “Mja wangu nitaje baada ya
Sala ya asubuhi saa na baada ya Sala ya Al-Asri saa Nami nitakutosheleza
kilicho baina ya Sala mbili hizo.” Imetolewa (hadithi) kutokana na Muadh RA
amesema “Hawajutii watu wa Al-Janna kitu isipokuwa wajutia saa iliyowapitia
bila ya kumtaja Allah Subhanahu Wataala ndani yake”. Amefikisha Sheikh wetu
Bwana wa Maimamu Allah Amrehemu (Sheikh Muhammed bin Yusuf Attfeish) kuwa
inapendeza kwa anaekaa katika kikao cha dhikiri (kumbuko) aseme kama alivyosema
Assidiq RA:
(
أشهد أن لا إله إلا الله وحده لا شريك له وأن محمدا عبده ورسوله
أشهد أن الدين كما شرع وأن إلاسلام كما وصف وأن الكتاب كما نزل وأن القول كما حدث
وأن الله هو الحق المبين ذكر الله محمداً بخير وصلى عليه وحياه بالسلام )
Kisha
akafasiri baadhi ya maneno yaliyo kuja hapa juu كما شرع yaani hukumu za sharia na والدين كما وصف yaani kutekeleza hukumu hizo na القول كما حدث
yaani kuifasiri Qur’ani tafsiri nzuri bila ya kuwa na mpingano au kumfananisha
Allah Subhanahu Wataala na baadhi ya viumbe vyake kama kufasiri الوجه kuwa ni dhati ya Allah na اليد kuwa ni Uwezo wa Allah
Subhanahu Wataala na الاستواء kuwa ni kushinda (Allah ni
Mshindi wa kila kitu).
Na
wakiwa jamaa wako katika kikao cha dhikiri na akawajia mtu aliekuwa katika
msimamo wa Dini mzuri na wamemchukulia kuwa ni Waliy katika Dini yake (yaani
wampenda kwa ajili ya Allah na kumuombea rahma na maghufira) basi ni wajibu wao
akiwajia mtu kama huyu kusogea na kumuekea nafasi ili akae na aambiwe kuwa hiyo
ni heshima kwa ajili ya uchaji wa Mungu aliokuwa nao na anaemkirimu
(kumheshimu) mtu kama huyu (mutawalla) kama aliekomboa mtumwa. Lakini kwa
upande mwingine akijiona kuwa haya anayofanyiwa kuwa ni kiasi chake (astahiki)
basi hapo kajiangamiza, kama ilivyosemwa: ameyafikisha Bwana wa Maimamu:
Anaejidai ana fadhila basi huyo anafedheha na anaejidai ana tabia nzuri basi
huyo ana tabia mbaya n.k. na lengo la maneno haya ni kuwa mwenye sifa nzuri
kweli kweli hajisifu bali yeye kinyume ya hayo ajiona kuwa ana kasoro ijapokuwa
akisifiwa na watu. Anaecheka katika kikao kama hicho basi hana thawabu yoyote
na aondoke kisha arudi tena kwani kicheko kinaua moyo na kinaondoa nuru ya uso
na anaetaka apate malipo mazuri aseme kila akiondoka kwenye kikao cha dhikiri
au mkutano:-
(
سبحان ربك رب العزة عما يصفون وسلام على المرسلين والحمد لله رب العالمين ، سبحانك
اللهم وبحمدك أستغفرك وأتوب إليك
اللهم اغفر
لي ذنوبي وتب علي )
Ametoa
Muslim katika hadithi ya Abi Huraira kutokana na Mtume Salallahu Alayhi Wasalam
Amesema:-
( ما جلس قوم مجلساً يذكرون الله عز وجل إلا
حفت
بهم الملائكة وغشيتهم الرحمة وذكرهم الله
تعالى فيمن عنده )
“Hawakai
watu kikao wakamtaja Allah Subhanahu
Wataala isipokuwa Malaika wawatanda na inawajia Rehma na Allah Subhanahu
Wataala anawataja kwa wale aliekuwa nao (Malaika)”.
Vile
vile kutokana nae amesema kasema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :
( ما قعد قوم مقعدا لم يذكروا الله سبحانه وتعالى
فيه ولم يصلوا على النبي صلى الله عليه وسلم إلا كان عليهم حسرة يوم القيامة )
“Hawakukaa watu kikao ikawa hawakumtaja humo
Allah Subhanahu Wataala wala hawakumsalia Mtume Salallahu Alayhi Wasalam
isipokuwa inakuwa majuto kwao Siku ya Kiyama”.
Inasemekana
kuwa muombaji (Dua) akiomba na akamsalia Mtume Salallahu Alayhi Wasalam kabla
ya Dua na baada yake hujibiwa (hukubaliwa) kwa sababu Allah akubali Sala ya
Mtume kwa hali yoyote basi haiwezekani airudishe kilichoombwa (Dua) baina ya
Sala mbili hizo isipokuwa ikiwa kuna upungufu kwa mja kama mfano aombe kitu
kilichokuwa haiwezekani kukiomba au bila ya Ikhlaas au bila ya kuwa na yakini
ya kujibiwa maombi, basi yote haya yakiwepo Allah hamtakabalii mja wake Dua.
Kumsalia Mtume Salallahu Alayhi Wasalam ni fardhi kwa mujibu wa amri ya Allah Subhanahu
Wataala kwa waja wake kufanya hivyo katika kauli yake:
الأحزاب: ٥٦
“Hakika Allah anamteremshia
rehema Mtume, na Malaika wake (wanamuombea Dua kwa vile vitendo vizuri
alivyovifanya) Basi; enyi Waislamu (mliopata neema hii ya kufundishwa haya na
Mtume) msalieni (Mtume muombeeni rehema) na muombeeni amani”.
Na katika kumsalia Mtume
Salallahu Alayhi Wasalam kuna fadhila kubwa iliyokuwa haiwezi kukadiriwa. Na
zimekuja hadithi nyingi juu ya suala hili na zifuatazo ni katika hadithi hizo:-
“Amekuja Mtume Salallahu Alayhi Wasalam siku hiyo na bishara nzuri yaonekana
katika uso wake basi akasema Salallahu Alayhi Wasalam Hakika amenijia Jibriil
AS akasema:- Huridhiki ewe Muhammad kuwa hakusalii mtu katika Umma wako Sala
moja isipokuwa nami Namsalia (anaesali hapa ni Allah Subhanahu Wataala ) Salaa
kumi (yaani Anamteremshia mja wake rehema). Na hakusalimii mja katika Umma wako
(hakuombei amani) isipokuwa nami namsalimia mara kumi. Amesema Mtume Salallahu
Alayhi Wasalam Hakika watu wa kwanza kwangu (waliokuwa karibu yangu kwa daraja)
ni wale wanaonisalia mie zaidi. Ametoa Arrabii, rehema za Allah ziwe juu yake,
katika musnadi yake ya juu (kitabu chake) kutokana na Abu Ubaidah kutokana na
Jabir bin Zayd kutokana na Ibn Masoud kasema:- Ametujia Mtume Salallahu Alayhi
Wasalam katika majlis ya Saad bin Ubaada akamwambia Shibr Ibn Saad:
Ametuamrisha Allah Subhanahu Wataala tukusalie basi vipi tukusalie. Akanyamaza
Mtume Salallahu Alayhi Wasalam hata tukasahau kuwa amemuuliza kitu kisha
akasema semeni:
(
اللهم صل على نبينا محمد وعلى آل محمد كما صليت على إبراهيم وبارك على محمد وعلى
آل محمد كما باركت على إبراهيم في العالمين إنك حميد مجيد والسلام كما قد علمتم )
Basi
baada ya Mtume Salallahu Alayhi Wasalam kutaja namna ya kumsalia akasema mwisho
wake “Na Salamu kama mlivyokwisha ijua” Arrabii akasema hapo Abu Ubaidah
akasema:
(
السلام عليك أيها النبي ورحمة الله وبركاته كما علمناه )
Na kuomba maghufira ya
madhambi ni wajibu baada ya kuyaacha madhambi hayo kwa kauli yake Mola aliyetukuka:-
آل عمران: ١٣٥
“Na
ambao wanapofanya uchafu (kufanya dhambi kubwa) au kudhulumu nafsi zao (kwa
dhambi ndogo) humkumbuka Allah na kuomba msamaha kwa dhambi zao.”
Na
kauli yake Subhanahu Wataala:
النساء: ١١٠
“Na
mwenye kutenda uovu (wa kuchukiza wenziwe) au akajidhulumu nafsi yake (kwa
kufanya kosa la kumdhuru mwenyewe tu) kisha akaomba maghufira kwa Allah,
atamkuta Allah ni Mwenye kughufiria na Mwenye Kurehemu. (lakini pia na awatake
msamaha hao aliowakosa mpaka waridhike)”.
Na
kauli yake Subhanahu Wataala:
الذاريات: ١٧ – ١٨
“Walikuwa wakilala kidogo tu usiku. Na wakiomba
maghufira (msamaha) nyakati za kabla ya alfajiri.”
Alikuwa Mtume Salallahu Alayhi
Wasalam akithirisha kusema:-
(
سبحانك اللهم وبحمدك اللهم اغفر لي إنك أنت التواب الرحيم )
Na
akasema:
( من
أكثر من الاستغفار جعل الله عز وجل له من كل هم فرجا ومن كل ضيق مخرجا ورزقه من
حيث لا يحتسب )
“Mwenye kuomba maghufira kwa wingi basi Allah
humjaalia faraji kwa kila huzuni (au uzito wa moyo) na humtoa katika kila dhiki
na humruzuku pale asipopafikiria.”
Na
akasema Salallahu Alayhi Wasalam:-
( إني أستغفر الله وأتـوب إليه في اليوم
سبعين مرة )
“Hakika mimi namuomba Allah maghufira na
natubu kwake mara sabini kila siku”.
Na
akasema :-
( إنه ليغان على قلبي حتى أني لأستغفر الله
تعالى في كل يوم مائة مرة )
“Hakika inanijia shaka katika moyo wangu mpaka
nikaomba maghufira kwa Allah Subhanahu Wataala mara mia kila siku”.
Na
alikuwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam husema katika kuomba maghufira:-
(
اللهم اغفر لي خطيئتي وجهلى وإسرافي في أمري
وما أنت أعلم به مني اللهم اغفر لي هزلي وجدي وخطئي وعمدي وكل ذلك عندي اللهم اغفر
لي ما قدمت وأخرت وأسررت وأعلنت وما أنت أعلم به مني أنت المقدم وأنت المؤخر وأنت
على كل شيء قدير )
Na
kutokana na Aliy amesema:-
Amenizungumzia
Abu Bakr na amesema kweli Abu Bakr, Radhi za Allah ziwe juu yake, amesema
nimemsikia Mtume Salallahu Alayhi Wasalam akisema:-
( ما من عبد يذنب ذنباً فيحسن التطهر ثم يقوم
يصلي ركعتين ثم يستغفر الله عز وجل إلا غفر له)
“Hakuna mja yeyote afanyaye dhambi kisha
akajitoharisha vizuri na akasali rakaa mbili kisha akamuomba Allah Subhanahu Wataala
maghufira isipokuwa hughufiriwa madhambi yake”
Kisha akasoma kauli ya Mola
Mtukufu:-
آل
عمران: ١٣٥
“Na ambao wanapofanya uchafu (kufanya
dhambi kubwa) au kudhulumu nafsi zao (kwa dhambi ndogo) humkumbuka Allah na
kuomba msamaha kwa dhambi zao.”
Amesimulia Abu Huraira
kutokana na Mtume Salallahu Alayhi Wasalam kuwa amesema:-
( إن المؤمن إذا أذنب ذنبا كانت نقطة سوداء في قلبه فإن تاب ونزع
واستغفر صقل قلبه عنه فإن زاد زادت حتى تغلف
قلبه )
“Hakika muumini akifanya dhambi hufanyika doa
jeusi katika moyo wake akitubu na kuacha (hilo dhambi) na akaomba maghufira
wasafishwa moyo wake kutokana na hilo doa lakini akizidi (kufanya hilo dhambi)
lazidi hilo doa (kuwa kubwa) mpaka lafunika moyo wake”.
Basi hiyo ndiyo "الران"
aliyotaja Allah Subhanahu Wataala katika kitabu chake:
المطففين:
١٤
“Sivyo hivyo! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao (maovu mpaka
yakaufunika moyo) waliyokuwa wakiyachuma”.
Kinga iliyopokewa kutokana na
Mtume Salallahu Alayhi Wasalam ni kama ifuatavyo:-
(
اللهم إني أعوذ بك من البخل وأعوذ بك من الجبن وأعوذ بك من أرد إلى أرذل العمر وأعوذ بك من فتنة الدنيا وأعوذ بك من عذاب
القبر اللهم إني أعوذ بك من طبع يهدي إلى
طمع ومن طمع في غير مطمع ومن طمع حيث لا
يطمع اللهم إني أعوذ بك من علم لا ينفع
وقلب لا يخشع ودعاء لا يسمع ونفس لا تشبع وأعوذ بك من الجوع فإنه بئس الضجيع ومن الخيانة فإنها
بئست البطانة ومن الكسل والبخل والجبن
والهرم ومن فتنة الدجال ومن فتنة المحيا والممات
اللهم إني أعوذ بك من التردي وأعوذ بك من الغم والغرق والهدم وأعوذ بك من
أن أموت في سبيلك مدبرا وأعوذ بك من أن أموت في تطلب الدنيا اللهم إني أعوذ بك من
شر ما علمت ومن شر ما لم أعلم اللهم إني أعوذ بك من جهد البلاء ودرك الشقاء وسوء
القصاء وشماتة الأعداء اللهم إني أعوذ بك من الكفر والدين والفقر وأعوذ بك من عذاب
جهنم اللهم إني أعوذ بك من شر سمعي وبصري ومن شر لساني وقلبي اللهم إني أعوذ بك من
جار السوء في دار المقامة فإن جار البادية يتحول اللهم إني أعوذ بك من القسوة
والغفلة والعيلة والذلة والمسكنة وأعوذ بك من الفسوق
والشقاق والنفاق وسوء الأخلاق وضيق الأرزاق والسمعة والرياء وأعوذ بك من الصم
والبكم والعمى والجنون والجذام والبرص وسيئ الأسقام اللهم إني أعوذ بك من زوال
نعمتك ومن تحول عافيتك ومن فجاءة نقمك ومن جميع سخطك اللهم إني أعوذ بك
من فتنة الغنى وشر فتنة الفقر وشر فتنة المسيح الدجال وأعوذ بك من الغرم والمأثم
اللهم إني أعوذ بك من صلاة لا تنفع ودعوة لا تستجاب وأعوذ بك من سوء العمر وفتنة
الصدر. وصلى الله على سيدنا محمد وعلى كل عبد مصطفى من كل العالمين آمين )
Na
anapotoka nyumbani inasemekana alikuwa akisema kama ifuatavyo:-
(
اللهم إني أعوذ بك أن أظلم أو أظلم أو أجهل أو يجهل علي ، بسم الله الرحمن الرحيم
ولا حول ولا قوة إلا بالله العلي العظيم ، بسم الله ، التكلان على الله )
Na
akiona mwezi umeandama husema:-
(اللهم أهله علينا بالأمن و الإيمان والبر
والسلامة
والإسلام والتوفيق لما تحب وترضى والحفظ ، ربي وربك الله )
Na
vile vile asema:-
( هلال رشد وخير آمنت بخالقك )
Na
katika Musnadi Arrabii imeandikwa kuwa akiona mtu mwezi umeandama hupiga
takbira mara tatu kisha husema:-
اللهم إني أسألك خير هذا الشهر وخير
القدر وأعوذ بك من شر يوم الحشر )
Na
akiogopa watu husema:-
(اللهم إنا نجعلك في نحورهم ونعوذ بك من
شرورهم )
Na
akipatwa na fikira (kitu cha kumshughulisha) husema:-
(
اللهم إني عبدك ابن عبدك ابن أمتك ناصيتي بيدك ماض في حكمك عدل في قضاؤك أسألك بكل اسم هو لك
سميت به نفسك أو أنزلته في كتابك أو علمته أحداً من خلقك أو استأثرت به في علم الغيب عندك أن تجعل
القرآن ربيع قلبي ونور صدري وجلاء غمي
وذهاب حزني وهمي )
Amesema
Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :- Hapatwi mtu na huzuni akasema maneno haya
isipokuwa Allah Subhanahu Wataala amuondolea fikira zake (zinazomshughulisha na
kumtia wasi wasi) na amletea badala yake faraji akaambiwa: Ewe Mtume wa Allah
je tujifundishe (maneno hayo) akasema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-
“Bali
inampasa anayeyasikia ajifundishe”.
Na
ukipata maumivu katika mwili wako basi eka mkono wako katika hapo mahala penye
maumivu kisha useme:-
mara
tatu
بسم الله
na
mara saba أعوذ بعزة الله وبقدرته من شر ما أجد
Na
ukitaka kulala useme:
(
اللهم إنك خلقت نفسي وأنت تتوفاها لك مماتها ومحياها اللهم إن أمتها فاغفر
لها وإن أحييتها فاحفظها ، اللهم إني أسألك العافية في الدنيا والآخرة ، باسمك ربي
وضعت جنبي فاغفر لي ذنبي ، اللهم قني عذابك يوم تجمع عبادك ، اللهم أسلمت نفسي
إليك ووجهت وجهي إليك وفوضت أمري إليك وألجأت ظهري إليك رغبة ورهبة إليك لا ملجأ
ولا منجا منك إلا إليك آمنت بكتابك الذي
أنزلت ونبيك الذي أرسلت )
Katika
Ad-dhahab (kitabu) cha Sheikh Mohammed bin Yusuf Attfeish Imam wa maimamu:
Lazima mtu awe na “khofu na matarajio” na yawe sawa sawa (yaani lazima mtu
aogope adhabu ya Allah Subhanahu Wataala ambayo ni Moto wa Jahannam na atarajie
rehma yake Subhanahu Wataala ambayo ni Janna na asawazishe katika moyo wake
baina ya mambo haya mawili) kwa kila iliyomuangukia taklifu juu yake hata ikiwa
yeye ni mtiifu kabisa kama Nabii na Malaika na khofu ya Manabii ni khofu ya
malipo na mwisho (yaani waogopa mwisho usiwe mbaya) na ijapokuwa wameahidiwa
kupata malipo mazuri lakini ni shani ya mtu mtiifu na mzuri kadiri
atakavyofanya aona bado hajafanya kitu kwa vile anavyojua haki nyingi sana za
Allah Subhanahu Wataala zilivyokuwa juu yake na ihsani yake juu yao. Na anasema
Rafiki wa Allah (Ibrahim) AS katika Dua yake:-
إبراهيم:
٣٥
“Uniepushe mimi na wanangu na kuabudu masanamu”
Na
kauli yake:-
الإسراء:
٥٧
“Hao wanaowaomba (wenyewe) wanatafuta
ukaribiano na Mola wao”
Na
kauli yake:-
الأنبياء:
٩٠
“Na wakituomba kwa shauku na
khofu”
Basi
hao ni Manabii na watu wa kawaida wao ndio wa kwanza wanaopaswa kusawazisha
baina ya khofu na matarajio kwani ikimzidia khofu aogopewa kukata tamaa.
يوسف:
٨٧
“Hawakati tamaa ya rehema ya Allah isipokuwa
watu makafiri.”
Na
ikimzidia matarajio (ya Rehema ya Mola Subhanahu Wataala) huogopewa kuwa na
amani (hana shaka ya kuingia Peponi).
الأعراف:
٩٩
“Hawaaminishi adhabu ya Allah ila watu ambao
(watakuwa) wenye khasara”
Na
anasema Al-Ghazali katika kitabu chake “Ihyaa”:- Matarajio na Khofu ni mabawa
mawili ambayo kwayo wanaporuka wanaojikurubisha (kwa Allah Subhanahu Wataala)
kwenda katika kila sehemu nzuri na vile vile vipando viwili ambavyo kwavyo
kinaondolewa kila kikwazo kinachozuia kwenda Akhera na haipelekei kukaribia kwa
Mwenye wingi wa rehema na raha za Peponi wakati matarajio yake (ya rehema za
Allah) yako mbali na mwenye mizigo mizito (madhambi mingi) na ametandwa na kila kinachofanya moyo uchukie kufanya hayo
(yanayopeleka Peponi) na kufanya viungo kuwa vizito kufanya vitendo hivyo
vizuri (kwa hiyo hawezi kufanya moyo wake upende na viungo vyake viwe vyepesi
kufanya amali nzuri) isipokuwa kwa kujipa matarajio ya kupata malipo mazuri
Akhera. Na kwa upande mwingine hawezi kujiepusha na Moto wa Jahannam ilhali
ametandwa na shahawa na ladha ya vitendo viovu (kwa hiyo hawezi kuepukana na
kuwa na shahawa na kupenda kufanya vitendo viovu) isipokuwa kwa kujiogopesha
nafsi yake kuja kupata adhabu ya Allah Subhanahu Wataala na ghadhabu yake”.
Lakini
haitaki(haiwi) mtu kutarajia rehema ya Allah na yeye yungali akimuasi kwa
sababu kufanya hivyo ni kuingilia hukumu ya Allah Subhanahu Wataala na haifai
kufanya hivyo (katika mipango na hukumu yake Allah kuwa mtu haingii Peponi
isipokuwa kwa kutubu na kuamini na kufanya vitendo vizuri na kubakia katika
njia hiyo). Na ni madhehebu ya “Al-Murjia”ndio wanaosema hapana budi Muislamu
anaempwekesha Allah kuingia Peponi hata akimuasi na akifa katika hali ya kufanya
“Kabira” (kosa kubwa kama kunywa pombe,
kuzini, kula riba makosa haya ikiwa mtu ayafanya na akafa bila ya kutubu basi
huingizwa Motoni milele). Na itikadi hii inakwenda kinyume na yaliyomo katika
Qur’ani na hata akili haikubali kitu hichi kwa mfano mfalme wako amekuamrisha
ufanye kitu au kakukataza kufanya na wewe ukampinga na halafu ukagoma hata
kuomba msamaha na kumtolea udhuru basi nini unafikiria utakuwa msimamo wako
kwake? Na inaingia akilini kuwa atakuachia bila ya kukujazi kwa kosa hilo ? Kwani akikuachia
wewe kutasababisha mwingine afanye kama wewe. Isisemwe kuwa Allah ni Karimu na
Yeye ni mwenye kughufuru na Rahimu kwani tutajibu kuwa hapana shaka kuwa Allah
alietukuka na mwenye uwezo amesifika na sifa hizo tukufu mnazozisema isipokuwa
Yeye ni Karimu na Mwenye kughufuru kwa yule anaejikaribisha kwake (kwa toba na
Imani na vitendo vyema) lakini kadhalika ni Mwenye malipo makali Mwenye
kushinda na Alipiza kisasi kwa yule anaemuasi. Ukitaka kujua hayo basi isome
Qur’ani kwani yasema:-
الأنعام: ١٥٨
“Siku
zitakapofika baadhi ya ishara za Mola wako (alizosema kuwa zitawafikia) basi
mtu (kafiri) haitamfaa imani yake ambaye alikuwa hakuamini zamani, au
(Mwislamu) hakuchuma kheri katika Uislamu wake.”
Na
amesema Allah kumuambia Mtume wake mwenye heshima:
هود:
١١٢
“Basi (ewe Mtume) Endelea na
uongofu kama ulivyoamrishwa; (wewe) na wale wanaoelekea
(kwa Mungu) pamoja nawe.”
Na uongofu maana yake ni kufanya wajibu na kuacha
yaliyokatazwa. Na Mtume Salallahu Alayhi Wasalam amwambia yule aliemuuliza juu
ya uongofu:-
قل
آمنت بالله ثم استقم
"Sema Nimemuamini Allah kisha uongoke."
Basi unaona Qur’ani na Sunna
zote mbili hazitosheki na Imani tu bila ya amali (vitendo) na hupati Aya katika
kitabu kitukufu ambayo inamuahidi muumini kuingia Peponi bila ya kufanya
vitendo vyema.
“Kwa yakini walioamini na kufanya
vitendo vizuri”
Aya zote hivi hivi,
halikadhalika haifai vitendo vyema bila ya Imani kama ilivyokuja katika hadithi
ya bint Haatim wakati alipozungumza juu ya baba yake kuwa katika ujahiliya
(kabla ya Uislamu) alikuwa akifanya mambo mazuri akasema Mtume Salallahu Alayhi
Wasalam :- “Kama angekuwa baba yako Muislamu
basi tungelimuombea rehema”. Basi itikadi na vitendo vimeshikana mshikano wenye
nguvu kabisa, ama mja auwache moyo wake ujae fikira mbaya na tabia chafu na
ajiingize kufanya mambo mabaya kwa mapendekezo ya nafsi yake kisha atarijie
maghufira basi matarajio yake haya ni ujinga na kujidanganya.
Amesema Mtume Salallahu Alayhi
Wasalam :- “Mjinga ni yule aliyefuata mapendekezo ya nafsi yake kisha
akatarajia kutoka kwa Allah Subhanahu Wataala kuingizwa Peponi”.
Asema Allah Subhanahu Wataala
:-
البقرة: ٢١٨
“Hakika wale walioamini na
wale waliohajiri (wakahama kuja Madina) na wakapigania njia ya Allah, hao ndio wanaotumai rehema za Allah.”
Amewahusisha kama hawa
kutarajia rehema. Unataka kuokoka nawe hukushika njia yake hakika jahazi
haliendi nchi kavu.
Kukhofu adhabu ya Allah
haipingani na kutarajia rehema yake kwani mambo haya mawili ni kama pacha
hayabandukani kama tulivyoeleza hapo mwanzo
ikiwa Mitume wa Allah AS wakhofu na watarajia basi wengineo wao bila shaka ni
wa kwanza kufanya hivyo. Ameingia Mtume Salallahu Alayhi Wasalam kwa mtu yuko katika
kutoka roho akamuuliza Je vipi wajihisi?
Akajibu najihisi naogopa madhambi yangu na natarajia rehema ya Mola wangu
akasema Salallahu Alayhi Wasalam haikutaniki mambo mawili haya katika moyo wa
mja katika hali kama hiyi (sakaratul mauti)
ila Allah Subhanahu Wataala ampa anayotarajia na humpa amani na yale
anayoyakhofu, ameitoa hadithi hii Anas bin Malik. Amesema Allah Subhanahu
Wataala :
فاطر:
٢٨
“Hakika wanaomuogopa Allah miongoni mwa waja
wake ni wataalamu (wanavyuoni)”.
Na yasemwa kuwa asili ya hekima ni
kumuogopa Allah na kumcha Mungu hakupatikani isipokuwa kwa kumkhofu.
الرحمن:
٤٦
“Na mwenye kuogopa
kusimamishwa mbele ya Mola wake atapata mabustani (Pepo) mawili”.
Khofu
na matarajio yanafuatiana katika baadhi
ya Aya za Qur’ani kama ilivyokuja katika kauli
yake Subhanahu Wataala:
نوح:
١٣
“Mumekuwaje mbona hamuweki heshima ya Allah”
Hapa maana yake kumuogopa
(kumkhofu) na amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-
( إذا اقشعر قلب المؤمن من خشية الله تعالى
تحاتت عنه خطاياه كما يتحات من الشجرة ورقها )
“Ukisisimkwa moyo wa Muumini kwa khofu ya
Allah Subhanahu Wataala yapukutika madhambi yake kama
yanavyopukutika majani mtini”.
Vile
vile kasema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam :-
( ما من قطرة أحب إلى الله تعالى من قطرة دمع
من خشية
الله تعالى أو قطرة دم أهريقت في سبيل الله تعالى )
“Hakuna tone linalopendwa zaidi na Allah
Subhanahu Wataala kuliko tone la chozi (lililotoka) kwa kumuogopa Allah au tone
la damu lililomwagwa katika njia ya Allah Subhanahu Wataala (kupigana jihadi).”
Ameitoa hadithi hii Abu Amama. Na katika Dua zake Salallahu Alayhi Wasalam
amesema kama ifuatavyo:-
( اللهم ارزقني عينين هطالتين تشفيان القلب
وتذرفان الدمع من خشيتك قبل أن تصير الدموع دما والأضراس جمرا )
“Ewe Mola wangu niruzuku macho mawili yenye
kumiminika (machozi) yanayoponesha moyo na kutoa machozi kwa kukuogopa wewe
kabla (haijafika wakati) hayajabadilika machozi kuwa damu na meno kuwa makaa ya
Moto.”
Ameitoa
hadithi hii Ibn Omar kwa Isnadi hassan (nzuri). Na wamesema baadhi ya watu wema
“Kulia kwangu kwa khofu ya Allah mpaka yamiminike machozi yangu mashavuni
mwangu ni kitu nachokipenda zaidi kuliko kutoa sadaka mlima mzima wa dhahabu.”
Anasema
Imam Al-Ghazaliy katika kitabu chake “Ihyaa”:- “Na kauli ya msemaji :- (kusema)
khofu ni bora au matarajio, hilo ni suali baya ni sawa na mtu kusema mkate bora
au maji na jawabu lake ni kuambiwa mkate bora kwa mwenye njaa na maji ni bora
kwa mwenye kiu na hali mbili hizi zikikutanika (njaa na kiu) inatizamwa ipi
iliyozidi mwenzake basi ikiwa njaa ni zaidi mkate bora na ikiwa kiu zaidi basi
maji ni bora. Na zikiwa (hali hizi mbili) sawa sawa basi mahitajio (ya mkate na
maji) kadhalika yanakuwa sawasawa. Kadhalika khofu na matarajio (kuogopa adhabu
ya Allah na kutarajia rehema zake) ni dawa ambazo kwazo zinatibiwa nyoyo, basi
yakiwa maradhi yaliyozidi katika moyo ni amani (na adhabu ya Mola Subhanahu
Wataala) na kujidanganya nayo basi khofu ni bora na ikiwa moyo umezidiwa na
kukata tamaa na rehema ya Allah Subhanahu Wataala basi matumaini ni bora”.
Na
ndio hivyo imesemwa “Ikipimwa khofu ya muumini na matumaini yake zitakutwa sawasawa.
Yasemekana kuwa Omar bin Al-Khattab RA kasema “Lau kama kungeitwa watu wote
waingie Peponi isipokuwa mmoja tu basi ningeogopa kuwa mimi ndio huyo mmoja” na
kila Muumini akikumbuka mwisho wake utakuaje Je atapata taufiki (mwisho mwema)
au kinyume ya hivyo (mwisho mbaya) basi humzidia khofu na matokeo huwa
hujiepusha na maasi na Allah Subhanahu Wataala ni huru kufanya na waja wake vile
Anavyotaka:
الأنبياء:
٢٣
“Haulizwi (Allah) anavyofanya (kwani yote ni ya haki) lakini wao
(viumbe) wataulizwa”.
Fanyeni kwani kila mmoja wenu
amesahalishiwa kuyafanya yale alioumbiwa kwa ajili yake. Twamuomba Allah
Subhanahu Wataala mwisho mwema na kufa katika mwendo mzuri.
Kuridhika na hukumu ya Allah
ni jambo lililo wajibu na kujisalimisha na amri Yake ni faridha. Na amri yake
Allah Subhanahu Wataala haina budi lazima iwe juu ya mja wake ameridhika nayo
au hakuridhika nayo. Akiridhika nayo hupata thawabu na hupewa nafuu katika
msiba wake uliompata na ikiwa hakuridhika hupita hukumu ya Allah juu yake na hukosa thawabu na juu ya hayo
msiba wake uliompata huwa mzito juu yake.
Amesema Mtume Salallahu Alayhi
Wasalam :-
قال رسول الله صلى الله عليه وسلم
إذا أحب الله عبدا ابتلاه فإن صبر
اجتباه وإن رضي اصطفاه
“Allah akimpenda mja humpa mtihani akisubiri
humchagua (kuwa katika waja wake wazuri) na akiridhika humchagua (katika
waliochaguliwa)”.
Amesema
Salallahu Alayhi Wasalam vile vile:
يا معشر
الفقراء أعطوا الله الرضا من قلوبكم تظفروا بثواب فقركم وإلا فلا
“Enyi
Mafakiri mpeni Allah Subhanahu Wataala maridhio kutoka ndani ya nyoyo zenu ili
mpate thawabu ya ufakiri wenu (kusubiria) na ama sivyo hampati chochote”.
Na
katika habari za Nabii Musa AS kuwa wana wa Israel wamemwambia “tuulizie kwa
Mola wako kitu gani ikiwa tutakifanya ataturidhia, akasema Musa Mungu wangu
umesikia walichosema Akasema Subhanahu Wataala “Ewe Musa waambie waniridhie
nami nitawaridhia”. Na inaunga mkono maneno haya hadithi iliyotolewa kutokana
na Mtume Salallahu Alayhi Wasalam kuwa amesema “Anaependa kujua kitu gani
alicho kuwa nacho kwa Allah Subhanahu Wataala basi atazame kile alichokuwa
nacho Allah Subhanahu Wataala kwake kwani Allah anamueka mtu (mahala) pale
mahala alipomueka mja Allah katika nafsi yake” na anasema “Amesema Allah yule
aliyekuwa hakuridhika na hukumu yangu na hakushukuru neema zangu na
hakuisubiria balaa yangu basi amtafute Mola mwengine asiyekuwa mimi.”
Imehadithiwa kuwa Yunus AS
amemwambia Jibriil AS : “Nielekeze kwa mfanyaji ibada zaidi
kuliko wote Duniani akamuelekeza kwa mtu ambaye miguu na mikono yake imekatika
kwa ukoma na haoni wala hasikii naye asema: “Mola wangu umeninufaisha navyo
(miguu, mikono, macho na masikio) ulivyotaka na umenichukulia ulivyotaka wewe
na umeniachia matumaini niliyonayo kwako Ewe Mwema Mwasiliaji”.
Na kuridhika na kinyume ya
mapendekezo (matamanio) ya nafsi (Muislamu asifuate ushawishi wa nafsi bila ya
kutumia akili) hiyo ni daraja kubwa katika daraja za watu wa Dini:
النازعات: ٤٠ - ٤١
“Na
ama yule aliyeogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake, akaikataza nafsi yake na
matamanio (maovu)(40).Basi (huyo) Pepo ndiyo itakayokuwa makazi yake.(41)”
Hapa
pana jambo muhimu, pengine huenda ikasemwa vipi basi (kuna faida gani) mtu
aomba Dua ili Allah amuepushie mabaya na hapana shaka hayo mabaya ni kutoka kwa
Allah? Tunajibu kuwa Dua haipingani na ridha (kuridhika na hukumu za Allah)
vipi itapingana nayo na Mitume wakimuomba Mola wao kama walivyozungumziwa
katika Qur’ani na kauli ya Ayub
AS :-
الأنبياء: ٨٣
“Na
(mtaje) Ayyubu alipomwita Mola wake (akasema): mimi imenipata dhara nawe ndiye
Unaerehemu kuliko wote wanaorehemu”.
Na
kila mmoja katika Manabii amemuomba Mola na wakitajwa hapa kwa ujumla:
الأنبياء:
٩٠
“Na
wakituomba kwa shauku na khofu. Nao walikuwa wakitunyenyekea”.
Na
kadhalika Mtume Salallahu Alayhi Wasalam akiomba Dua kwa wingi juu yakuwa alikuwa katika
daraja kubwa ya ridhaa, kisha Dua ni Ibada bali ndio kiini cha Ibada. Na baadhi
ya mafisadi waropoka kwa kusema maasi ni katika mambo yalioandikwa na Allah
basi vipi (wanasema) alaumiwa anayefanya hayo maasi kwa hiyo ni kinyume ya
kuridhika na hukumu ya Allah Subhanahu Wataala. Tunawajibu kuwa huu ni ujinga wa
hali ya juu na kukosea katika kufahamu mambo kwa hiyo jawabu linalofaa kujibiwa
mtu kama huyu ni kuambiwa “basi hakuna haja ya kupeleka Mitume ili waamrishe
watu mazuri na wawakataze mabaya kwa sababu Allah ndio kisha waumba hao kufanya
maasi. Na maneno haya hayasemi mwenye akili yake anaetambua zuri na baya kwani
Allah Amewakosoa katika Kitabu chake wale wanaoridhika na maasia:
يونس:
٧
“Na
wakawa radhi na maisha ya Dunia na wakatua (roho zao zikatua) kwa hayo.”
Akasema
:
التوبة:
٨٧
“Wameridhika
kuwa pamoja na wanaobakia nyuma na nyoyo zao zikapigwa mhuri (zikazibwa)”.
Na kuna hadithi inayosema:-
( من شهد
منكرا فرضي به فكأنه قد فعله )
“Mwenye kuona uovu akawa radhi nao basi ni kama yeye kaufanya (huo uovu)”.
Na nyengine yasema:-
( لو أن
عبداً قتل بالمشرق ورضي بقتله آخر بالمغرب كان شريكا في قتله )
“Lau kama mja ameuliwa mashariki na akaridhika
kwa kuuliwa kwake (mja) mwingine magharibi, angekuwa mshirika katika mauaji
yake”.
Na suala la “Al-wilaya”
(kupenda mtu mwema kwa ajili ya Allah) na “Al-Baraa” (kumchukia mtu muovu kwa
ajili ya Allah) limeambatana na hadithi hiyo ya juu na lau kama maneno ya hao
wenye makusudio mabaya (mtu kufanya maasia kaandikiwa na Allah kwa hiyo
halaumiwi) ni sawa ingebatilika “Al-walaya” na “Al-Baraa” vipi akasirike mja na
asiwe radhi kwa yale aliyohukumiwa ndugu yake na Allah Subhanahu Wataala,
kuzini, kuiba na kunywa pombe, basi ikilazimu kuridhia vitendo vya hao kwa
sababu wamefanya yale walioandikiwa na Allah ikiwa hivyo itakuwa imepingwa
hadithi ya Mtume Salallahu Alayhi Wasalam inayosema:
( أوثق عرى الإيمان الحب في الله والبغض في الله )
“Katika vishiko vya Imani vilivyokuwa na nguvu kuliko vyote ni
kupenda kwa ajili ya Allah na kuchukia kwa ajili ya Allah.”
Na asema:-
( إن الله أخذ الميثاق على كل
مؤمن أن يبغض كل منافق )
“Hakika Allah amechukua ahadi juu ya kila Muumini amchukie kila
Munaafiki”.
Basi ikisemwa kila kitu ni kwa
hukumu (Qadhaa) ya Allah na majaaliwa yake(Qadar), na kwa hiyo maasi vile vile
ni katika maandiko na majaliwa ya Allah ni sawa sawa kwa sababu tukisema
kinyume ya hivyo tutakuwa tumeivunja Tawhiid na upande mwingine tukisema kuwa
hayo maasia ni katika maandiko ya Allah basi vipi tena tuchukie mtu kuyafanya
itakuwa tumechukia hukumu yake(Qadhaa) Allah. Jawabu lake ni kuwa sisi tumeamrishwa
kumchukia anaefanya maasia na tumpende anaemtii Allah Subhanahu Wataala na sisi
(Waislamu) tukiamrishwa kufanya jambo na Allah
Subhanahu Wataala tunasema سمعنا وأطعنا “tumesikia na tumetii” na sio kila ibada (معقول
المعنى) yaingia akilini mfano udhuu wa Sala
wajiosha kila kiungo mara tatu lakini kwa sababu umeamrishwa kufanya hivyo
unafuata bila ya kuuliza maana na hekima yake na kadhalika ( القضاء
والقدر) Qadhaa na Qadari ni siri katika siri za
Allah kwa hiyo haijuzii kuchunguzwa na kuulizwa kwa nini? Vipi? Amesema Mtume
wa Allah Subhanahu Wataala :-
( القدر سر الله فلا تفشوه )
“Qadari (maajaliwa ya Allah)
ni siri ya Allah basi msiifichue”.
Allah
Subhanahu Wataala hufanya atakayo kwa mja wake na juu ya mja kufuata (kutii)
alioamrishwa asipinge wala asiende kinyume na inatuwajibikia kuwa na adabu na
heshima tusijiingize katika mitelezo kama hii(
inayompeleka mtu katika ghadhabu ya Allah). “Kama
nzi alishia katika sehemu zenye maradhi” (katika mwili wa binaadamu). Ikiwa
binaadamu hukatazwa kusema kwenye siku yenye joto “leo joto sana ”
kama kwamba
ashtakia. Basi ikiwa jambo kama hili
dogo haifai kuliingilia, vipi kuingilia
mambo yanayohusika na vitendo vya mja na malipo yake, huku ndiko kujasiri
kukubwa juu ya mipango ya Allah Subhanahu Wataala.
Na
aambiwe huyu mjinga (anaejasiri kuingilia mambo ya Allah Subhanahu Wataala)
chukua pesa zako na vitu vyako uvitupe njiani avichukue yeyote anaepita njia
kwani ukifanya hivyo itakuwa katika majaliwa ya Allah Subhanahu Wataala.
Imetolewa kutokana na Omar bin Al-Khattab RA kuwa amesema:
( لا أبالي أصبحت غنيا أو فقيرا لأني لا أدري أيهما خير لي )
“Sijali nimeamka tajiri au
maskini kwani sijui ipi katika hali mbili hizi ni kheri kwangu”.
Na
Dua yetu ya mwisho ni kusema:
( الحمد لله رب العالمين
والصلاة والسلام على رسول الله وآله وصحبه أجمعين )
No comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.